BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 13 March, 30, 2008

Filed under: Editorial,Photography/Picha,Wanawake na Watoto,Weekend Special — bongocelebrity @ 11:04 AM
Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Wakati mwingine huwa ni zaidi ya hata ya maneno elfu moja.Ukiisoma picha hii vizuri utaweza kuona mengi.Hatuhitaji kuandika maneno mengi ili kukuwezesha wewe msomaji na mtazamaji kupata ujumbe.Picha hii ambayo ni ya kina mama huku wengine wakiwa na watoto wao migongoni(sijui kina baba wako wapi hapa) ni kutoka katika kijiji cha Bermi huko Babati,kaskazini mwa Tanzania. Picha ni kwa hisani ya peacecorpsonline.org.Hii ndio picha yetu ya wiki hii.
Advertisements
 

18 Responses to “PICHA YA WIKI # 13”

 1. Gervas Says:

  Hapa tunaweza sema mengi, ila wao wala hawaoni kama wanamatatizo, sababu wamezaliwa wamekuta wazazi wao, bibi zao wakifanya hizo kazi, na wanazichukulia km, part ya desturi zao. Hata ukiwaambia kwamba kuna kitu kinaitwa haki za wanawake, au usawa watakuona mzushi. Kuna ukuta mkubwa kati ya Elimu ya jadi na Elimu dunia. Swali, nani awanasue wakinamama kama hawa ambao naamini ni asilimia 80 ya wanawake Tanzania hawajui kitu kinachoitwa usawa? hata walio mijini bado pia. Serekali ililitambua hilo na kuwa-undia wizara yao, Je Bajeti ya wizara hii hufanya kazi gani? maana naamini kina mama hawa kuwapa pesa haitawasaidia, wanahita ELIMU ya utambuzi wa kujua nini kinaendelea duniani. Naona ndala wamevaa wamme zao, maana ni zamu zamu. afu hizo khanga waligawiwa kipindi cha kampeni …..inifuacti inaniuma saana!!

 2. Gervas Says:

  Japo wanaonekana wazee lakini naamini kati yao hamna aliyevuka miaka 21. Midume inawabebesha mimba wakishatimiza miaka 15 tu…damn midume!!

 3. Mswahilina Says:

  Mama, mama, mama;
  Mama kabeba kikapu kichwani;
  Mama kambeba mtoto mgongoni;
  Mama hajavaa hata kandambili;
  Mama anatembea pekupeku;
  Mama huyu inabidi amnyonyeshe mtotowe;
  Mama huyu inabidi apike kwa ajili ya familia;
  Kweli Mama zetu wa Kiafrika wanateseka sana.
  Mungu mbariki Mama.

 4. solange Says:

  mhhh mwanamke kweli shughuli za kijamii zinamuhusu…kama alivyosema gervas hapo unakuta ni kibinti cha 21yrs lakini anaonekana ni nyakoo…

 5. matty Says:

  Mwee jamani inauma sana baba unamkuta anakunywa ulanzi tu kilabuni mama anachota maji na kubeba kuni, kulima na mtoto mgongoni mhhhhhhhh jamani wanawake tujikomboe.
  Gervas kipende kiswahili infuacti sio kiswahili!

 6. Kekue Says:

  Haya maisha haya!! yani jamani kuna watu wanaishi maisha ya tabu mpaka basi. Ee Mungu wasaidie afya njema na nguvu amin!! Hakuna cha zaidi.

 7. changalamacho Says:

  Hawa wote walitakiwa bado wawe mashuleni,pengine High School kama siyo Vyuo Vikuu.Bado vijana sana.Lakini ghafla maisha yao yamekatizwa na Mazingira Duni yaliyopo vijijini na kugeuzwa VITOEO vya Wanaumme waliojawa na uchu wa Kujaamiana!Ukiona matukio kama haya yametapakaa nchi nzima basi ujue Taifa hilo linajichimbia kaburi.A Nation with No Future!Tukumbuke kwamba kina mama au to be more precise WASICHANA VIJIJINI ni ‘endangered species’.Wanatakiwa walindwe hadi wafikie angalau kiwango cha Sekondari jamani!Ni taifa gani ambalo kina mama waliokatizwa masomo yao elimu ya msingi wataweza kulea watoto watakao lazimika kufika Vyuo Vikuu?Msichana yoyote asikubali kabisa kukatiza maisha yake kwa njaa ya siku moja!Ukishindwa kabisa kwa sababu ya umaskini BASI LAZIMISHA KUTUMIA CONDOM!Mwanamme akikushinda nguvu PIGA KELELE OMBA MSAADA KWA MAJIRANI.wasichana wote mnao soma jengeni mazoea ya kutembea na FILIMBI NDOGO mfukoni kwa usalama wako.There will be no future without Women!Educated Women for that matter!Mtoto wa kike mpe elimu utakuwa umemkomboa na madhara yote ya unyanyasaji.This World will be Noothiiiiiing without a WOMAN!-james brown.

 8. changalamacho Says:

  Its a Mans’ World.But this world would be nothing without a Woman.So, lets protect the young girls who are a vulnerable species and who will fall prey to the unsuspecting predators, Midume iliyokosa haya wala chembe ya fadhila na ustaarabu!Msichana wa miaka 13 huoni haya wewe baradhuli ulokosa adabu kwa mama zako!Fikiria ni Binti yako alokutwa na janga hilo la kukatiza masomo na kwenda kuwekwa unyumba na Chokoraa ambaye hakumaliza hata darasa la nne,utajisikiaje?

 9. mbaguzi Says:

  uchumi tunao tunaukalia hii inasikitisha kama upo nje ya maisha haya lakini kama unaishi kijijini hawa mama wa gredi hii ni mido clasi manake wanauwezo wa kuvaa khanga mpya kuna maisha mabaya sana vijijini kwetu kuliko haya hawa wanakula good time manake hapa wenyewe wanaona kama wapo ktk drive thru ya mcdonald ndani gari full ac ndala wanazo zimewekwa kwaajili ya krismasi au pasaka

 10. Gervas Says:

  Mswahilina, mama kabeba mtungi na anatoka kuteka maji, na siyo kikapu. Ni kweli mama anateseka, sasa nini kifanyike? au ndo tuishie kuwashangaa tu?
  Matty, … infuacti nimekuelewa!!

 11. Gervas Says:

  Matty, tatizo langu nilizaliwa pale Maruku, sasa hawa watani wameshaniambukiza hizi “inifuacti” halafu nilipofika darasa la saba tu nikaanza kunywa ile kule tunaiita ” E -kaitaba!” kwa straw za ki-local afu na senene unapewa kwenye jani la mgomba. ha-ha- ha.

 12. Chris Says:

  Mtani ushaanza kuwa Mswahilina?

 13. Malenga Says:

  Mambo hayo yanaweza yakakusikitisha,kukuudhi,kukusononesha na hatimaye kukukasirisha hususani pale usipojua kisa…Hao akina mama wapo katika chama cha wanawake ambao husaidiana katika mambo mbalimbali.Katika kijiji chao wao msichana aolewapo humtolea zawadi mbalimbali.Sasa kutokana na shida ya usafiri ndiyo maana wanaonekana wanatembea kwa miguu.Pia kwakuwa ni vyama vya wanawake ni vigumu kuwaona akina baba…..Lakini achilia mbali suala la hao kama waonekanavyo pichani, nakubaliana wa nyote mliotoa maoni na mitazamo yenu juu ya maisha ya baba na mama,kwamba asilimia kubwa, Mama ndiye anakabidhiwa jukumu kubwa la uangalizi na utunzi wa familia na baba anamangamanga na kupiga chenga tu.Hela ya kumwachia mama hana lakini ya ulabu ipo!!!!Kweli mgawanyo wa maisha unatupa taabu

 14. matty Says:

  Mtani unajua Mwalimu Mswahilina anachoka kila siku mwanafunzi Gervas hasikii wala habadiliki inabidi namimi nimsaidie si unajua tena.

  Gervas namimi nimekupata senene kweye jani la mgomba ladha halisi ya chakula bora au sio? ila punguza rrrrrrr kwaenye kila sentensi.

 15. Gervas Says:

  Matty, mimi nilishashindikana, mwalimu wangu alinicharaza bakola mpaka basi tu kachoka mwenyewe, nikajua tatizo sio mimi bali jamii nilikokulia. Hivi manataka kusoma ujumbe? au herufi zimekaaje? tukianza kuwachunguza kwanza hata sentensi mnazoandika zina makosa ya kisarufi kibao…typing errors nk, mimi nawatizama tu!

 16. pyupyu Says:

  kuna mdau hapo juu anuliza nini kifanyike,swali zuri sana. mimi nafikiri kila mmoja wetu hapa anaweza kupunguza hili tatizo kwa namna moja ama nyingine.
  Tuna ndugu zetu huko vijijini wako kwenye hali hii ama zaidi ya hii,sasa basi sisi ambao tuna mwamko kidogo tuwaamshe wenzetu kule.
  Tuwafahamishe umuhimu wa elimu kwa mana hapa suala kubwa ni ukosefu wa elimu,tusisubiri hadi serikali iende huko.
  kuna vijiji vingine hata viongozi kufika huko ni ndoto,sisi wenye ndugu zetu na tunaenda huko walau mara moja baada ya miaka miwili mitatu ndio tupeleke mabadiliko.
  Naamini tukishirikia kwa hili tutaweza.

 17. Lina Says:

  Jamani this picture does say a lot sana. To me it says more than umaskini na shida. It says what a village life is, it says what mothers go through to make sure they feed, cloth and educate their children. To me, just me, it shows a perfect love, the most love that a mother can give her children. Mi nimezaliwa na kukulia kwenye kijiji karibu sana na hiki, kama ningewezaa kuwaona hawa kwa karibu naweza kuwafahamu 🙂 Well, mi nilibahatika kuendelea na shule, but believe me nikiwa nyumbani nikuwa hivyo hivyo. Ndoo ya maji, kanga kiunoni, hamna malapa….just all that. I know I don’t have to do it most of the time, but to me thats what everyone else does, ndiyo maisha. And I am never happier anywhere else than wakati niko nyumbani.
  And I tell you this, these women are happier than the rich lot. Now again you try to wonder, what is life all about? is it about living happily? or is it about fighting constantly for what someone else thinks is your right? To these women, their right is to do what you see they are doing, and they do it with all their hearts, and they are happy that way. Lakini nilivyosoma the comments, when you look at them you see umaskini, unyanyaswaji na ukosefu wa elimu. Lakini hivi sio kweli mara nyingi, it is just a different way of living, at least different from cities. For me, this is a very unique and special life, and as much as I will go to school, this is the only life I wanna live, because this is what ‘life’ means to me.
  Na waume 🙂 wako vilabuni 🙂 I know thats not too good, but mara nyingi ni bora wawe huko kuliko kuwa nyumbani, maana wakiwa nyumbani ni ugomvi tu….well, I don’t miss that one.
  Ah, jamani sasa nimekumbuka sana home 😦

 18. Lina Says:

  🙂 And the things they are carrying sio vikapu au mitungi :):) they are majiko ya mkaa – wanayatengeneza kutumia udongo, I think they are going to sell them. Ni mazuri kweli, sasa ukiyaona yanauzwa mijini you better buy them, vile sasa mtakuwa mnajua yametoka wapi 🙂 You will be supporting mama zetu.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s