BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NIMENG’ATUKA + UZINDUZI WA ALUTA CONTINUA! April, 3, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya,Tamasha — bongocelebrity @ 10:33 AM

 

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu,hatimaye wakati umewadia.Tunaongelea uzinduzi rasmi wa albamu mpya kutoka kwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule almaarufu kama Professor Jay(pichani).Albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Aluta Continua inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho,tarehe 4 Aprili ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,uliopo maeneo ya Upanga jijini Dar-es-salaam.

 

Aluta Continua itabeba nyimbo 10 ambazo kwa mujibu wa Prof.mwenyewe na kwa mujibu wa single chache kutoka ndani ya albamu kama vile Hapo Vipi,Ndivyo Sivyo na hivi karibuni Nang’atuka,ni wazi kwamba Aluta Continua ni moto wa kuotea mbali.

 

Katika uzinduzi huo ambao utakuwa wa kwanza kabla hajaelekea mikoani kuzindua pia albamu hiyo kwa mashabiki wa huko,Prof.Jay anatarajiwa kusindikizwa na wasanii mbalimbali maarufu kutoka Bongo na Afrika Mashariki kama vile Jose Chameleon(Uganda),Jua Kali(Kenya),Blue 3(Uganda) ,Ambwene Yessayah ‘AY’, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, Besta na Rehema Chalamila ‘Ray C’. Wengine ni Feruzi Mrisho ‘Ferooz’, Issa Shaaban ‘Matonya’, Lawrence Malima ‘Marlow’,Mandojo na Domo Kaya, Nakaaya,Nonini and P-Unit pamoja na wengineo wengi.

 

Baada ya hapo uzinduzi utaelekea mikoani ambapo mikoa kama vile Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Iringa, Morogoro na Mara ndio ambayo inatarajiwa kupata burudani hiyo.

 

Albamu hii ni ya kimataifa zaidi kwani imetengenezwa katika studio mbalimbali kama vile 41 Records(Dar-es-salaam),MJ Records(Dar-es-salaam), Mo Records(Mwanza) Ketebull Records(Kenya),No End Entertainment(Uganda) Contact Studio( Kigali-Rwanda) na Jam Works(South Africa).

 

Kiingilio katika uzinduzi huo wa kesho ni Tshs 7000.Wasambazaji wakuu wa albamu hiyo ni GMC Wasanii.Usikose kesho ndani ya Diamond Jubilee.

 

Wakati huo huo,Prof.Jay hivi majuzi ametoa single yake ya Nimeng’atuka ambayo pia imo ndani ya Aluta Continua.Isikilize kwa kubonyeza player hapo chini.

 

28 Responses to “NIMENG’ATUKA + UZINDUZI WA ALUTA CONTINUA!”

  1. Chris Says:

    That’s my first time to listen and get blasted by the song. I always say Prof J has some serious talents! Dont stay on his ways.. He got rappin’ pipes to blast the verses….a.k.a mistari

    Feel the song… reallly its rockin’… though its political n’ I hate politics…

    But with all the talents this dude has, I feel like his beats are a kinda repetitive… be creative on that… wish you the best though…

  2. Saidi Situ Says:

    Mheshimiwa naona ana suti ya bei mbaya sana ya D&G. Si mchezo, wakamshauri aonyeshe label kwenye picha ili wenye wivu mjinyionge. Anayesema mziki bongo haulipi anyooshe mkono.

    None? Yeah i thought so
    Kila kitu kinajionyesha. Na mimi naanza kuchukua mazoezi ya sauti.

  3. Dinah Says:

    Duh! Akyanani Mmenishitua nilifikiri kang’atuka kwenye game…..nakuja, ngoja kwanza ni-calm down….huh!

  4. Hellen Says:

    Si mchezo,kweli wewe mc shupavu!! unastahili pongezi bro!!!
    keep it up!!

    Hellen.

  5. Komba .H Says:

    Mzee wa Mitulinga,Ubahatishi kazi zako zinakubalika hongera kwa kuzindua album ya aluta continua.Big up,tuko pamoja

  6. debra Says:

    Alizaliwa akiitwa Jeseph asa ivi jizooo,heavy weight mc,wa mitulinga yaani majina kibaoooo…..
    Usilewe sifa mazee,uko tite kino kinooooma.Kila la heri chalaangu…..Nuff Ras pekt 4u brother.
    PamoJAH

  7. solange Says:

    hakufagilia sana wanguuu…yani umetulia.

  8. zama Says:

    uko juu mtuwangu

  9. kamo Says:

    prof.j kweli una kipawa.naomba mungu uzidi kutuangushia mindundo kalikali kama kawaida.asanta.

  10. Dar Hotwired Says:

    @ chris ( First Poster )

    I understand what you say that he Prof J sort of uses the same beats over and over again.

    Lakini you have to consider that he is only “limited” to venues he can get beats from. Why i say this is coz most producers in Bongo copy one another and are not very original themselves. You can see the case of Mandugu digital. They had a couple of dope beats at first but now all tracks produces by them seem to sound the same.

    Truth be told tho, Prof Jay still slices all his beats like a hot knife on butter. Thats the least he can do. Now that i think about it, maybe thats why hes such a lyrical guy. Maybe all he had going on for him was the rappin’. So of course he will tend to step his game up even though the producers are not.

    Having said that, hongera sana Prof Jay. I will be coming down there to get you the best possible deals for yourself. Big up Big One Production and Crew.

    Simply Simple.

  11. Dinah Says:

    Bomba-bomba! Wee ng’atuka tu huo haukuwa mwenzo mzuri 🙂

    Hakuna kama yeye ndani ya Bongo that 4 sure. Jamaa kazi zake zinaonyesha ukomavu na upeo wake wa kiakili . Toka ameanza hakuna track katoka nayo ya “madongo” au “misifa” yeye ana-base kwenye maswala yaliyomo kwenye sehemu kubwa ya jamii ya kibongo (real life), anagusa watu wengi na sio yeye as yeye.

    Pro J wewe ni best male artist of all times unahitaji tuzo pekee ya kuwepo kwako ktk “game”.

    Kila la kheri!

  12. sikubaliani Says:

    Prof J w r 2gether i love u

  13. Kamanzi Says:

    Hao wasuka nywele, wapakamikorogo na wavaa heleni wakiume wanaojiita wanamuziki wa kizazi kipya wangejaribu kuwa kama huyu jamaa. Manake mziki una ujumbe sio ushenzi wa nakupenda nakupenda kila wakati. Huyu anaweza kujiita mwanamuziki wale wengine ni mashoga tu.

  14. any Says:

    toa label kwenye koti?

  15. Liemy Says:

    Big UP Prof. J

    vaa suti na lebel kwa raha zako.

    Bongo mambo tambarare kweli, naona chaa msingi ni mtu kujishughulisha na kujituma bila kukata tamaa. Ukifanya hivyo lazima utafanikiwa.

    All the best,

  16. Bigy Says:

    Big up Prof jay. Nyimbo zako always zinaonesha unafikiria kabla ya kuimba. Sio simplistic. Kwa upande wangu nasema unajitahidi na unatufikirisha kwa nyimbo zako. Ndio maana wengine sasa wanasema ni wewe unang’atuka, wengine watafikiria jingine n.k. Ndi fasihi yenyewe hiyo.

  17. Amina Says:

    we kamanzi usinichekeshe na kweli huyu yupo real sana, na wala hajitutumui siyo hao wengine na beef wameweka mbele utafikiri wanaelewa maana yake utasikia na beef beef mhhh

  18. kingo Says:

    this dude has some brains upstairs!two thumbs way up!

  19. jose Says:

    porofesa jei hawezi kuimba laivu kama
    bi kidude! lakini hongera,unaonekana kama
    mmarekani.kupritendi ni haki yako mkuu!!

  20. Kamanzi Says:

    Haki ya nani Amina kama ningekuwa na uwezo ningewapiga marufuku hawa *** wa kizazi kipya kujiita wanamuziki. Hivi kweli gitaa upigiwe, kinanda upigiwe halafu wewe kazi yako kubana pua tu na kuingiza sauti tu kwanini usiimbe kitu chenye maana? Wangekuwa wanaingiza na vyombo wenyewe wangefanyaje? Halafu wanajiita masupastaa sijui kwa kusuka au kwa mkorogo? Utasikia kwenye nyimbo zao yes no nyingi na neno la kiingereza wanalolijua ni baby gal. YAani kila wimbo nakupenda baby gal wananikera. Tutafanyaje Tanzania uhuru umekuwa mwingi acha wajiite watakavyo ila hawana mbele wala nyuma kimuziki.

  21. KELVIN JONES Says:

    HUYU KAMANZI ANAONEKANA NI MMOJA KATI YA WATANZANIA WENYE MAJUNGU FITINA ROHO YA KUAMINI KUSHINDWA NA KWANINI JAY ANAJITAHIDI KIMSINGI ANASTAHILI PONGEZI ONDOA FIKRA MGANDO KAKA NI WAKATI WA KIZAZI KIPYA MADUKANI KUMEJAA AINA NYINGI ZA MUZIKI KUANZAIA AMBAO NI WA VYOMBO HALISI NA HUU WA KIZAZI KIPYA AMBAO KIMSINGI NI WA KWENYE COMPUTER ZAIDI KWA HIYO UNA UAMUZI WA KUCHAGUA UTAKACHO ,KAMA HUPENDI JAMAA WA KIZAZI KIPYA WANAVYOPERFORM NI BORA UKAKAA KIMYA ILI UNEKANE MWENYE BUSARA KULIKO KUROPOKA NA WATU WAKAKUONA M2 MZIMA HOVYO AKA KIUMBE MZITO,VIJANA WETU WAKIFANYA VIZURI TUWAPONGEZE WAKIKOSEA TUWASAHIHISHE LAKINI KWA JINSI ULIVYOFANYA WEWE NI KAMA UNAWASAGIA VILE UNGEONEKANA MTU MWENYE MAWAZO MAPYA NA THABITI KAMA UNGETOA USHAURI KWA JAMAA KULIKO KUSAGA WENZAKO WANATENGENEZA PESA WE UNABAKI KUWASAGIA , SHAURI LAKO ,MWISHO HEBU JARIBU KUFIKIRIA KAMA WEWE UNGEKUWA MWANAMUZIKI WA KIZAZI KIPYA HALAFU HAYA MAONI ULIYOTOA WEWE YANGETOLEWA DHIDI YAKO UNGEJISKIA VP ,JIFUNZE KUISHI KADIRI YA NYAKATI SWAHIBA ,KILA LAHERI VIJANA WA BONGOFLEVA ENDELEEENI KUTENGENEZA PESA ILA INABIDI MBADILIKE KATIKA MAISHA HALISI, CHAIN NA MAGARI YA KUENDEA KWA VIMADA WENU SIYO DILI JIFUNZENI NAMNA YA KUWEKEZA ILI MPATE PESA ZAIDI KULIKO KUPONDA RAHA ,NAMAANISHA POMBE NGONO NA STAREHE KWA UJUMLA ,VINGINEVYO MNAJITAHIDI ILA WENGINE KATI YENU INABIDI WAJINOE ZAIDI

  22. Dinah Says:

    Kamanzi;

    Wanajulikana kama wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, wasanii wa muziki wa dansi, wasanii wa muziki wa asilia nakadhalika.

    Ni kweli kabisa kuwa ili sauti fulani ziitwe muziki huwa kuna kuwa na mchanganyiko wa vionjo tofauti ikiwa ni pamoja na sauti ya msanii.

    Hakika wanamuziki ni yule anaeweza kucheza na vyombo, sauti ili kuzalisha muziki waliobaki ni ama wasanii, wachezazi, waimbaji, watunzi au perfomers n.k.

    Mfano rahisi ni Ally Zoro yule ni mwanamuziki kwa vile anaweza kucheza na vyombo na wakati huohuo kuimba. Swala la usupa star/u-celebs hauna uhusiano na uanamuziki au usanii bali jamii inavyowapokea hao wasanii au kazi zao.

    Pro J sio mwanamuziki bali msanii wa kughani, Ali Choki ni mwimbaji na sio mwanamuziki…..Bob Marley ni mwanamuziki….

    J’2 njema.

  23. nyarubamba Says:

    Duh,kamanzi umeua ile mbaya!pamoja na jamaa hapo juu kujitetea lakini umeziba kinoma.Anyway,ukweli umesema hata Dinah anazuga tu, lakini kimoyomoyo anasema kweli!

  24. Msanii Says:

    Si utani. Lazima uache lebo ili wote waione. But D&G isn’t quite an expensive brand by an artist’s standards….lol. I like Prof. Jay’s Jay-Z like outfits (as opposed to many other fake imitators), but truth be told, leaving the label on a new piece of clothing is a little bit cheesy. Hata hivyo kamua kamua baba!!

  25. Kamanzi Says:

    Kelvin Jones don’t get me wrong. I never intended to trash any of these so called new generation musicians and certainly not Prof J of all people. As the matter of fact I think Prof J, Afande Sele and a bit of Lady Jaydee have been doing quite an outstanding job under some difficult circumstances of the music industry in Tanzania.

    What I realy want to stress out is that, since they don’t trouble themselves with music arrangement, they are at least expected to come up with something tangiable. Most of the so called music in this industry is centred on love while there is a lot to educate Tanzanians about (please refer to the hit song DARUBINI KALI by Afande Sele).

    Take Jose Chamelion for instance, his hit single “Jamila Analia” was so relevant to Ugandan situation that it was used by UNICEF in their commercials. That’s what I call new generation music, singing with purpose.

    Fellow Tanzanians, you will only progress when you start taking criticism positively. And there is nothing like majungu I have on those poor musicians. I am just too big for that Mr. Kevin its pity that we know not each other otherwise you would have proven my point.

    Cheers!!!!

  26. KELVIN JONES Says:

    ANYWAY POA MWENZA ,ILA NEXT TIME TUMIA LUGHA LAINI BASI, OTHERWISE HUTAELEWEKA, NDO MAANA NIKAJA NA MAONI HAYO,POA SIKU NJEMA £££££££

  27. Kamanzi Says:

    Peace and Love Kevin!!! Mambo ya kawaida hayo. Wala usikonde nipo na wewe kama amani na upendo ila kama alivyosema Prof J, nataka yeyote anayeingilia fani isiyo yake AN’GATUKE na kuwaachia waliojaliwa na manani.

  28. KELVIN JONES Says:

    Kamanzi MAMBO VP MWENZA NIKO BUSY KIDOGO NAJIANDAA KWENDA COLLEGE ILA KUNA MASWALI NAKUULIZA KWA UFUPI NTAANGALIA MAJIBU NIKIRUDI, UMEMUONA HUYU MDAU JMASHAKA WENGINE WANAMUITA MWANA KIJIJI ,SIJUI KWANINI, NAOMBA UNIPE MAONI YAKO JUU YAKE ,KWA KUWA NIMEVUTIWA NA STYLE YAKO YA KUONA MAMBO.WAPO WANODAI JAMAA MSANII ,JMAA KAVAA SUTI NADHIFU ILA MARA NYINGI WAVAA SUTI HUWA HAWAFAI ,SI UNAJUA TENA SAMPULI ZA MAJAMBAZI WA KUAMINIWA (WANASIASA) ISIJE IKAWA ANAWAINGIZA WADAU KING KIULAINI, NIPE MAONI JUU YAKE ,NIJIBU CHINI YA HII MAONI YANGU TAFADHALI ££££££££


Leave a reply to Liemy Cancel reply