BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DOWN THE MEMORY LANE March, 17, 2008

Filed under: African Pride,Fashion,In Memory/Kumbukumbu,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Pichani ni viongozi wa taifa letu mwanzoni kabisa mara tu baada ya kupata uhuru mwaka 1961.Jambo moja ambalo limetuvutia mpaka kuamua kuweka kumbukumbu hii ni mavazi ya “waheshimiwa”.Ukitizama utaona kwamba kumbe wakati tunapata uhuru,wengi miongoni mwa viongozi wetu,walikuwa wanathamini mavazi ambayo hata kwa kuyatizama tu unaweza kutambua kwamba ni mavazi ya “kiafrika”.

Sasa nini kilitokea baada ya hapo?Mbona leo hii ni nadra sana(kama huwa inatokea) kuwaona viongozi wetu wakitukuza mila,tamaduni na desturi zetu japo kuanzia kwenye mavazi tu?Mbona wenzetu wa sehemu zingine za Afrika kama vile Afrika Magharibi wao wanaendelea kujinadi na mavazi yao ya asili?Ni kweli kwamba sisi hatuna vazi la taifa au tumezembea tu kuwa nalo?

Je unawatambua viongozi unaowaona pichani?Kama jibu ni ndio basi tusaidiane katika kuweka kumbukumbu sawa.Shukrani za pekee kwa Michuzi kwa kuhifadhi picha za kumbukumbu kama hizi.

Advertisements
 

16 Responses to “DOWN THE MEMORY LANE”

 1. Gappi Says:

  Nafikiri hilo ndilo vazi letu la taifa maana hata machifu wengi wa zamani walivaa hivyo. Vazi hili halivaliwi kwa sasa ni kutokana na kasumba ya kupenda kuiga vitu vya mataifa ya ulaya na amerika.

 2. Mbarikiwa Says:

  Hii ni hazina yetu. Naona walio hai ni takribani wawili tu. Waliotuacha Mungu Mwenyezi awalaze pema peponi. Amen

 3. Knoah Says:

  Sawa mavazi ya “Kiafrika” lakini sio Kitanzania.Sisi tunaiga iga tu. Baada ya hapo kumbuka walituletea Chu En Lai eti vazi la “kitaifa” – tuliiga waChina. Kama mavazi haya ni muhimu, mara ya mwisho umemwona wapi Mtanzania au kiongozi kavaa hivi?

 4. bongosamurai Says:

  Nawatambua wote kama wazalendo walipenda kuona Tanganyika iliyojaa neema. Huu ndio utambulisho wao bila kujali majina.

  Mgolole (kama sijakosea) aliouvaa hayati baba wa taifa ungefaa kabisa kuwa vazi la utambulisho wa taifa letu. Haya mambo ya suti tumeiga tuu kutoka nchi za magharibi kwa kutaka kuonekana civilized…!

 5. athmani ally Says:

  Hii picha naikumbuka. Nzuri sana. Nakumbuka ilipigwa wakati mimi ndo nastaafu usalama wa taifa wa enzi hizo.

 6. mkaku Says:

  Ukiniambia waliiga mavazi ya machifu wakina mangi marealle na chifu mkwawa (sio adam sapi) nitakuelewa maana wale sijui waliiga kutoka wapi. Ndio maana wao kama viongozi w ncho waliona wavae kama machifu wao ni vazi la kwetu kabisa nenda maktaba utaona machifu walivaaje enzi hizo

 7. Gervas Says:

  Bc hatuwezi tena kurudi huko, maji yalishamwagika tayari, saizi ni umarekani na uingereza tu kwa mambo yote, kuongea, kuvaa,mziki..yoo! whats up?. Picha hii ni dream team ambayo hatutaipata tena. Tumetoka kwenye ukoloni live sasa hivi tupo kwenye ukoloni mamboleo, na baada ya miaka kumi tutakuwa kwenye ukoloni mambokesho!!

 8. Gervas Says:

  unajua ukoloni ni mzuri sana mi nashauli wakoloni warudi tena, hasa wajeremani, maana sisi hatuwezi kujitawala tena ni ufisadi tu. wajeremani walitutawala muda mfupi tu lakini waliacha reli ya kati na wachina wakatujengea ya Tazara. Saizi tumebakiza kuvaa suti tu natengeneza shavu. wana blog..hivi ile story ya “kawawa funika kikombe” ni ya kweli? au mgabe awe raisi wa afrika ndo tutatoka.

 9. Chris Says:

  Mzee Athman Ally ulikua na umri gani muda huo? Maana inawezekana ukawa ni mzee sana hata kuchana toilet paper huwezi.

  Kuhusu hilo vazi, hao hao wanaosema hatuna vazi la Taifa au “tuliunde” ilhali ni kama hilo lipo hawavai. Nani atakaevaa? Kikwete na baraza lake na wewe na mimi tunataka Suit safi, jeans n.k.

  Anaesema hilo ni la Africa na si la Tanzania nadhani anakosea kwa sababu hilo vazi nafikiri lilikuwepo kabla ya hata kuwa na interaction na other parts of Africa. Na waafrika tamaduni zetu zinaendana.

 10. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Kumbukumbu nzuri ya viongozi wetu.

  kuhusu mavazi, ni kweli ni vizuri kufikiria kuwa na vazi la kitaifa, lakini liwe ambalo linafaa kufuatana na mazingira, uchumi na matumizi ya hilo vazi.

  Suala la kuona tu kuwa kila kitu cha kizungu ni kibaya au ni kasumba mbona hatutaishia hapa. Maana hapa hii ni picha ya wakati wa Uhuru kama ni hivyo kwa nini tusirudi nyuma miaka 200 au zaidi kabla ya ukoloni ambapo wengi walitembea sehemu kubwa ikiwa haikufunikwa kama huko ndiko kuuenzi Utanzania ?

  Mimi nikiangalia kwa makini mikao, mavazi na hata mitindo ktk hiyo picha naona tayari tulishaiga vitu kibao toka uzunguni, uarabuni n.k . Maana tunaona tai shingoni, suti, shuka (za vitambaa vilivyotengenezwa viwandani), viatu, saa mikononi hata na vidani shingoni na zaidi ya yote ule mchano ujia wenye ‘way’ kichwani n.k

  Ni kweli suala la kung’an’gana na suti (tena wengine huvaa four pieces na tai halafu ukae juani hapo Dar au Dodoma eti ukisikiliza speeech ya mh. kwenye siku ya Kitaifa ni kujitafutia kuugua bila sababu. Hata katika vikao, ndio maana watu husinzia ovyo.
  Hata hivyo niseme pia kuwa mimi hiyo Lubega sijui Mgolole (mswahilina sahihisha) bado sioni kuwa ni vazi zuri hata kama ni la asili maana mtu unakaa unabebana na kushikilia shuka kubwa wakati wote kiasi cha kukufanya hata ushindwe kutumia mikono yako yote vizuri kwa kazi nyingine.
  Halafu bado unakuta ndani wana mashati na suruali, kwa nini nitafute kuumba joto wakati wote wakati hatuna baridi wakati mwingi! Na pia tuzingatie uchumi, kwa nini nivae mita 5 za kitambaa kama 2 zinanitosha?
  Vazi liwe affordable, decent & comfortable!

 11. Dullah Says:

  Kuna yoyote anaekumbuka majina yao wote waliopo kwenye picha? kama yupo si vibaya kuyataja. Kwenye picha hii ninaowafahamu ni Baba wa taifa, Kambona na Kawawa. Thanks BC.

 12. Mswahilina Says:

  Asante sana BC kwa kutukumbusha ‘Enzi zetu’.
  Kuhusu vazi: mie kwa maoni yangu ni vyema watu wabadilike, maana itafikia wakati wengine watasema wazee wa zamani walikuwa hawavai nguo kabisa, hivyo kudumisha mila tusivae nguo. Wa-Tanzania tukubali tu, tumeshaiga vitu vingi vya Wazungu, kuvaa Suti ni ‘kakuigwaga’ kadogo sana ukilinganisha na MWANAMUME mwenye akili zake timamu anavaa hereni ‘kama mashoga wa nchi zilizoendelea’

  Gervas, kwenye hoja #8 ni ‘nashauri’ sio ‘nashauli’ kama ulivyoandika.
  Kuhusu story ya “kawawa funika kikombe” hiyo niwaachie waungwana waliokuwa wanaandamana na Rais kwenda nje ya nchi.
  Kuhusu suala la Mugabe kuwa Rais wa Afrika hiyo ni ndoto tena kati ya zile ndoto za Alnacha.

  “Tukipende Kiswahili” ; “Tuzungumze na Tuandike Kiswahili Fasaha”

 13. majita Says:

  “Tukipenda kiswahili”; “tuzungumze na kuandika kiswahili fasaha”Sawa.Nanukuu “……….waungwana waliokuwa wanaandamana na Rais kwenda nje ya nchi”.Mwisho wa kunukuu.Hiki ndo kiswahili fasaha.Mhhhh azafali mimi wa shamba majita sijasema.

 14. Kimori Says:

  Nadhani kabla ya kuongelea vazi la taifa au la Kitanzania nafikiri ingekuwa busara kujua historia ya mavazi katika nchi yetu. Kama sikosei, nguo tumeanza kuzivaa kama karne tatu au nne hivi zilizopita (wana historia watanisahihisha).

  Kinachofanyika kote sasa hivi ulimwenguni ni kwamba wabunifu wa mavazi huja na mitindo mabli mbali ambayo inakwenda na wakati. Hata hivyo ukiangalia kwa makini mitindo hiyo hujirudarudia baada ya miongo fulani. Hayo mavazi yanayoitwa ya kitaifa kwa nchi nyingi yamebakia tu katika kumbukumbu na huvalika labda katika sikukuu fulani fulani na si wote waliyonayo au huyavaa!

  Sisi kwa vile hata nguo tuliletewa tu, hatuna cha kujivunia kuwa ni cha kwetu maana wabunifu wa mitindo wa karne hizo hatukuwanao. Kama tutaamua sasa hivi kuwa na vazi la kitaifa basi bado ni kuiga tu kwa sababu “hatuwezi kuvumbua gurudumu katika karne hii”. Hata hivyo kutokana na utandawazi na uhuru wa kuvaa mtu anavyopenda tusing’ang’anie sana vazi la kitaifa maana tuna mambo mengi sana ya kujivunia kama taifa na si mavazi tu.

  Kuna mtu ametoa maoni na kusema kuwa hata wanaume wanaotoboa masikio na kuvaa heleni ni utamaduni wa wazungu. Naomba nitofautiane na hilo wazo. Mimi nilizaliwa katikati ya karne iliyopita lakini makabila kama ya wakurya na hata wamasai wanaume wamekuwa wakitobolewa masikio na kuning’iniza heleni tena nyingi tu! Ndugu zangu wakurya ambao nawafahamu vyema ni kwamba masikio yanatobolewa kisha yanavutwa na kuning’inia yakiwa yamevishwa heleni nzito! Wazungu wameiga tu juzijuzi.

  Nadhani watingiga, wamang’ati, wasandawi wananielewa vizuri sana ninaposema kuwa hatuna vazi la kitaifa!

 15. Mswahilina Says:

  Mie ninakubali kuwa kwa wakati huo (katikati ya karne ya 20) makabila mengi hapa Bongo Wanaume walikuwa wanatoboa masikio na kuvaa hereni pamoja na nguo za kimila.
  Ninawasihi basi, wale Wanaume wanaotoboa masikio na kuvaa hereni wavae pia nguo za kimila sio kuvaa suruali na mashati kama ‘Mashoga’ wa nchi zilizoendelea.

 16. amina Says:

  mhh mi ndo sijui kabisa


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s