BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DUNIA YA TATU March, 15, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya,Weekend Special — bongocelebrity @ 10:00 AM

 

Baada ya kutamba kwa muda mrefu,wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mandojo na Domokaya au ukipenda “wazee wa magitaa” wameamua kuongeza nguvu kwa kumuingiza kundini msanii ajulikanaye kama Squiza. Na kutokana na ongezeko hilo,wameamua pia kubadili jina lao kutoka Mandojo na Domokaya na sasa watajulikana kama Dunia ya Tatu au D3 wakiwa ni wasanii watatu kama wanavyoonekana pichani.

 

Wengi mtakuwa mnatambua jinsi ambavyo Mandojo na Domokaya waliwahi kutamba na vibao vyao kama vile Dingi,Wanok nok,Niaje na nyinginezo nyingi.

Wakiwa pamoja hivi karibuni wasanii hao wameiambia BC kwamba wameamua kuongeza nguvu na kubadili jina kwani wameamua kutoka kivingine huku wakiendelea kuweka nakshi miziki yao kwa kutumia magitaa na vyombo vingine.Mpaka hivi sasa wameshatoa single inayokwenda kwa jina We Nenda ambayo hivi sasa wako mbioni kutengeneza video yake.

 

D3 wanasema hayo yote ni katika maandalizi ya kutoa albamu yao ya kwanza wakiwa kama D3.Kazi zao nyingi hivi sasa wanazifanyia ndani ya studio za 41 Records.BC inawatakia kila la kheri D3.

 

Advertisements
 

11 Responses to “DUNIA YA TATU”

 1. Gervas Says:

  Vijana mimi nawakubali saana na style yenu hasa Mnavo-chana (Rap). Hii single yenu sijaipenda sana, Mandojo, domokaya, na Squeezer nyie ni vichwa. Ninavyoona Kati ya wasanii wa Bongo wenye vipaji kwenye tatu bora mpo. hebu tizama wimbo Dingi, au Squizer alivoimba na “nature” Mkipata director mzuri wa kuwashauli mpangilio wa ku-flow, mtafika mbali…beyond borders!!…… Big-up people!!

 2. Edwin Ndaki Says:

  Wanok nok watu wa kusinzingiziaaaa menooo ya watu washkaji wanarushikiaa…

  Ile ilikuwa balaaa..hapo navuta taswira nipo malimbe,SAUT hukoo kwenye ma mapanki yangu ya Hubert Sauper.

  Vijana nawakubali sana na “mabanjo”..kama wasemavyo wenyewe.

  Squeezer..namkubali pia dude lake naja au wimbo alioimba na ndugu yake Dataz..mr afisa….

  Kila la kheri D3…kama vipi mimi pia nina mistari yangu…mniweke kunduni tuwe ni D4…

  Mmeungana,tulieni mfanye kazi,maana Clouds wanatamani mkosane ili waandae show..natania tu.

 3. Mswahilina Says:

  Ninawakubali vijana wanafanya mambo makubwa.

  Gervas, ni KUWASHAURI sio ‘kuwashauli’ kama ulivyoandika

 4. Gervas Says:

  Edwin uminichanganya …wakuweke wapi??

 5. Edwin Ndaki Says:

  aaaa..aaa tungo tatat siyo…aaaaaa aaaaaa

  mimi wapine nichane verse ya mwisho….aaa aaaaaaaaaaa

  Gervas naona umemua kupiga ikulu….

  jpili njema

 6. Chris Says:

  Domokaya amenyoa zile rasta?????? Wakaze buti….

 7. Michelle Says:

  mhhh nanyi mmezidi mbwembwe acheni kuwaiga Wa america mnaonekana malimbukeni tu na hivyo vidole, tutavikata mwishowe looo!

 8. mtz Says:

  Michelle umeongea ukweli; hayo mabuti na joto wapi na wapi. Mtatuita tu wabeba mabox but maaaaaan tunafaidi huku.

 9. solange Says:

  jamani hawa vijana walivuma mpaka basii…”basi nenda kamambie baba eeeoo yaeee mziki wangu chacha masela wanaupata sema chachaaa…” mmekaa kimya sana jamani.

 10. amina Says:

  hizi sura za ganja..ila mziki wa bongo jamani…hawavumi kama mwanzo ilikua eeeh kila kona ni hip hop banjo

 11. Gman Fremah. Says:

  hapo ni pwaaaa ila waangalie mtu mwenyewe waliyemlejesha kundini. Kweli ana umoja!? maana asije ikawa ni baada ya wiki tatu akalibomoa kundi ambalo limekuwa very strong kati ya makundi mendi hapa BONGO. (Tanzania) Si kama napinga lakini huyo jamaa tunamwomba alitunzie kundi hilo heshima kwani likivunjika sisi kama wapenzi bila shaka tutajua ni yeye. Ma squiza plz jenga kundi kama ulivyolikuta. Wanangu ndojo & d.kaya!!! ni fagio tu baba la mlingoti bendera badi hapafuatwi upepo. (mzehe wa mcmamo) daima msimamo
  Tuko pamoja!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s