BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUNAPOMKUMBUKA SHEIKH ABEID A.KARUME April, 7, 2008

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kitaifa ya tangu kufariki kwa Sheikh Abeid Amani Karume miaka 36 iliyopita.Raisi huyo wa kwanza wa Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi huko visiwani Zanzibar.

Ni uongozi wa Hayati Sheikh Amani Abeid Karume na Hayati Julius Kambarage Nyerere ambao ulitupa Tanzania tunayoijua hivi leo ukiwa ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu mwaka 1964.

Kumbukumbu ya mwaka huu ya Sheikh Abeid Amani Karume inakuja huku bado kukiwa na “mpasuko” wa kisiasa huko visiwani hususani kuhusiana na suala zima la muafaka ambalo mpaka kufikia hivi sasa bado hayajapatikana maafikiano ya kueleweka.Ni imani yetu kwamba muafaka utakuja kufikiwa na amani itazidi kutawala.

Ili kujua au kujikumbusha vizuri historia ya Sheikh Abeid Amani Karume bonyeza hapa na hapa bila kusahau kutembelea mtandao wa zanzinet.org ambao umesheheni mambo mbalimbali kuhusu visiwa vya Zanzibar ikiwemo pia historia kamili ya visiwa hivyo. R.I.P Sheikh Abeid Amani Karume.

Katika picha hii ya zamani anaonekana Mjane wa Sheikh Abeid Amani Karume,Fatma Karume(kulia), akiwa na Mama Sophia Kawawa(marehemu) katika moja ya mikutano enzi hizo.Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

Advertisements
 

27 Responses to “TUNAPOMKUMBUKA SHEIKH ABEID A.KARUME”

 1. Gervas Says:

  Huwa najiuliza kila mara hivi nani alimuua karume? na kwa misingi gani aliuawa? je hiyo misingi iliyopelekea kuuawa Karume ni kweli haina uhusiano wowote na mpasuko wa siasa uliopo sasa zanzibar? je kabla ya vyama vya siasa kuanza Tanzania, ni kweli hapakuwa na mgawanyiko wa wazanzibari? walikuwa wamoja kweli? sababu nahisi huu mpasuko wa sasa hausababishwi na matokeo ya changuzi zilizopita pekee yake, kuna chanzo haswa. Kuna anayefahamu lolote juu ya haya niliyouliza hapa? naomba msaada wana-blog.. maana leo ni siku ya Kudadavua mambo kadhaa, its Karume day.

 2. Anonymous Says:

  Soma siasa za Zanzibar utajua yote hayo tafuta makala za zaamni za Rai iliyokuwa ya Generali Ulimwengu kila kitu kiko wazi. Kuna vitu vinaitwa AfroShiraz na Hizbu party. Hizbu ilikuwa ya Wapemba na Afro Shirazi ya Waunguja na wengine waliotaka kujikomboa chini ya usultani. Hizbu hawatambui mapinduzi yaliyomtoa Sultan kwa sababu majority wana asili ya uarabu. Na Afro Shiraz ndio waliofanya mapinduzi ya kumng’oa Sultan na kuweka utawala uliopo madarakani, hii Afro Shiraz party iliyounda serikali ya Mapinduzi ZNZ ndio iliyoungana na Tanganyika na baadae chama hicho kiliungana na TANU mwaka 1977 na kukazaliwa CCM.

  Hayo mambo ya siasa za visa Zanzibar yanaanzia tangu wakati wa kutawaliwa na Sultani ambako si unajua tena mambo ya matabaka ya rangi, na ubaguzi wa rangi na thamani ya bwana na mtwana. Sasa kulivyotokea mapinduzi ndio uhasama ukazidi kuendelea kati ya wanzazibari weusi na washirazi na wazanzibar wenye asili ya alikotoka Sultan.

  Angelikuwepo huyo bingwa huyo ungesikia cha Muafaka wala cha nini na hata hii CCM sijui kama ingekuwepo nafikiri kila nchi ingebaki na chama chake cha siasa.

  Samahani siwezi kuingia zaidi ndani ya hii ishu ni sensitive ndio inayoleta siasa za kubaguana ya huyu muunguja na huyu mpemba na ubaguzi wao unaenda mpaka kwenye nafasi za kazi za masomo na kadhalika, iko deep sana sio kama watu wanavyofikiri. Na ukizingatia sasa hivi hao waunguja ni wengi sana kuliko wapemba (wapemba wengi walikimbia ZnZ hata kabla ya awamu ya 3 na wamejikita sehemu mbali mbali duniani) ni rahisi sana kwa CCM kushinda kura ya maoni, inawezekana kutokana na historia ya siasa zao wanachama wa CCM walioko Unguja wakasema hatutaki serikali ya mseto. Hivyo CUF wataloose chance ya kuwa sehemu ya serikali ya ZNZ ili kuondoa huo ubaguzi uliopo miongoni mwao. Na walivyo na ushabiki na ushindani sijui itakuwaje hiyo siku ya kura ya maoni kama vile chungwa na ndizi Kenya!

 3. Gervas Says:

  Duh, anony.. hapo juu, nakushukuru saana, maana maelezo yako japo ni machache lakini yame-hit point kwa mtu muelewa. najua sio mimi tu, watu wengi hawajui hasa chimbuko la soo ya Zanzibar. Kumbe sio issue ya kukurupukia tu na kutoa judgment ya mpasuko wa zanziabar. Asante kwa niaba ya wengi.

 4. Mswahilina Says:

  Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, Mwenyezi Mungu akulaze pema peponi. Amen.

  Hayati Mama Sophia Kawawa, Mwenyezi Mungu akulaze pema peponi. Amen.

  Mlikuwa majemedari wetu Watanzania kwa nyakati zenu.

 5. mkereketwa Says:

  Nakubaliana na maelezo yako hapo juu, na ukitaka kuona kasheshe ya watu hawa inabidi utembelee Zanzibar ujionee. Nilifanikiwa kuwa zanzibar kati ya mwaka 1992 – 1995 wakati machafuko ya siasa ya vyama vingi imeanza na niliyoyashuhudia sintosahau hadi leo. Jazba yao ni ya hali ya juu na kama ulivyosema imeanza siku nyingi vizazi hadi vizazi na watu wameendeleza historia na kuweka vinyongi moyoni mwao. it’s all about history. Mambo yatabadilika tu iwapo wakakubali kujiita na kujitambua kama WAZANZIBARI AU WATANZANIA THAN MNGAZIJA OR MPEMPA OR…. Hali hii inaendelea hadi nje ya nchi kwani sisi wote ni watanzania lakini bado utaona kuna mgawanyiko mkubwa baina yetu. Wabara hatujali kama mtu ni mmatumbi, mgogo, mchanganyiko wa mgogo na mzungu au mhindi. Kama kuna jambo limetokea kama msiba au ugonjwa la mtanzania yeyote linanigusa na kama kushiriki kwa hali na mali. THIS IS THE PROBLEM!

 6. Kasusula Says:

  Shukrani sana wadau wote wawili hapo juu , aliye uluza swali na aliye jibu swali, swali ni safi na muhimu sana na jibu linalidhisha mno, ni wengi tulikuwa hajui huo ukweli na ukungu kidogo sasa umetutoka.
  shukrani

 7. Kasusula Says:

  Shukrani sana wadau wote wawili hapo juu , aliye uliza swali na aliye jibu swali, swali ni safi na muhimu sana na jibu linalidhisha mno, ni wengi tulikuwa hatujui huo ukweli na ukungu kidogo sasa umetutoka.
  shukrani

 8. Kyoma Says:

  Wazee maojua historia ya mzee Abeid Amani Karume, nimefuatilia hiyo website iliyotolewa hapo juu….baada ya bonyeza hapa na hapa…http://www.bookrags.com/biography/abeid-amani-karume-sheikh/ . Hivi maelezo yaliyoandikwa kuhusu asili ya mzee Karume na jinsi alivyo uawa ni sahihi?

 9. Bablii Says:

  Tunakumbuka kifo cha Karume, ni vizuri pia tukakumbuka sababu za kifo chake!

  Mimi simwana historia, lakini kwa sababu nimejitahidi kuifuatilia historia ya zanzibar kabla na baada ya mapinduzi, kwa kusoma vitabu mbali mbali vya historia, vikiwemo vile vinavyoeleza kwa kuegemea watawala (CCM), vile vinavyoogemea wapinzani(CUF) vile vilivyotungwa na waandishi huru na zaidi nimehadithiwa na shuhuda aliekuwepo wakati wa vipindi vyote hivyo (Bibi yangu Mungu amlaze amrehemu ahera aliko), nathubutu kujiita gwiji la historia ya zanzibar tu!

  Ukitaka kupata sababu za kifo cha karume, vizuri ukasoma kitabu kiitwacho “UKWELI NI HUU” Kitabu hichi bahati mzuri kimetungwa na mmoja wa mawaziri wa SMZ, kabla hajaaamuwa kuisaliti jamii yake na kukubali kupewa uwaziri (Hivi sasa anaomba kitabu hichi kisisomwe tena! lakini ndo hivyo tena Jani likisha anguka halirudi tena mtini…). Pia waweza kusoma kitabu kiitwacho “KIVULI KINAISHI” ingawa kitabu hichi kimeandikwa kisanii sana, lakini kiufupi anazungumzia hali ya zanzibar baada ya mapinduzi ya 1964

  Kwa hakika kifo cha Karume ni matunda ya mbegu aloipanda baada ya mapinduzi. Madhila, mateso, dhiki, mashaka,jitimai la roho, maonevu, dhulma, manyanyaso, mauwaji na kila aina ya kisicho stahili kufanyiwa kiumbe kilicho hai, basi ndicho walichofanyiwa wale waliohisiwa kutoyakubali mapinduzi ya mwaka 1964, mapinduzi yaliyo mpinduwa “Mpemba” Mohd Shamte! Ndio hakuna muarabu aliepinduliwa 1964, ni mapinduzi yakumuondoa mpemba madarakani, ndo maana mpaka kesho hawataki mpemba arudi madarakani (ndo maana hawezi abadani kukubali serkali ya mseto)!

  Baada ya mapinduzi, kuna waliochukuliwa majumbani mwao, usiku wakila chakula na familia zao, eti wanaenda kuhojiwa lakini mpaka hii leo hawajarudi tena majumbani mwao (1964 mpaka 2008)…! Kuna waliolishwa chumvi pishi nzima (pishi ni sawa na kilo 2.5) nje ya markiti (soko) la wete na kupigwa
  viboko eti wao ni hizbu! Loh kuna ambao dada zao walinyanyaswa , mama zao wakauwawa akiwemo huyo Mahmud (alielipiza kisasi kwa kumuuwa karume). Waswahili wanasema “mwenda tenzi na omo hurejea ngamani” Kwa hiyo pamoja na kuwafanyia unyama familia yake akajikuta anamlea huyu mahmud (ni mfano wa Firauni na Mussa), akampandisha vyeo jeshini, kumbe ndo anamrahisishia kazi ya kumrudi! Basi
  ilipofika nyakati za alasir tarehe 7/4/1972, Mahmud akalipiza kisasi (ndio kwa mujibu wa dini yake Alkisasu l-haki) “Auwae kwa upanga huwawa kwa upanga”

  Lakini bado matunda ya 1964 tunayavuna, maana serkali ya zanzibar imekuwa ni ya wa unguja na wapemba ndio watawaliwa,siasa za chuki, majungu, fitna dharau ilimradi, tafrani. Wapemba wamekuwa kama wageni kwenye kisiwa chao!
  Ah ambae hajenda Pemba aende akaone, asije sema mie muongo nabawatuka atiiiiii.

  Ngoja ni sign off…wasije wakanipoteza

 10. Matty Says:

  Asante sana Gervas kwa kuuliza Swali la maana na jibu tumepatiwa linalordhisha, maana hata mimi nilikuwa sijui kitu kuhusu kuuawa kwa Karume.
  Asante wachangiaji Anonimous hapo juu na Bablii.

 11. Ms Bennett Says:

  inaonekana wewe bablii ulitaka waarabu waendelee kukaa kwenye ardhi isiyo ya kwao mapka leo.bravo sheikh abeih karume na mwalimu Nyerere kuwatimua masultani na usultani wao,hawa watu wanakasumba sana wameacha ubaguzi mpk leo kwa hao wanajiita waarabu watanzania

 12. Ms Bennett Says:

  inaonekana wewe bablii ulitaka waarabu waendelee kukaa kwenye ardhi isiyo ya kwao mpaka leo.bravo sheikh abeid karume na mwalimu Nyerere kuwatimua masultani na usultani wao,hawa watu wanakasumba sana wameacha ubaguzi mpk leo kwa hao wanajiita waarabu watanzania

 13. Gervas Says:

  Babii, Kuna kitu kinaitwa “biasness” katika uandishi wa vitabu ambapo mwandishi anakuwa either negatively or positively influenced na habari ambayo anataka kuiandikia kitabu hicho, mwandishi anatakiwa kuwa neutral. Sasa hapa msomaji unatakiwa kuwa makini kidogo, japo vitabu ulivovitaja sijavisoma. Mimi nafikiri hii dhambi ya kubaghuana haitaisha maana inaonekana inapandikizwa kizazi hadi kizazi. Kwa mtindo huu hata hao mnawaita wapemba wakiingia madarakani sio siri kazi ya kwanza itakuwa kulipiza kisasi. Nasikia kuna wengine walikimbilia wingereza wanajiita wakimbizi, wakachana passport zao Jk alivoenda Wingereza wakaanza kumuomba tena wapatiwe pass mpya na hali waliukana Utanzania. Mbona kuna Wapemba wengi tu wanamafankio makubwa ya biashara bara? maana Sheria ya nchi haimkatazi mtanzania yeyote kuishi popote ndani ya nchi. Mbona hata Bara kuna mikoa mingi tu haina maendeleo kabisa, wilaya hazina umeme!, Pemba ni sawa tu na mikoa mingine kama Kigoma, Rukwa n,k. Mimi nafikiri swala la zanzibar litaisha/pungua kama wananchi wake kwanza wapunguze jaziba, waondoe “dhambi ya ubaguzi” huku swala la mpasuko likishughulikiwa.

 14. Chris Says:

  Simply forum its a medium for open discussion or voicing of ideas. This discussion has added sthg that I didnt know.

  Thanx for Gervas, any and Bablii… Babli ntapataje hivyo vitabu UKWELI NI HUU and KIVULI KINAISHI…

  Cheers guys.. Long Live BC

 15. Amina Says:

  mmh mi nasoma tu hata sielewi kitu hapo ,ila nimeshukuru jana ilikua holiday sikwenda kazini

 16. Amina Says:

  Wajina una mambo!! kama hukuelewa ungewauliza Kina Gervas na Bablii kinachokutatiza ni nini; kwa hiyo umeridhika na kutokuelewa kwako??!! basi hukuwa na haja ya kuandika kitu…

 17. Anonymous Says:

  Tatizo ndilo hilo kama nilivyosema mwanzo la ubwana na utwana ambalo bado wako wanaoamini kuwa wao ni mabwana ni haki waliyopewa na Mungu kuwa mabwana, sasa haiwezekani watwana wakawatawala mabwana! Ndio maana sikutaka kwenda ndani zaidi ya hayo. Na kigumu ni hili suala la visasi na ushindani na ubishi usio na kichwa wala miguu. Era ile ya usultani ilishapita na Karume aliwalazaimisha watu wenye asili ya kiarabu waolewe na waafrika kwa nguvu na yeye alioa hao wenye asili ya kiarabu (mwangalie mwanawe na mjane wake) ili kuvunja ule uhasama wa matabaka mawili waone kuwa wao ni wamoja. Alitaka kuvunja hilo kwa kuwa na kizazi ambacho ni mchanganyiko wa mabwana na watwana. Huyo Bablii hawezi kukubali hata siku moja hiyo historia iliyoandikwa na weusi. Wengi mmesoma vitabu vya Adam Shafi na aliwahi kutolewa humu BC, lakini rudieni tena kuvisoma, ameandika kwa mtindo wa hadithi lakini ameelezea kwa mapana hali ilivyokuwa visiwani. Huyo sijui nani alifurushwa wakati wa mapinduzi ndio nasikia hapa kutoka kwa Bablii, lakini historia inatwambia Sultani aliyekuwa akitawala alikimbilia Dar wakati wa Mapinduzi na akaondokea Dar kurudi kwao.

  Ni kama vile suala la watusi na wahutu (kimfano tu wa visasi vya kikabila sio kihistoria) Na kama vile tunavyomkandya Mugabe (bila kujua kuwa kulikuwa na makubaliano ya serikali ya UK kuwalipa fidia walowezi na kuwarudisha huko walikotoka ili asilimia 90 ya Weusi wapate ardhi iliyokuwa ikishikiliwa na asilimia 10 ya wazungu (hapa ni mfano tu tunavyoshabikia ya Muafaka bila kutafuta undani wake) .

  Narudia tena mpemba ana mtazamo wake kuhusu mapinduzi (kuondolewa madarakani kwa nguvu bila ridhaa) na muunguja ana mtazamo wake kuhusu mapinduzi (kujikomboa kutoka kwenye utwana na unyanyasaji) na kila mmoja ataandika kulingana na tasfiri na mtazamo alionao kuhusu hilo suala.

  Kosa kubwa lilifanyika baada ya mapinduzi hakukuwa na reconcilliation ambayo ingeleta kusameheana na kuondoa siasa za visasi kuwa huyu alinifanyia hivi wakati wa utwana na huyu alinifanyia hivi wakati wa mapinduzi. Kungekuwa na tume kama ya Askofu Desmond Tutu ya South Africa ambako watu walipata nafasi ya kuyatoa moyoni yaliyowasibu na kupatanishwa na kusameheana.

  Na hata Kenya kama hakutakuwa na hii kitu ya kusameheana na kuendelea mbele badala yake watu wakakazania visasi, basi hata hiyo serikali ya mseto haitafaa kitu. The same applies to Zanzibar, lazima waingie katika hiyo process ama baada ya serikali ya mseto au kabla otherwise ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Wanasiasa wanatakiwa watibu majeraha ya zamani ambayo yako ndani ya makovu yasiyotaka kupona.

  Nyie hamshangai hawa wazanzibari asilimia kubwa ni dini moja, lakini hata hilo la kusameheana wao wahalioni kama ni sehemu ya dini, asiwadanganye mtu uislam una mweka kwenye daraja kubwa mwenye kusamehe hata Mtume Muhamad (SAW) alifanyiwa visa alipigwa, na mambo kadhaa lakini alisamehe hakuwawekea watu visasi miaka na miaka.

  Mwenyezi Mungu tunamkosea kila siku na mbali na kuwakosea wenzetu lakini hutusemehe makosa yetu mara tu tunapomuomba msamaha.

  Mwisho kwa sensitivity ya huu mjadala wapo ambao nitakuwa nimewakwaza, hivyo basi naomba wanisamehe kabla sijaomuomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa niliyoyaaandika kwa mkono wangu. Hii ni humility!

 18. Bablii Says:

  Chris…
  Hiki kitabu kiitwacho KIVULI KINAISHI mpaka 2000 Kilikuwa kinatumika kwa A’ elevel (watu wa lugha), na hichi UKWELI NI HUU, naskia mandishi amesimamisha uchapishaji wake, lakini ntajitahidi kukutafutia, nikijuwa kinapatkana wapi ntakujulisha

  Anon hapo juu unanichanganya, mara wasema aliepinduliwa ni muarabu, mara wasema wapemba wameondolewa madarakani bila ridhaa…! Ukweli utabaki pale pale Mohd Shamte alikuwa mpemba wa mtambwe -pemba (ambako ndiko anakotoka maalim seif). Usidanganywe, nisawa na uongo unaodanganywa kuhusu Idd Amin eti alikula nyama za watu!

  Kumbuka mtu akitaka kukudhuru huanza kukupa sifa mbaya kwanza, ndo maana hata mwizi hapigwi kwanza mpaka aitiwe mwizi mwizi ndo hufuata kipondo..!

 19. mie Says:

  Karume hakuzaliwa Mwera bali alizaliwa Malawi.Huko Mwera hawana nyumba wala nyumba.Aliingia znz akiwa amebebwa mgongoni na mama yake.Ila sio siri amefanya mengi ya maendeleo ambayo toka auwawe hakuna prezo hata mmoja aliefikia hata nusu ya aliyoyafanya.Pamoja na hayo aliuwa wengi ambao walionekana tishio kwake kama kina Hanga kwa kuwafunga mawe ya shigo na kuwatumbukiza baharini.siasa za znz ni ngumu mno.

 20. Albert Says:

  KWA WOTE WATOWA MAONI MNAKUMBUKA KULIKUWA KUNA MTU MMOJA KATIKA KESI YA UHAINI AKIITWA ME X NA MPAKA LEO HAKUWEZA KUTAJWA JINA LAKE LAKINI ALIKUWA ANAFAHAMIKA SANA NA IPO SIKU AMBAYO MMUNGU AMEIWEKA ATATAMBULIWA NA ULIMWENGU KUWA ALIKUWA NDIO MR X

 21. Amina Says:

  we unayeeita amin usinizingue mi nimeandika ninachojua sasa unaniambia nilikua sina haja ya kuandika kivipi?kwani wewe nani?

 22. Mama Says:

  Asante sana wachangiaji hapo juu. Pia asante Albert hapo juu kuhusu case ya uhaini huyu mtu (ME X) hadi leo nimekuwa nikufuatilia ni nani hasa (his true identity), lakini sijawahi pata jibu. Kuna mtu anayejua jamani labda atuambie???

  Hayati Abeid Karume alikuwa ni m-Malawi. Babu wa baba yangu aliwahi kuniambia kuwa Karume alikwenda Zanzibar kipindi kile cha biashara ya utumwa akiwa mtoto mdogo ila ndio hivyo inafichwa kihistoria. Wakati huo wanyasa wengi walikumbwa na hii biasahara haramu kama vile Tanzania bara ilivyoathirika. Ndio maana watoto wake wamesoma Malawi. Hata rais Karume aliyeko madarakani hivi sasa watoto wake pia wamesoma Kamuzu Academmy nchini Malawi. Hadi leo ukienda Unguja kuna baadhi ya familia wanakwambia asili yao ni wanyasa. Babu wa baba alizaliwa unyamwezini Tabora na kuchukuliwa utumwani (Unguja) na amefia huko 1989 akiwa na umri wa miaka 93.

 23. Chris Says:

  Ntashukuru sana Bablii….

 24. Anon Says:

  Visiwa vichache sana vina natives, vingi wakazi wake ni wahamiaji kutoka mainland kwenda kwenye hivyo visiwa hasa vikiwa visiwa vidogo, kwa mfano utawakuta wangazija na washirazi mafya (mafia) lakini si wangazija au washirazi tena washakuwa watu wa mafya, na hata visiwa vya Unguja na Pemba watu wa asili mbali mbali walihamia kwa shughuli za uvuvi na biashara hasa ya utumwa. Ndio maana kuna ishu ya ubwana na utwana. Lakini mbele ya Mungu watu wote sawa hakuna huyu aliumbwa kuwa bwana na huyu mtwana, mbora kati ya watu ni yule amchae Mungu!

 25. Rocky Says:

  Kwa historia yenye picha nyingi ziendazo na maelezo mafupi yenye kina kuhusu masuala ya kijamii, historia, kisiasa na maendeleo toka 1898 – 2008 (karne 2 yaani miaka 200) tembelea website: http://www.zanzibarhistory.org
  Humo kuna khabari zitakazo jibu kiu chenu cha majibu kuhusu visiwa vya Zanzibar

 26. Kekue Says:

  Jamani kuna watu wanajua mambo mengi huku!!!! He!! Big up sn, mi sina tofauti na Amina manake nilikuwa sielewi chochote, asanteni sana wajameni.

 27. junior Says:

  waheshimiwa anony na baslali nashukuru sana kwa michango yenu ambayo kwakweli siyo tu imenitoa ujinga kuhusu siasa za zanzibar bali imeubadilisha mwelekeo wangu wa kuwaona cuf ni washari,waroho wa madaraka nk nk
  Lakini ningeomba mrudi tena na mnifahamishe haya yafuatayo
  1.Kama mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni ya kumuondoa Mohamed shamte ambaye ni mpemba na nijuavyo mimi ni kuwa huyu bwana alikuwa waziri mkuu.je muundo wa serikali ya zanzibar kipindi hicho ulikuwaje?je kipindi hicho zanzibar ilikuwa ni monarchy na sultan ndiye alikuwa na kama kiongozi wa nchi na shamte ni mamluki tu?Na shamte kama waziri mkuu,je aliwaletea wadhira,manyanyaso nk nk yoyote watu wa unguja?
  2.Mnaweza kuniambia kwa nini mwalimu Nyerere alimpenda sana Dr.Salim A.Salim na hata kumpa vyeo vikubwa vikubwa wakati akiwa na umri mdogo tu na hata kumtaka awe Rais wa Muungano mara kadhaa ilihali wajumbe wa CCM zanzibar hawataki kabisa Dr.Salim awe rais wa muungano?
  Ntanguliza shukrani zangu


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s