BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 15 April, 13, 2008

Filed under: Photography/Picha,Tanzania/Zanzibar,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:29 AM

Sehemu ya jiji letu la Dar-es-salaam.Kwa wengine jiji hili ni tamu kuliko mfano wakati kwa wengine(walio wengi) jiji hili ni chungu pengine kupita shubili.Nani wa kulaumiwa?Wengine wanasema inategemea tu unajua vipi kuzichanga “karata” zako.Wengine wanasema inategemea unamjua nani.Wengine wanasema inategemea unatoka katika familia au ukoo gani.Wengine wanasema yataka zaidi ya “bahati”.Wewe unasemaje? Hii ndio picha yetu ya wiki hii.¬†

Advertisements
 

7 Responses to “PICHA YA WIKI # 15”

 1. Gervas Says:

  Kwangu jiji ni chungu, hasa ninapofikiria yafuatayo;
  1. ikifika saa kumi na mbili afu upo kariakoo au Posta au unataka kujimuvuzisha home mbagala/gongolamboto.
  2. ninapoamua kulala bila kuoga sababu tu ya ukosefu wa maji, au maji yanayochotwa miferejini na kuuzwa mia tano kwa ndoo.
  3. Tokana na uchovu hapo juu, naamka asubuhi nakugundua kuwa vibaka wamebomoa dirisha na kunipora vitu.
  4. Utamu wa jiji kwangu unabaki ndoto haswa ninaposoma taarifa kwamba watu niliowapa dhamana ya kuniletea haya maendeleo ndo kwanza wahusika wakuu walio kunywa uji wa mgonjwa na akafa.

 2. changalamacho Says:

  Jiji la ‘BONGOLALA’! Aliyesema Bongo hakumalizia alikuwa anatuheshimu tu.Nakuhakikishia zaidi ya nusu ya wakazi wa jiji hilo wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.Zaidi ya robo tatu ya jiji ni makazi ya ‘Squatters’.Pato la Wastani la kila siku kwa kila mkazi ni chini ya Dola Moja ya Marekani japokuwa wapo Matajiri wachache wenye utajiri wa kupindukia.Ni jiji tegemezi ambalo halijitoshelezi lenyewe kwa mahitaji yake,mahitaji mengi ni kutoka nchi za ughaibuni.Viwanda vingi(kama vipo) vinazalisha kwa kiwango cha chini sana tena kwa gharama kubwa na mishahara ya wafanyakazi ikibakia kuwa duni na isiyokidhi mahitaji.Ongezeko la watu ni kubwa zaidi kuliko ukuaji wa uchumi na ongezeko la huduma za kijamii.Bandari ndiyo tegemeo kubwa la mapato ya ushuru serikalini kwa bidhaa zitokazo nchi za nje.Hakuna anaye jali kinacho endelea nchini au hatma yake kwa vizazi vijavyo.Hakuna anaye jali ajira kwa vijana wetu wanaomaliza masomo yao itatoka wapi kwa mwenendo huu wa ukuaji wa uchumi.Kila mfanyabiashara atataka awe na hifadhi ya mapato yake katika dola za kimarekani lakini siyo katika shilingi yetu wenyewe.Hiyo ndiyo Bongolala au jiji la Dar es salaam.Hata nchi zilizo gubikwa na machafuko ya kisiasa na tukazisaidia sisi wenyewe kurejea katika hali ya kawaida kiutawala hivi sasa zimepiga hatua kimaendeleo na kutuacha wenyewe tukiendelea kushangaa na kupigana ‘siasa za danganyatoto’!

 3. DUNDA GALDEN Says:

  Kweli Bongo land.wengine huliita kila aina ya jina yote katika kulisfu jiji hilo ikiwa kwa wema au ubaya.mimi nimezaliwa na kukulia hapo jijini kati na kindimbwi ndibwi cha jiji hilo Nyamwezi na Ndovu Kule Congo na Jangwani ndiko walipokuwa wakikaa ndugu zangu,Nimeona mengi na ya kuuzunisha kwa wageni na hata wenyeji.km kanyaboya utapeli Hatari ni pale usiku unapoingia kwani kuna watu wanamka na kutuacha sis tuliamka toka asubuhi kkujiandaa kwa mapunziko na uchovu wa mchana kutwa ikiwa shuleni au makazini lazima ulale kimagutumagutu.Limeitwa Bongo kwa sababu wakazi lazima watumie Bongo kwenye mizungo ya kila siku lazima kichwa na akili ziwe kitu kimoja kila wakati hapo jiji
  we acha
  BUT I LIKE MY HOME LAND IN THE CITY TOWN BANDALI SALAMA

 4. trez Says:

  Hilo ni jiji ambalo aadhi ya watu hata uwaambie waje ulaya hawawezi kukuelewa mana wanaishi maisha ya juu na mazuri kuliko hata walioko nje ya nchi.Ujanja wako maisha yote Bongo ulaya shopping tu.

 5. zama Says:

  maisha ya bongo( mji wa maraha ) matam sana ukiwa na pesa utakula kuku kwa mlija tu lakini ukiwa unamtegemea mtu maisha magumu sana

 6. Michael Says:

  HERI MIMI SIJASEMA.
  BONGO NI MSIBA KWA WENGI WETU.

 7. Gebo Arajiga Says:

  Maisha ya dar sio mazuri hata kidogo nimezliwa hapo na kukulia hapo na sasa hivi natafuta maisha Arusha lakini ki ukweli dar watu wengi wanalala njaa hawana uhakika wa maisha bora hata kidogo katika picha tuuuuuuuuuuuu…….. jiji ni zuri kupindukia laakini utaisghije ndani yake mtu wangu wengi waamechangia vizuri sana


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s