BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PROF.ANNA TIBAIJUKA NA MWENGE WA OLIMPIKI March, 27, 2008

Filed under: African Pride,News,Wanawake na Watoto,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 1:12 PM

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN Habitat), Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka(pichani), ni miongoni mwa watu sita mashuhuri barani Afrika walioteuliwa kukimbiza Mwenge wa Olimpiki utakaokimbizwa jijini Dar es Salaam, Aprili 13, mwaka huu.Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa.

Advertisements
 

26 Responses to “PROF.ANNA TIBAIJUKA NA MWENGE WA OLIMPIKI”

 1. usinijue Says:

  si niliona sikumbuki blog gani imedai ladyjd na wenzie ndio watakao kimbizana na huo mwenge,zile zilikua redio mbao ama?tusichanganyiane habari

 2. any Says:

  Big up mama Tibaijuka,. Unafanya kazi kubwa sana, tangu economics department, sasa uko UN!.

 3. Dinah Says:

  Kwanini iwe huyu mama na asiwe mwanamichezo kama vile Bai, Matumla na wengine waliowahi kushirikia michezo hiyo ya Olimpiki au hata ile ya jumuia ya madola? Kwani ni nani hasa anahusika na uchaguzi huo?
  na kwani nini watupangie tarehe 13 ambayo wengi wanaamini ni ya bahati mbaya?

  Nime-mind!

 4. Edwin Ndaki Says:

  Kielelezo cha kuwa mama zetu,dada zetu,wake zetu,wapenzi wetu,ma x gal wetu tukiwaheshimu,kuwawezesha au kuwapa nafasi,hakika Wanaweza.

  Wakina dada changamoto hiyo mnaweza.Siku zote naamini adui mkubwa na wakwanza wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.

  PILI.
  Olimpiki ya safari hii siipi shavu kabisa hasa kitendo cha hao ndugu zake na “Blus Lee” wachina cha kukomalia kuwa Tibet waendelee kuwa “vitegemezi” vyao.

  Wasu majita..upo mwanakwetu…maana nosindikana no siga!

 5. Mswahilina Says:

  Wa-Tanzania tuna hazina nzuri ya wasomi.
  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ubariki Ulimwengu.

 6. binto Says:

  tukipunguza chuki na wivu, tutafika mbali washamba utawajua tu, kufwatilia maendeleo ya wenzao, punguzeni majungu watanznaia.

 7. xxxxx Says:

  hiyo kuhusu lady jay dee ni redio mbao tu..ilikuja ikakanushwa badae

 8. Kekue Says:

  Hongera sana mama kwa kazi unazofanya!!! kiti ingine nimependa the way ulivyo appear simple hapo juu, lakini ni kawaida ya maprof!!

 9. Matty Says:

  Hongera Aunt yangu kwa kuwakilisha safi sana mwanamama wa kihaya wakola waitu! ubakeise bona!

 10. Nemy Says:

  Nakubaliana asilimia mia moja na Mr Ndaki,wanawake tuanze wenyewe kujengeana uwezo ndo tuwaalike wengine. Tunaweza. kwa kweli Nosindikana no siga, but unasonga mbele hakuna kustop.

 11. Gervas Says:

  Mswahirina, hawa wasomi wanaoshine leo waliandaliwa na mfumo mzuri wa elimu uliokuwepo jana, Je tutaweza kuwapata watu kama hawa Kesho? kwa mfumo huu wa ufisadi? HALAFU hata mimi sioni lojiki ya mama wawatu kukimbiza mwenge, kwa nini wasimpe hata kingwendu atimke mkuku na huo mwenge? tena atajaza watu kuliko huyu mama!

 12. any Says:

  why can u say something positive about women? japo kwa siku moja? wamekufanyia nini wanawake? I just want to know

 13. Mswahilina Says:

  Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka ninakufagilia Mama, kumbe nasi Wa-Tanzania tumo. Kuna na mwenzako akina Dr. Asha-Rose Migiro wote ninawapongeza sana.

  Dinah: ninakunukuu “kwa nini watupangie tarehe 13 ambayo wengi wanaamini ni ya bahati mbaya” hao wengi mnaoamini hivyo ni wewe na nani?

  Edwin Ndaki: andika ‘Brus Lee’ sio ‘Blus Lee’ pia acha ukabila (‘nosindikana no siga’ maana yake ni nini?)

  Matty acha ukabila ninakunukuu “Hongera Aunt yangu kwa kuwakilisha safi sana mwanamama wa kihaya wakola waitu! ubakeise bona!”

  Gervas: ninaitwa ‘Mswahilina’ sio ‘Mswahirina’

  Wadau wenzangu TUPENDE KISWAHILI FASAHA.

 14. binto Says:

  kweli huyu tibaijuka amekaa simple, hamna kubwaga bwaga . ndio inavyotakiwa mtu simple.

 15. Chris Says:

  Kumbe Matty ni wakora waitu…..

 16. kyekue Says:

  Matty kumbe we muhaya na Mrs Tibaijuka ni aunt yako? hongera sana, ni mchapakazi sana huyu mama. mie ni mchaga n ili kuweka sawa utanzania na Mrs Tibaijku ni aunt yangu si unajua tena watanzania wote ni ndugu?Kiukweli she is a role model, we are proud of you mama Anna.

 17. matty Says:

  Haaaaaaaaaa ha samahani mwalimu Mswahirina nimemaanisha Asante sana wasalimie wote.

  Chris lazima nijivunie ukabila wangu! karibu kwetu BK!

 18. matty Says:

  Halafu Chris BK tunakula senene kwa wingi karibu uonje!sijui mtani wangu Gervas anaweza kula na asirudisha chenchi?
  Lakini Gervas ukizipata kwa ulanzi ndo zenyewe te te te!!!!!!!

 19. Gervas Says:

  Mswahirina, rekebisha hapo kiswahili chako, siyo… ‘ukabila’ ni ‘ukabira’. mbona unamatatizo ya kuchanganya r na l ? mwalimu wako wa kiswahili alikuwa nani? au kamusi yako ilichapishwa Kakamega? Matty, inifuacti hao insecti wanakata stimu ya ulanz

 20. Chris Says:

  Kumbe Matty u-mtani wangu…..

 21. Mswahilina Says:

  Gervas umeshindikana, nineamua nikukabidhi Mwalimu Dunia maana Wahenga walisema: “asiyefunzwa na Mamaye hufunzwa na Ulimwengu”.

 22. matty Says:

  Ndio Chris Mtani wangu wa jadi sema unaniambiaje??mambo ya senene,ndizi nk.wewe unayaweza?

  Kyekuu mimi kila mtu ni ndugu yangu hata wewe waweza kuwa mdogo/dadangu wala usijali kwa hilo.

  Gervas kipende kiswahili umemaanisha nini uliposema infact?

 23. Chris Says:

  Sio ndizi matoke…. mimi baba yenu unajua ni mambo ya nguna…. tena udaga+ulezi au mtama…. balaaa hapo….

 24. matty Says:

  Hahaha Chris mimi nguna siliwezi nimezoea matoke tu!

 25. any Says:

  I like her hair style na mavazi yake, hakuna mashuka begani. lol

 26. kano Says:

  nywele fupi lakini ametulia zake, basi baadhi ya wasichana ughaibuni wanapenda sana kuchambua watoto wa watu, wasichana punguzeni majungu ndio maana hamuendelei, kuweni wastaarabu jamani, wenzetu w anchi zingine hawako ivyo, acheni kupiga wenzenu majungu, na muwape support.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s