BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JE NI HALALI AU BUSARA? April, 9, 2008

Filed under: In Memory/Kumbukumbu,Serikali/Uongozi,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 12:41 PM

Picha hii ilipigwa jijini Dar-es-salaam miaka hiyo. Kutoka kushoto ni Hayati Samora Machel aliyekuwa Rais wa Msumbiji, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Graca Machel aliyekuwa mke wa Samora Machel na Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa.

Kwanini tumeiweka hii picha hapa? Nia sio tu kumbukumbu bali ni kwa sababu msomaji wetu mmoja ameuliza swali ambalo tunadhani linahitaji maoni ya umma na sio ya BC pekee. Anasema kwamba; baada ya Samora Machel kufariki, mke wake Graca Machel(baada ya miaka kadhaa),alikuja kuolewa na swahiba wake,Mzee Nelson Mandela “Madiba” kitu ambacho kilimpelekea kuandika historia ya kuwa “first lady” katika nchi mbili tofauti.

Sasa mwenzetu anauliza;je ni halali au jambo la busara kwa mtu kumuoa mke au kuolewa na mume wa rafiki hasa kama ameshafariki kama ilivyotokea kwa Samora Machel na Nelson Mandela? Nini maoni yako?

Picha kwa msaada wa Issa Michuzi

Advertisements
 

29 Responses to “JE NI HALALI AU BUSARA?”

 1. Malenga Says:

  Mambo hayo!!! Jambo kama hilo linapotokea watu hulipa sura na mitazamo tofauti kulingana na wakati na mazingira yanayohusika kama sio wahusika wenyewe.Kumwoa mke wa marehemu rafiki yako kwa mila zetu haijatulia.(Ingawa sehemu nyingine ni kitu cha kawaida)Maana hapo inaonyesha wazi kuwa,ulikuwa unamtamani huyo mke toka rafiki yako akiwa HAI.Hiyo haileti tofauti sana na Kurithi ndoa ya kaka. kwa sababu wakati mwingine marafiki mkishibana mnakuwa kama ndugu kiheshima. Baadhi ya makabila ni jambo la kawaida.Kula ni kula mbaya kukomba mboga…

 2. michelle Says:

  Malenga, umesema kweli,inaonyesha kuwa mtu akimuoa mke wa rafiki yako au kuolewa na mume wa rafiki ambao ni wafu yaonyesha kuwa ulikuwa ukimtamani huyo mke wa rafiki yako ua huyo mume wa rafiki yake., huo ndo ukweli.!!!!!!!!!!!!!

 3. Bablii Says:

  Mie naona huyo alieuliza swali hana tofauti na wale wahindi wanaosema yule mtoto aliezaliwa na vichwa viwili ni mungu wao…!

  Kwani rais ni nani? Ukiwa rais unapunguwa au kuzidi nini katika ubinaadamu wako? Hivyo ni vyeo tu lakini havikuongezei kitu wala kukupunguzia kitu katika ubinaadamu wako, bado utahudhunika ukipatwa na chakuku hudhunisha, utaona njaa, utakwenda haja, utatamani, utapenda n.k

  Haina haja ya ku complicate vitu vya kawaida, eti mandela kumuowa mjane wa machel ni halali au busara? Kwa ufahamu wangu mie, Jambo lolote linaangaliwa katika mtazamo wa sura mbili 1. Kidini 2.Utamaduni wa jamii husika, sasa kuhusu Uhalali inategemea dini ya wawili hao jee inaruhusu? Jibu ndio, kwa hiyo ni halali
  Kuhusu busara, hapo ni vigumu kukubaliana, kama unaujuzi na elimu ya psychology (saikolojia), basi busara hazifanani!

  Mfano, wewe unaweza kuona ni busara kujisaidia njiani ukiwa umabanwa na haja sababu hutaki kuchafua nguo, mwengine ataona busara kujisaidia nguoni mwake sababu hataki kukera wapita njia na kuchafua mazingira..! You get a point? Kwa hiyo Busara ya Mandela na wife wake haiwezi au inaweza kuwa sawa na wewe (itakuwa sawa kama utakubaliana nawao)

  Kabla hujakitafsiri na kukidadavua kitu kiweke kwenye uhalisia wake kwanza!

  Umenisoma?

 4. Ed-USA Says:

  Suala hili BC linaangaliwa kulingana na mapokeo au mitazamo ya imani, tamaduni, mila na desturi.

  Mimi kama mkristo naliona suala hili halina wakulaumiwa au kuhukumiwa kati ya wahusika watatu yaani marehemu Samora, Craca na Mandela.

  Kikristo ndoa ni kwa waliohai, na mwanandoa anaruhusiwa kuoa ama kuolewa linapotokea tukio la kifo yaani kumpoteza mwenzi wake. Vilevile mwanandoa anaweza kuoa ama kuolewa iwapo ndoa imevunjika kutokana na yeyote kati ya wanandoa kufanya uasherati yaani kutembea nje ya ndoa. Hailazimishwi kuoa baada ya ndoa ya kwanza kufikia tamati, inakuwa ni uamuzi wa mhusika kama ataki kuishi maisha ya ujane n.k. Ukipima kwa mzani huu, wahusika wote watatu hawana hatia wala lawama. Kinachobaki ni vijimaneno vya wanadamu kama walivyojaliwa kuwa na midomo ya kupayuka watakavyo.

 5. eva moses Says:

  sioni ubaya wowote…mume wake alifariki….and on the wedding vows it says ’til death do us part’….so iliyo baki ni kuwatakia maisha mema.

 6. Ms Bennett Says:

  huyu mama graca ni mrembo sana huwa namfagilia sana,kweli nimeamini old is gold,mshono wa kitenge aliovaa mama graca kumbe ndo ilikuwa mishono ya enzi hizo,siku hizi wanawake wengi tukishona kitenge kwa chini sketi inakuwa kama aliyovaa mama graca.na mama nyerere pia kapendeza na dila lake,mi nilidhani kuvaa dila ni fashion ya siku hizi kumbe tangu enzi za kina mama maria nyerere.wanawake waafrika oyeeeeeeeeee

 7. Kimori Says:

  Inaonekana mama Graca Machel ni bomba sana na hata kupelekea Mandela na Mugabe hawaelewani mpaka leo….kisa – wote walitaka kumuoa Graca…haijatulia!

 8. Amina Says:

  Huyu Graca ingekua bongo ningemfananisha na wale mademu wanaopenda waimba bongo flava utakuta keshatembea na wanamuziki hata watano..kwa huyu namwita mpenda vyeo,anapenda maraisi..siyoo sawa kabisa

 9. Tonny Says:

  Aisee… mie nimezimia na kasuti ka Baba Wataifa kalikua bomba.. Tehehetehetekhe….

  Swala jingine mbona poa….. kama mtu anatembea na mke wa rafiki yake anaona bomba itakuaje ndoa hiyo ambayo hata dini inaruhusu.

 10. Matty Says:

  Mimi nadhani kidini inakubalika kama mumewe kafariki lakini kibinadamu ni aibu na si busara inaleta picha kuwa walikuwa wanatamaniana tangu mwanzo au labda walikuwa wanauhusiano wa kimapenzi kwa kuibia ndo maana wakaoana baada ya Samora kufariki.
  Haya Mama ushakuwa first lady wa 2countries!

 11. Kekue Says:

  Mi naona ni sawa kbs!!! ” alafu huyu Mama alikuwa mrembo usifanye masihara cheki Nyerere anavyomungalia!!! tehe tehe…..

 12. SARA Says:

  Mimi naona sawa, kwani mbona m2 anaolewa na binamu sembuse wao. acha hizo mz wangu c unajua tena mambo ya global

 13. salma Says:

  mh!!!!!!
  iyo kali

 14. Bongo pixs Says:

  Kwa mtazamo wangu nadhani hakuna kitu mbaya imetendeka hapo, sijui kama Madiba alikuwa anamtamani tangu zamani ila ukweli ni kuwa alikuwa jela kwa kipindi kirefu na alipotoka kakuta mambo ndivyo sivyo kwa bibie winnie, na papohapo bibie Graca yuko lonely na ndo wa adhi yake ati, sasa mlitaka aanze kutafuta viruka njia? na kwa umri na heshima yake si ndo ingekuwa balaa, Kidini na kibinadamu yaruhusu kwani hajavunja ndoa ya swaiba wake masheli jamani. kumbuka hata wake tulionao sasa tulianza kuwatamani ndipo tukajitosa na hatimaye tunao hadi leo, na wapo ambao pamoja na kuoa bado mwatamani na kutembea na wake za rafiki zenu bila aibu yoyote wakti hao maswaiba wenu wangali hai.

 15. Mswahilina Says:

  Huyu Mama Graca Machel naye ni Binadam kama wewe na mimi na anahitaji kutimiziwa vyote vya maumbile kama wewe na Mimi.
  Kuolewa kwake na Mandela baada ya Mumewe wa Kwanza Samora kufariki ni bahati yake na ndivyo alivyoandikiwa.

 16. mkereketwa Says:

  Wote hapo juu read your bible na Qur’an na vitabu vingine unavyoamini, mbona mambo ya ndoa yamewekwa wazi. Nani haramu na nani halali, ndoa inavunjikaje? kwa mauti au kutengana. Majibu yote mtayapata. Mimi ni Muslim! Talaka ikiishaandikwa basi halali kwa mtu yeyote yule kupiga goti kwangu na nikikubali imeswihi, ikiwa huyo bwana siyo haramu kwangu. Read your books guys! They did well kuliko kuendeleza boyfriend and gilrfriend ambayo haijahalalishwa kwenye kitabu chochote cha Mwenyezi Mungu!

 17. Makumbi Says:

  Hapana! hapana! kulikuwepo na urafiki wa mashaka, mandela hakupaswa kumuoa mke wa rafiki yake bali alipaswa kumsaidia kwa hali na mali kuhkikisha kuwa mke wa rafiki yake anabaki kama mama wa familia aliyoiacha marehemu. Hii ni wazi kuwa rohoni mandela alifurahia kifo cha samora, na ni wazi kuwa uhusianao wao ulikuwepo tangia samora akiwa hai! hapanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

 18. nyandaro Says:

  Jamani sidhani km walikuwa na uhusiano b4,ila naamini mtu akifa ina maana na ndoa pia imekufa,na huyo mama alikuwa hai vilevile ana mahitaji ya kimwili km binadamu mwingine na labda mtu aliyekuwa karibu nae akisymphathyze nae by then ndiye mzee madiba sasa angefanyaje,sidhani km kuna ubaya especially baada ya kuhalalisha.

 19. Kamanzi Says:

  Tatizo sana sioni kama lipo kwa hawa wawili kuoana, tatizo kubwa ninaloliona ni kwamba Mandeka kamwacha Winnie ili amuoe Graca. Haileti akili kwamba upo wakati huko nyuma Graca alimuita Winnie shemeji leo imegeuka mke mwenza? Najua Graca alitaka tu kujiongezea CV kwa kuolewa na Madiba.

  Kinachonikere ni kwamba kila mtu duniani anamtambua Mandela kama mtu mwenye moyo wa huruma na kusamehe ndio maana aliwaachia makaburu huru baada ya kuwa raisi. C ha kushangaza, mtu huyo huyo alishindwa kumsamehe Winnie baada ya kukosea. Mnafiki sana mzee huyu.

  Tuseme ukweli kwa wale tuliowahi kumuona Winnie, Graca jamani hafikii hata nusu ya uzuri wa Winnie. Nakumbuka walipokuja Dar baada ya Mandela kuapishwa uraisi, kila mwanamama Dar alianza kuchana, kuvaa na mitindo ya Winnie. Mwanamama yupo fiti hadi leo. PEACE N LOVE

 20. Gebo Arajiga Says:

  Ebwanaa Eeeh sipati icha inawezekana walitongozana kipindi marais hawa wakitembelea si unajua,basi baada ya kuona jamaa yake amefariki akaamua kuolewa naye ubaya mimi siuoni.

 21. tonny Says:

  Hakuna baya lolote lililofanyika hapo.Baada ya Mama Winnie Mandela kusakamwa sana na Makaburu kiasi cha kumfanya Mzee Mandela ashindwe kupata utulivu wa akili na hivyo kuhatarisha hata uongozi wake pindi tu alipofunguliwa kutoka gerezani,ilibidi yafanyike mahesabu makali hapo ili ionekane kana kwamba Mandela na Winnie wametengana kabisa.Swali likaja kwa umri ule alionao Mzee Mandela, na baada ya afya yake kutetereka sana alipokuwa kifungoni kwa kipindi kirefu sana nani atakaye ziba pengo lile la Winnie katika hafla za kitaifa na katika kufuta taswira iliyojengeka kwa makaburu kwamba huenda bado Mzee Mandela pengine alikuwa akiendeleza mahusiano ya kisiri na Winnie ambaye Makaburu walijaribu kumpakazia kwa kila hali ili aonekane hafai kabisa katika uongozi Afrika ya Kusini.Kimsingi,kwa umri ule mkubwa aliokuwa nao Mzee Mandela hakuhitaji Mke mwingine tena zaidi ya kuwa na wasaidizi tu wa kumtunza nyumbani.Mzee Mandela anao Mabinti wakubwa tu aliozaa na Winnie.So, there is no way these people can separate permanently the way Kaburus think!Mama Winnie bado anaheshimika sana Afrika ya Kusini na bado ana sauti kubwa sana katika Chama cha ANC hususan hivi sasa kikiwa chini ya Uongozi wa Jacob Zuma.Na inasemekana ni kutokana na ushawishi mkubwa sana alionao Mama Winnie Mandela katika safu za ANC(rank and file) kwamba aliweza kumfanya Zuma aibuke na ushindi mnono dhidi ya Tabo Mbeki.Wapo wanaosema kwamba kosa moja kubwa alilolifanya Mbeki hata kupoteza Popularity miongoni mwa wana ANC ni kupuuzia nguvu ya kisiasa aliyokuwa nayo Mama Winnie Mandela.Kwa hiyo ili kumfanya Mzee Mandela aendelee kupewa heshima yake kama BABA WA AFRIKA chaguo la Mama Graca Machel halikufanyika kimzahamzaha hivi kama wachangiaji wengi walivyo fikiria.Kwanza kwa usalama wake mwenyewe na ili kulinda hadhi yake Mzee Mandela kumpata Mama mwenye umri mkubwa na mwenye sifa za kukabiliana na hulka za uongozi wa ngazi ya juu, Mama aliyeyafahamu fika mazingira ya kisiasa Afrika ya Kusini, pamoja na sifa nyinginezo yote hayo kwa pamoja yalimfanya Mama Graca Machel awe chaguo pekee.Siyo sana kwa sababu Mzee Mandela alihitaji Mke bali kwa sababu muhimu zaidi ya KUMPATA MWENZA WA KUMFARIJI NA KUZIDI KUMPA MATUMAINI ZAIDI MZEE WETU NELSON MANDELA. Ikumbukwe kwamba Msumbiji ilitoa mchango mkubwa sana katika ukombozi wa Afrika ya Kusini.Kwa hiyo Mama Graca Machel alipewa heshima kubwa sana Afrika ya Kusini kwa sababu hiyo.Hakuna aliye ombea awe mjane.Na hakuna aliyetambua huko nyuma kwamba itakuja tokea siku moja akaolewa na Mandela.Lakini yote ni mipango ya Mungu.Tuwaombee waishi kwa usalama na Mungu amlinde Mzee Nelson Mandela.

 22. Gervas Says:

  Woooote naona mnabwabwaja tu, hebu kwanza tazameni umri wao!! jamani nauhakika kabisa majogoo yao wala hayawiki. huko kuwowana ni kwa ajili ya heshima tu ya kukaa pamoja na kuondosha upweke. Mandela Katoka jela kachoka, karudi kakuta Winnie ameshakandamizwa na tujamaa mtaani, wala hawakuwa na uhusiano. Kwanza mandela alifanya poa maana Graca alikuwa anamajozi ya kuomboleza kitu ambacho kingemuua haraka, mandela nae alikuwa na Presure za jela. Hivo wadau ndoa yao wazee hawa wala sio ya kukandamizana kama wengi mnavofikiria, nii kufarijiana tu. Big up Madibaaaa!! Madiba akifa, Mugabe anaendeleza libeneke.

 23. Mzalendo Says:

  Jamani tuache mambo ya udaku usio na maana, hivi lini tutajifunza kujieleza kwa point?

  Ni pointless kuhusisha suala la ndoa ya mandela na shinikizo la makaburu, kwa ushahidi upi? Tunafikia kupotosha tunapofikiri Mandela na washauri wake walikosea kwa uamuzi waliofikia. Inaonekana ni kama walikuwa wababaishaji na hilo sio kweli. Jamani, Winnie alikuwa na mwanamume mwingine wa pembeni (inawezekana zaidi ya mmoja) kama taarifa zilivyokuja kugundulika baadaye. Labda hakuwa na kosa baada ya kujua mume wake amefungwa maisha na hakuna matumaini ya kuja kuishi kinyumba.

  Anayemshutumu Mandela kukosa msamaha kwa Winnie nafikiri anachemsha. Kusamehe inategemea na mazingira ya kosa. Ni suala zito sana hili na inaonekana Winnie alifanya uamuzi binafsi na kumficha mzee wakati akimtembelea gerezani. Kwa nafasi nzito kama aliyokuwa nayo mandela (rais wa nchi), ilibidi busara kubwa ifanyike kusawazisha mambo. Kuna watu humu wanaliangalia hili suala kwa mtazamo wa tendo la ndoa zaidi. Nafikiri kwa umri wa wahusika kilichoangaliwa zaidi hapo ni heshima. Na hata baada ya yote kutokea, mandela ameendelea kuheshimiwa duniani kote isipokuwa kwa wadaku wachache.

 24. Chimo.Rabat Morroc Says:

  Wachangiaji Wezangu Mmechangia mengi na wako waliochangia vizuri wengine wametumia Busara tena wengine Busara zaidi ila kuna waliotumia Jazba, Nimewahi Kusoma Jarida Moja La ki belgiji miaka ya mwisho mwa tisini kulikuwa na Makala yenye kuelezea Ukweli na Undani Wa Mtafaruku Wa Maisha Ya Bi. Winnie Mandela kuwa wakati mheshimiwa anatumikia kifungo alikuwa ana mahusiano Nje ya ndoa yake pia likizidi Kuchambua Jarida hilo Lilibainisha Kuwa Mheshimiwa Mzee Wetu alikuwa hawezi kusukuma tena Mashine(inaelezewa kwa undani Kuwa Gerezani yeye na wenzie kina Walter Sisulu walipata Mateso makubwa kutoka kwa Makaburu )kama ni Graca kihistoria Mandiba alishakamatwa wakati anaolewa na Hayati Samora je ni Wapi hapo alipomtamani? Na Amini kuwa Bi. Winnie bado ana Mvuto kuliko Bi. Graca ila inategemea je Ni yupi kati yao bado anaitamani Na haja Tosheka na Dunia. Kilichotumika Kwa Hao Wawili Ni Kusitiriana Na Kufarijiana tu. Nadhani Mheshimiwa licha Ya kuwa mwenye Wingi wa hekima pia ana washauri Wengi Waliomzunguka Angetaka Kupata Mashine Bomba ya Kuendesha angepata ila hakuwa na nia hiyo Kweni haoni Kama ana mabinti wakubwa Leo akatafute Msichana Rika ya Dzi dzie Sio Zake Ubaya Huwezi Kuwa Kiongozi Wa Taifa Kubwa kama ilivyo RSA Kisha Status yako huna Mke Mzee Mandela Sio Kama Alivyo Mugabe mpaka leo anacheza kitandani na Mke Kama Binti yake. Hayo Ni ya kumwachia Mfalme Muswati wa Swaziland Na sio Wazee wetu hawa Wanaopaswa Kuwa Mfano kwa Jamii

 25. zawad haji Says:

  mhhhh….!!!!!!!!!!! mi naona shwari tu kwani huyo alikuwa mjane ana haki ya kuolewa. wacha waburudishane kwa raha zao wazee wa watu.

 26. mtuya Says:

  mimi naona poa tu.hao ni watu wazima pia walijiuliza kabla ya kufanya hivyo bila shaka, hata naona maoni ya yatakuwa mengi na yenye kutofautiana kulingana na mila na destuli za kila mdau;mbona ni muda sasa tangu mzee Mandiba na mama Graca wameoana sio wasauz wala Mozambique wame wamehofu au kutilia shaka jambo hili. mia naona pooooowa tu.

 27. Ncha ya Kisu Says:

  Haya Maswala tusiyajadili katika mtazamo kitoto
  Nakumbuka mzee Madiba Mwenyewe aliwahi kuulizwa swali hilo na akaweka wazi Mzee wa watu!kuwa yeye ni binadamu kama wanadamu wengine !na ujana wake akuweza Ku enjoy Uraiani kama vijana wengine bali JELA! Baada ya kuachana na mkewe,hilibidi avute jiko yaani kuoa mke ambaye ana Historia na uzoefu kidogo unafanana naye! yaani MKE ambaye alikuwa au amewahi kuwa mpambanaji! Na Bi.Graca Simbine a.k.a Graca Machel sifa hiyo anayo,pia si mgeni katika ugumu wa maisha na mengi kisha yaona,hapakuwa na ubaya wowote ule kuhunganisha udugu Katika ya Mzee Madiba Na Bi.Graca Simbine

 28. mpogolo Says:

  Huyu jamaa wa usalama mwenye miwani mieusi si Mizengo Pinda? wadau saidieni?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s