BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

GEORGINA-MARIJANI RAJABU April, 4, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Kama mzaha vile robo tatu ya mwaka 2008 ndio ishakatika. Nikitizama nyuma naona ni kama hivi majuzi tu tulipokuwa tukitakiana kheri ya mwaka mpya.Unadhani kuna ukweli fulani kwamba siku hizi zinaenda mbio kuliko kawaida au ni uzushi wa bongo zetu tu?

Kwetu sisi hapa BC ni Ijumaa nyingine, wakati wa burudani. Mdundo wa leo ni wimbo maarufu sana wa Georgina kutoka kwake Jabali la Muziki,Marijani Rajabu.Kama hujawahi kuusikia au kuucheza wimbo huu, iwe kwenye sherehe ya kifamilia, harusi ya kaka,dada au mshikaji, iwe kwenye ile baa iliyopo pale kona au vinginevyo basi si ajabu umri wako hauruhusu hata wewe kuingia ingia kwenye mitandao kama hii(natania au?).

Bonyeza player hapo chini upate burudani. Ijumaa Njema.

 

Advertisements
 

4 Responses to “GEORGINA-MARIJANI RAJABU”

 1. mnaku Says:

  Napenda kuwasahihisha ndugu zangu wa Bongo Celebrity.Ni kwamba tumemaliza robo ya kwanza ya Mwaka huu wa 2008,na siyo robo tatu ya mwaka huu.Robo tatu ya mwaka huu tutaimaliza mwezi wa tisa ndugu zangu.Habari ndo hiyo,ila tunashukuru kwa huu wimbo wa jabali la muziki,Mzee Marijani Rajabu(marehemu)

 2. DUNDA GALDEN Says:

  Home boy ndani ya maradhi ya nyumbani
  Ahhhh wapi Kongo bar enzi je unakujua Pombe Shop? Enzi zile uko nyumbani moja moto moja baridi leo Michuzi umeuwa kaka
  We utani huo enzi zile wewe uko kwenu wapi sijui teh teh natania. leo umeuwa wangu nyongo mkalia maini,ahsante filigis mzaa chema alipo kuwa ananisindikiza machozi yakimtililika yote hayo BC ni hicho kibao cha Jabal
  watu heshima kwako Jabal wiki end njema ndugu na jamaa zangu uko bongo na wana wa BC Dunda Galden
  Na CHAFOS CHAI GODA,(DARWIN AUSRALIA)

 3. Mswahilina Says:

  Big up BC. Unatukumbusha enzi zetu. Ninakushukuruni kwa kutupa burudani hii murua.

 4. Msema Kweli Says:

  Asanteni! BC kwa kunikumbusha nyumbani enzi zile,
  nilikuwa nikimuona marehem Jabali la mziki Marjan rajab
  mwana manyema akitoka shuleni kwake Tambaza anaenda
  katika mazoezi ya mziki na bendi yake ya mwanzo Safari
  Tripers baadaye Dar International pale mtaa wa mchikichi
  Kariakoo.
  Mlaze pema peponi Mola


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s