BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“DUNIA MSONGAMANO”-NDALA KASHEBA April, 11, 2008

Filed under: Burudani,In Memory/Kumbukumbu,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni ijumaa nyingine tena. Kama kawaida yetu ni wakati wa kupumua kidogo na kutafakari yaliyojiri na kupanga yajayo hata kama hatuna uwezo kamili wa kujua yatakuwaje.Ni mipango tu.Bila mipango hakiendi kitu.Ni wakati mwingine wa burudani. Leo tunayo heshima kubwa kumkumbuka Hayati Freddy Supreme Ndala Kasheba(pichani). Huyu ni miongoni mwa magwiji wa muziki ambao Tanzania imewahi kuwa nao.

Wimbo unaitwa Dunia Msongamano. Ndala Kasheba hapa alikuwa na kundi zima la Orchestra Safari Sound. Ujumbe uliomo ndani ya wimbo huu, kama binadamu yoyote akiuzingatia, ni wazi kwamba kuna mambo fulani fulani ambayo atayaepuka.Migongano mbalimbali tuliyonayo wanadamu, kuanzia kimawazo mpaka kivitendo ni kwa sababu wengi huwa tunasahau kwamba kila mtu ana akili zake.Kizuri kwangu, kibaya kwako na mambo kama hayo.

Hapo chini ni baadhi tu ya maneno kutoka kwenye beti za kwanza kwanza za wimbo Dunia Msongamano. Zisome kwanza kisha bonyeza player hapo chini uusikilize wimbo wenyewe. Ijumaa Njema. R.I.P Ndala Kasheba.

 

DUNIA MSONGAMANO
Mawazo yamenijia leo,
Ya Mzee wangu alokuwa akisema,
Dunia ni msongamano wa watu wenye akili tofauti,

 

Ukitaka kuishi vema fikiri kabla ya kujibu,
Jifunze kwa walimwengu, na walimwengu wajifunze kwako,
Dunia ni kuona mambo,
Na halafu kuyasahau

Wengine hupendelea kufurahia,

Wanaposikia fulani kafa,
Kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu,
Namuomba Mwenyezi anipe maisha ooh 

Advertisements
 

10 Responses to ““DUNIA MSONGAMANO”-NDALA KASHEBA”

 1. Ed Says:

  Thanks Mr. Muandishi, weekend yangu imeanza taratibu kabisa. Naomba special request, ya kutuwekea hivi vibao halisi kabisa vya kitanzania kila Ijumaa. Kwani vinatukumbusha mbali sana

 2. salma Says:

  big up!!!!!!!!!!!!!!! babu

 3. tonny Says:

  Ndalla Kasheba was the Carlos Santana of Bongo!.Jamaa alikuwa Genius wa kupiga Solo Guitar.Mungu amlaze pema peponi!Tutaendelea kuuheshimu mchango wake katika kuendeleza Muziki Tanzania.Kwa wale watakao kumbuka pilikapilika za pale Safari Resort Kimara miaka ya themanini mwanzoni hakika watakuwa na majonzi makubwa wakisikia jina la Kasheba likitajwa.Marquies WHITE HOUSE UBUNGO, Ndalla Kasheba na SAFARI SOUNDS safari resort Kimara, Michael Enock na DDC MLIMANI PARK Kinondoni ilikuwa Golden Triangle ya Burudani enzi zile! Hata kama ulikuwa na KISUKARI kilishuka! acha nicheke…! If History was anything, the Present should have come from the Past………..Ndalla Kasheba, Supreme, the Soloist Maestro……he really loved and cherished Tanzania……GOD BLESS YOUR SOUL!Kina King Kiki, Assossa, & Co msikate tamaa hakikisheni vipaji vyenu vinasambaa kwa vijana wanao chipukia. NGUZA VIKING namuombea kwa Mungu busara itumike ili siku moja naye ajikute yuko huru na kuendeleza utamaduni wetu. Ikiwa Mwenyezi Mungu anaweza kusamehe, iweje Binadamu akufuru hilo agizo?

 4. kwa kweli wimbo huu umenikumbusha mbali sana, wakati huo tanzania tulikuwa tukijivunia utajili wa vipaji vya muziki. ndala kasheba alikuwa anatisha sana kimuziki na hasa alipokuwa akilichalaza lile gitaa la nyuzi kumi na mbili. nyimbo hii ya dunia msongamano imejaa ujumbe mkubwa juu ya maisha yetu na jinsi wanadamu tusivyopendana. inafikia wakati watu wanafurahi wanaposikia mtu fulani kafa.

  Wimbo huu kasheba aliutunga mara baada ya kutoka hospitali alipokuwa amelazwa kwenye miaka ya mwishomwisho ya 80 wakati alipokuwa amelazwa , habari zilisambazwa kuwa amekufa, ilikuwa habari kubwa wakati huo. na ndipo baada tu ya kupona akaibuka na tungo hiyo,wimbo huu ulitingisha kweli kweli na ulikuwa unapigwa kalibuni kila siku na RTD ambacho kilikuwa ni chombo pekee cha utangazaji tanzania.

 5. Asante sana ndugu yetu kwa kutupa hizo kali za zamani, ila nimesoma huo wimbo dunia msongamano halafu nikausilkiliza nimeona umesahau beti moja kama sikosei inasema hivi”matatizo mengi yamenikuta maisha nusu nimeishapata naelekea uzeeni sasa lazima niwe na utulivu kwani kuishi kwingi nikuona mengi”
  asante kwa kutupa hizo endelea kaka
  mdau kutoka uk

 6. Saidi Situ Says:

  Naona Mkongwe akiwa kazini. Hawa wasanii wa namna hii vipi? Mbona wameacha kuwika kama zamani au viwango vyao vidogo ila tu walikuwa wanabebwa na Radio Tanzania?

 7. DUNDA GALDEN Says:

  Kufa kwa binadamu hupangwa na mungu iweje binadam ufarahia?hayo yalimkuta ndugu na jamaa zangu kule Bongo nyumbani walipofurahi kufa kwa mzazi(…………..)ili wapate kugawana mali hakika sisi binadamu tufinyu sana na fikila sasa
  hamna mali watu wamebaki kama walivyo zaliwa ahsante BC kwa hicho kibao kwani yalinikuta kwenye familia yangu mungu mpe uhai mrefu Baba mzazi hapo bongo kweli ulisema kuwa uyane kama kibao hiki kinavyosema I MISS HOME MUSIC.REAL THAT WAS MUSIC KWELI HII IJUMAA
  CHAFOSA CHAI GODA (DARWIN AUSTRALIA)

 8. Juma Kitunguu Says:

  Mdau hapo juu, huu wimbo haukutungwa mwishoni mwa miaka ya themanini. Wimbo huu ulitungwa mwanzoni wa miaka hiyo yaani mwaka 1984 na ulikuwa katika ile albam ya “Marashi Ya Pemba.” Kuna ndugu yangu fulani alikuwa anafanya kazi pale RTD alinitepia hii albamu wakati huo, nasikia haibu kusema kwani sikumlipa Kasheba kwa kazi yake. Hii albamu ilikuwa na nyimbo 6 zifuatazo: Marashi Ya Pemba, Ma-Cele, Asha Said Mwita, Dunia Msongamano, Garba, na Ntale. Duh miaka inakimbia kweli yaani naona kama vile jana tu wakati nilipokuwa nakula hizi starehe toka RTD. Huku Kasheba na Safari Sound wakitamba na Garba pamoja na Hasira za Chunusi, Maquis nao walitamba na Milionea wa Mapaenzi pamoja na Karubandika. Nginde nao walikuwa na Hiba, Pata Potea, Pesa Part I & II, Mnanisengenya Bure, na taifa kubwa Msondo walikuwa na Fatuma, Pamela, Ama Zake Ama Zangu….Wazee wa kazi Bima Lee walikuwa na Imaculata, Flosie, Tujemaso, Fungua Macho, n.k. wakati jabali naye alikuwa na Dunia Uwanja wa Fujo, na Mwanameka…dah Mungu ibariki Bongo yetu! Kwa sasa Fleva ndio inaua kabisa vipaji vya wasanii Bongo kwani hawana mwelekeo.

 9. Mswahilina Says:

  B.C., mmenikumbusha mbali sana. Endeleeni vivyo hivyo.

 10. Asante sana mdau mwenzangu kwa kuweza kukumbuka mwaka rasmi wa kibao hicho cha dunia msongamano. sikukosea sana maana ni miaka hiyohiyo ya 80. kwa kweli wakati huo ndio kulikuwa na muziki bwana.
  Sijui kwa nini wanamuziki waliobakia awaendelezi libeneke. mungu aiweke roho ya marehemu Ndala kashebe mahali pema peponi-AMINA.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s