BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JAMILLA NA MISS TOURISM QUEEN INT’L. April, 11, 2008

Filed under: Fashion,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:14 AM

Juzi huko kusini mwa China katika mji wa Zhengzhou uliopo katika jimbo la Henan, kulifanyika mashindano ya urembo yajulikanayo kama Miss Tourism Queen International 2008. Mashindano yalifanyikia ndani ya ukumbi wa Zhengzhou International Vonvestion & Exhibition Centre. Mji wa Zhengzhou upo umbali wa kilomita takribani 680 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo wa Beijing.

Tanzania ilikuwa inawakilishwa na mrembo wetu Jamilla Juma Munisi.Hata hivyo Jamilla hakufanikiwa kufua dafu katika mashindano hayo ambapo mshindi aliibuka kuwa mrembo kutoka Peru aitwaye Silvia Cornejo.Peru ni nchi ndogo tu iliyopo katika bara la Amerika ya Kusini.

Mshindi wa pili alikuwa ni Miss China, Tong He na Miss Canada, Sahar Biniaz, alikuwa mshindi wa tatu; Miss Montenegro, Dasa Zivkovic, alikuwa wa nne; na watano alikuwa, Miss Japan, Akemi Fukumura.

Pichani Mrembo wa Tanzania, Jamilla Munisi(kushoto), akiwa na mrembo kutoka Rwanda, Karine Rusaro Utamuliza, ambaye pia alishiriki mashindano hayo pindi yalipomalizika hiyo jusi.Hii ni kumaanisha kwamba safari ya Tanzania katika anga za kimataifa za mashindano ya urembo bado inasuasua. Tutafika tu siku moja.Au vipi?Kwa habari zaidi kuhusu mashindano haya tembelea tovuti yao rasmi kwa kubonyeza hapa.

 

Advertisements
 

4 Responses to “JAMILLA NA MISS TOURISM QUEEN INT’L.”

 1. Gervas Says:

  Waa-waaa!! Jamila kwa kupeperusha bendera yetu na jina Tanzania kwa mara nyingine tena beyond borders, nafikiri wandaaji wanapata changamoto mbali mbali kwa kushiriki, tatizo nafikiri hawatoi feedback kwa wadada wanaochipukia (public) ili wajiandae kuzikabili changamoto hizo. Kama kamati ya urembo itakuwa inapita mikoani au kwa kutumia tu vyombo vya habari kutoa elimu kwa wadada wanaokuwa wanaweza wakadevelop interest na kuwa na sifa zitakikanazo. Nafikiri tatizo letu bongo kama tunavofanya kwenye fani zingine, soka, urembo, models na michezo kwa ujumla ni kwamba tunapiga tizi gumu miezi miwili kabla ya kwenda kwenye mashindano, badala ya kuanza kuandaa washiriki tokea wadogo. Jamila hongera saana ulipofikia.

 2. trii Says:

  jamani wala mi sikuwa na habari kama kuna mrembio kaenda kushindana,jamani waandaaji tangazeni tuwajue warembo wetu.

 3. jamy Says:

  Congraturation!!!!!!!!!!!

 4. solange Says:

  nimependa weusi wako dada jamila…..hongera na usikate tamaa.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s