BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DOWN THE MEMORY LANE;THE BEST PM EVER? March, 26, 2008

 

Kama kawaida yetu,tunapotumiwa swali/maswali na baadhi yenu ambayo kimsingi tunahisi hatuwezi kuwa na jibu/majibu yenye uhakika au yanayojitosheleza,huwa hatuna budi kuomba msaada kutoka kwako msomaji.Katika mfulululizo huo huo; msomaji wetu mmoja ametuandikia akiomba kupata maoni kuhusu nani unadhani ndiye amewahi kuwa Waziri Mkuu bora kushinda wengine wote katika historia ya nchi yetu ya Tanzania mpaka hivi sasa?

Msomaji wetu huyu, anasema, kwa upande wake,Hayati Edward Moringe Sokoine (pichani) ndio aliwahi kuwa Waziri Mkuu bora. Unakubaliana naye?Kwa upande wako,ni Waziri Mkuu yupi ambaye unadhani ni bora kushinda wengine mpaka hivi leo?

Advertisements
 

42 Responses to “DOWN THE MEMORY LANE;THE BEST PM EVER?”

 1. nyarubamba Says:

  BC,kujibu swali lako kwa uhakika na usahihi itakua ni vigumu sana.Kwani kila ambaye amewahi kuwa waziri mkuu amekua katika madaraka katika kipindi ambacho ni tofauti na mwingine ama aliemfuata au kumtangulia.Pia priorities na strategies katika kipindi husika zinatofautiana.Uongozi katika ngazi hiyo sio sawa na kazi kama ualimu,kwamba kila atakae fundisha darasa la saba basi atatumia mitaala inayofanana au shabihiana.Hivo ni vigumu kutoa maksi labda kama kuna mtu ambaye anaeweza kulevel ground ili kuwafair na wale wote waliokwisha kuwa mawaziri wakuu.Nitatoa mfano,unadhani wakati “Simba wa Yuda”anachukua maamuzi yale katika kipindi kile ni sawa kabisa na kipindi ambacho Sumaye alikua waziri mkuu?.Enzi zile tulikua katika vijiji wakati huu ni Ufisadi ni tofauti kabisa.Nadhani kama kungekua na vigezo labda,nasema labda tungeweza.Pia kumbuka kuna popularity ya ghafla kama ya ndugu yetu Mzee wa Baragashia na mambo kama hayo,kuna umuhimu wa kucontrol baadhi ya vigezo ili kuweza kuwagrade mawaziri wetu wakuu.Hivo kupata jibu sahihi ni vigumu sana.

 2. Ben Says:

  waziri mkuu bora Tanzania alikuwa Edward Lowasa peke yake, kwa maana alikuwa bora sana kwa kujishughulisha na masuala ya ufisadi kama Mirich Mond, Mi poor Mond na mengineo so kwa kifupi alikuwa maarufu na bora kwa ufisadi, na kufukuza viongozi wengine kama District C, Regional C, Madiwani ili aweze kufisadi vizuri .ingawa vipofu walikuwa wanaona ni kiongozi bora kumbe alikuwa bora kiongozi, Na nukuu kidogo wadau.
  NIMESEMWA SANA.
  NIMETUKANWA SANA NA VYOMBO VYA HABARI.
  NIMESHUSHIWA HESHIMA YANGU KWA TAIFA.
  NIMESIMANGWA SANA.
  NIMENYANYASIKA SANA.
  NIMEUMBUKA SANA.(kwani uliambia ufisadi?)
  WAMENINYANYAPAA SANA.(Si ugonjwa wa ukimwi ni ufisadi wako tuu)
  WAMENIANGALIA SANA(ulidhani watu vipofu?)
  WAMENISHUSHIA HADHI(ulitaka kuwa kama Bush?)
  WAMEIBA NGO’MBE ZANGU( Ulikuwa hujui dawa ya fisadi ni kufisadiwa vyake.)
  WABUNGE WENZANGUA HAWANA NA MAPENZI NA MIMI( Kwani huna mke???)
  RAIS WA JAMUHURI SIKU HIZI HANIPIGII SIMU KAMA ZAMANI( bora aongee na matonya ombaomba kuliko fisadi)
  NI HAYO TUU WADAU.
  bY
  Me.a.k.a You

 3. Kwize Says:

  Namuunga mkono huyo ndugu yangu, Hayati E M Sokoine ndiye wazili mkuu bora katika mawaziri walio pita

 4. senator Says:

  yap, alikuwa kiongozi bora kwa wakati wake ila buy now dunia imechenge mno. Nadhani hata nyerere tunayemtukuza alishaona inaenda pabaya akang’atuka nina wasi hata huyu mambo yangekuwepo huko hali ingekuwa ngumu.

  Nadhani Magufuli angapewa nafasi he would be the best

 5. Kekue Says:

  Niseme tu alikuwa ni mzuri kutokana na stori ninazozipata kumhusu yeye coz kipindi hicho mwanawane nilikuwa sehemu fulani tehe tehe!! Matty ulikuwa umeshazaliwa? Jamani ebu niambieni eti ni kweli alikuwa anapita nyumba kwa nyumba kuangalia una nini na unafanya kazi gani unalipwa sh. ngapi, then analinganisha na vile vitu ulivyonavyo na pesa unayopata?? Nikasikia eti watu walikuwa wanatupa vitu, wanaficha pesa manake ilikuwa soo… ebu niambieni mliokuwepo kipindi hicho je, ni kweli hayo niliyoyasikia kuhusu huyu baba??

  I wish kama alikuwa kweli anafanya hivyo angekuwepo kipindi hiki cha MAFISADI au mafisadi wasingekuwepo??

 6. Dogo Says:

  Probably Mr Mizengo Kayanza Peter Pinda. Na ma-PM waliotia fora kwa kuboa au kuchemsha ni Bwana Mmasai au EL na mwenzake aliyesoma Masters kwa mwezi mmoja FS ambaye inasememekana ni shemeji yake our x president BWM

 7. Kamanzi Says:

  BC acha kutukumbusha Moringe au unataka tulie? Eti unasema best PM ever? Au ulimaanisha kiongozi bora ever? Hayati Mwalimu mwenyewe aliwahi kuulizwa kama Sokoine angekuwa hai angemchagua Mwinyi kama raisi. Alijibu kwa kusema Sokoine!! Kisha akaonyesha alama ya dole yaani alimkubali. Haiwezekani mbinguni wala duniani kumfananisha na akina Warioba, Malecela, Sumaye (natamani kulia ninapomtamka), Lowassa (Ustake nife mimi) au huyu Pinda (maneno yamezidi vitendo).

  Hii serikali bomu tuliyonayo ingempata Sokoine mmoja tu tusingekuwa hapa tulipo. MAgufuli alijitahidi kufuata nyayo, serikali ya JK ikisaidia na magazeti ya Habari corporation ya yule muiran wakamchafua mpaka leo ni kama hayupo. Ila Shafi aliwahi kuandika kwenye kitabu cha kuli, YANA MWISHO HAYA. Mungu ibariki Tanzania

 8. kijiwe Says:

  Kwa maoni yangu he was the best na mpaka hivi sasa apart from Nyerere huyu jamaa hata angekuwa Rais ingekuwa mwake pia.
  I think BC ungeongenzea kaswali kengine kuwa “je alikuwa na sifa za kuwa rais wa tanzania?”

 9. Bablii Says:

  Ha ha ha BC a very simple answer! Wallah mimi katika maisha yangu yote nliyowahi kuishi hapa duniani (67), hakuna waziri mkuu bora, safi na wakupaswa kuigwa kama EDWARD LOWASA aka “edo” aka “kanya west” aka “richmonduli” Huyu kwangu ni kiboko ya wote! Huyu ndo ameweza kuthibitisha maneno ya Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi kwa vitendo kwa “Watanzania ni vichwa vya wandawazimu”

  Bravo Lowasa, natamani urudi tena uje umalize zilizobaki, maana sijui pesa za kuwapeleka JWTZ commoro zilitoka wapi.

 10. LWABULINDA JOSEPH Says:

  NI KWELI EDWARD MORINGE SOKOINE KATIKA HISTORIA YA NCHII NI WAZIRI MKUU BORA KATI YA WOTE. SIFA YAKE KUBWA NI ALIKUWA MKWELI, MCHAPAKAZI NA MUADILIFU SIFA AMBAZO ZIMEWAPIGA CHENGA WENGINE AMBAO NI “MABWANA NDIYO”

 11. Chris Says:

  Kazi + Maamuzi aliyofanya ndo yanafanya asifiwe na kuwa lulu ambayo haitasahaulika ktk kumbukumbu za watanzania. Binafsi nimemsoma kwenye vitabu na mashuleni lakini naona alikuwa ni muadilifu zaidi. Mafisadi wote wa sasa wanakula ni kwa sababu ya misingi mizuri aliyoiweka huyu jamaa na wengine.

  Ataendelea kuwa kuwa kiongozi bora milele ktk historia ya Tanzania.Si unaona EL alivyoanza u-PM alijaribu kuvaa viatu vya huyu jamaa (sijui alidhani kwasababu ni Mmasai mwenzie), ameshindwa vibaya sana. Wewe kama fisadi huwezi vaa viatu vya kijamaa hata siku moja.

 12. changa la macho Says:

  Tatizo la kimsingi ambalo lipo ni kwamba kwa mujibu wa Katiba iliyopo sasa ni vigumu kupima kwa uhakika nani aliweza kuwa Waziri Mkuu bora zaidi kuliko wengine.Zipo sababu kadhaa.Kubwa ya msingi ni kwamba mwenye mamlaka ya mwisho katika kuiongoza nchi na kupitisha maamuzi mazito ya mwisho katika masuala nyeti ya kitaifa atabakia kuwa Rais wa nchi kwa mujibu wa Katiba iliyopo.Maana yangu ni kwamba wakati mwingine Waziri Mkuu ataweza kuonekana bomu katika utekelezaji wa majukumu fulanifulani lakini ni vigumu kubaini iwapo ‘UBOMU’ huo umetokana na maagizo ‘duni na hafifu’ pengine ya Rais mwenyewe ambayo kiutaratibu Waziri Mkuu asingeweza kukataa kuyatekeleza.Na kadhalika na kadhalika.The Rest is History, if you know what I mean!

 13. Faizer Says:

  mh huyu baba Mungu amlaze pema peponi, sidhani kama kuna PM anayemfikia mpaka sasa!

 14. Faizer Says:

  Jamani wana blog mimi ni Mtanzania mwenzenu naomba kujiunga nanyi katika blog hii,naishi Dar es salaam TZ.Nimekuwa nikisoma mara nyingi mambo mengi mazuri toka hapa pamoja na coments zenu naomba mnikubali tafadhali.

 15. Longolongo Says:

  Orodha ya Mawaziri Wakuu kufuatana na Ubora wao:
  01) J. K. Nyerere
  02) R. M. Kawawa
  03) E. M. Sokoine
  04) S. A. Salim
  05) J. S. Warioba
  06) J. S. Malecela*
  07) C. D. Msuya
  08) F. T. Sumaye
  09) E. N. Lowasa*
  10 M. K. P. Pinda

  * wote wenye nyota bado tunafuatilia uadilifu wao, lakini walikuwa bora kwa kipindi chao maana hakuna aliyewapinga wakiwa madarakani zaidi ya kuwashutumu baada ya kuachia ngazi.

 16. kijiwe Says:

  nyarubamba na changa la macho mbona mnamhate marehemu sokoine?
  mtake msitake he was a good leader acheni unafiki

 17. Faizer Says:

  hi wana blog,mimi nimekuwa ni mfuatiliaji mzuri sana wa blog hii na ningependa kuwa mmoja wenu tafadhali naomba mnikubali.

 18. Chris Says:

  Faizer wakaribishwaaaaaaa?NI Faiza yupi weye? Mswahilina hebu mkaribisheeeeeee,ila usimkosoe… teheteheteheeeeeeee…….

 19. Matty Says:

  Halo halooo leo ni welcome party tunakukaribisha Faizer jisikie upo nyumbani japo hapa watu hawapigi hodi, Amina uko wapi,Kekuu, Any,Michelle kuna mgeni hapa mkaribisheni na ukiondoka uage karibu sana!

  Kekuu mimi simjui kabisa huyu jamaa maana nilikuwa sijazaliwa! lakini nasikia alikuwa mtu makini sana sio kina Lowasa!

 20. amina Says:

  mhh mimi namsikia huyu ila nilikua simjui…kipindi hicho nilikua mdogo sana,ila we ben umenichekesha sana..na wewe faizer karibu nitafte namba yangu ni hii 911 crime stopers

 21. Gervas Says:

  Hakuna ambaye atalinganishwa na Sokoine. ilikuwa hamna kuchekeana katika maswala ya maendeleo. yeye na mwalimu walionyesha mfano wa kutojilimbikizia mali, maana alikuwa na suti mbili tu. Hata wakati mauti yanamkuta ilikwa apande ndege kurudi dar toka Dodoma ila kupunguza garama alisema atatumia gari. Mwalimu alimuandaa kuingia ikulu lakini haikuwa hivo, naamini tungekuwa mbali. Sera ya uhujumu uchumi ambapo mabepari waliojilimbikizia mali zilitaifishwa ndo ilimpelekea mafisadi wa enzi hizo wamdedishe. Anyway tunaweza pata mwingine.

 22. Mswahilina Says:

  Edward Moringe Sokoine,
  Alikuwa Waziri Mkuu makini kuliko hata Mchonga meno. Alikuwa ananena anayotenda na alikuwa anatenda anayonena. Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi Amen.

  Faizer, karibu sana kwenye Blog hii ya BC. Kila mdau anakukaribisha kwa mikono miwili.
  Jitahidi sana kuandika kiswahili fasaha, usichanganye R na L kwenye maandishi yako, ukiona hili linakutatiza jaribu kutumia kamusi ya kiswahili sanifu.
  Karibu sana Faizer kwa maana sijawahi kuona mdau mwingine akiomba kukaribishwa kwenye hii blog ya BC.

 23. chami Says:

  Kwa kweli mtachangia lakini ukweli utabaki palepale Marehemu Sokoine hakuna wa kumfikia hata chembe,hata haya matunda ya uwekezaji ni yeye ndie aliyemshauri hayati Mwl Nyerere kuwa tufungue milango kwa wawekezaji wawekeze nchini mwetu,alisema uwekezaji ni sehemu moja wapo ya kukuza uchumi wetu ambao kwa wakati ule ulikuwa umeshayumba,aliongeza kuwa wataweza kukusanya kodi kutoka kwa wawekezaji hivyo kuongeza pato la taifa pamoja na kupata ajira kwa watanzania,alikuwa mwadilifu wa kweli na si maneno kama hawa mawaziri wakuu waliopita,na hakumuonea haya kiongozi mbadhirifu hata kama alikuwa ni waziri alimshughulikia bila wasiwasi wowote,na hata vita dhidi ya walanguzi wakati ule alisema ataanza na wakubwa kwanza,tofauti na hawa wenzetu wa sasa wanakemea rushwa lakini wanawakamata wadogo wakati wao ndo magwiji wa rushwa.hakujilimbikizia mali kama hawa wa sasa ambao tumeshuhudia wakiwanyang`anya hata wananchi ardhi,na nina imani kabisa hata huyu Magufuli angekuwa ni waziri enzi za Sokoine hakika uwaziri angefukuzwa kwa SERA yake ya ubinafsi wa kuuza nyumba za Serikali wakati tayari wamejingea mahekalu huko Mbezi beach na Tegeta,hivyo wanataka hizo nyumba baadae wazipangishe wakati walimu hata nyumba za kukaa hawana na wanafunzi wanakaa chini,Nampa pongezi JK kwa kusimamisha zoezi hilo la ubinafsi.

 24. Liemy Says:

  duh no comment,bwana wanaojua habari zake labda wazazi wetu.
  Sisi tunajua fisadi ni losawasa ukianzia na sumaye

  ila historia ya sokoine inatuambia alikuwa mtu mzuri by then

 25. Liemy Says:

  duh no comment,bwana wanaojua habari zake labda wazazi wetu.
  Sisi tunajua fisadi ni losawasa ukianzia na sumaye

  ila historia ya sokoine inatuambia alikuwa mtu mzuri by then

  R I P SOKOINE

 26. any Says:

  Sikumpenda kabisa, alisababisha watu wakatupa sukari mtoni eti wasikamatwe walanguzi, mtu unatoka Ng’ambo na colgate na emperial Leather *sabuni ya kuogea*, eti unaitwa mhujumu uchumi. Eeh, wamasai hawana majina zaidi ya Edward? Lowasa sikujua ni wajina wake Sokoine.

 27. Jicky MM Says:

  Nadhani so far Sokoine alikuwa the best executive leader in the country. Na inawezekana waliomwondoa walikuwa mafisadi wa wakati ule, lakini kwa kuwa wengi wetu tulikuwa gizani, watoto, au hatukuwa na uwezo wa kuchambua mambo, na pengine tulikuwa ‘naive’ ndio maana hatukujua; na hata kama mtu angejua asingeweza kusema lolote kwa sababu ya udikiteta wa wakati ule na kutokuwepo kwa uhuru wa kupashana na kujadili habari, Je mpo??

 28. Mzalendo Says:

  Japokuwa nilikuwa elimu ya msingi wakati huo, lakini nilishuhudia kwa sehemu uongozi wa sokoine mpaka alipotutoka mwaka 1984. Jamaa alivuma sana hata wakati wa msiba ilikuwa huzuni kila mahala huko bongo. Nafikiri alikuwa kiongozi mzuri katika mfumo ule wa chama kimoja chini ya sera za kijamaa.

  Naungana na mtoa mada mzuri hapo juu kuwa ni vizuri tungetoa maelezo kwa vigezo na nyakati katika kuwalinganisha hawa waheshimiwa na wale mafisadi. Nafikiri tutaelimishana vizuri iwapo tutatofautisha mfumo ule wa ujamaa chini ya chama kimoja, na huu tulionao leo ambao umefungua milango kwa wazawa kujinafasi.

  Japokuwa sikuwa mkomavu katika kuelewa mambo hasa ya kisiasa wakati ule wa mheshimiwa sokoine chini ya uongozi wa baba wa ccm, lakini yapo ninayoyakumbuka nisingependa yajirudie. Mfano upatikanaji wa bidhaa muhimu kama sukari, mkate, mchele n.k. ilikuwa ni hekaheka tunapangishwa foleni na wanaofanikiwa kununua ni wachache. Kwa kifupi sera za kupambana na wahujumu wa uchumi zilileta usumbufu mkubwa sana kwa wananchi. Tatizo katika mfumo ule wa chama kimoja hakukuwepo kukosoana na kuwekana sawa, kiasi kwamba kila jambo lilikuwa linakubalika tu hata kama lina madhara kwa wenye nchi.

  Leo hii tunashuhudia mabadiliko japokuwa serikali ya chama tawala inajiuma kutoa ufafanuzi ni mfumo gani unaendesha taifa letu changa. Nionavyo mimi demokrasia ya wakati huu ni tofauti na wakati ule sokoine anavuma na kuliendesha bunge chini ya chama kimoja. Nafikiri hata sokoine angetawala nyakati hizi, angekutana na changamoto nzito sana kama anazokutana nazo mwanafunzi wa nyerere mheshimiwa rais Kikwete.

  Tukumbuke kuwa, hata mwalimu nyerere alishaona tokea mbali kuwa kuna mabadiliko yanakuja yasiyoweza kuepukika. Ndio maana akaamua kung’atuka akijua mechi imekuwa ngumu.

 29. Kekue Says:

  Matty, Any,Amina, kijiwe, majita, mama wa kichaga, michelle na wengine hivi mlivyoanzaga kuchangi humu mliomba ukaribisho?? Haya unayeomba kukaribishwa karibu!!! Makubwa haya!!

 30. amina Says:

  matty mi nipo saa nyingine nachoka kuchangia nabaki kusoma comments tu…si unajua mi mbishi sasa naogopa kushushuliwa teh teh teh

 31. changalamacho Says:

  Unasikia rafiki yangu Kijiwe,katika Blog hii hapendwi mtu wala hachukiwi mtu hapa!Utaweza kuwapima hao Mawaziri Wakuu ikiwa tu umepewa vigezo vya kuwalinganisha na si vinginevyo.Msifunikwe macho watanzania wenzangu.Hebu nieleze tofauti zilizopo baina ya kazi wazifanyazo viongozi wafuatao:Waziri Mkuu,Makamu wa Rais,Rais mwenyewe,Waziri Kiongozi wa ZNZ, na Rais wa ZNZ! Is it really worth it in terms of costings?Ni Waziri Mkuu bora yupi katika mfumo upi wa Kidemokrasia?Waziri Mkuu yupi aliyekuwa ni Mkuu wa Serikali(Head of Government) mamlaka kikatiba ya kuteua Baraza lake la Mawaziri?Au yeye mwenyewe alisubiri ateuliwe kama wanavyo teuliwa mawaziri wengine?Atakua na tofauti gani na mawaziri wengine katika utaratibu huo wa mfumo wa utawala?Mtabakia kudanganywa tu kila siku hapa. Cha Mlevi Huliwa na Mgema! KALAGA BAHO NA UBOZI WAKO.hakuna waziri mkuu aliyepata kuwa bora zaidi ya wenzake kila mmoja alikuwa akitekeleza majukumu aliopewa na Bosi wake FULL STOP!Kama yupo ambaye hakuguswa na kashfa ni kwasababu huzijui tu ndugu yangu.Kunywa uji wako wa Ulezi ukalale! Alamsiki.

 32. kwa kweli ndugu Eduard morringe sokoine ndiye waziri mkuu bora kabisa ambaye mpaka sasa aijapata kutokea mtu kama yeye. najua kwenu vijana wa sasa sio rahisi kumjua kwa kuwa alikuwepo kabla yenu. mimi nina wasihi vijana wote kujalibu kupata habari juu ya mtu huyu. sokoine alikuwa jasili sana na mkomavu kiakili. alitoa maamuzi magumu sana ili kuiokoa nchi, alikuwa mtu wa watu na alikuwa mtetezi wa kila mtu bila kujali matabaka. wahujumu uchumi wakati huo aliwabana sana na hakuna aliyethubutu kuiibia nchi yetu na aliyefaulu kuiba alipokonywa mali na kushitakiwa. alitokea na wala atatokea tena waziri mkuu kama sokoine.
  mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu eduard moringe sokoine, Amina

 33. Faizer Says:

  ahsanteni sana Chris,Matty,Amina na wote kwa kunikaribisha.

 34. Edwin Ndaki Says:

  RIP kaka wajina.

  Hakika sisi tumashahidi na historia lazima itakulinda na kukutetea kwa jinsi ulivyo simama nasi.

  FAIZER karibu sana,ingawa itabidi tukupatie contact za Matty maana ndio muhasibu wetu ili umpatie kiingilio.Number yake ni0756 400 400.

  Mwisho..watu wangu woote wa Bc niliwakumbuka,nilikuwa namalizia Pasaka.Si unajua wengine huku Songea,tukianza kunywa ugimbi hatumalizi kama ule wimbo wetu..tuyamalembe kunyumba mpaka tumale ugimbiii eeee hee eee ..haiwezekaniiii…Teehee..teee eee

  siku njema..Nimerudi..Gervas upo wapi..au na wewe umepiga arua ukwayani?

 35. Gervas Says:

  Hamna wakumfikia wala kumfananisha na Moringe. Yeye na mwalimu mbali na kutotaka masihara kazini walionyesha maisha ya kutojilimbikizia mali. sokoine alikuwa na suti mbili tu. na alilenga kwa maslahi ya wananchi. with whom can u compare?

 36. Dinah Says:

  Nafikiri Salim, Malecela na Msuya ndio walikuwa bora….waliopita sikuwepo waliofuata hamna kitu…..kuna matumaini Pinda atakuwa bora zaidi ya wote….tusubiri.

 37. Longolongo Says:

  Sokoine alipofarikia aliacha Wake 2 mke mkubwa akiwa na watoto 9 na mke mgodo akiwa na watoto 5.
  Ni kweli hakujilimbikizia mali bali alijilimbikizia watoto.

 38. Matty Says:

  Faizer Karibu sana!Amina hii welcome Pary itakuwa kwa Dan pale k/nyma darajani sasa nitakuja nimevaa kimin na kitop ili hata faizer aweze kunitambua.
  Kekuu usiwe unauliza maswali hayo hapa wageni watakuwa hawapigi hodi tena, ohoooo!
  Wewe ndaki haiwezekaniiiiiiiiiiiiiiii x3 bora umemwambia faizer alete kiingilio kabisa ili tukajipongeze kwa Dan darajani k/nyma siku ya kupary (welcome pary) ni lini tena???
  Gervas uko wapi?? bado unagema ulanzi tu??

  Mswahilina kipende kiswahili tumia lugha fasaha (what is mchonga meno?)

 39. Malenga Says:

  Faizer, unakaribishwa kwa moyo mkunjufu…Jisikie upo kwenu.
  Lugha fasaha hupendezesha, lakini lugha sanifu hung’arisha zaidi kijiwe chetu hapa BC. Hata hivyo isiwe tija ya kukuogopesha..wewe andika uwezavyo yatakayopinda Kifimbo cheza wa humu ndani atakuweka sawa.
  Karibu sana

 40. Juma Rioba Says:

  Wanasheria wanaelewa vizuri sana jinsi sheria iliyopitishwa leo isivyoweza kutumika kufanya maamuzi ya mambo ya miaka iliyopita.
  Hatahivyo si nia yangu kuongelea sheria.Nachotaka kusema ni kwamba, bila msingi wa watu kama Newton, Galileo Galilei,Socrates, n.k. mawazo endelevu yaliyozaa matunda tunayoyaona katika social science na natural science yasingekuwapo.Huwezi kupata wazo jipya nje ya wazo lililokwishakuwepo tayari.Huwezipata kitu kipya nje ya kilichokuwepo tayari.Hivyo basi,Japo mawazo ya wanafalsafa nlowataja hapo juu hayatumiki kwa sasa kama yalivyokuwa(ukilinganisha na yalivyo sasa), bila hayo sayansi ya jamii na hii ya “asili” isingekuwa hapa ilipo.
  Aliyoyafanya Nyerere na Sokoine kwa wakati ule yalikuwa ya msingi mno kwa wakati ule na pia yaliweka msingi wa yanayotokea sasa. Hata Marekani ukiwauliza miaka 10 tu iliyopita walikuwa wapi watakwambia ni tofauti sana na sasa lakini hawawezi kufungua vinywa vyao kusema”yale hayana maana-ni ya miaka 10 iliyopita”. La!Hii ni kwa sababu ya miaka 10 ama 100 iliyopita ndiyo msingi wa ya sasa.Kumbuka ndege(ya kusafiria) ilivyoanza kutengenezwa-utacheka sana-Hivyo basi tusi-judge mambo kwa kuangalia muda huu tulionao. Kila jambo la sasa lina mwingiliano mkubwa mno na jambo lililopita. TV unayoiona sasa, ninakuomba ukasome historia ujue chanzo chake ni nini. Ilianza kama mchezo wa kitoto lakini sasa inaonekana kitu cha ajabu.Miaka 50 ijayo TV hii hii unayoiona ya ajabu itaonekana kitu cha kawaida mno na pengine kisicho maana kwani wakati huo tekinolojia itakuwa juu mno!Je, utasemaje kwa hilo?
  Nyerere na Sokoine si malaika walifanya mabovu lakini kimsingi walifanya mambo kuendana na wakati wao.Tanzania ya sasa si Tanzania tutakayokuwa nayo miaka 50 ijayo.

 41. changalamacho Says:

  Juma Ryoba SO WHAT!

 42. Bigy Says:

  Siku zote tunapenda kusikia mambo yasotufanya kufikiri. Likiwa la kufikirisha tunasema “so what”. Anyway tuendelee kuongelea stori kama-“kafumaniwa”, “arogwa” n.k.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s