BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

FACE OF TANZANIA FINALISTS April, 14, 2008

Filed under: Bongo Reality TV,Fashion,Urembo — bongocelebrity @ 5:46 PM

Kampuni ya kitanzania ya Beatiful Tanzania Agency inayojihusisha na mambo ya urembo hapo jana imewataja washiriki watano bora kutoka katika shindano linalojulikana kama Face of Tanzania, ambao watakwenda nchini Afrika Kusini hapo kesho kwa ajili ya kupata uzoefu mbalimbali katika fani hiyo. Kampuni hiyo ipo chini ya usimamizi wa warembo maarufu wa kitanzania, Irene Kiwia na Nancy Sumary.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo kwa vyombo vya habari, warembo hao watano ambao wametajwa kuwa ni Edna Makanzo,Emmy Malau,Irene Shirima,Neshino Laizer na Yvone Joseph. Warembo hao  ni miongoni mwa warembo 16 walioanza shindano hilo kabla ya kuchujwa na kubakia warembo 10 na hatimaye 5 hivi sasa ambao ndio wanaelekea Afrika Kusini kwa uzoefu zaidi.Warembo hao ndio wanaotarajiwa kushiriki katika fainali tarehe 26 Aprili katika ukumbi wa Ubungo Plaza.

Wakiwa nchini Afrika Kusini, washiriki hao wanatarajiwa kutembelea makampuni kadhaa ya uwakala wa urembo kama vile O-Model Afrika na pia kufanya mazungumzo mbalimbali na warembo wa kitanzania wafanyao shughuli zao huko kama vile Happiness Magessa na wengineo ili kujua zaidi undani wa shughuli hizo.

Pichani juu ni warembo hao watano wakiwa na maboss wao Irene Kiwia(mbele kulia) na Nancy Sumary(kushoto) wakati wa utangazwaji wa majina ya warembo hao katika hoteli ya Regency Mikocheni jijini Dar hivi leo. Warembo hao waliosimama kutoka kushoto ni Edna Makanzo,Emmy Malau,Irene Shirima,Neshino Laizer na Yvone Joseph.Mikononi wameshikilia pasi zao za kusafiria

Advertisements
 

34 Responses to “FACE OF TANZANIA FINALISTS”

 1. Chala Says:

  jamani dada wa kimasai hongera sana … kwa pamoja tunawakilisha…

 2. trii Says:

  safi sana huyo wa arusha+zanzibar wapo bomba sanaa.

 3. ma'reen Says:

  Am glad Neshmo yumo…but please work hard on her,she is a strong masai girl and can do wonders in the world of modelling ila bado anahitaji mazoezi ya catwalk na exposure of course.

 4. Matty Says:

  Afadhali muende south mkajifunze mapoz kidogo maana mapozi yenu bado kabisa.
  Wote ni warembo na ni changamoto kwenu waandaaji kama mnataka hawa mabinti wafike mbali ni lazima muwape mazoezi ya kutosha na wasiwe waoga hata wanapopiga picha.
  Msichana wa pili kutoka kushoto kwangu nakufagilia sana ningekuwa judge ungepita maana unaconfidence si za kitoto and u deserve to be a model.
  Nancy nawewe sasa hiyo ndo rangi yako au ushaanza mambo ya mkorogo?sikuelewi kabisa.

 5. SIYA Says:

  n ayule mmasai wao walimuweka?astakafilullla

 6. mdau Says:

  irene na nancy, hongereni sana kwa kazi nzuri ya FOT..
  nawapongeza wote kwa kuingia tano bora ila mimi kama mimi sijafagilia kabisa watu kama watatu hivi ktk hiyo tano bora..
  but ndo wameshachaguliwa no p..
  tusubirie huyo mshindi..
  sasa mtakuwa mwaturushia hayo matangazo ya huko bondeni au lah..

 7. wakunyumba Says:

  watoa maoni, nafikiri wote muwazima,
  huyo mmasai mbona kazubaa hivyo? au u- model hauna uchamgafu? nawapongeza waaandaji,

 8. kimaro Says:

  kwani mmasai sio mtu,hebu mwacheni atajifunza na atakuwa model mzuri tu,kama mna hasira nae ndio kashaingia tano bora mlie tu.
  she is very strong.

 9. Nahla Says:

  Duh kumbe watu bongo bado wanasafiria hizo paper za temporary pass..bado tuko nyuma jamaniiiii

 10. ma'reen Says:

  Jamani ule ukweli usemwage…Irene Kiwia has a very pretty face!Ana kauso fulani ka cute ambako hakahitaji make up,I mean she is naturally beautiful!

 11. happy Says:

  hi,
  hongereni sana Nancy & Irine,mmejitahidi kututafutia warembo pasipo ufisadi,kama mpenzi wa Face of Tanzania nnaimani hao wawakilishi wetu watafanya vizuri.
  ushauri kwa dada wa kimasai ajitahidi na catwalk pia ajiamini anaweza,.
  my view
  Emmy is the best, she has confidency and all qualities to be representative of our country,second reprepresentative is Vyone. But all in all they are all desrve to be visura wanaojitambua.

 12. tatu Says:

  Nancy na irene kwanza nawapa hongera ya kuwapiga sop sop hao mamodel kazi nzuri walivyoanza na sasa tofauti sana tu mie hapo namfagilia sana Emmy na Edna wako juu kati yao lazima mmoja atoke kidedea.

  Nashino hongera sana waliokuwa wanakuponda mara ujui kutembea mara nn? umewapiga bao sasa jaribu kuwa unaonyesha katabasamu kiduchu na jitahidi kutembea mwana utawakimbia wamai wenzetu kule hehehe safi sana.

  yani nimefurahi sana Eligiver kutolewa maana alikuwa anajishauwa sana nae ajiona yupo juu alafu alitegemea ushindi sijui aaah atajiju.

 13. smilegirl Says:

  Nawapongeza wote walioingia tano bora, hongereni sana. mkajitahidi vema huko muendako, kila la heri. Safi sana yule eligiver ametupwa nje, alikuwa ananikera mno, anajishaua, alijiona yeye ndo yeye tayari ameshakuwa super modo, na pia anataka umaarufu kwa nguvu, aangalie sana asijeishia pabaya, mfano siku ile walipokuwa wanakaribisha wageni kwny bongo star search, alitaka kila mtu amuone, ama kweli kizuri chajiuza kibaya always chajitembeza, t’care+b’gud mpendwa huo ni ushari wa bure usije juta maisha yako yote kwa hayo makuu unayoyataka.

  Hongereni tena tano bora, emmy ongeza bidii mpendwa kwani unajitahidi sana pia hata majaji wanaonyesha kukukubali, all da best usiache kumuomba Mungu kwani yeye ndo muweza yote hata hapo ulipofikia ni mapenzi yake. T’care and b’gud always.

  Samahani, siwafahamu hamnifahamu ninatoa tu maoni, so mnaweza kuyafanyia kazi au kuyaacha pia.KILA LA HERI.

  ASANTENI.

 14. hatbah Says:

  nawapongeza irene na nancy kwa yote wayafanyayo kuwaondoa mabint katika umasikini.ni vizuri mlivyoamua kuwachukua hata mabinti wa mikoani hususani vijijini.nimefurahi sana kwa jitihada mlizozifanya mpaka Neshino ameingia tano bora.kweli hamna roho za uchoyo.Mola atawazidishia.leo watu hawayatayaona mema mnayofanya ila kwa mola mnafungu lenu.mafanikio ya neshino ni mafanikio ya wale malaika wa mungu jamani.cha msingi asije akapata halafu akamsahau mumewe na watoto kwani atakua amefanya dhambi kubwa sana.
  neshino unabahati kupata mume kama wako aliyekuruhusu ukatoka nyumbani na kumwachia ulezi wa watoto kwa ajili ya kutafuta riziki.kaza buti utafika mbali.hata hao kina naomi camble,irene kiwia,nancy sumary,happiness magesa,miriam odemba na ma miss/model wote hawakuzaliwa wanajua sote tunajifunza na unajifunza kutokana na makosa.fata mfano wa luiza mbutu mama brian wa twanga pepeta kutoka “nimetoka kwetu mahenge nimekuja dar es salaama kutafuta kazi” mpaka leo anaitwa mamaa b na umati wa watu si mchezo.jaribuni kukumbuka luiza na kichuma chake akikigonga huku akiimba kwenye hawavumi lakini wamo kipindi kilichokua kikirusha na itv,lakini leo luiza ni mtu katika watu,anajitahidi kweli huyu dada.neshino usisahau ulikotoka mpenzi.ninaimani utafanikiwa.pia ukumbuke kulipa fadhila,mshukuru mungu kwa kukupa hiyo nafasi na bahati ya pekee pia washukuru sana nancy na irene pamoja na uongozi wote wa majaji,walim na kampuni kwa ukarim wao kwako pamoja na jitihada zao.keep it up,nakupenda na nakutakia kila la kheri,mola ndie atoaye riziki na kila mja anafungu lake!!!!!!!

 15. amina Says:

  hongera neshino usione aibu,mtoe mumeo na wanao kimasomaso,.fanya kazi kama mtumwa ili uishi kama mfalme,ila chunga nyau wasikuachanishe na mumeo,mpende na umuheshim sana.mfundishe na yeye,sawa dada neshino?

 16. anna Says:

  nimefurahi sana kusoma ujumbe wa hatbah,ametoa point nzuri sana,anaonekana anahekima na anaridhishwa na kufurahishwa na maendeleo wa watu wengine.ni vizuri kujali maslahi ya watu wengine sio kua kama kina sumaye,richmond,lowasa,karamagi na hao kina chenge!!!!

  hongera sana neshino jua wewe sasa ni kioo cha jamii zote hususan wamasai hivyo ukiruka ruka na kutafuta u supa staa wa kuandikwa kwenye kiu,ijumaa,sani kwa skendo chafu basi umeharibu taswira nzima hivyo utawanyima wengine kazi kwani kuna watu wanasema u model na miss au urembo ni uhuni mimi nasema sio heshima ni kujiheshimu kabla hujaheshimiwa.kuzaliwa kijijini sio tija,endelea na libeneke

 17. jasmin Says:

  natamani nikujue ulipo hatbah,tunahitaji vijana wenye upeo kama wewe tanzania yetu isonge mbele,watu wanamsakama mmasai wa watu bure kwani alipenda kuishi shamba na kuzeekea huko?acheni uchoyo.

  mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ,visura wamejitahidi mpaka hapo hasa huyu mmsai wetu nae pia ni binadam mwenye upeo na upendo ndio maana amefika hapo wala hakupendelewa jamani,msitie mtoto wa watu majungu,mara mseme amezubaa,mara na huyo mmasai nae kwani yeye funza au mavi,kueni watu wenye kukubali na kuridhika.

  hongereni nancy na irene mungu amewapa vipaji na upendo wa ajabu,wanawake tupendane na tuendelezane.tuendelee kuwapa irene na nancy ushirikiano,sapot ili waweze kuwawezesha mabinti kimaisha.mola awaongoze ndugu zangu.

  hatbah naomba nikufaham unaonekana unabusara,hekima na upendo.text yako inajieleza.je,wewe ni mwanaume au mwanamke kwani jina lako kidogo lina utata.samahani kama nimekuboa ila umenifurahisha sana.hongera sana

 18. noela Says:

  hongera irene na nancy kwa kazi nzuri na nzito mnayoifanya ,nimesikitika binti wa dodoma hayumo humo na wenye vieleele wote nje kama ellgiver,jamila ila msikatee tamaa next time punguzeni kelele

 19. Tobi Says:

  I think Yvonne will win. Since the beginning she is the best of all and she has improved much since than!

 20. Saidi Situ Says:

  Hao sio ma model wa TZ ni ma model wa Nancy na huyo rafikiye asiyefahamika,

 21. baker Says:

  Hongera sana wadada! good work for Tanzania model najua siku moja mtafika viwango vya juu vya ma miss najua safari bado ni ndefu sana, Ila nawashauri kitu kimoja mkiwa kama ma model! unapopata nafasi ya picha kama hivi inabidi muwe na ma pozi ata mtu akiangalia anajua ni models wa kweli. Lakini apo kuna wengine unaweza kusema sijui ni watu gani! hamjui kuwa picha inauza ndugu zangu?? Angalieni picha za ma model from western wanavyotoka bomba. Najua mmenisoma na next time mtatoka na ma pozi makali yaliyokwenda shule. Nawatakia kila la kheri.
  mzee wa ma oppinion.

 22. Pearl Says:

  Majaji wa face of tz hongereni kazi nzuri.Ila mi nina maoni kidogo kuanzia mlivyoanza hichi kinyang’anyiro hasa wakati mlipokua mna wajaji hao washiriki.Kweli kuna wakati mlikua mnatumia lugha sio nzuri hasa nakumbuka hiyo siku washiriki mliwapeleka kampuni ya REDDS.Mliwapa kazi ya kuandaa tangazo ila lugha aliyokua anatumia yule Victoria haikua nzuri hata kidogo.

  Nanukuu alivyosema ila sikumbuki ni kundi gani aliwaambia yafuatayo:
  ”yaani mlichofanya ni funza uozo tena wale funza wanaotoka kwenye samaki waliooza”.
  Mwisho wa kunukuu.

  Kwa upande wangu sikupenda kwasababu angeweza kusema tu kuwa kazi yenu si nzuri na sio kutumia lugha za dharau because kwani yeye anajua nini kuhusu kuandaa matangazo na anawajaji wale basing on what wakati hajasomea hiyo kazi???? kila anaeishi bado yuko kwenye learning process na new discovery kwahiyo lugha zenu majaji zisiwe kama vile nyie mmeshafika mahali pa ukamilifu.

  All in all kazi nzuri tano bora naikubali sana.
  Regards.
  Pearl.

 23. Mtukwao Says:

  Hata mmsai naye ni mtu!! ni binadamu kama walivyo binadamu wengine!! anajina lake…why don’t guys call her by her name????????? kwanini mmuite mmsai??

  I do agree kabila lake ni mmsai but that is not her name!! let respect each other guys!! when are we (watz) gonna grow-up so we can talk and act as matured people??? shame on y’all who called her “mmsai”

  tujifunze kuheshimiana is one of human’s rights!!!!

  “you make be proud when you call me by my name”… Mayer Angelous

 24. lukay Says:

  hongereni kwa kazi nzuri yakumtafuta FOT..yani hapo ni emmy tu ndo mshindi wengine sijaona bado..neshno hongera sana kwa bidii nyingi maana ukiangalia from the day wapimwa kule kwenu duh ni balaa but nau hata pedo wavaa umeadvance my dia..WEL THE REST HONGERENI

 25. mimmy Says:

  hongera sana waandaaji wa shindano hili. pia nimefurahi sana kwa kumpa nafasi mmasai. kwani anaweza kuwa model mmoja hatari sana, ni muda tu, kwani ni kitu ambacho hata kukiona alikuwa hajawahi. hatuwezi kujaji kama wajanja wengine.

  nakushauri nancy, hiyo shot hair style haikupendezi kwani una kichwa kibaya. bora uendelee kusuka nywele zako zilezile za bandia.

 26. zawad haji Says:

  Hiii!!!BIG UP SAANA Irine na nancy kwani mnaonekana hamna roho za kwa nini. halafu kitu kingine jamani kama mtu huelewi omba ufahamishwe kama huyo Saidi Situ eti hamfahamu Irine na hao models ni wa Nancy na huyo rafiki yake, mhhh…. just u be mzalendo Said watakucheka watu…

 27. Twaha Figo A-City Says:

  Washiriki nawapongeza sana,lakini waandaaji wamechemsha sana yaani,mashindano hayana msisimko uliotakiwa alafu majaji hamjui kujaji,c kwamba m2 ukiwa mrembo ndo ukawa na kipaji cha kuwa jaji na mshauri wa urembo,hapana,hapo ilibidi hata waandaaji mngetafuta majaji waliosomea mambo hayo kuliko kuigana tu maamuzi yenu kama inavyojitokeza sasa.

 28. juma Says:

  hongereni sana Iren &Nancey good job wadada tutafika tu

 29. Cute guy-DSM Says:

  Hello mashabiki wote wa modeling
  Nikiwa 1 wa mashabiki wa urembo na mitindo,nafurahishwa sana na jitihada za baadhi wa watu waliojitolea kukuza sanaa hii inayosahaulika.sio siri kwa bongo bado sanaa hii haipewi sana kipaumbele kama sanaa nyingine sijui kwa nini,tena afadhali ya mashindano ya urembo(beauty pageants) yanajulikana kuliko ya mitindo(modeling pageant)walio wengi hawajui,na hii inachangiwa sana na vyombo vya habari hawaipi sana kipaumbele kama michuano mengine,kama wenzetu wa south africa.wako juu sana katika sanaa acha mitindo,mimi binafsi nilishaingia mkataba na kampuni flani kwa ajili ya kufanya modeling lakini nilikata tamaa mapema nikaacha.ila sio neno kidogokidogo ndio mwendo,iko siku nasi tutafika.
  Tukija katika Face of Tanzania,kidogo inatupa matumaini kuwa nasi tunaweza kufika mahali,Irene na Nancy wamejitahidi ila kidogo walichemka wakati wa Scouting,hakukuwa na haja ya kupanda milima eti kutafuta visura,utaratibu huo kidogo ulikuwa mgumu ingawaje walifanikiwa kiasi
  Kwenye camp pale Regeancy kambi ilikuwa bomba,walijitahidi kuwaweka models katika hali ya kimashindano zaidi.
  Pia nawapongeza sana washiriki,walijitahidi sana hasa kwenye mazoezi magumu kama yale ya kupose na nyoka kwa ajili ya picha,lilikuwa zoezi gumu kupita yote lakini sikuamini walipoweza,binafsi nawapongeza sana washiriki,na pia Nancy,aliwasaidia sana Models waliokuwa waoga.Nancy keep it up mama,you strong women sio mwoga
  Mimi mwanaume lakini kwangu lile zoezi cjui kama ningeliweza,wale wadudu sipatani nao kabisa
  Kuhusu Top 10 niliapriciate ila Top 5 mhh.. cjui likuwaje Elligiver asiwepo,kuna mmoja pale alicover nafasi yake jamani,amejitahidi sana dada yangu yule ila ndo hivyo tuwaachie jurgies ndo weshaamua ila usikate tamaa Elligiver safari ndo inaanza,i hope wadau wa mitino wamekuona.

  Wadau poleni sana kwa maelezo marefu,hii nafasi niliitafuta nitoe dukuku langu
  Kama mtapenda kuchat zaidi nami,email yangu ni salimhero2002@yahoo.com,namba yangu ni 0713132101.tuma mail au piga sio kubeep ok
  Regard
  Cute guy

 30. GRACIE JESSIE Says:

  MIMI KAMA MIMI NAPENDA SANA FANI YA UANAMITINDO LKN JINSI YA KUTIMIZA NDOTO ZANGU NDIO TABU SIJUI MUNAWEZA KUNISAIDIA VIPI KWA MAMBO YA UREMBO NA KUFANYA MATANGAZO BILA YA KUPATA MALIPO YOYOTE

 31. LULU Says:

  Wadada wana mvuto
  nitapata wapi nafasi ya kushiriki na mimi.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s