BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NAIBU KATIBU MKUU UN NA PAPA BENEDICT XVI April, 19, 2008

Naibu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Dr Asha- Rose Migiro(kushoto) akisalimiana na kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani,Papa Mtakatifu Benedict XVI jana kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York.Anayetabasamu kulia kabisa mwa picha ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.

Papa Mtakatifu Benedict XVI yupo ziarani nchini Marekani ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Marekani tangu ashike wadhifa huo wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani. Alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juzi, Papa aliwaambia viongozi wa dunia kwamba heshima kwa haki za binadamu ulimwenguni kote ndilo suluhisho la matatizo yote yanayoikabili dunia hivi leo.

UN Photo/Mark Garten.

Advertisements
 

7 Responses to “NAIBU KATIBU MKUU UN NA PAPA BENEDICT XVI”

 1. Albert Says:

  sasa watanzania msome hali ya ulimwengu ilivyo na msiwe wenye mawazo ya kizamani angalieni huyu Papa Mtakatifu Benedict XVI historia alikuwa miongoni mwa kudi lile la one (Race ) na leo hii yeye ni kiongozi wa makanisa hii inamana kuwa binadamu anabadilika lakini viongozi wetu Tanzania hilo hawalitaki

 2. Malenga Says:

  Mtakatifu…….mmmm (takasika)

 3. Amina Says:

  haya sisi wengine hatuyajui mambo haya tusije tukachingia pumba

 4. hatbah Says:

  ni picha nzuri na inaonyesha ishara nzuri pia lakini je mbali na kuomba amani huyu katibu mkuu anaisaidije tanzania ambako ndiko alikozaliwa?ufisadi umezidi ikiwezekana labda huyu papa ben nae aje atuombee labda watu watamkumbuka mola na kurudi kundini kwani sidhani hawa mafisadi wanakumbuka kama kuna MUNGU na kuna KUFA.

  Mtu mmjoja unajilimbikizia mali kibao utazikwa nazo?kwa nini hatukumbuki kua KUNA MUNGU NA KUNA KUFA KISHA TUTAACHA KILA KITU DUNIANI.Je braza Ditto leo atazikwa na majumba au mapesa aliyooyacha?

  NINAOMBA USIKU NA MCHANA MUNGU ATUEPUSHIE HUYU SHETANI.ROSE MIGIRO AMEFIKA MBALI KWA BARAKA ZA MUNGU KWANI SIDHANI KAMA ANGEFANYA UFISADI KAMA WA CHENGE,SUMAYE,UNCLE MKAPA,LOWASA,KARAMAGI,MSABAHA,MEJI NA WENGINE ANGEWEZA KUONEKANA DUNIANIA.

  DADA ROSE MIGIRO KUMBUKA KUJENGA NYUMBANI USISAHAU KWENU KWA MARAHA YA ULAYA.HUENDA UKAWA SI FISADI ILA UKAWA MWACHA MILA.JARIBU KUA FISADI KAMA HUJAPIGWA SHABA.HUKO KWA WATU.TULETEE MAENDELEO MAMA.

  mungu ataendelea kukuletea neema kwa mema yako.namkaribisha papa tanzania.

 5. Twaha Figo A-City Says:

  Duh,ebwana maza Migiro at least unatupaisha wabongo kimataifa.

 6. BABA MTAKATIFU BENEDICT XVI KARIBU TANZANIA TUNAKUSUBIRI KWA HAMU KUBWA,UJE UTOMBEE MAANA MAFISADI WAMEZIDI KUWA WENGI

 7. Gebo Arajiga Says:

  Sawa anatuwakilisha vyema sana huyu mama SWALI JE? ATATUSAAIDIAJE SISI WATANZAANIA KUTOKANAA NAA MAATATIZO AMBAYO SASA YAMEANZA KUIKUMBA VIBAYA NCHI YETU,NJOO NAAIBU KATIBU MKUU USULIISHE ZANZIBAR KATI YA CUF NA CCM NJOO UKEMEE WANAOUA ZERUZERU,NJOO UKEMEE UBADHIRIFU UNAOFANYWA NA VIONGOZI WETU UWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII…………………YANI MAMBO NIMENGI MNO JAMANI LAKINI ……SISEMI HADI YATAKAPOTIMIA NIKIWAA MSTALI WAA MBELE BI-UP MAMA MIGIRO TUNAKUTEGEMEA UA MNASEMJE WACHANGIAAJI WENZANGU KAMA NAKOSEA SEMENI


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s