BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WHEN TWANGA TOURED THE UK April, 13, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 10:02 AM

Wakinadada waliopo mbele pichani ni waimbaji na wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta.Mnaowafahamu kwa majina mtatusaidia.Wanaume wawili waliopo nyuma yao ni Jesse Malongo(kushoto),Meneja wa Club Afrique iliyopo Canningtown,London na Baraka Msilwa,Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ASET ya jijini Dar-es-salaam ambao ndio wamiliki wa bendi ya Twanga Pepeta. Picha hii ilipigwa mwaka jana wakati Twanga Pepeta walipozuru Uingereza. Ni kwa hisani ya Ayoub Mzee.

Advertisements
 

38 Responses to “WHEN TWANGA TOURED THE UK”

 1. iii Says:

  mtumeeeeee…..
  mbona wanatisha ivo?duh,make up za kulazimisha
  mkorogo plus fake make up equals disaster.

 2. Gervas Says:

  MSAADA JAMANI
  Siwaongelei kina dada hawa tu pichani bali kwanini wadada wengi siku hizi hubadili nyuso zao hata miili ili wawe white ( wafananena wazungu) na kuvaa mawigi, hivi kumbe ngozi yetu nyeusi na nywele zetu ngumu nyeusi ni dhambi eeh?? au uchafu? Hivi kuna kitu ambacho wazungu wameiga/walishaiga kutoka kwa wa-Afrika? hapo huwa sijui naomba mwenye jibu anieleweshe. Mnisamehe niliowagusa,

 3. Cindy Says:

  hahahahahahah uwiii make=disaster good hhahahahah

 4. Chris Says:

  Very artistic in painting their faces……

 5. Bablii Says:

  Duh nikisema sana ntaambiwa nachonga…! Lakini this is too much, utafkiri wacheza show wa “wanne star group” Hivi uk hakuna vioo? ha ha ha… I bet kama walijiangalia kwenye vioo kabla ya kupiga picha! Vinyago si vinyago, ili mradi istihizai tu!

 6. any Says:

  make up na mkorogo juu! lahaula

 7. michelle Says:

  Jamani tuna wasanii, wa- kitanzania hapa America mimi nimetembelea site yao kama mwataka kuwaona basi do hao site yao ni http://www.themissionband.org

 8. kaled Says:

  Hatuzarau kazi zao na tunapenda burudani zao lkn wenyewe wanatia kichefuchefu….huo mkorogo utakuwa wa jik na parachichi, kudadadek

 9. Amina Says:

  mhh wanatisha bc toa…hatuwataji hata mmoja mi sitaki ..du

 10. zama Says:

  mbona wana tisha ivi mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa naogopa atali wanawake wezangu wanajialibu poleni sana

 11. tatu Says:

  mkorogo oyeeeeeeeeeeeeee

  wapi mama maimathaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 12. jamy Says:

  Mkorogo umepitwa na watati, hivi kuna raha gani ya kuweka matumbo njenje!!!!!! du! mnatia kinyaaa.

 13. Kamanzi Says:

  Dada zetu kwa kweli wanatia huruma ila mimi nasema siwalaumu. Naamini wanapaka mkorogo kwa kuwa wanaume wa kibongo wanapenda kinadada weupe. Kama kweli wakaka wa kibongo wangewakubali kinadada natural wala wasingelazimika kujitafutia makansa ya ngozi namna hii. Nasikia kule usukumani weupe wanapewa ng’ombe wengi zaidi ya weusi, hamwoni kwamba hata tamaduni zinawalazimisha kinadada kuweka mikorogo?

  Nakumbuka upo wakati nilikuwa Burundi aisee nyie watu unatural mali. Wale kinadada wa kitutsi wengine weusi tii lakini muonekano wao sijapata kuona. Jamaa niliokwenda nao wakagoma kurudi bongo mapema eti wanataka kufanya debrefing ya vikao wakiwa huko huko bila bugudha ya kifamilia kumbe wameona uzuri wa mwafrica. Mnigeria mmoja akaimba YOU ARE MY AFRICAN QUEEN, hebu wakaka wa kibongo tuwaache dada zetu wawe natural bila kuwapa pressure ya kutafuta weupe.

  Halafu we Luiza Nyoni tuliimba wote kwaya pale parokia ya sinza lini umeanza kutwanga na kupepeta? Wapi jirani yangu Banza Stone siku hizi?

 14. Salim K Says:

  vinyago kwisha kazi. Kwanini usione ufahari kwa rangi yako ya asili. Ama kweli kichwa kisichoakili husumbua kiwiliwili.

 15. Chala Says:

  jamani duh hiyo mikorogo kwakweli sijaipenda halafu mmeweka make up juu i wish mjione dada zangu jamani we have a very unique color please achanani na mikorogo pakeni vipodozi vya kawaida visonyochubua nyuso.

  thankx

 16. Matty Says:

  Mh! hii mikorogo nayo imezidi lol! mtu utafikiri anaugonjwa flan hivi hadi noma hapo mtu akifanyiwa operation hata ngozi hazishoneki jamani acheni kujikoroga namna hiyo mnajiletea kansa tu!
  Mimi naowatambua hapo pichani ni Aisha Madinda na Luiza Mbutu.
  Gervas unajua baadhi ya wasichana wanaamini wakiwa weupe watavutia sana kuliko wakiwa weusi ndo maana unaona wanajikoboa kiasi hicho!kumbe wangejua kuwa na naturo colour ni vizuri zaidi.

 17. solange Says:

  kuna hao wadada wawili wa nyuma mmeweka make up za kawaida… hao wa mbele wamenichosha na hizo make up zao lakini luiza kaniuwa kabisa…..sura zingine jamani luiza usilazimishe hayo marangi sana humo usoni…yani umezidi kuwa mbaya.

 18. changalamacho Says:

  Jamani, hawa walikuwa Unyagoni,kulikoni? Reception mbona hivyo? Uzuri wa kuzaliwa wanao,sijui wanakitafuta nini dada zangu? Mambo ya Cosmetics-Urembo yana utaalamu wake jamani.Tuwe tunauliza kwanza msije mkatuletea kilio!Marijani alipata kuimba kuhusu masahibu haya!Nabakiza sisemi sana,vibaya hivyo!Tafuteni makeups zinazo endana na rangi ya ngozi mwilini mambo yatakuwa bomba kina auntie!

 19. Subby Says:

  Mambo ya podari hayo jamani, si unajua tena angel face, unataka uonekana kama ‘angel’. Basi na kucheza uchi na hizo angel face utafikiri wari wa kimasai au wa kigogo wamepaka poda wanatoka jandano wanasubiri siku ya kutoka.

  Kupaka make up ni kazi na ni art, watu wanalipwa kwa kazi hiyo sasa kutaka mambo ya dezo ndiyo hayo,angalau angempeleka mmoja wao kusomea hiyo fani ya make up artist, angewastiri kundi zima. Maana angewapaka make up kulingana na rangi za ngozi zao na wangependeza tu. Ila Lwiza ukimuangalia katika nyimbo ile ya Tumetoka kwetu Mahenge tumekuja Darisalama aliyoimba na Chemundugwao alikuwa natural black, sasa duh amekuwa mmanga koko kwa mkorogo.

 20. mtukwao Says:

  It’s lack of selfesteem, ushamba, elimu duni pamoja na ulimbukeni wa maisha ndo inawafanya wajikobowe namna hiyo .

  It’ll take them awhile to realize how fool they are!!!

 21. SIYA Says:

  mhhh wajuaji wameshainia hapa,dina bado sijasoma na comments zako

 22. Kekue Says:

  Ss lwiza anakaribia kuwa kama Michael Jackson, tehe tehe!!!!!!!!!!!!!! huu weupe huu!!

 23. masanja Says:

  uzungu kumbe mzuri sana sasa mwana wane hawa wadada wakivua nguo sehemu nyingine weusi kama mie masanja mkandamizaji mweh! ila serikali niliisikia ikisema inapiga marufuku vipodozi vikali sijui yameishia wapi maana ilitakiwa vipodozi vikali visiwepo tuone watajikobolea na nini??????????

  uso soda miguu ile ukinjwa unavaiblate sijui inaitwaje tena

  habari ndio hiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

 24. salu Says:

  Emu kwendeni huko nyie wote mlio wakandia si wao na maamuzi yao nyie kinawauma nini wabongo bwana mnaigana huyu kaandika hivi na wewe unaandika hivi na wewe uliye sema luiza sura mbaya we yako umeiyona ngoja uzae wakwako utaona atakuwaje

  mtajiju mtakavyo jibu am out

  ovyoooooooooooooooo!!!!

 25. gordon brown Says:

  PODAAAAA!!!!! AAAHHHHHHH!

 26. Ncha ya Kisu Says:

  Hiii!! HIVI NDIVYO WANAVYOPOKELEWA WASANII!
  WANAPOANDIKWA HABARI ZAO! hiwe gazetini au mtandaoni!
  Hakuna maoni yenye mtazamo wa kutia moyo! wala kuwapa Changa moto wanamziki wetu!Lakini hapa zingewekwa habari
  za Koffi Olomide !wabongo wangemfagilia sana!
  Acheni Ushamba na Roho za Kwanini?
  TWANGA PEPETA !SONGENI MBELE

 27. kijiwe Says:

  wewe salu unaanzisha beef nimekushtukia….wadau mmnamuona mchokozi huyu?

 28. Nina Says:

  Mkorogo nomaaaaaaaaaaaaaaaah dada zangu.

 29. Amina Says:

  kijiwe achana nae huyu anatafta bifu nimemwona..eti tunaigana ,tunaigana kivipi n avitu tuunaviona hapa vinatisha

 30. Justine Tack Says:

  Shughuli mnayofanya ni nzuri akina dada ila mmezidisha mno mkorogo na angel face.

 31. baker Says:

  My God what tha hell is that???????????
  Look so weird!!!!!!!!, what is the point of trying to look like ur from western while ur not???
  shame on you galzzzz

 32. Nana Says:

  Huu mkorogo unatisha. Wasichana wazuri tu weupe wao natural unatosha kabisa. Sasa kwanini unataka kuwa kama jini? I’m black and proud

 33. ama kweli mmependeza si utani
  keep it up
  huo ndio usanii

 34. Inye Says:

  Ndugu zangu MKOROGO Acheni!!!! wale wadada wa nyuma wawili waliofichika, hao ndo wao natural lakini msishangae December ukakutana nao wakiwa weupeeeee!!!!!

  Black is beauty be proud of your colour and its makes you shine. Hapo wamekuwa kama zombieesss

 35. chimaa Says:

  mmependeza nyie na uo mkologo ni mambo yenu binafsi hayatuhusu. big up twanga

 36. Shazmin Says:

  lwiza safi sana sijaona ukitaka utakate zaidi weka kwenye chai,ubwabwa na mbogamboga za majani ule utaona utakua safi zaidi

 37. hans Says:

  hamna lolote hao, kiboko yao fm academia tu, wataloga mpaka wachoke lakini ukweli uko palepale musiki umeshawashinda sasa

 38. robbi Says:

  niliogopa sana nilivyoona picha mara ya kwanza nikafikiri wamevaa “ugly fake masks” au ni “clowns”…hivi hiyo bendi haikuweza kutafuta wasichana ambao ni wazuri wa asilia….there is a lot of tanzanian women who are naturally beautiful without trying and even without makeup and fake everything……..mimi ngozi yangu ni nyeusi na naipenda saaaaana


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s