BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PRIDE OF TANZANIA March, 19, 2008

Filed under: Fashion,Fashion Designer,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:03 AM

 

Kama kuna mafanikio yoyote katika masuala ya urembo ambayo Tanzania inaweza kujivunia,basi vielelezo vya mafanikio hayo ni mabinti wawili wanaoonekana pichani.Kushoto ni Nancy Abraham Sumari ambaye mwaka 2005 aliibuka kuwa Miss World Africa na Flaviana Matata,Miss Universe Tanzania 2007 ambaye pia aliipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini Mexico katika mashindano hayo ya dunia na kushika nafasi ya sita huku akiacha gumzo duniani kote kwa kuwa mshiriki wa kwanza wa mashindano hayo ambaye aliingia na “kipara”.

Usiku wa leo,Flaviana Matata, anatarajiwa kuonyesha mitindo ya mavazi ya mbunifu wa mitindo,Angelo Elly Mlaki katika Ukumbi wa Kituo Cha Utamaduni Cha Ufaransa(Alliance Francaise Cultural Center) kilichopo jijini Dar-es-salaam.Maonyesho hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Compass Communications ambao ndio waratibu wa Miss Universe nchini Tanzania.

Advertisements
 

33 Responses to “PRIDE OF TANZANIA”

 1. solange Says:

  flav nakupenda yani hivyo ulivyo nakupenda tu….gud lucky ma dia katika harakati za kupambana na life.

 2. Matty Says:

  Warembo juu juu zaidi!mmependeza wenyewe na viwalo vyenu Flaviana hako kakoti sijui kijasti bcoz sijakapenda na wewe Nancy kilichokusibu Kunyoa nywele nini??na hizo tite nini nini tena sijui za nini miguuni na joto lote hilo Bongo?haya ni chaguo lenu wenyewe kwa raha zenu.

  Nawatakia Pasaka njema wadau wote wa hapa longalonga place,Mama wa Kichaga,Amina,Chris,Gervas,Albert,Kekuu,Subby,Any,Michelle, Mswahilina, Edwin Ndaki na wote niliowasahau jamani hatukaribishani??.

 3. Edwin Ndaki Says:

  Pongezi sana kwa wote wawili hakika ni jambo la faraja kwetu tukiwa ni watanzania.

  Kikubwa wakumbuke wao ni vioo katika jamii yetu,hivyo ni vema watumie nafasi zao katika kufanya kampeni mbalimbali za kuinua sauti na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.Mfano, suala la kupambana na ajira mbaya ya watoto.

  Kila la kheri katika mikakati yetu ya maisha.

  Tufika tu.

 4. mzawa Says:

  Wa!wawa!waa ! tuanwakubali warembo wetu hawa wa bongo
  kazeni buti mabint

 5. Rehab Says:

  huyu binti nancy ana mvuto kweliii..

 6. Edwin Ndaki Says:

  Matty wewe tena,
  usijali tutakuwa wote k-nyama pale darajani kona,kwa Dani…aa aaaa kula mdudu…aaa najua umenipata..mambo ya tafadhali iwe kavu na ndizi mbili…

 7. Gervas Says:

  Matty, Asante kwa salaam za Pasaka, yaani ndo umenikumbusha kumbe mara hii imeshafika pasaka? duh mambo ya kukaa huku bush noma sasa. ngoja nikafanye booking la ulanzi kabisa. Huyu Nancy ni butifu ila naona mapeema ataanza nenepa kama dadake, na nadhani hajapendeza kukata nyele.

 8. Mswahilina Says:

  Warembo wa Tanzania hao wamependeza, Wametangaza Utanzania wetu, ni Mabalozi mahiri kwetu.

  Matty, asante sana kwa salamu za Pasaka.
  Nami naungana nawe nikiwapa heri na fanaka wadau wote wa blog hii. Ushauri wangu kwa wote ni kuwa wadumishe Amani katika kila watakalofanya kipindi hiki cha pasaka na kuendelea maisha yao yote.
  ‘Hepi Ista’.

 9. Chris Says:

  Pride of Tanzania…. wanasema USISEME TANZANIA IMEKUFANYIA NINI, JIULIZE UMEIFANYIA NINI TANZANIA? Nakubaliana na hii kauli kwa zaidi ya 80%. Maana kuchapa kazi kwangu ndo kunainua Tanzania na serikali yangu ya kifisadi (wanapata za kuchota).

  Lakini nifanyapo jambo la maana serikali yangu inabidi ione huo mchango wangu kipekee,kama nilivyoifanyia/ipeperusha in different capacities… whether ni kisanaa,kiuchumi etc.

  Kama mara 2 au tatu BC mmekua mkitoa picha za wasanii wetu, ambao wameipeperusha bendera za Tanzania kwa capacities zao, swali inamaana hii kauli PRIDE OF TANZANIA na zingine za namna hiyo ni za upende upi?Serikali/wananchi ndo these heroes are their pride au these heroes ndo inabidi wawe pride of Tanzania? Je inamaana serikali thamani kwako inakua unaporudi tu uwanja wa ndege pale na maua… then kila kitu kwake?

  Yuck, this shit really piss me off… Hao mabinti wote ilibidi wawe na mikataba sehemu wanapiga mzigo, sasa hv utasikia wamepigwa mimba… inabaki walifikia level hiii…. na inakua history before their time to be history..

  Matty x-mass si ilikua jana? Mara tu Pasaka? Ngoja niangalie calendar, u may be duping me…. Aiseeeeee karibu sanaaaaaa mtu wangu………..Ndo kwanza good thursday…. Karibu isubirie…

 10. any Says:

  wee Matty kijust cha mwenzio kimekukosea nini? yeye kakipenda, kama wewe hujakipenda sio shughuli yako, huenda na lile bazee lako unalolipendaga yeye Flavian halipendi sema tu wewe hujawekwa apa! Easter njema. hehehe.

 11. Gervas Says:

  Any, ukishakuwa public figure ni kwamba unawatachi watu wengi, Nancy anapresent bado watanzania, hivo wanampenda aendelee kuwa butifu, sasa usimshangae Matty akitoa comment kuhusu hicho ki serewali, maana hata mimi naona hajapendeza, kawa kama chakubanga!!

 12. any Says:

  Gerivasi ngoja nikuambie its hard to please jamii nzima, yeye ameona apo katoka kisawa sawa, ivo tusimsakame. Apo hakuwa kwenye maonyesho wala nini kajivalia casual tu, ivo mwacheni apumue, huyu mtoto mmemsakama sana jamani! Can we just support her than criticizing bila sababu za msingi!

 13. any Says:

  sorry Gervas mimi nilikuwa namwongelea Flavian, maana Matty ame comment kuhusu blauzi alovaa! sio Nancy, huyu nancy apo alichemsha, joto dar na soksi hizo ni noma

 14. binto Says:

  wenye wivu utawaona wanatafuta kila njia ya kukuweka chini, tanzania kweli jamani, punguzeni majungu.

 15. Gervas Says:

  Pasaka njema Any…..karibu kwetu

 16. Matty Says:

  Ahaaa Any kumbe mkuki kwa nguruwe ehee!!!!!!!!!mimi ijapenda kijasti bcoz narudia tena mimi (me) na wewe hujapenda hizo soksi za Nancy sasa nani kakuuliza kitu hapo?? mama tulia tuli na mawazo yangu katu usiyaingilie na mimi sitofatilia yako, na kuhusu lile bazee langu nikivaa huwa natoka chicha kuendana na umbile langu kama anavyopendezaga Sata Tomas.lol!give me abreak!

  Wewe Edwin Ndaki pale k/nyama darajani haaaaaaaaaa sijapita siku yingi itabidi nikipata chance nijidropishe pale nipate yenyewe kavu kabisa na pipipili kali!hhhhhaaaaaaaaaaaa utamu.

  Gervas ukiagiza ulanz niagizie na mimi mkangafu lita 3 na nyamspu sahani moja iwe na mchuzi khaaaaaaaaa raha sana kwa mama nani tena/?????
  Haya Chris kalenda yangu inaonyesha pasaka tayari sasa sijui imekosea??najua iko sahihi….PASAKA NJEMA WOTE.

 17. Michelle Says:

  Salaam za pasaka kwa ndugu zangu wapendwa Gervas, Dullah, Mswahilina, Binto, Chris, Matty, Any pamoja na wengine wote, mbona kimya Dullah vipi tena? ujumbe ni wakati wa kukaa sawa kiroho Pasaka njema.

 18. any Says:

  Tuliza mpira wewe, soksi zake nazipenda sema kazivalia mazingira sio yenyewe. Swali la nyongeza?

 19. kyekue Says:

  yaani ndugu yangu any we kweli kiboko , kwa picha ya kagame na mkewe ulimponda sana Salma na shuka lake. Nikajua labda una mtazamo tofauti katika maswala ya vivazi. Nashangaa hapa unachomweleza Matty, kumbe unajua kuwa fika Salma na shuka lake yeye ndio kalipenda na wewe halikuvutii. nkiki maaa, asavali ukae kimya kwa vile unajua kuwa kila mtu ana test yake katika maswala ya mavazi…….ni maoni tu mpendwa wangu katika bwana

 20. any Says:

  hujanielewa mkeku. nilichouliza ni kazi za hizo shuka/upande.

 21. any Says:

  kekyue, hakuna nilikosema lile shuka halinivutii? Niliuliza matumizi ya hilo shuka, au lina maana gani? ni symbol ya nini? au ni status, au ni dress code kwa wake za marais, maana dadangu anna Mkapa sikumwona nalo! au ni ari mpya? i was just curious? sijalitaka wala kulikataa huo upande, nimeuliza matumizi yake, najua kila mtu ana chaguo lake, akiamua kuvaa kimini sawa, akiamua kuvaa mgorori, kivyake, sina haki ya kumpangia mtu mavazi. Peace Kekyue.

 22. Matty Says:

  Any ingekuwa ni mechi wewe ni mshindi nimekubali kushindwa!!!!haya na hapa kumbe ni bungeni lol! sikujua have a nice easter!

 23. Matty Says:

  Asante sana Michelle kwa salamu ok…tuko pamoja!

 24. Ze bebi Says:

  Flaviana this is for you!!!
  Umezidi, na acha kuvaa midosho……….
  Find stuffs of ur class, omba msaada usaidiwe hata kwa hao wenzio.wanakudeku tuuuuh….unatokea full ki-beki tatu mtu wangu.,,kwa roho safi tuh wangu

 25. Saidi Situ Says:

  Hakuna uzuri wowote hapo, kuna wembamba wawili tu. Inabidi washauriwe wakawe assessed (measure) waanze kutumia msaada wa bush.

 26. Kekue Says:

  Tehe tehe uuwi mbavu zangu!! Gervas umenikumbusha mbali sana jamani enzi za kina Chakubanga hivi wapo????

 27. amina Says:

  mhh matty mi nikisema nitashambuliwa humu ila mhh,bora niumie ndani kwa ndani flaviana hicho kijasti kama /////…edwin ndaki mbona nilikua kidarajani kwa dani sijakuona?nilikua nakula shuwain pale siku ya pasaka

 28. Matty Says:

  Amina wewe si ustadhati?? kumbe na wewe mtaalamu wa ze na nihiiiiiiii mix na pilipili?? tuwe tunashtuana shosti!

 29. Dell Says:

  Flaviana is truly beautiful. Heart and soul. Go Sweetheart – give them something to talk about.

 30. amina Says:

  matty mi mwislamu jina tu,,ila shwain napeleka ila home hawajui ndo yale yale ya nimo kujiita nadya…weka rosti na kachumbari

 31. binto Says:

  flaviana achana na mahaters wataongea sana achana nao.

 32. Shuu Says:

  binto sibora uongee kiswahili..mahaters ndo nini?

 33. Matty Says:

  Yaani nikiona hii picha najisikia aibu mimi kutokana na tuvazi twao khaaaaaaaa! Any personal decision nyingine zinanifanya nikose uvumilivu kwa kweli!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s