BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JK AZINDUA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA March, 26, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,News,Serikali/Uongozi,Television,Watangazaji — bongocelebrity @ 10:29 AM

 

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete,akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo mchana jijini Dar-es-salaam.TBC imezinduliwa upya rasmi leo pamoja na nembo/logo mpya ya shirika hilo.Kuanzia sasa, iliyokuwa Televisheni ya Taifa (TVT) itaitwa TBC-One na iliyokuwa Radio (PRT) itaitwa TBC-FM na pia kutakuwepo na External Service itakayoitwa TBC International.

Wengine pichani (kulia kwa JK) ni First Lady,Mama Salma Kikwete na Tido Mhando ambaye ndio Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.Kabla ya kurudi Tanzania kushika wadhifa huo mpya,Tido Mhando alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC)

 

Nembo mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).Nembo ina kauli mbiu ya Ukweli na Uhakika. Ni matumaini yetu kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa na si vinginevyo.Picha zote na Ahmad Michuzi.
Advertisements
 

19 Responses to “JK AZINDUA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA”

 1. Dinah Says:

  Bomba-bomba, ukweli na uhakika bila kulindana….kila la kheri.

  By the path, Kighana Mama Salma na Huyo m-baba(Mhando) wanaowakilisha ujumbe kuwa ni mume na mke au pea/couple kwa vile wamevaa sare. Tufanje research za mavazi kabla hatujavaa na kuruhusu picha kwenda kimataifa kwani inaweza kusababisha misunderstanding. 🙂

 2. Kimori Says:

  Kuna kitu mimi nashindwa kuelewa watanzania wenzangu labda mnieleweshe. Hivi kweli rais wa nchi hana shughuli zingine nyeti za kufanya mpaka awe tu mara kwa mara anazindua TBC, Mlimani City, nk, kazi ambayo hata waziri angeweza kuifanya? Si mara ya kwanza kusikia kuwa rais anazindua “upuuzi” mwingi tu nchini au imekuwa ni fashion kumualika rais hata mpaka kwenye birthday?

 3. Mconel Says:

  Mimi ninachoshangaa, logo ina TBC ni abbreviation ya kiingereza then kauli mbiu ni kiwsahili, kwani nini wasieke kiingereza pia? kwa sababu nadhani TVT ilikuwa ya kiswahili na wamefanya mabadiliko nusu,Mmechemsha.

 4. Chris Says:

  BC mbona hamko hewani? Mmetekwa nyara? Au mmeamua kujiunga na hiyo TBC? Nasikia inavipindi vizuri sana hiyo TBC?

 5. Matty Says:

  Haya jamani tujulisheni na wengine hivyo vitenge vinapatikana wapi na sie tukanunue tushone na tuweke shuka begani wamama oyeeeee!!!!Any uko wapi leo!

 6. Najiuliza tu!Kwanini hili shirika kila naposoma linasisitiziwa kwa kiingereza yaani; TBC kuliko SUT aka Shirika La Utangazaji Tanzania? Nazinguka kidogo nionapo TBC halafu msemo chini yake uko kwa kiswahili;Ukweli na Uhakika.

 7. Gervas Says:

  BC vipi? mbona kimya? au ndo na wewe walishaku-Jambo Forum? maana jana JK nimesikia anakoromea the abuse of the freedom of speech, amewambia owners mtajuta, Kipanya sijui amemwelewa? waachieni wamarekani bwana wenye pure democracy, nchi zetu bado ubabe mwingi, ukifungua mdomo tu rungu….ngoja nijinywee the ulanzi wangu hapa.

 8. binto Says:

  na viongozi wanaotumia madaraka vibaya waondolewe haraka sana, haswa wale walio nje ya nchi, ambao hata kazi za maana hawafanyi.

 9. kijiwe Says:

  TBC si wameiga BBC?
  upuuzi mtupu!
  i told you guys huyu jamaa msanii kinoma 2010 anachaguliwa tena LOL au copy yake ili imlinde

 10. amina Says:

  bc mi nataka hicho kitenge nitapata wapi?urafiki kipo au pale mnazi mmoja nitapata

 11. mtanzania Says:

  hiyo nembo jamani kubwa sana!! inaziba karibu nusu ta screen!! fanyieni editing tafadhari

 12. Mimi Says:

  Jamaa Tido kwa sababu alikuwa BBC sasa analeta kasumba za TBC wakati lugha yetu ya taifa ni kiswahili. Kwani wakiliita SUT (SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA) kuna ubaya gani?. Nchi zote zilizo makini zinaweka mambo yao kwenye lugha zao, sasa hawa wanaleta ushamba wa kikoloni wakati asilimia kubwa ya wananchi ni waswahili na wanaongea kiswahili. JK naye kila analoambiwa yeye anafuata mkumbo kama bendera bila hata kufikiria maslahi ya wabongo wa kawaida walio wengi ambao ndio wenye mali. Nchi yetu bwana hah!, ovyo kweli.

 13. binto Says:

  mama kikwete unavaa vipya kila siku.

 14. Mswahilina Says:

  Dinah: umenichekesha kwa kufananisha waliovaa nguo zinazofanana.
  Kimori: TBC, Mlimani City, nk, sio “upuuzi”.
  Mconel: Tanzania tunatumia Kiswahili na Kimombo.
  Gervas: Hongera kwa kuandika kiswahili fasaha.
  Kijiwe: sio upuuzi, pia JK sio Msanii, na ujue kuwa Mungu akimpa uzima ni ‘LAZIMA’ achaguliwe 2010.
  Mtanzania: andika ‘tafadhali’ sio ‘tafadhari’ inavyoeleweka kwa mtanzania halisi anaandika kiswahili (kitanzania) halisi.

  TUKIPENDE KISWAHILI NI LUGHA YA AFRIKA.

 15. kijiwe Says:

  Mswahilina: awe au asiwe msanii hiyo ni opinion yangu kama wewe unaona siyo msanii poa tu hiyo ni opinion yako na naiheshimu so tafadhali heshimu ya kwangu pia.

  naku quote “na ujue kuwa Mungu akimpa uzima ni ‘LAZIMA’ achaguliwe 2010”

  mbona unajichanganya mwenyewe? kwani mi nimesemaje si nimesema ATACHAGULIWA TENA au?
  soma tena tafadhali.

 16. kijiwe Says:

  Halafu wewe Mswahilina mbona unapandisha jazba kwa spidi?
  Kimori kaongea point ya maana na ninakubaliana na yeye kuwa hizo kazi za kufingua TBC,Mlimani City n.k hata mawaziri wanaweza kuzifanya.Amezidi kuwa kila kitu kwa hiyo wazalendo hatuna budi kutoa maoni yetu kuhusu usanii kama huu.

 17. siza Says:

  nikwambieni tbc hawajaiga bbc..nilikua naperuzi kitabu kimoja kilitungwa na mwl nyerere jana nikakuta picha ya zamani miaka ya 60 mwl anaongea na vyombo vya habari moja wapo ya mic imeandikwa tbc..sasa mi ninachhooona wamejaribu kufufufa tena tu hili jina,msiangalie mbele angalieni na nyuma mnauhakika kama wameiga bbc?

 18. changalamacho Says:

  Nembo au kifupisho cha TBC kinapendeza kukitamka na hakileti ukakasi ulimini.TBC is OK.Chini yake maneno yanasomeka, UKWELI NA UHAKIKA, sawa sina tatizo nalo,yanafaa na maana nzito.Sina uhakika kama kweli CCM au SERIKALI ikiboronga watakuwa na ubavu wa kuikosoa waziwazi bila ya upendeleo wowote.Tusubiri tuone.Wadau wa TBC tutalifuatilia hilo kwa karibu zaidi.Pendekezo langu hapa ni kwamba juu ya kifupisho TBC ni vyema yangekuwepo maneno yasomekayo,SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TANZANIA, badala ya English Version yake ya Tanzania Broadcasting Corporation, kwa faida ya wote , wanao zungumza Kiswahili na wale wanao zungumza English. TBC ni ya kimataifa .Kwa hiyo mseto huo utakubali vilivyo. Hali kadhalika jitahidini TBC kuboresha ile ‘BACKGROUND SHOWROOM YA USOMAJI WA HABARI’ kama zinavyo onekana za wenzenu.Ukutani kuwepo na DIGITAL SCREEN KUBWA kwa ajili ya matukio,mahojiano,na pazia.Otherwise Tiddo pongezi mabadiliko katika Quality ya Vipindi hususan asubuhi katika JAMBO AFRIKA tumeanza kuyaona.Kila baada ya Nusu Saa pawepo na HABARI KWA UFUPI hata kama ni dakika moja tu.Asubuhi tathmini ya magazeti ifanywe na watu waliobobea katika Fani mbalimbali kama SKYNEWS wanavyofanya au TV Channels nyinginezo.Tangazeni zaidi Mazingira na Vivutio vya Utalii Nchini.Vitawaongezea matangazo zaidi ya Biashara.Kazi njema.

 19. Sebastian Peter Says:

  Ninapenda Kumpongeza sana Mheshimiwa Tido Mhando kwa juhudi zake za kulifanya Taifa letu liwe juu Ki-HABARI. Nchi inaonekana kuwa inakwenda wala si kwamba imesimama sehemu moja kama zamani!!!!

  Hongera Tido, Hongera Serikali Tukufu, Hongereni wafanyakazi woote wa TBC, maana kutoka TBC hapo kale kuja RTD na sasa inarudia tena TBC, Tanganyika Broadcasting Corporation, na sasa Tanzania Broadcasting Corporation) kweli huyu Mheshimiwa Mhando anaijua Historia ya Nchi yetu.

  Ninaomba nijue kama wanaweza kupokea nyimbo kwa njia ya Mtandao, pia sijaona website ya TBC ikiwezekana nijulishwe niweze kuiona.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s