BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MWENGE WA OLIMPIKI KUTUA DAR HIVI LEO. April, 12, 2008

Filed under: Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:59 AM

Mwenge wa Olimpiki unatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-salaam leo usiku ukiwa katika mfululizo wa mbio zake ulimwenguni. Tanzania ni nchi pekee barani Afrika ambapo mwenge huo utakimbizwa.Kimsingi, Tanzania imepewa heshima kubwa na nafasi nzuri ya kujitangaza ulimwenguni kwani leo hii vyombo vyote vya habari vya kimataifa vinaangalia jinsi gani mwenge huo utapokelewa nchini Tanzania.Je tutaitumia fursa hii ipasavyo? Hili ni suala la kusubiri na kuona.

Hata hivyo, mwenge wa olimpiki mwaka huu umekuwa ukikumbana na upinzani mkali kila ulipokwenda kutoka kwa waandamanaji na wanaharakati wa haki za binadamu. Hii ni kutokana na China(ambao ndio waandaaji wa michezo ya olimpiki mwaka huu) kushutumiwa vikali kwa kuwa na rekodi mbovu linapokuja suala zima la kuheshimu haki za binadamu.Chachu ya mambo yote haya ni kutaka kujitenga kwa Tibet ambayo mpaka hivi inahesabika kuwa ni sehemu ya China.China haitaki Tibet ijitenge.

Viongozi mbalimbali ulimwenguni wametishia kususia sherehe za ufunguzi wa michezo ya olimpiki mwaka huu endapo China haitakubali kimsingi kurekebisha rekodi yake ya haki za binadamu.

Wakati huo huo, mshindi wa tuzo ya Nobel, mwanamama/mwanaharakati Wangari Maathai kutoka Kenya ambaye alikuwa awe miongoni mwa wakimbizaji mwenge wa olimpiki hiyo kesho jijini Dar-es-salaam amejitoa. Wangari Maathai amejitoa ikiwa ni harakati zake za kuunga mkono wanaharakati wenzake duniani katika kuitaka China iheshimu haki za binadamu. Bonyeza hapa usome alichokiandika kuhusiana na kujitoa kwake.

Je, watu wetu maarufu wanaotarajiwa kuwa miongoni mwa wakimbiza mwenge huo kesho jijini Dar-es-salaam kama vile Prof.Anna Tibaijuka na wengineo nao walitarajiwa au walitakiwa kujitoa? Vipi kuhusu msimamo wa serikali yetu kuhusiana na suala zima la China, olimpiki na Tibet?Maoni yako tafadhali. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na mbio za mwenge wa olimpiki jijini Dar,bonyeza hapa.

Pichani juu ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar-es-salaam, Alfred Tibaigana, akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar-es-salaam kuhusiana na suala zima la utaratibu na ki-usalama wakati wa ukimbizwaji wa mwenge huo kesho.Kushoto kwake ni Prof.Anna Tibaijuka,Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa(UN Habitat) na Mstahiki Meya wa jiji la Dar-es-salaam,Alhaj Adam Kimbisa.

Advertisements
 

One Response to “MWENGE WA OLIMPIKI KUTUA DAR HIVI LEO.”

  1. Mateka Says:

    Sitatoa maoni kuhusu uhalisi wa madai ya Tibet, lakini nahusunika kuwa swala la awali la kupinga juhudi za china juu ya Darfuri limesaulika. China kama Mataifa ya Magharibi Imeamua kuweka mahitaji ya kiuchumi mbele ya maisha ya Mwafrika.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s