BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

RAGE AREJEE TFF? March, 31, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,Michezo,News,Soka,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 12:05 AM

Kwa mpenzi yeyote wa soka nchini Tanzania,jina Ismail Aden Rage (pichani) sio geni.Jina hili ni miongoni mwa yale majina ambayo yamekuwa yakisikika katika medani za ulimwengu wa soka nchini Tanzania kwa muda sasa hususani tangu enzi akiwa Katibu Mkuu wa wa kilichokuwa Chama Cha Soka Tanzania(FAT),sasa TFF na baadaye Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Jina la Rage lilizidi kutawala vinywa vya wapenzi wa michezo nchini Tanzania, hususani soka, baada ya kushitakiwa kwa kosa la wizi wa mali na fedha za FAT kesi ambayo ilipelekea kupewa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia za makosa hayo.Hata hivyo, alikata rufaa kupinga kifungo hicho na kabla ya rufaa hiyo kusikilizwa, Desemba 2005, alitoka kwa msamaha wa Rais.

Kufuatia hali hiyo Rage alibaki nje ya TFF kupigania rufaa yake na Alhamisi wiki iliyopita, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na Damian Lubuva, walimfutia makosa yaliyokuwa yamemtia hatiani Rage.Hivi sasa Rage ni Mkurugenzi wa timu ya Moro United.

Sasa hivi majuzi klabu 12 kati ya 14 za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetaka aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ismail Aden Rage, kurejea katika wadhifa wake.Unaweza kuisoma habari hiyo kwa kubonyeza hapa.Nini maoni yako?Je Rage arejee TFF?

Advertisements
 

35 Responses to “RAGE AREJEE TFF?”

 1. kwa kweli hivi vilabu vya michezo vimeishiwa. hivyo tanzania hakuna mtu mwingine zaidi ya Rage? kila kukicha tunasikia jina la mtu mmoja tu, ndio maana soka la bongo aliendelei, hakuna mawazo mapya. wakati wa akina rage na wenzie umekwisha.
  tunatakiwa kuingiza damu mpya ya uongozi ili kuleta mabadiliko ya kweli na si vinginevyo. tukiendekeza akina Rage basi tutabakia kichwa cha mwenda wazimu maisha yote.

 2. changalamacho Says:

  The answer is A BIG NO.HAPANA.Tunataka akili mpya na mawazo mapya katika TFF.Alikuwa mzuri wakati ule siyo sasa.Abakie pembeni akitoa ushauri tu kama sisi wengine.Akitaka agombee Uongozi katika Klabu za Mpira nchini lakini siyo tena katika TFF.Amesha vijua vichochoro vingi mno vya Ulaji katika uongozi wa mpira nchini.Akirudi TUTA UAWA, with all due respects!Namshauri ili kutunza heshima yake asigombee tena katika TFF bali labda katika Klabu akipenda.Mchango wake bado utahitajika nje ya TFF.tuwape vijana nao nafasi ya kuongoza waonyeshe upeo wao katika soka la kimataifa!

 3. Mswahilina Says:

  Ndio, Rage arudi TFF maana alionewa.

 4. amina Says:

  arudi kufanya nini?huyu mwizi bwana….ila ndo kulindana na kusafishana

 5. Ana lolote huyu jamaa, ni mnafiki mkubwa. Ni kweli aliiba sana yeye na mwenzie ndolanga sema mwenzie alimzidi ujanja akasave ktk kesi. Na ndio maana enzi zao FAT ilikuwa inaendeshwa kihuni na ubabaishaji tu. Nashangaa kwanini baadhi ya watu bado wanamtaka arudi tena, Hivi hawa watu hawajiulizi aliifanyia nini FAT alivyokuwa katibu zaidi ya kuongeza mtaji wake wa daladala huko kwao Tabora?Ata hiyo Moro united yenyewe anayoingoza kwa sasa imemshinda, Moro united ya sasa sio kama ya zamani. Mtu gani alikuwa anaiba mpaka mipira!!!

 6. POLE na Hongera kwa matokeo ya mahakama kuu kuhusu ndugu HAGE.

  Katika umuhimu wa kuendeeleza mchezo wa mpira wa miguu Tanzania ni vizuri ndugu Hage kuhusishwa tena katika ngazi za juu za chama cha michezo(TFF).

  Uzoefu na utaalamu wake kikazi utaleta mafanikio mema kwa mchezo wa mpira na mengineyo.

  MICKEY JOHN AMOSI
  COPENHAGEN-DENMARK

 7. Dullah Says:

  Wee Mickey! huna hujui lolote! kwanza hata jina la huyo wako Rage hujui kuliandika. Rage ana utaalam gani katika soka? uzoefu alionao ni wa kuiba na kuhonga wajumbe wa FAT ili waendelee kumchagua na ukumbuke enzi hizo wengi wao walikuwa “Vihiyoh” STD 7 Rage mwenyeye ana buyu la form four sidhani kama anaweza kurudi madarakani because in order to be a leader of TFF you must have a Degree. Usishangae kusikia Rage ana PhD.

 8. Gervas Says:

  Mahakama inaendeshwa kwa ushahidi, kama hakuna ushahidi mahakama inakuachia hata kama uliiba. Mimi nafikiri TFF ya sasa ni ya kisasa zaidi kuliko enzi za FAT, kweli mnakubali kuweka Mvinyo mpya kwenye mtungi mkukuu?… it will defenetely be corked!!, hapa wenzangu wagema ulanzi mnanielewa. huwezi jua hawa wakuu wa vilabu wanaomtaka arudi ni kwa wema upi, labda Rage alijua kula nao vizuri ndo maana wanampigia debe,, hayo ni mawazo yangu mimi.

 9. Chris Says:

  Mswahilina na Mickey John Amosi uzoefu wa Rage na utaalam ambao nyie wawili tu ambao nawaona ni mafisadi pia (ashakum si matusi) uliiweka Tanzania wapi ktk ramani ya soka? Ni nini haswa Ndolanga na Rage waliifanyia Tanzania ktk soka during their tenure of office…..

  Tuacheni ukereketwa… tuwe realistic mno kwa maendeleo ya Tanzania…

 10. Kimori Says:

  He was a victim of 2005 gereral elections. he won’t come up with a new substance!

 11. matty Says:

  mimi sijui chochote na sitachangia kitu ila ndugu yangu Gervas nimekupataaaaaaaaa!

 12. mzalendo Says:

  RAGE ALIONEWA KWA SABABU ALITAKA KWENDA KWAO KUGOMBANIA UCHAGUZI,MGOMBEA MWENZAKE ALIMTOSA,NA WEWE UNAOSEMA HAJAFANYA KITU,HUJUI SOKA LA BONGO,KIPINDI CHA RAGE TIMU ZILIKUWA HAZINA WADHAMINI,TIMU YA TAIFA ILIKUWA INAKODIWA BUS,KWENDA MPAKA SOUH AFRICA KWENYE MATCH,KWA THREE DAYZ,UNADHANI NI RAHISI KUSHINDA,NDO MAANA MNAONA MAKOCHA WETU HAWANA MPANGO,TATIZO LA WABONGO MPAKA IJE NGOZI NYEUPE NDO MUITHAMINI,KWELI NGOZ I NYEUSI HAINA BAHATI,NJE TUNADHARAULIKA NA MPAKA KWETU,MAXIMO TIMU IKIFUNGWA UTASIKIA LAKINI ILIONESHA SOKA,KISA MBRAZILI,ANGEKUWA MBONGO PALE AMESHAFUKUZWA SIKU NYNGI,SASA HIVI TFF MAMBO SAFI,NADHANI NI WAKATI MUAFAKA AREJESHE KOCHA WA KIBONGO,HIZO HELA ANAZOKULA MAXIMO MBONA NYINGI SANA,NA TIMU ANAKAA NAYO MUDA MFUPI,WAHEZAJI WENGI WANAKAA NA MAKOCHA WA NYUMBANI WAKIWA KWENYE TIMU ZAO,

 13. Dullah Says:

  Gervas,The court of law procedure base upon evedence not witness e. Witness can lied Evedence can not lied also truth is not always in the facts, sometimes it is in the meaning.

 14. Chris Says:

  Mzalendo sasa hapo nani asie jua soka?Unasema ngozi nyeupe haina bahati… unamuongelea Maximo na Rage… Unaongelea kocha na aliekuwa kiongozi wa FAT? Hujui hizo post ni mbili tofauti. Kama alikua anafuja cash timu lazima ipande bus! Weka kumbukumbu zako vizuri ndo useme kuhusu kwamba time hizo hakukuwa na wadhamani… Ur arguments are baseless…

 15. Gervas Says:

  Dullah…what is the hell is “evedence” and “witnesse”, are you referring witness and evidence? so what do you call these two in swahili? your statement is quiet confusing in the eyes of a layman like me…ha-ha-ha, anyway tukipende kiswahili na kizungu tuwaachie hao wadhungu!

 16. Dullah Says:

  Gervas, Namaanisha “Ushahidi” na “Shahidi” ni vitu tofauti.

 17. eugenia Says:

  unajua siku zote watanzania ni watu wa kuponda tu pia ni watu ambao si honesty ni mandumakuwili walimuonea Sir Rage lakin by the first hawakuwa wamemtendea haki ndio maana akakata rufaa alikuwa akijiamini kwamba hakufanya kile ambacho walimsingizia amefanya na result ilikuja kutoka yuko innocent . Pia mi nakumbuka kwa mchango wake ktk soka alijitolea kwa kila kitu pia alikuwa mzalendo Keep it Up Sir usjal watu wanasema nini bali angalia nini ambacho wewe unaona ni bora kwako decide by ur self kwamba utaamua kurudi or not uamuzi ni wa kwako unajua ule usemi kijicho cha chura hakimzuii tembo kunywa maji so let them talk tena wanaongea wakiwa hata hawana evidence wa kile ambacho wanasema mahakama ndio chombo cha mwisho cha kupata haki sasa kimeshamuachia baada ya kumuona hana hatia sasa hivi si mwizi kama vile ambavyo mlimuona sa hivi ni raia mwema sasa nashangaa hao wadau bado wanamuita ni mwizi .Shida yetu watanzania huwa tunapenda kuwavunja watu moyo pasipo kufikiria kama unafanya right thing au ni kwa manufaa yetu tu hamtaki kuona mtu anapigania kile ambacho anaona yeye ni Right.

 18. mkweli Says:

  yaani kweli watu wengine mmekosa kazi!!! kazi kuponda, kwani nyie mmeshachangia chechote iwe tff au timu ya taifa.. juzi tu hapa twiga stars walikuwa wanahitaji michango ili washiriki vizuri!! wadau hamkujitokeza!!!,.. kama kweli mna uchungu na mpira, fanyeni mambo, anzisheni timu za watoto mitaani kwenu,yaani contribute au stimulate the development of soccer in tanzania!!! sio kutukana na kubwabwaja bila mpangilio!!! in short, practice what you preach, I mean how can u criticize anything in which you do not dwell your self in!! its absurd!!!…..

  kuhusu Rage, Rage ana haki ya kugombea nafasi yeyote anayotaka, haki ambayo kapewa kila Mtanzania, besidea he was convicted even before the case went into trial….yaanii mtu aiibe mipira 50 kati ya 10,000!! kama kweli watanzania tunajali ubadhirifu kiasi hicho, basi tuakamate wezi wengine wote, kwasababu wezi ni wengi, hata wewe ukihonga traffic, by law umeibia serikali, that is badala ya kulipa fine unamhonga traffic, hence unainyima serikali haki yake, revenue…

  conclusion, naomba watanzania tuji-examine wenyewe before we start pointing fingers!!…peace

 19. Amina Says:

  WE mkweli ulikja hapa kujibishana ila kwa kifuppi hujapata mtu,haya ya rage tumeshayasahau..kwani sisi tunaopinga unatujua ni kina nani hadi unasema tuanzishe timu zetu za watoto?kama tunazo je?sisi hatuwezi kujilinganisha na huyu au kuji examine,tutaji examine kivingine siyo kwa kulinganisha na huyu bwana mwizi asiemjua nani?hata kama atafanya ndumba akarudishwa tff lakini kubali ni mwizi,na kuhusu kukamwata kwa wezi ambia vyombo husika usituambie sisi wachangiaji humu..hapa anaongelewa rage.na kukutwa hata hatia siyo tatizo kwani we hujui mambo ya bongo bwana,au siyo mbongo wewe?mbona dito alitoka?kwani hakuua?

 20. ifra Hassan Says:

  kwa mtazamo wangu Rage anahaki ya kugombea. Nahakuna binadamu ambaye hana makosa na kila mtu anajifunza kutokana na makosa. anahaki ya kupewa nafasi nyigine na kusikilizwa, haimanishi kwambwa mtu akianguka haruhusiwi kusimama, anaweza akasimama na asianguke tena. we unaesema ni mwizi umeisaidia nini timu yako.? kabla ya kutoa maoni yako fikiria kwanza

 21. Twaha Figo A-City Says:

  Kwanza kabisa nampa pole sana brother Rage kwa kifungo alichotumikia,Pili napenda kusema kuwa Rage anastahili kurudishwa haraka iwezekanavyo katika kuiongoza TFF kwa sababu sisi wapenzi tunaamini ndo kiongozi wakweli pekee wa soka aliyekuwepo sasa nchini Tanzania,ninaposema kiongozi wa kweli ninamaana ni mtu ana anayejua vizuri mpira wa africa na fitna zote zilizopo,Nathubutu kusema iwapo kama Rage angekuwepo madarakani kipindi ambacho stars ilishindwa kufuzu kwenda Ghana basi Stars ingefuzu.

 22. Amina Says:

  hehehehe Rage ni mwizi wa kutupwa kama atarudi siyo kwa haki sababu tumeshazoea bonhgo viongozi wanaiba na wanabaki madarakani

 23. Hekima Says:

  Jamani I frankly think that a leader is a fighter hence Rage is one!!!yaani ameka jela 10 months but still he got out and fought back, and guess what people? Justice prevailed. So for all those who think he is a “mwizi”, just go on and think that cause everyone is entitled to their own opinion. However just get the facts right. Nakama yeye (Rage) amehonga kwenye his last rufaa, then why didn’t he do it from the very start? the truth is he didn’t then or the time of his last appeal. But then again we all here in the world for a reason, some are here to hinder the progression/success of others i.e “amina” and others to motivate i.e myself.

 24. Amina Says:

  we unataka kusema nini we hekima

 25. usiniguse Says:

  hongera Mr Aden Rage.nakutakia mafanikio mema .kwani najua wewe sio dhuluma.usijali watu kuongea .maneno hayaui,kama ume survive jela. you can always beat it outside.keep up the good spirit!!

 26. Hekima Says:

  inaa maana hujaelewa? is it too deep for you amina?what i meant is self explanatory, kazi kwako!

 27. mkweli Says:

  dada Amina, kwanza kabisa mi sikuja kubishana! nimekuja ku-express mawazo yangu. Na kama tayari una timu ya watoto hongera, hata kama imeundwa na wadogo zako, au watoto zako, n.k; as long as team yote poa. Alafu sijasema tujilinganishe na Rage, neno nililotumia ni “examine”, sikusema tujiko-‘compare’ na Rage. by examining ourselves, i meant tujiangalie tumefanya katika kuchangia maendeleo ya mpira nchini mwetu, thats what i meant by examining ourselves. Maanake binadamu wengi tunatabia ya kupoint fingers, wahenga walisema nyani haoni makalio yake! yaani tunatabia ya kukosa watu, bila kujikosoa kwanza, mi nina amini huwezi ukawa unahubiri neno la bwana, huku unalivunja at the same time; yaani muhubiri, should always practice what he preaches!

  kuhusu wizi::::niliamua kutoa mfano wa moja ya mashtaka ya kwenye kesi kuonyesha the absurdity of the case! alafu unamanisha nini unaposema kwamba kukumbwa na hatia sio tatizo? i mean kama unsema jamaa ni mwizi then it definitely matters!

 28. Amina Says:

  Rage ni mwizi kwa kifupi hata kama karudi madarakani bongo tumeshaizoea ,,,,,habari ndo hiyo sasa nyie fanyeni ku compare na ku examine shauri zenu

 29. mkweli Says:

  niwie radhi dada amina ila inaonyesha hukwenda shule wewe, au labda ulikuwa hupay attention darasani!! au labda hufahamu hata mashtaka yenyewe , matokeo yake unatuhumu watu, ina wezekana mtu akaiba kweli mipira 50 kati ya 650 (hili ni mojawapo ya mashtaka)… alafu eti Rage afungwe miaka mi3 na ailipe tff 1000$ huku ndolanga amriwa ailipe TFF 3000$ ila hafungwi!!! kesi inachukua miaka karibu 6, alafu judgement inatoka 2005, kabla ya uchaguzi!! connect the dots my dear amina and u will definitely smell something fishy!!!! that is, african politics at its best!!!!…….

 30. Hekima Says:

  yaani…”mkweli” you so on point am out pf words so I’ll just quote you, “african politics at its best” maanake I could have not said it better myself. Sasa “dada Amina” if you have not put one and two together, then I and “mkweli” are wasting our time. A word of advice, get the facts straight!!!!

 31. Amina Says:

  kwa kifupi nyinyi wawili rage ni mwizi nawewe unaeniambia mi sijaenda shule kwani unanijulia wapi?inaonesha wewe ndo hujaenda shule maana unabwabwaja tu…huyu msomali wa tabora ni mwizi na mwenzie ndilanga wote wezi nanyinyi wezi,hata mkiandika kiingereza hapa rage mwizi

 32. mkweli Says:

  dada amina punguza jazba. mbona unaji-contradict mwenyewe: unesema kwamba mi sikujui wewe, kwa hiyo siwezijua kama wewe umeenda shule! true, ila at the same time unatuita mi na hekima wezi, kwani unatujua sisi!! unaleta double standards! the same double standards ambazo zili mu-implicate Rage; Rage anafungwa huku ndolanga anaambiwa alipe 3000$! tuweku emotions zetu pemebeni, ila at the same time tu we critical; but tusiendekeze criticism za kishabiki au za chekechea!tuwe WAKWELI!!…..

 33. mkweli Says:

  once upon a time

 34. Amina Says:

  rage mwizi mwenzenu mliiba mipira wote inaonesha

 35. Hekima Says:

  there is no need to argue with a fool…. so go figure Amina!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s