BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

CHENGE ATUA DAR, ASEMA NI SHUTUMA ZA “VIJISENTI” April, 16, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 8:48 PM

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge, jana alirejea nchini akitokea China na kukataa kujibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya shilingi anazodaiwa kuzihifadhi katika akaunti nje ya nchi.

Chenge ambaye aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana saa 9:00 alasiri na ndege ya Emirates alisema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwa vile tuhuma zilizotolewa dhidi yake zinachunguzwa.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani juu ni Waziri Chenge alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutua jijini Dar.Photo Credit: Mrocky.

Advertisements
 

42 Responses to “CHENGE ATUA DAR, ASEMA NI SHUTUMA ZA “VIJISENTI””

 1. coco Says:

  Nilishangaa sana kusikia hiyo kauli yake akisema ni VIJISENTI. jamani watanzania tutaendelewa kuchezewa na hawa viongozi wetu tuliowaamini mpaka lini? inasikitisha sana

 2. Chala Says:

  jamani wa TZ wenzangu huyu jamaa nimjanja sana kwanza eti anasema vijisenti wakati vingetumika kwa ajili ya wananchi saa hizi tungepiga japo kahatua kengine kamoja, kwanini asijiuzulu ??? kwani kila mmoja anasema uchunguzi ukikamilika ndio tutajua ukweli:” uchunguzi wa hawa watu uwa hauishi kwanini mi naona wakati umefika zikiundwa kamati kuwepo na wananchi raia wa kawaida japo mmoja kila tume jamani wenzetuhizi tume wanabebana sijui ni 10percent au ni nini??? kwanza mtu akikaa madarakani ma miaka sio fresh kwani kuna wananchi wanaomaliza vyuo wanao uwezo mkubwa wa kuongoza nchi sana tu. mtu anakaa mpaka anzoea anakuwa hajali tena maslahi ya taifa anajijali yeye… ndio anakuwa hajuai kama kuna watoto ambao hawajuai watakula nini watavaa nini , vijijini wanawake wanateseka kwa huduma duni, hajui hayo yayamuumi na wla haitokaa imuume coz wanawe kwanza wanasoma nje ya nchi,hawaijui hata tafrani ya usafiri wa daladala…inauma sana jamani hawa mafisadi ..na balali kwani bado yupo hospitali??? au anafanyiwa uchunguzi kwa huko huko…….mmmhhh

 3. Tonny Says:

  Jamani Watanzania kumbe tuko wachache tunaoipenda Tanzania ijayo kwa zati. Ningekuwepo hapo kwenye kumpokea na nikapata mtu wa kunipa bomu la kujitoa mhanga ningefanya hivyo kwa kuokoa Watanzania walio wengi wanaoishi maisha duni.

  Yaaani hata mmoja hakuna aliyerusha hata jiwe!!

  Inanisikitisha sana…..

 4. Amina Says:

  Jamani mmeona dharau zao hawa watu eti ni shutuma za vijisenti..kwake yeye anaona vijisenti kahiyo anazo nyingi zaidi ya hizo?makubwa

 5. Mzalendo Says:

  Look at the facial expressions za hao waandishi..especially dude in brown LOL..Mnanuna nini 2005 si ndio nyie nyie mlipiga kura..tuache UNAFKI WATANZANIA!! Hili tulijitakia wenyewe…kikwete mmempa uraisi bila kujua past yake na marafiki zake wakaribu majambazi…sasa tukubali matokeooo

 6. kyekue Says:

  Ohhh Chenge, umetubonyeza kizenji!!!!

 7. anisa Says:

  ameiba bwana wee na nina uhakika yake yamejulikana wapo wengi tu.na kwa bongo ninavyoijua yatakuja na yatazimika hivihivi.

 8. Pearl Says:

  I know its not a crime to be rich,but the question is where did he get all that money from?????hata kama angekua ameajiriwa na serikali tangu akiwa ni mtoto wa mwaka mmoja still asingekua na pesa zote hizo na hata kama ni urithi sio kweli kwa sababu ni wazi kuwa wazazi wa zamani wenye watoto wenye umri wa Chenge hawakua na utajiri wa kiwango hicho.
  Huyu atakua ni wale wanaitwa jichukulie chako mapema.
  Oooohhhh dia Chenge i pit you.

 9. Edwin Ndaki Says:

  Ni kweli ni tuhuma a vijisenti tu.

  maana anajua kuna madili mengine ambayo amecheza ambayo amakula pesa ndefuu kuliko hizo.

  Ipo siku bubu atasema tu.

  tutafika tu

 10. Bongosamurai Says:

  Kaleweshwa na ukwasi alio nao ndio maana anaona ni vijisenti wakati kwenye jimbo lake la uchanguzi wapiga kura wake wanataabika kwa ufukara..!

 11. Ama kweli fisadi ni fisadi tu! Mimi nakumbuka niliwahi kuiba kipande cha kuku miaka ya nyuma, kikaitishwa kikao cha kijiji, leo hii fisadi anasema Sh Bilioni 1 ni vijisenti.

  Kweli, Tanzania italiwa na wenye meno

 12. changalamacho Says:

  I just pitty Chenge.He should have known better that Politics was such an unthankable octopus!Never toy around with it!Ukisha pata Mkwanja wako ni mbele kwa mbele.Ukisubiri sifa umeumia!Pole Baba hata Yesu alifia Mslabani!

 13. Kamanzi Says:

  Ee Mungu wangu uliyeumba mbingu na nchi. Tazama mwanao ninaililia nchi yangu Tanzania. Ona mfalme wanadamu wasio na huruma wanavyoinyonya nchi hii pasi na aibu. Mbona un awaacha waendelee na ubaya huu?

  Tazama maskini wale wasiojua kama watakula hata mlo mmoja kwa siku wanavyokulilia. Angalia wafungwa wale waliotupwa jela ama kwa makosa wasiofanya au madogo madogo tu. Angalia mama yule kijijini anayejifungua njiani maana zahanati ipo mbali. Angalia watoto wale wanaoshindwa kuendelea na shule maana maisha magumu. Waokoe baba maana ukweli ni kwamba wapo mafisadi wanaowanyonya.

  Kwanini usishuke eehe Mungu mkuu na kuibadili Tanzania. Njoo tukuone kwamba wewe uliye mtetezi wa wanyonge upo kuwasaidia wenye shida. Mafisadi wataendelea kutusimanga hata lini Mungu nawe umekaa kimya? Shuka Mungu mkuu tukuone maana watanzania wamekata tamaa maana hawamwoni wa kuwaokoa kabisa. Wasio haki wameneemeka zaidi ya wenye haki, hivi ni halali Mungu mkuu?

  Shughulika na mafisadi popote walipo na hakikisha Mungu wangu ya kuwa hawaendelei tena. Nimeona nikuombe wewe maana najua uweza na nguvu vina wewe milele hata milele. AMINA na AMINA!!!!

 14. kijiwe Says:

  Kumradhi wadau mimi naomba niwape kaswali.
  Hakuna dili lolote linalohusisha kisu cha nguvu linalopita bila A.G kulijua.
  Pesa nyingi na madili mengi yalipigwa wakati huyu jamaa alikuwa A.G.
  In short this guy is filthy rich na mi naona mnapoteza muda kulalamika sababu msafiri kafiri na asingekuwa msafiri angetuliza huu moto wa ufisadi lakini sababu yeye ndiyo kuwadi mkuu wa uchafu huu anastrategize njia mpya ya kuwapiga changa jingine.
  Solution ni kuwa violent lakini i doubt kama its the best way otherwise laana inazidi kusambaa katika pace ya time bomb.
  I really love tanzania lakini inatisha hii hali mpaka mtu unatamani kuwa snipper uwaeliminate wote hawa ambao wametajwa kwa ufisadi maana its getting too much sasa….

 15. Dinah Says:

  Kinachoudhi na kukatisha tamaa ni sisi wachache kulalamika wee nakupoteza muda alafu hakuna kinachofanyika, vyombo vya habari vinashikilia bango mwanzo wa “Saga” lakini hawajui kuwavalia njuga hawa jamaa mpaka wafirisiwe au kurudisha mali ya Mvuja jasho (tax) au hata kuchukuliwa hatua za Kisheria.

  Igeni mifano ya wenzenu huko magharibi jambo kama la Balali, Lowasa na huyu na wengine waliokuwa kwenye uongozi wakati hawa jamaa wakiiba nakusaini mikataba feki wangehakikisha haachiwi mtu, vyombo vyote vya habari vingeshirikiana kuibua (waliohusika ila hawako madarakani sasa), kufuatalia na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukua mkondo wake.

  Lakini hapa Nyumbani mpaka UK’s newspaper The guardian waseme ndio mnajifanya kufuatilia ili ionekane mnafanya kazi kumbe mnatuyeyusha tu kama Serikali yenyewe. Hamjui wajibu wenu. Manaudhi sana.

 16. abbou Says:

  Ndo uzuri wa kudanganyika na Tshirt za njano, kofia, kanga na vitenge+ vijisenti wakati wa uchaguzi! ndo jibu lake hilo , acha waendelee kuzitafuna.

 17. Mswahilina Says:

  Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

 18. Chris Says:

  He has the back-up of Kikwete, ulitegemea ajibuje?….. Limeshatudodea…. Si mliwachagua kwa weupe na ushabiki…. haya sasa tulinywe tu….

  Mtu kama huyu ni kumpeleka uwanja wa Taifa na kumnyonga huku…. ITV, TVT, Star TV etc wakiwa wanaonyesha LIVE.

  Kikwete and his corrupt allies are taking the peace we’ve in Tanzania for granted….

 19. Kurwa Masaba Says:

  I have been following the EPA scandals for some time, and other allegations such as this old one –BAE system- that have been leveled to our party leaders, government officials, member of our parliament and other private and local officials for some time now. I have come to conclusion that it’s the right time now that we run our country on truth by following the laws that have been made to both- people in high offices and those that are supposed to be served by.
  Recently I was reading a British newspaper which cited Mr. Chenge as having (billions –equivalent of our local) money in one of the banks here in UK. Britons take it too serious on any offshore money accounts to its citizens on the basis of tax and legitimacy. The whole point is to ensure that it account all their incomes also -knowing how all its bank are handling money transaction inside and outside their country. Back to what I read, Mr. Chenge, will have to answer all those questions on how he got all that amount of money at the first place and if- that money was also obtained from an illegal practices. It has been okay for some times now to see that people who hold big offices can go away with any allegations. It’s the high time for Members of the parliament or Government officials to either save our country or leave their position and decide to run their business, on which, this will help them be free from problems of interest if not conflict of interest. Let me be straight here, I am not condemning or saying that Mr. Chenge is now guilty ,that’s why earlier I used the word “also”, on the second allegations because , people who hold these top position seems to think that the laws applies for them in the way addressed on the books. What we have been seeing is that, to them -they are innocent until proven guilty, but vice versa to other citizens who don’t hold high offices or positions, its assumed that they are guilty until proven innocent.
  What I know now is Chenge would still be in China on that trip with the president and would never come home if these allegations were to be reported by our local newspaper. If I am not mistaken, what we do know now is these allegations were written or generated from a newspaper in Britain, and that’s why- not to paint the picture bad, Mr. Chenge was forced to return home to answers those allegations. I am sure he would still be in China if those allegations were addressed or were coming from a newspaper let’s say Majira, or Nipashe , both would be stories or rumors that would let go away. Thanks God the Britons did not let this issue go away, no matter how long it would take, but all the info would have to be known later . To me, this is one of many opened and continuation or follow up to come on their side on allegations’. This allegation involved both -their companies, our members of parliament, Gorvment official and a sizeable number of cru-pious and greedy Tanzanian businesses personal on dealing with these Radar issue.
  What I am thinking on my side or view concerning this allegation is to suggest Mr. Chenge, to resign immediately, waiting for his innocence or guilt to be proven by the court of law as he is entitled too. But, also should give a way on the pure and non interfered process to take way. I have been wondering for so long now, why other Ministers who also were engaged in greedy issue like Msabaha and the others are not resigning on their MP’s positions. The Prime Minister need to let people know that once a Minister resign on a ministerial position due to their blunder etc, will also be required to resign there second positions as Members of the parliament. The notions that they are elected by Wananchi’s, and therefore are entitled to remain as Member of their constituency , despite them doing blunder is wrong. The problems they have caused are Wananchi’s problem and not only ministerial problems and the notion of giving them another chance to be heard or listened is to give them a chance to feel that they are superior to others and can still do anything. We are more than 30 millions Tanzanian who among us we have talent -educated, experienced and well groomed citizens who can run our country right. I do understand that It’s expensive to re-run the MP’S election but, its worthy to let anyone who has been elected by citizens to understand that they are there to save them, and not playing with them. Let people who need to have money offshore have them as business people and not as government official who use their power to collide or force with other greedy business men and cite a conflict of interest.

 20. mnyoge Says:

  Jamani wa tz huyu jamaa aache kazi !!! vijisenti nini?
  Mali ya Umma anaita VIJISENTI?

 21. michelle Says:

  Tanzania nchi, ambayo imekuwa kimbilio la wengi, Mungu alitubariki akatupa amani, lakini sasa hata si amani tena tunauzana sisi kwa sisi kwa laana za vizazi na vizazi, nchi inauzwa kwa haya majitu ya Kenya majambazi wakubwa, ili tu mpate pesa enyi mafisadi mliolaaniwa toka mtumboni mwa mama zenu, hizi laana zitawafuata vizazi na vizazi vyetu na Mkono wa Mungu uwe juu yenu, eti unasema vijisenti, vingeweza kusaidia wananchi wenye shida. wewe Mr chege na Mr Richmond mnawapandikizia watoto wenu laana za milele, Mungu naazione kashfa zenu za kusema vijisenti, Kama Mungu aishivyo hamtafika mbali!!!!!!!!!!!! kikwete kazi kwako inabidi huyu mhuni aachie ngazi kabla sijajilipua na kummaliza.

 22. kijiwe Says:

  LOL —
  Mtu kama huyu ni kumpeleka uwanja wa Taifa na kumnyonga huku…. ITV, TVT, Star TV etc wakiwa wanaonyesha LIVE
  inatisha but sounds funny

 23. jamani mi sioni kama Chenge ana kosa lolote kula rushwa kimsingi rushwa ni njia ya kujiongezea kipato katika karne hii hususani kwa wale ambao wanauota utajiri, kimsingi kila mtu anakula alipo sasa wamaomtuhumu chenge sijui wanafikiria nini rushwa haijaanza leo wala jana kwa hiyo kama mtu unaweza kutengeneza pesa kwa udhaifu wa watu sioni kam ni hatari,pili ukiwa kiongozi na usipokuwa tajiri watanzania wenzako wanakushangaa kwa kuwa wanaona hujatumia nafasi yako vizuri,mimi nasikitika sijui kwa nini mzee wangu hakuwa mwanasiasa akafanya kama walivyofanya meghji ,lowassa na karamagi ,tatizo ye alikazania shule ili awe daktari haya sasa nasikitika atakufa maskini manake wagonjwa hawaongi hela ya maana zaidi ya pesa ya soda tu,BINAFSI NAONA CHENGE NA WENYE PESA WENZAKE WOTE ,I MEAN WALE AMBAO PESA ZAO ZIMETOKANA NA SIASA KOSA KUBWA AMBALO WANANIBOA NI KUJA KUHIFADHI PESA ZAO HUKU NG’AMBO NINGEWAONA WA MA ANA KAM WANGEIFADHI KULE BANK YA MAENDELEO MWANGA ,AU HUKO BONGO ILI WATU WAKOPESHWE PESA ZINDELEEKUZAANA ,HATA HIVYO HAKIJAHARIBIKA KITU HUKU NI SALAMA ZAIDI,SO SIWALAUMU WANASIASA WOTE WALA RUSHWA WAZURI,ENDELEENI WAZEE, MWISHO WATANGANYIKA SIKU WAKIACHA KUWA WATU WA MANENO NA KUMAANISHA KWA VITENDO NDO SIKU AMBAPO NCHI ITAKAA SAWA ,MIAKA ZAIDI YA 40 ,CHANA KIMOJA TU MADARAKANI WANABADILISHANA BABA MAMA MTOTO NA MUDA SI MREFU TUTASIKIA WAJUKUU ZAO SUBIRINI TU,SIKU WATU WAKIVUA UKONDOO NA KUVAAA UCHUI NDO KIDOGO NCHI ITAKAA SAWA ,KILA LA HERI CHENGE ,EDDO LOWASSA ,NADHIRI KARAMAGI+MWANAMKE WA SHOKA MAMA ZAKHIA M,

 24. michelle Says:

  ni ajabu sana nchi umetawaliwa na watu wa mataifa mengine, viongozi wetu wakihongwa tu kidogo tayari wanauza nchi, kwa mfano wahindi wamefanya Tanzania nchi yetu ya weusi kuwa India walala hoi hawana mbele wala nyuma, wakihonga tu wanapata passport, hata ambao hawajazaliwa bongo, mwaka jana alikuja huyo Mungu mtu wao agha khan barabara za mitaa ya hapo upanga zikafungwa wananchi wasipite, kisa wahusika wamepewa kitu kidogo, wahuni hawa Wahindi kwao shida mpaka miguuni wanakula vitu vya ajaabu, wananchi hawana haki kuliko muhindi, hili msipo liangalia Laana hazitawakosa kwenye vizazi vyenu majambazi waoongo wakubwa. tutaliitia jina la Bwana lazima mungu ashughulike nanyi mashetani wakubwa ninyi.

 25. mtz Says:

  Wako wapi watu wa CCM London?? , mnajiandaa kuwa mafisadi baada ya kuona box halilipi.

 26. Chala Says:

  jamani Wa Tz wenzangu unajua pia hii rushwa ianzia kwenye root kama kunamdau mmoja hapo kasema alianza Kwa A.G, hao ndio wenyewe kuna wahindi huko akina Zak…….kazi yao ni kuwagawia hao ma PT kila mwezi pesa ya bure tuuuu …yapo hayo. inaumiza sana pale tunapokuwa tunadanganywa na maneno mafisadi ni wengi kupita kiasi…kajisemea prof J “Rushwa imeshika hatamu karibia itakuwa halali” maana kama rushwa haipi ufisadi haupo atii… roho inaniuma sana inabidi tuangalie kwa makini wa kumchagua 2010 awe rais awe Mbunge awe diwani yeyote yule sasa imefika wakati tusiangalie vyama tuchague kiongozi aliyekuwa bora tu.”””Ewe mwenyezi Mungu inusuru Nchi yetu””

 27. Pope Says:

  Dinah nakuunga mkono 100%
  Kuna watu wanaona bora liende!! mi nadhani kuna haja ya kuwa responsible kwa kila mmoja wetu ipo siku Whistle Blowers watasikika, Tunachoongelea ni RUSHWA, Pili angalia idadi ya pesa, pata picha hiyo ingechangia kwenye Kuboresha elimu, au huduma za afya au hata kuendeleza miundo mbinu ya bara bara na mawasiliano, Je hao wanaosema vijicents wanajua kuwa huko Mlimba kuna Mazao huwa yanaoza kwa kushindwa kusafirishwa kufika kwenye soko!!!? Unajua kuwa kuna watu wanalima kisha wanaishia kumwaga mazao mengine kwa kushindwa pa kuyapeleka? Hatukatai kula kazini jamani NDIO ULE HADI MBEGU???????????

  Kurwa where is Tinah Masaba?

 28. Pope Says:

  Watu wengine bwana sasa mchangiaji namba 23.
  Anyway ndio uhuru wa kujieleza huu, inawezekana unafaidika kwa namna moja au nyingine na kamfumo hako!!

 29. zama Says:

  Ukiifikilia nchi hii unaweza ukalia naawa mafisadi sinaatalakusema balali wamepiga kelele mwisho kimyaaaaaaaaaaaaa anaendelea kulakuku na familia yake Richmond zimeundwa tume mpakasasa watu wamechoka waliojiuzulu bado wanakula kuku kwamlija awajachukuliwa atua yoyote Sasa Chenge zitaundwa tume mpaka basi nasa nasana atajihulu au atafukuzwa kazi sasa naela zake ataendelea kuwa nazo sasa Ichi inaena wapi na kwasababu mafisadi awachukuliwi atua nzito kama kwena jela maisha au kufilisiwa UFISADI AUISHI MILELE MAFISADI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

 30. dido Says:

  wewe chenge acha utoto wenzio wanakufa na njaa wewe unasema vijisenti fikiria na wenzio wanashida hata kuupata huduma hospitalini sababu hawana kitu na ww unaita vijisenti mpumbavu nn natamani niwe karibu yako nikutoe koromelo lako upotee kabisa sitaki ata kukuona

 31. Kamanzi Says:

  JEMBE HUJUI USEMALO. Hakuna sababu yoyote unayoweza kuitoa itakayowatoa hao mafisadi. Unadai wangeweka pesa bongo ingesaidia? Nasema kwa kiasi finyu mno na naongea kama mchumi sio mwanasiasa hapa. Nitakupa tu mifano ya kawaida ili nisikuboe na jargons za kichumi.

  Lowassa na Karamagi wanamili TICTS kwa maana kwamba wameweka kitega uchumi chao bongo. Niambie watanzania wanafaidika vipi? Mkapa, Yona na wengine ninaowaweka kwenye mabano wanamiliki mgodi wa Kiwira ambao pia upo nchini. Tafadhali nieleze wewe mtanzania unafaidika vipi na huo?

  Kampuni kama Meremeta, Richmond na nyinginezo zote ingawa wanataka kuficha zipo ndani ya nchi (Yes asikudang’anye mtu Richmond ni ya US). Niambie mtanzania anafaidika vipi na hilo?

  Sasa nitakupa economic perspective ya jinsi gani watanzania wanaumia. Katika uchumi wa nchi yoyote moja kati ya kigezo kinachotumika ambacho hakifai kuona maendeleo ya nchi ni kuangalia Gross Domestic Product (Ongezeko la uzalishaji wa nchi). Tatizo ni kwamba ongezeko hilo linaweza kuletwa na wachache tu na wala si kwa watanzania kwa ujumla kwa hiyo huwezi kutumia GDP kama kigezo. Na hili ndilo linalotokea Tanzania, yaani tangu Mkapa hadi leo Tanzania inasifiwa kwa kuboresha uchumi lakini ni kwamba ongezeko la uzalishaji linaletwa na MAFISADI ambao ni wezi wachache.

  Ndio maana World Bank, IMF na UNDP wameamua kuwa na kipimo mbadala cha kuangalia uchumi ambao ni kuangalia welfare ya wananchi (yaani uwezo wa wananchi kupata chakula, malazi, makazi, huduma za afya, elimu, ulinzi, haki, usawa n.k). Unapotumia kigezo hiko, Tanzania ni nchi ya mwisho kwa umaskini Africa na sina sababu ya kueleza ni ya ngapi duniani. Yaani tunakuwa nchi maskini kuliko zote wakati huo huo wapo matajiri Tanzania ambao wanuwezo wa kushindana na matajiri walioko katika nchi za magharibi (ndio maana Chenge anaweza kumudu gharama za mwanasheria toka US).

  Nakupinga na wala sikubaliani na wewe ndugu yangu JEMBE kwamba kwa MAFISADI kuwekeza ndani ya nchi ni faida. Tatizo lililopo ni kuwa na uneven distribution of income (mgawanyo usiosawa wa kimapato) baina ya watanzania. Kadri mafisadi wanavoongezeka ndipo mgawanyo unazidi kuwa tofauti na wale wanaojua historia za chumi mbalimbali duniani watakwambia ndugu Jembe kwamba huko ni kutengeneza bomu ambalo mlipuko wake hata mafisadi hawatauzima. Nitakupa mifano michache.

  Nchini China kulikuwa na kitu wanaita Cultural Revolution ambapo wananchi wenye hasira walivamia wote wenye mapesa, wakawapiga na kuwakabidhi majembe ya mikono wakalime. China ya leo inayoitetemesha hata Marekani, imetokana na mapinduzi hayo ya kihistoria.

  Nchini Cuba, kulikuwa na MAfisadi waliokuwa vibaraka wa MArekani. Iligharimu comrade Fidel Castro (namwomea uzima) na comrade Che Guevera kuwang’oa mafisadi wale na kutengeneza Cuba ya sasa ambayo tangu mwaka 1963 imekuwa imewekewa vikwazo vya kiuchumi na MArekani lakini bado welfare ya wananchi wake iko juu zaidi ya wamarekani wenyewe. TATIZO mgawanyo usiosawa wa kimapato.

  Nisiandike sana ila nakuomba bwana Jembe usiwatetee mafisadi hata siku moja maana sisi tunaoipenda nchi yetu unatutia uchungu mno. MUNGU IBARIKI TANZANIA na WALAANI MAFISADI WOTE WALIOKO NJE NA NDANI YA NCHI YETU TUKUFU TANZANIA. AMEN

 32. DUNDA GALDEN Says:

  BS IJUMAA LEO KUNA KIBAO GANI MMETULETEA?MARADHI TOKA UKO NYUMBANI ACHANANE HUYO CHENGE UKIANGALIA KWA UNDANI HAPO UTAPATA CHENGA JINA TUU HATARI AKUBALI KUJIELEZA AU KUACHIA NGAZI
  VIVA TANZANIA HOPE FULL J.M.KIKWETE
  DUNDA GALDEN(AUSTRALIA)

 33. changalamacho Says:

  Nakwambia katika sakata hili la Chenge kuna watu ‘HARDCORE MAFIOSO’ hawazidi hata 20 hivi wako pembeni wanachekelea kinachoendelea na kumsikitikia kwa yale yaliyomkuta.Its very unfortunate.Tuombe Mungu tu wasianze kutajana.Maana itakuwa Balaa nakwambia.Katika Politics kuna Babu yangu mmoja aliwahi kunipiga kijembe hichi:’If you are in Power and you know you are Corrupt, the best way to protect your authority and your soul is ‘corrupt everybody else in the ranks’.Give them enough rope, sooner or later they gonna hang themselves and you will remain safe’.It all started in Day One.Nawasikitikia sana Civil Service, imeoza ile mbaya!Mimi nafikiri hizi tuhuma tunazo zisikia sikia katika Chama sijui au katika taasisi nyinginezo NI CHA MTOTO tu ndugu zangu!Maana Civil Service itahitaji KUPIGWA DEKI YOOOOOTE KISIBAKIE KITU.Kama tumedhamiria kuikomboa nchi hii.Wapo katika Civil Service ambao hawapendezeshwi kabisa na uchafu huu unaoendelea hapa nchini.Lakini tatizo ni lilelile.Wamezibwa midomo.Hakuna atakaye thubutu kuropoka na kuyaweka maovu yote hadharani.Kila mmoja tayari ana madhambi yake.’If you think you are corrupt, CORRUPT EVERYBODY ELSE if you want to remain SECURE in your Authority!Watumishi wetu wa serikali wanaishi Nyumba za Vioo.Nani mwenye ubavu wa kumrushia mwenzie mawe?Hakuna mwenye Ubavu wa kumgusa Chenge.Wewe subiri utanipigia simu!

 34. Kekue Says:

  Mbona anajiamini sana, eti VIJISENTI!!!! Jamani, jamani.
  Sasa Ndaki unasema tutafika tu, rafiki yangu tutafika lini kwa style hii???

 35. sweetoh Says:

  “Mwiziiiii anaweka WANTED”

 36. KAMANZI kumbe we ni mzalendo ,mi mfanyabiashara ,na nakuambia kwa vyovyote vile alivyofanya chenge na wenzie hata kama ungekuwa wewe ungefanya mianya ya kuchukua pesa kiulaini ni mingi mama mjazito tandahimba au mgonjwa anayekosa dawa bugando anakuhusu nini wakati tunaishi ktk nchi ambayo mambo yote ni pesa, na pesa ndo heshima, utu hakuna ,siwezikubadili msimamo wangu ht iweje bado nawaunga mkono wachakarikaji kama chenge na wenzie (kwangu siwaoni kama mafisadi kama wengi wenu mnavyodai badala yake nawaona wajasiria mali wa kiwango cha juu,)kwa kutafuta pesa kwa nguvu zote na popote ,inabidi ifike wakti tukubaliane ,ni lazima ukubali siasa sio wito tena kwa nchi za dunia ya tatu na dunia nzima kwa ujumla ,bali ni biashara kama una uwezo na wewe wekeza huko,tatizo la wasomi wetu ni maalwatan wa kupiga domo baa,ktk blogs kuhusiana na hekaya za uchumi lkn nikikuuliza umejitoa vp huwezi kunieleza ,babu fidel na che guevara walikuwa tayari kufa kwa ajili ya ustawi wa jamii zao tanzania watu hao ktk kizazi hiki hakuna amini usiamini kamanzi nakwambia ukweli,yakupasa uelewe 2010 inakuja siasa ni biashara lazima uwe na mtaji wa kununua kura chenge asipotafuta hizo pesa kura atanunulia nn,wakati flani mh arcado ntagazwa aliwahi kulalamika katika media kwamba alifanyiwa fitna ktk kura za maoni ,kwa kuwa alikuwa na mkono wa birika ,na yeye ni mmoja kt ya viongozi waadilifu (kwa mujibu wake ),mpaka hapo unaona isivyolipa kuwa muadilifu ktk siasa za nyumbani,point yangu ni kuwa chenge na wenzie kiasilia sio mafisadi(km inavyodaiwa ) ila kama kuna nafasi ya kupata kitu na system inaruhusu sioni kwa nn usichume pesa ,2010 inakuja watz hawa hawa wanopigia kelele ufisadi (si ajabu na wewe mmoja wao mtampa kura jk) ,naamini mtakuwa mmesahau kuwa kavurunda kupita kiasi kuanzia 2005,uadilifu ,sijui utiifu ni altaren na kunakofanana na huku ktk sias a ni pesa na maslahi tu. wenu JEMBE

 37. kijiwe Says:

  aisee mchangiaje 23 you sound like mwana system either baba yako,mama yako,mjomba au ndugu yako anakufaidisha na huu ufisadi.
  there is noo waay mtu clean mwenye machungu na nchi yake akapromote corruption.you should be ashamed of yourself and fearful to your God if you have one!
  ni hayo tu

 38. Mama Says:

  Hata kama ni pesa zake halali kwa nini akaweke Jersey na sio UK mainland?

  Jersey yajulikana kama taxi heaven for money laundry, oligarchs, mafia, drugs dealers, etc. na ndio maana serikali ya Uingereza imetilia mashaka. Tena kwa kiongozi kuweka pesa Jersey ujue hapo kuna namna na yatia aibu. Mtu mstaarabu haweki pesa Jersey island jamani, ataweka UK mainland.

 39. mdunger Says:

  Yaani inauma jinsi wanavyoitafuna nchi,lakini makosa ni yetu,tunawachagua wenyewe tena kwa kishindo.Sasa kwa kuwa hatuwezi kuwawajibisha, uchaguzi ujao tuamue,tuacheni unafiki kwani,ukichagua kijani kuwakomoa wapinzani,unajikomoa na wewe kwa shida tuzipatazo kutokana na ufisadi wao(umeme-richmond,bandari-ticts etc)WATANZANIA TUAMUE KUIOKOA NCHI YETU LA TUTAIKOSA KABISA

 40. kijiwe Says:

  kumradhi wadau kuna kafisadi junior kameingia katika hii lobby nina usongo nako.
  wewe jembe vipi?
  ngoja nikuquote
  1.”kuchukua pesa kiulaini” – kama angechukua pesa kilaini basi zingejulikana tangu alipozichukua.lakini zimejulikana baada ya investigation. huo ni wizi na siyo kuzichukua pesa kiulaini
  2.”mama mjazito tandahimba au mgonjwa anayekosa dawa bugando anakuhusu nini” – hiyo ni dalili ya roho ya korosho na umimi
  3.”pesa ndo heshima” – labda kwako wewe na siyo kwa watanzania wote kama kwako ni heshima nenda askari monument strip naked halafu uone kama hutadharauliwa na kupigwa mawe sanasana utaonekana kichaa
  4.”kwangu siwaoni kama mafisadi kama wengi wenu mnavyodai badala yake nawaona wajasiria mali wa kiwango cha juu” – ujasiria mali siyo kuficha pesa nje ya nchi unless una invest nchini ili pesa zi circulate within the country
  5.”kwa kutafuta pesa kwa nguvu zote na popote ,inabidi ifike wakti tukubaliane” – usiwalazimishe watu kusupport ujambazi na wizi
  6.”ni lazima ukubali siasa sio wito tena kwa nchi za dunia ya tatu na dunia nzima kwa ujumla” – ndiyo siasa SIYO wito lakini tafadhali iwe opinion yako na siyo kutulazimisha maana kwa wengine siasa ni wito na ndiyo maana wengine wanaenda shule wakisoma politics mpaka wanafikia PHD
  7.”ila kama kuna nafasi ya kupata kitu na system inaruhusu sioni kwa nn usichume pesa ” – ndiyo kama kuna nafasi chuma pesa kihalali na siyo kuiba KITU?
  wewe dizain ni kafisadi junior na siyo mfanyabiashara kama unavyojiita sababu hata ethics za economics inaelekea huzijui huwezi kufananisha wizi na ujasiriamali because if you do it means watu kama akina Mengi siyo wajasiriamali.

 41. Bigy Says:

  Kama hiyo hela ni ya wizi basi arudishe na afungwe.Kama ni yake atoe vielelezo aendelee kuwa huru.
  Tutaendelea kuwapigia magoti wazungu na kuwa inferior kwao kwani tumeshindwa kufanya vitu vidogo tu ambavyo wamefanya kuwa na maendeleo. Hivi ni:
  1)Kutoamini kwamba kiongozi ni mungu ama mtu wa kutetemekewa.
  2)kushindwa kufuata sheria tulizojiwekea wenyewe na kupelekea undugunization, ukabila na kuoneana haya
  3)kupenda kupata mafanikio kirahisi kwa kutopenda kazi.
  Ni hayo tu.
  Nasikitika bwana anasema ‘vijisenti’ akiwa ndani ya taifa maskini kama TZ!Sounds weird!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s