BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BOB SANKOFA NA FOTO BARAZA April, 10, 2008

Filed under: Blogs,Mahusiano/Jamii,Marafiki,Photography/Picha — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ukimuita celebrity, Bob Sankofa atatabasamu tu kama sio kuangua kicheko kabisa.Haamini sana kwenye suala zima la u-celebrity.Anaamini zaidi kwenye kazi na kufanya kile mtu unachokipenda kutoka moyoni. Pamoja na kukataa kwake kuvishwa kofia ya aina yoyote ya u-celebrity, kama wewe ni mfuatiliaji wa maendeleo ya watanzania mtandaoni na mpenzi wa kuona au kutizama picha, basi jina la Bob Sankofa litakuwa sio geni. Huyu ndiye mmiliki wa ile blog makini ya picha iitwayo Mwenye Macho au kwa kifupi MM.

Jina Bob Sankofa sio jina lake halisi lakini ndio jina ambalo siku hizi limemkaa zaidi. Jina lake halisi ni Philemon Msangi. Yeye ni mwanafotografia, mtengeneza filamu, mjasiriamali na zaidi ya yote ni mwanablogu.Siku chache tu baada ya Zimbabwe kupata uhuru wake,Bob alizaliwa.Usihangaike kupiga hesabu,alizaliwa 29/04/1980.

Ingawa blog yake iliyosheheni mapicha hajaifunga(anadai lazima iendelee kuwepo) hivi karibuni Bob amekuja na kitu kinachoitwa FotoBaraza. Kumbuka Bob ni mpenzi wa kutupwa  wa sanaa ya picha.Akiona picha nzuri, anaweza kuitizama mpaka macho yaanze kumuuma ndio atashtuka na kuendelea na shughuli zake zingine.

Bob anasema FotoBaraza ni aina mpya ya mtandao.Ni vuguvugu jipya.Ni mahali pengine ambapo wanajamii wanakutana na kupasua hoja mbalimbali, kutizama na kuweka picha, kupiga soga, kuzungumza Kiswahili na zaidi kuunganishwa na wanajamii wengine kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.Jamii inaunganishwa na FotoBaraza.Kwa kuzingatia jinsi ambavyo upigaji picha siku hizi umetawala(hususani tangu ziingie simu za viganjani zenye kamera), Bob anasema FotoBaraza ni kitu muafaka kabisa katika wakati unaostahili.

Basi tusiseme mengi sana.Kwanini usitembelee FotoBaraza na kujionea mwenyewe na pia kujiunga na wanajamii wenzako? BC inatoa hongera kwa ubunifu wa namna hii. Bonyeza hapa utembelee FotoBaraza.

 

 

 

 

 

Advertisements
 

7 Responses to “BOB SANKOFA NA FOTO BARAZA”

 1. Kamtu Says:

  Hongera sana Bob,tuko pamoja

 2. mie Says:

  ua handsome bro

 3. Tonny Says:

  Mie naona umemzimia Bob.. mpatie agonge tehetehehekhetekhe……………………………

 4. asaki Says:

  kaka unasmile zuri

 5. Dinah Says:

  kazi nzuri hata meno na kucha zake nzuri pia 🙂

 6. SIYA Says:

  nakwambia kuna vimilupo humu videmu vya bongo flava vimehamia na kwa bob…mmmh

 7. Winfrida Says:

  Hallow Bob!

  Congratulations you have made it.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s