BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MORANI SITA NA LONDON MARATHON April, 12, 2008

Filed under: Tanzania/Zanzibar,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:59 AM

Kama kuna watanzania ambao hivi sasa wanaitangaza nchi yetu kimataifa basi hao si wengine bali vijana/morani sita wa kimasai ambao wanatarajiwa kushiriki mbio za Marathoni za London(London Marathon) kesho tarehe 13 Aprili,2008 jijini London nchini Uingereza.

Morani hao wa kimasai ambao watashiriki mbio hizo kwa ajili ya kuchangia miradi ya maendeleo huko kijijini kwao kaskazini mwa Tanzania wamekuwa kivutio cha aina yake na gumzo lisiloisha.Hivi karibuni walifanyiwa mahojiano na kituo maarufu cha televisheni cha Al-Jazeera.Tizama mahojiano hayo katika video hiyo hapo chini. Bonyeza hapa usome jinsi mojawapo ya magazeti ya huko Uingereza yalivyoandika kuhusu morani hawa.BC inaungana na watanzania wote kuwatakia ushindi.Shukrani Pius Mikongoti kwa video hii.

 

 

     

Advertisements
 

12 Responses to “MORANI SITA NA LONDON MARATHON”

 1. Mswahilina Says:

  Vizuri sana.
  Watanzania tunaweza.

 2. Subby Says:

  Mmm huo mwimbo na hiyo sauti inabidi waimba Opera wa UK wakajifunze kwa wamasai kuimba!

  Hongereni kwa kuchangisha pesa kwa ajili ya maji kijijini kwenu, mmefanya jambo la maana kwa jamii yenu!

 3. Wow! Very beautiful! I am wishing them luck on the race.

 4. eva moses Says:

  ok, good luck all.

 5. Pope Says:

  Kweli nimeamini kidhungu ni kukaza na kulegeza ulimi,Jamaa kajieleza vizuri sana, Hongera Akwii

 6. Ram Says:

  hapa inafaa wapewe hongera wamasai kwa kuweka mila zao na tamaduni zao pamoja na lugha yao na zikawa leo zinatambuliwa katika kila kona ya duni jengine baya zaid ni makabila mengi hivi sasa Tanznaia yamepoteza mila na tamaduni zao kwa kufuata mtu fulani kuwa mbia kuwa eti sio nzuri muwache na muwe na kiswahili tu ule ulikuwa ni uporaji kumpora mtu sehemu ya maisha yake , wazee mliokuwa hai sasa jaribuni kuwafunza vijana mila na lugha zenuza kikabila kwa wale wenye makabila na faida zake itaonekana huko mbele ukizingatia ulimwengu wa sasa watu wanarudi katika mila na mambo ya nyuma

 7. Dullah Says:

  Michelle, Upoo!! Nasubiri maoni yako kuhusiana na hoja ya kabila letu. Talk 2 u later.

 8. DUNDA GALDEN Says:

  KILA LA KHERI
  BAADHI YETU WATAKUJA KUWASINDIKIZA
  NA KUPEPELUSHA BENDERA YETU
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
  DARWIN_AUSTRALIA

 9. Msanii Says:

  Are there some subtle condescending undertones in this interview or is it just me?

 10. Kurwa Says:

  Safi sana.
  Lini mtawatangaza katika Marathon za nchi nyingine, hasa zile kubwa na maarufu zinazokusanya habari na kuonekana dunia nzima pia – kama Boston Marathon, Newyork Marathon na Tokyo Marathon- ili pia wachangishe fedha na kukuza utalii wetu.
  Nimefurahi sana.

 11. annabell Says:

  honestly am proud of them, at least tanzania inazidi kujulikana, nilisoma kwenye gazeti la daily mail la uzunguni mwandishi mmoja akaandika eti hao wamasai wameombwa wavae chupi wakati wa kukimbia kwa sababu za kiafya!!! eti wasipate michubo!! eee nikajisemea ata hii dili uku ugaibuni….siri hazarani….
  big up much…..tanzania is my IDENTITY!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s