BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MESENJA KALETA BALAA! March, 28, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni Ijumaa tena.Baada ya mapumziko ya sikukuu ni wakati mwingine tena wa kutafakari na kupanga mikakati.Maisha ndivyo yalivyo,hakuna kusimama wala kungoja.Kila siku ni mchakamchaka.Raha na karaha ndio mtindo.

 

Zipo nyimbo ambazo zikipigwa,kwa njia moja au nyingine,ni lazima zikukumbushe jambo au mambo fulani.Kama hukumbuki enzi zile za mchana mwema chini ya utawala wa RTD peke yake basi unaweza kukumbuka kuyaruka majoka huku noti nyekundu zikiwa na thamani.Ili mradi tu,kwamba hivi leo kila kukicha kheri ya jana!Yaani kwamba dunia ile ilikuwa nzuri kuliko tuliyonayo hivi sasa.Najua kwamba hoja hii inaweza kuwa pana.Lakini leo sio wakati wake.Ijumaa ni wakati wa kubwaga manyanga chini na kupumzisha akili.Majirani zetu(kule ulipo Mlima mrefu!!!) wao siku hizi wanasema ni wakati wa “kubanjuka”.

 

Leo tunao Bima Lee Orchestra.Wimbo ni Mesenja.Naam,mesenja yule yule aliyeleta balaa.Za nyumbani akapeleka ofisini na za ofisini akapeleka nyumbani.Nyumba unaweza kuiona ndogo ukifanya masihara.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.

Advertisements
 

19 Responses to “MESENJA KALETA BALAA!”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Ijumaa ipo paleee palee.

  Yaani uspime m2 wangu.Hapo nakumbuka nipo Arusha,nasukuma gurudumu la maendeleo ambalo leo hii hatujui kama limefika au limepotea labda watu wamelichukua wakatengenezea majiko.

  Nakumbuka kipindi hicho RTD kulikuwa na vichwa kama marehemu Bahati komba ,hapo akija na lile”track” taili jenerooo..kutoka arushaaaa…”

  asikwambie m2 sisi wazee wa kuchuja nafaka,kulikuwepo na bia za “Guiness” fupi tulikuwa tunaziita shotii au kawawa..tee tee.

  Baada ya kusikiliza kisa cha messenja huko muda si muda utasikia dude la vijana jazz kama sio Maria la Manetu basi utawasikia maasimu wao Washirika stars watu njata njata..

  jamani tumetoka mbali.Enzi hizo mtoto ukimuona mtu mzima lazima umpokee mkoba.Ila leo hii du..vibaka wengi nani akubali kupokelewa.

  Huku kwetu Gezaulole ndio tulikuwa mara nyingi tunashinda hapa kwenye duka la ujamaa tukipanga foreni kusubiri sukari au sabuni.Msiniulize nina umri gani maana enzi zetu hata “birth certificate ilikuwa bado”..tee teee

  Ijumaa njema

  Tutafika tu.

 2. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  BC. Big up.
  Bima Lee Orchestra, Mesenja kaleta balaa.
  Umenifikisha, umegusa pale patamu.
  Endeleeni vivyo hivyo B.C.

 3. Gervas Says:

  Ha-ha-ha ha! BC umenikumbusha mbali kinoma, darasa la sabaaaa nasubiri lunch nikisikiriza “mchana mwema”

 4. Mswahilina Says:

  BC. umenikumbusha mbali.

  Edwin Ndaki, alikuwa akiitwa Bart (Bartalomew) sio Bahati, andika ‘tairi’ sio ‘taili’, andika ‘foleni’ sio ‘foreni’.

  Gervas andika ‘nikisikiliza’ sio ‘nikisikiriza’.

 5. usinijue Says:

  weacha tu,yani zamani niujumbe kwenda mbele katika music,yani tulikua na karedio kamoja tu ka RTD lakini starehe yake kubwa,unakumbuka ford wa oss,mwisho wa mwezi wa vijana jazz,ebwanaeee unakumbuka mambo kwa soks wa dr remy ah bc we endelea kutukumbusha kila friday najiona kama nipo mw`nyamala komakoma

 6. Malenga Says:

  Hongera BC umeweka tena moja ya zile sauti ambazo mimi naziita za dhahabu.Mzee Max Bushoke kweli hazina haiozi na hakuna ziada mbovu

 7. slim Says:

  Hapooo!1 Umenikumbusha sauti ya Max bushoke. Shukran BC

 8. Saidi Situ Says:

  Jimbo gani hili mtu anaongea hadithi. Huu wimbo ulikuwa mzuri enzi zile wakati fasion ya kuzungumza juu ya beats ilikuwa juu. Ingekuwa huyo muheshimiwa ndo ametoa hicho kibao leo hii ingekuwaje? embu fikirieni. Angemshinda afande sele na kitu karata dume kwa mauzo? Sidhani hata kama angekuwa kwenye top 10.

  Shukran kwa kutukumbusha wengi uozo ambao tulikuwa tunalazimishwa kusikiliza enzi hizo.

 9. Gervas Says:

  Mswahirina, naomaba tena urekebishe hapo kiswahiri chako. umenikumbusha mbari…..na sio umenikumbusha mbali, nawasi wasi na kamusi yako unayotumia, nafikiri itakuwa imeandikwa ‘dikishonare’ na sio kamusi. kidumu chama cha mapinduzi!

 10. Mswahilina Says:

  Gervas, du!

  Saidi Situ, Ingekuwa ni wewe uliimba mwenzako akasema ni UOZO ungejisikiaje? ‘lakini ninayaheshimu maoni yako’.

 11. Msanii Says:

  Saidi Situ acha kuponda babaa. Tena wala usianzishe malumbano ya muziki wa “kizazi kipya” kwa sababu watu tushashusha insha humu ndani mpaka machweo. BC endelezeni libeneke. Kama wengine walivyosema hapo juu, kwa kweli mmenikumbusha mbali sana enzi za RTD. Bingwa umepigwa jua la saa sita unasikilizia mzee Omar Jongo ashushe taarifa ya habari saa saba. Ila mambo yote saa mbili kasorobo kipindi cha michezo. Hapo mwanangu matokeo ya mechi ya Lipuli na Tukuyu Stars yanashushwa na mchizi nani sijui yule kutoka Radio Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini. Wakati kanda ya kati ndani ya Jamhuri stadium CDA Dodoma wanakiputa na Pamba ya Mwanza wana “tout poissant lindanda” (or something like that…lol) watoto wa Kawekamo!! Enzi hizo Ushirika Moshi na Pamba ndizo zilikuwa Brazil za bongo kwa kutandaza kandanda safi. Wakati huo Said Sued “Scud” na mzee wa kazi Makumbi Juma washaipiga Simba kama bao tatu hivi.

 12. Bonge Says:

  Gervas, hata kunakili unashindwa, mwenzio kaandika jina lake Mswahilina na siyo Mswahirina!! Ndo maana hata maoni yako hayajatulia!!

 13. Gervas Says:

  Bonge, kudandia treni kwa mbele ni hatari……haya shauri lako na ubonge wako, basi yatulize basi maoni yangu naona unakuja mzima mzima!!!

 14. Amina Says:

  mi simo naona wengine humu wanaleta habari za kufananisha na bongo flava

 15. DUNDA GALDEN Says:

  Kaka hapa Darwin wote uuliza kwani kesho si ijumaa kutakuwa na kibao gani kipindi cha mapunziko tunamsubili mwana BC Dunda Galden na kuanza majadiliano ijumaa iliopita ilikuwa babu kubwa lakini hii ya leo home is home wote midomo chini tukumbuka mbali sana pale mtaani Nyamwezi na Ndovu kipindi kile cha likizo za shule za msingi za msingi.huuu ndio music yalio baki tusogeze siku kutokana na wakat kuwa ukuta
  CHAFOSA CHAI GODA NEVER DIE

 16. Pamoja na kuheshimu maoni ya kila mdau, lakini maoni yako, bwana Said kitu, ni ya kusikitisha sana. sina uhakika kama unajua muziki vizuri. kumfananisha afande Sele na Maximilian Bushoke, kwa kweli umekosea sana.

  Akina Max, Bichuka, Gurumo na wengineo ambao sijawataja hapa ndio nguzo ya muziki wa tanzania. na wataendelea, kuimba, kutunga na kuielimisha jamii kwa miaka mingi tu na hadi watafikia uzee wao kabisa wakiwa wanamuziki, na sio kama hao uliowataja wewe na unaopenda kuwafananisha na wazee hawa ambao, baadae wataishia kuwa wafanyabiashara na kazi zingine, baada ya kipindi hiki cha muziki wa studio kitakapokwisha.

 17. BLACKMANNEN Says:

  Kijana “Roy” wa Bimalee katoka mbali. Kajaliwa sauti kijana huyu, sijui kama bado yu hai, yaillah maisha yetu ya Bongo ni ya kubahatisha kila kukicha!

 18. Anthony Angasisye Kisondella Says:

  Jamani mie mumemikumbusha mbali saaaaana, kwa kweli kipindi hicho RTD ilikuwa redio ya kizawa, kwani hivi sasa wapepoteza muelekeo na kupiga nyimbo ambazo sijui ndio ndio kwenda na wakati; nakumbuka enzi hizo mtu ulikuwa uchezi mbali na vipindi kama kumekucha, asubuhi njema, mchana mwema, chaguo la msikilizaji, jioni njema au usiku mwema, au ifikapo saa 12 jioni unabadili idhaa toka idhaa ya Taifa kwenda idhaa ya Biashara hadi saa 4 usiku huko hutakosa kusikia kama sio nyimbo ambazo leo tunaziita music was music. Kama sio msondo, basi sikinde, kama sio maquiz basi duku duku, n.k

 19. Anthony Angasisye Kisondella Says:

  Wapi Jumbe wa Jumbe, wapi Roy Bashekanako, wapi Jerry Nashion Dudumizi (Marehemu), wapi Athumani Momba (marehemu), Kweli Bimalee tutawakumbuka


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s