BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

75 WAHOFIWA KUFARIKI MERERANI- ARUSHA March, 29, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,News — bongocelebrity @ 5:23 PM

Zaidi ya watu 75 wanahofiwa kuwa wamefariki dunia huko katika machimbo ya Mererani mkoani Arusha kutokana na mafuriko yaliyolikumba eneo hilo maarufu kwa uchimbaji wa madini.Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa na hapa na hapa.

BC inaungana na watanzania wote ulimwenguni kuwapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao au walio katika jitihada za kupata habari zozote kuwahusu ndugu,jamaa na marafiki zao.Jitihada za uokozi bado zinaendelea huko mkoani Arusha.Tunaendelea kufuatilia na tutaendelea kupashana habari kadri zinavyozidi kupatikana

Pichani ni wachimbaji wa madini Mererani wakiwa katika jitihada zao za kutafuta riziki.

Advertisements
 

10 Responses to “75 WAHOFIWA KUFARIKI MERERANI- ARUSHA”

 1. usinijue Says:

  mungu awarehem wote waliopoteza maisha katika kutafuta riziki,,,,,,,,amin

 2. Gervas Says:

  Serekali nafikiri ingesimamia zoezi zima la wachimbaji wadogo wadogo kwa kuwalazimisha wawe kwenye vikundi maalumu ambapo watapewa mikopo midogo itakayowasaidia kununua machine nyepesi za kuchimbia na kuimarisha mashimo yao, sio kuwaacha kila mtu anajichimbia hovyo hovyo kila hatua moja shimo. Kwa sababu leo yametokea Merelani hatujui kesho yatatokea wapi labda Tunduru, au Tanga, au Maganzo, au nyarugusu au buhemba?. Sikuzote serikali yetu huchukua hatua baada ya maafa kutoakea na wala sio tahadhali kabla. Masikini, walala hoi siku zote hawana mtetezi katika jamii, ni victims wa majanga yote ya asili njaa, mafuriko, labda ukimwi tu ndo wa wote. Jamani tufanyeje?

 3. Chris Says:

  My condolences to their lovely ones and hommiez. Death has never been easy especially when it involves young, energetic and true Tanzanians who died in the course of working.

  Mungu saidia….

 4. Mswahilina Says:

  Mwenyezi Mungu, Mungu wa rehema, aliyewaumba; hatimaye amewarudisha kwake.
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amin.

 5. solange Says:

  mmhh kazi ipo jamani….poleni wafiwa, mie kinachonishangaza kwanini wanazama wakati wanaona hali ya mvua kwamba inaweza kunyesha anytime na ikaleta maafa?kwanini mlio juu msiwacal wenzenu mkiona mvua kubwa juu mana hao huko chini wao hawajui lolote kwa wakati huo….just like 1998 pia walikufa hivi hivi…uchungu haswaaa kwa hizo familia zilizoachwa…na wameokolewa 6 tu……

 6. matty Says:

  Wote jamani wapumzike kwa amani namuomba Mungu awape uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki zao!
  Hii nchi sijui itawawezesha watu wa chini lini? wao wanalipwa vizuri,kula na kulala pazuri, kazi ofice nzuri lakini hawajali watu wa chini iko siku tu kama anavyosemaga E.Ndaki tutafika tu!

 7. Kekue Says:

  Mungu wangu!!!

 8. changalamacho Says:

  Hivi Wizara ya Madini na Nishati tuna Kitengo cha Wachimbaji Wadogo wadogo?Au Kimekufa?Kama kipo kazi zake ni zipi hasa,ni kutayarisha SERA TU au?Maradhi yote ugua lakini Ugonjwa wa Akili USIOMBE!

 9. Chala Says:

  mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu ndugu zetu hao mahala pema peponi…. ndugu yangu hizo wizara zinafanya kazi maofisini mijini na kwenye mashangingi yao.. mpaka yatokee maafa ndio wanatia timu…Mungu saidia hata viongozi wa zamani totolewe waje wapya wenye akili zilizochangamka watuokoe jamani watu wachi tunaangamia ya rabii..

 10. mammy Says:

  Mungu ailazepema miili ya marehemu wote amin,Mungu azifariji familia zao


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s