BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DITOPILE MZUZURI HATUNAYE TENA! April, 20, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi,Uncategorized — bongocelebrity @ 8:59 AM

Habari ambazo zimetufikia kupitia vyanzo mbalimbali zinasema kwamba aliyewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Athumani Ditopile Mzuzuri amefariki dunia ghafla leo asubuhi kwenye Hotel ya Hilux mjini Morogoro alipokuwa amefikia kwa mapumziko kidogo akitokea Dodoma.Kifo chake kimethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro,Dr. Meshack Mmasi.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Mpaka kufariki kwake, Marehemu Ditopile ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za ki-uongozi serikalini, alikuwa akikabiliwa na kesi ngumu ya mauaji ya dereva wa daladala,Hassan Mbonde, tukio lililotokea katika maeneo ya Kawe jijini Dar-es-salaam mwaka jana.Tutaendelea kuwaleteeni habari zaidi kuhusiana na msiba huu kadiri tutakavyozipata.Pole kwa ndugu,jamaa na marafiki wote wa marehemu.

Advertisements
 

57 Responses to “DITOPILE MZUZURI HATUNAYE TENA!”

 1. Kipanya1 Says:

  INALILAH WAINALILAH RAJIUN.
  SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE NDIYO MAREJEO YETU SOTE.

  NAPENDA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA KAREHEMU “Ukiwaona Athuman Ditopile Mzuzuri.
  PIA KWA WATANZANIA WOTE KWA MSIBA HUU. ALIKUWA KIONGOZI SHUPAVU NA SHUJAA WA TAIFA HILI.

  ALLAH ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMEMA PEPONI

  AMINA

 2. ibrahim Says:

  Inna lillahi wainna ilayhi raaji’un

 3. Gervas Says:

  Man made judges can be biased but God is final and Supreme judge who cannot even be bribed. Never revenge on earth!! always allow God to revenge for you. Roho ya marehemu Ditopile na yule Dereva wa daladala aliyetangulia zilazwe mahala pema peponi……..Amen!

 4. Subby Says:

  Innalillahi wainaillaihi rajiun,

  Yeye mbele katangulia sie tuko nyuma yake hatujui siku wala saa.

  Poleni wafiwa Mungu awape moyo wa subira!

 5. michuzi Says:

  ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kepteni Mstaafu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri amefariki leo Aprili 20,2008 majira ya saa 3:00 katika Hotel ya Hilux iliyopo Mkoani Morogoro.

  Ditopile ambaye Aprili 21 (taarifa nyingine zinasema ni Aprili 24)alitakiwa Kisutu katika kesi yake ya tuhuma za mauaji amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60 kwa kile kinachoaminika ni shinikizo la damu.

  Ditopile alifikia Hilux ,Morogoro akitokea Tabora akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam kwa mapumziko akiwa ameambatana na mkewe mdogo,Tabia.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa hoteli hiyo Joseph Kitambi, Ditopile alifika hotelini hapo Aprili 18, majira ya saa 5:30 usiku,ambapo alipatiwa chumba No.106.

  Kitambi alisema Aprili 19,majira ya saa 5:00 usiku watumishi wa hoteli hiyo wakati wakifunga shughuli zao za huduma, Ditopile alikuwa bado hajarudi hotelini kutoka kwenye shughuli zake ambazo amekuwa akizifanya kwa muda wote tangu kufika hotelini hapo.

  Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo alisema, Aprili 20 majira ya saa 2:30 asubuhi mkewe Tabia alitoa taarifa ya kuzidiwa kwa mumewe na kuomba msaada ambapo wahudumu walifika katika chumba chake na kumwangalia na kukuta akiwa amelala kwenye kochi,na alionekana kuwa ni mtu asiyejitambua,na kutoa taarifa kwenye hospitali kuu ya Mkoa kwa msaada zaidi.

  Mkurugenzi huyo aliiambia habari leo kuwa marehemu alifariki kabla ya kupata kifungua kinywa cha asubuhi ambacho hutolewa na hoteli hiyo kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi majira ya saa 4:30.

  Alisema kuwa wauguzi wa hospital walifika katika hoteli hiyo,na kumchukua kwenye gari,akionekana kama mtu ambaye ameshafariki,na kumpeleka hospitalini kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi.

  Hata hivyo Mkurugenzi huyo alidai kwa kipindi chote ambacho Ditopile amekuwa katika hoteli hiyo,alionekana kuwa ni mtu aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi,kutokana na mwili wake kudhoofu na nyuso kutokuwa na uchangamfu.

  Aidha alidai kuwa wakati wafanyakazi hao wanautoa mwili wake nje kwa kushirikiana na madaktari waliofika kutoka hospitalini,walikuta mswala wa kuswalia,ambapo mkewe alidai kuwa mumewe aliamka alfajiri na kuswali swala ya asubuhi,kabla ya mauti kumkuta.

  Baada ya mwili huo kufikishwa hospitalini Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Dkt.Meshack Masi alisema alipokea taarifa kutoka kwenye uongozi wa hoteli hiyo,iliyoeleza kuwa Ditopile amezidiwa hivyo wanahitaji msaada haraka.

  ‘Kweli tulipokea taarifa hizo…walikuwa wakiomba msaada haraka…na sisi tulituma gari pamoja na wauguzi mara moja kwenda pale Hilux hoteli na kumleta hapa hospitalini’alisema Daktari Masi.

  Hata hivyo Dkt.Masi alisema baada ya wauguzi kufika hotelini hapo,na kuuona mwili wake waligundua kuwa ameshafariki na kuubeba mwili wake na kuupeleka hospitalini hapo na kuulaza wodini grade 1, kwa ajili ya kuudhibitisha,kabla ya kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Thobias Andengenye alisema kuwa marehemu alipotoka mkoani Tabora alifika Mkoani Morogoro na kwenda Wilaya ya Mvomero kwa ajili ya kukagua mashamba yake yaliyopo kwenye eneo la Mgongola akiwa na mkewe mdogo Tabia kabla ya kufika Morogoro Mjini ambapo alipata malazi.

  Aliongeza kuwa baada ya kukagua mashamba yake marehemu aliondoka Wilayani Mvomero na kuja Morogoro Mjini ambapo alifika majira ya saa 3 usiku na kufikia kwenye hotel ya Hilux iliyopo Mjini hapo kwa ajili ya kupata malazi ambapo alipewa chumba No.106.

  Alisema marehemu aliitumia siku ya Aprili 19,kutembelea ndugu na jamaa zake kabla ya kurudi nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam,na kudai kuwa alirudi hotelini hapo majira ya saa 12 jioni,ambapo alitarajia kuondoka Aprili 20 kurudi nyumbani kwake.

  Katika ziara ya marehemu ya kutembelea na kusalimiana na ndugu zake,pia alipata wasaa wa kumtembelea Chifu Kingalu Mwana Banzi wa 14 wa kabila la waluguru.

  Kwa upande mwingine mdogo wake na Marehemu, Selemani Mzuzuri,alipohojiwa alisema hana lolote la kuzungumza na kueleza kuwa bado ana majonzi mazito ya kifo cha kaka yake,hivyo hataweza kuzungumzia jambo lolote.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jeneral mstaafu Said Kalembo ambaye alifika hospitali ya mkoa wa Morogoro akizungumza na waandishi wa habari alisema kwamba mwili wa marehemu unatarajiwa kuchukuliwa na gari la jeshi na kusafirishwa kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo iliyopo Dar es salaam.

  Baadhi ya viongozi ambao walifika hospitalini hapo kumuona Marehemu ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Said Mwambungu,Katibu wa CCM Mkoa Mary Chatanda,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Eng.Petro Kingu,Meya Prof.Romanus Ishengoma,Naibu Meya Amir Nondo,pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa chama na serikali.

  Ditopile ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa,amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Lindi na Tabora kabla ya kukabiliwa na kesi ya Mauaji.

  Habari kama hizi na picha nenda pia lukwangule.blogspot.com

 6. Kimori Says:

  Life is very short….we have to live it uprightly!
  RIP

 7. DUNDA GALDEN Says:

  INNALI LILLAHI WAINNA ILAYHI RAAJI`UN,Mungu ailaze roh ya marehem mahali pema amsamehe makosa yake.
  INSHALLAH

 8. Chris Says:

  My condolences to his family members….

  Aiseee nasikia fisadi Chenge kajiuzulu… plse update us…. tupeni news….

 9. Bablii Says:

  Kila kilichozaliwa, na kufa nilazima!
  Na hayakuwa maisha ya duniani ila ni upuuzi mtupu..! Lakini kwa pumzi tuipatayo wakati mwengine binaadam hujisahau, tuka takabbar, tukijiona tumemiliki roho za watu wengine mikononi mwetu, hujawa na kibur na jeuri, tukasahau kwamba sisi sote waja wa mungu, na kwake ndio marejeo.

  Naomba nisiwe mnafiki kwa kuanza kumsifia Ditto na kumtakia madua ya kwenda peponi.

  Mimi nnachoweza kusema ni Mungu mlipe Ditto vile anavyostahili…!

  Kwa tuliobaki hai, wale wenye vijisent kwenye account za Uk, wale wenye miradi ya Kiwira, wale wenye miradi ya Richmond, wale wenye dili za EPA,wale wahafidhina wasio taka muafaka zanzibar, wale mafisadi wote wa nchi hii! Ningeomba kwa msiba huu mpate tanbih, mlete fikra, mtanabah na mjuwe kwamba hayo yote mfanyayo iko siku mtakufa, mali na fedha zote mtaziacha hapa hapa duniani, kikubwa watu mliowaacha wakiwa hali duni kwa ulafi wenu basi watawakumbuka kwa maovu yenu, hata wakiwasifu basi ni sifa za kinafiki, kwa maana haziwasaidii kitu.
  Naam kisha mtakutana na alie m’bora wa kuhukumu!

  Familia ya Ditto, kwani mkuki kwa nguruwe tu…!
  Hivi nanyie mnajuwa kulia kumbe?! Nanyie mnapata hudhuni?!
  Uko wapi ule ubabe, kibri na dharau mlizokuwa mkionesha pale mahakamani? Hata mkafikia hatuwa kuwapiga waandishi wa habari! Mkaimba nchi ina wenyewe…!
  Wallah laiti mngejuwa kwamba dunia hii mwenyewe ni mungu tu…!

  Ah! haya basi nanyie leo onjeni, kama waliyoyaonja familia ya yule dereva wa dala dala aliekatishwa uhai wake na risasi ya kaka yenu!

 10. Mama wa Kichaagg Says:

  R.I.P,

  Bwana ayajua mapito yetu na majuto ya matendo yetu.

  Wengi watalaumu kitendo cha kumuua Konda/dereva wa daladala pale Kawe , LAKINI wasisahau kwa Mungu hakuna dhambi ndogo wala kubwa, ZOTE NI DHAMBI.

  “Kuiba ni dhambi, kusengenya ni dhambi, kuzini ni dhambi, kusema uongo ni dhambi, kufisadi ni dhambi, wivu ni dhambi, kuonea ni vyambi, kutowajibika (nyumbani/kazini) nk ni dhambi!”

  NA ASIYE KUWA NA DHAMBI BASI AENDELEE KUMSAIDIA MUNGU KAZI YA KUMHUKUMU MAREHEMU.

  R.I.P. DITOPILE NA POLE NDUGU NA MARAFIKI WA KARIBU

 11. Saidi Situ Says:

  Huyu jamaa amekufa kabla haki haijatendeka. Yaani hili linchi mara mia tuiuzie America ili iifanye dampo la Nyuklia kila mtu achukue hela yake aangalie mbele.

 12. kimk Says:

  Inallilah,
  Huyu bwana na chenge hawana tofauti kwa kauili za maudhi.
  Si huyu aliyemtwangwa risasi dereva wa dala dala!!!!

 13. Saidi Situ Says:

  Mimi siwezi kuwa mnafiki nasema kweli huyu jamaa nitamkumbuka kama Muuaji aliyeruhusiwa kukata mitaa. Na bado huko anaenda kupokelewa na yule dereva wa daladala.

 14. Ali Says:

  INALILAH WAINALILAH RAJIUN KILLER HAS GONE AS WELL HUO NDIO MWISHO WA BINADAMU KWA M MUNGU NDIO MAREJEO YETU MMUNGU ATAMUWEKA ANAPOSTAHIKI KUWEPO

 15. Mbarikiwa Says:

  Mwenyezi Mungu, muumba wa Mbingu na Nchi aliyemuumba Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri, hatimaye amemchukua.

  Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

 16. Subby Says:

  Muislamu hasa mwenya kujua uwezo wa Mungu na neno kadri/kudra ya Mungu na hatma, mwanadamu mwenzie na hasa mwislamu mwenzio akifanya jambo baya au akitengeuka inatakiwa badala ya kumcheka au kumlaani ni kuomba kwa Mwenyezi Mungu na huwa tunaomba hivyo hivyo ‘innallillahi wa Innaillaihi rajiun’. Kwani sie wanadamu hatujui hatma yetu wala hatujui kitakachotokea mbele yetu japo dakika moja ijayo seuze siku au mwaka.

  Mwanadamu afurahiae madhila ya mwezie na kumlaani hajui na yeye kitakachomkuta maana mitihani ile ya mwenzie anayoichekelea basi Mungu humpa kama ile au mikubwa zaidi ya ile. Lakini huwa tunajifanya waislam lakini nafsi zetu hazitaki kurudi kwa Mola wetu. Nani ajuaye pengine Marehemu Ditto alilia na kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu kwa makosa yake na hayo ni siri yake na muumba wake hakuna anayejua wala atakayejua. Je siye, tuliojawa na vibri na jeuri ya kumhukumu kiumbe aliyeumbwa na Mungu kama vile tu watakatifu na wakamilifu? Je tunaijua hatma yetu, kama mama wa kichaga alivyosema, sidhani kama tuna haki ya kutoa hukumu kuwa Mungu atamfanya hivi au vile anaweza kukufanya wewe yale umuombeayo mwenzako. Waislamu huombeana mema na maghufira na hujiombea wenyewe mema na maghufira pia, hakuna anayejua hatma yake hapa duniani mpaka yeye ajifanye kijogoo wa kutoa hukumu ajivike joho la Mungu kwa kibri tu kwa kuwa anasauti au ana uwezo wa kusema atakavyo. Hata kama ndugu wa marehemu walikosea hakuna mwenye haki ya kuwahukumu ila Muumba peke yake, maana sie pia si malaika tuna udhaifu wa kibinadamu.

  Na aliye malaika humu ndani ambaye hajamkosea binadamu mwezake achilia mbali kumkosea Mungu na awe wa kwanza kurusha jiwe ama sivyo tuache kazi ya Mungu ifanywe na Mungu.

  Kuna watu wanapenda kuvaa joho la Mungu humu sijapata kuona. Huwezi kuwasikia hata siku moja wanatoa kauli nzuri kuhusu mtu si kwenye blogu hii ya BC, si ya Michuzi na kokote utakapoona wamekoment basi ni negative. Hapo sijui wameshawauzi watu wangapi na sijui kama wamepata au watapata bahati ya kuwaomba msamaha. KIBRI NI JOHO LA MUNGU!

 17. klontjen01 Says:

  poleni sana kaka dito kaenda kwa mbonde sasa

 18. Kingson Says:

  Poleni na msiba wafiwa.

  Duniani tenda wema uende zako……Maisha tunayoishi ni mafupi tukiweka kumbukumbu zikiwemo nzuri au mbaya. Tunajifunza kupitia watu kwa mazuri au mabaya wayatendayo. Mungu ndio mtoa hukumu ya haki. Kila mmoja wetu atasimama mbele yake mtoa hukumu ya haki.

 19. Chala Says:

  Inalilah raju’n… Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema peponi ..amsamehe na dhambi zake amin.

 20. Amina Says:

  saidi situ kuna dongo lako humu umetumiwa…soma comments vizuri zote mheshimiwa!mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi…rama ditopile pole kwa msiba uliokukuta.. pamoja sana tu

 21. Salim K Says:

  Inna llillah, MwenyeziMungu amsamehe dhambi zake na amuingie peponi kwa rehma zake

 22. salma Says:

  mwenyezi mungu amuweke mahali pema peponi amina, ampunguzie adhabu ya kaburi kwa mema na mbaya Inshaala apokee kitabu chake kwa mkono wa kulia, nawapa pole ndugu jamaa na marafiki wote na wadau wote wa bc.

 23. beatrix Says:

  ASIYE NA DHAMBI NA ATUPIE MAWE JENEZA LA DITTO,
  KILA MTU ANA DHAMBI HAKUNA ALIYE MSAFI. HUU SIO WAKATI WA KUMHUKUMU DITO.
  POLENI NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA DITO
  BWANA ALITOA BWANA AMETWAA AMEN.

 24. gaetano Says:

  kusema uongo dhambi na msema kweli mpenzi wa mungu,,mimi sijahuzunishwa na kifo cha huyu mtu hata kidogo,ni hayo tu.

 25. TATU Says:

  YANI SUBBY UMETOA MANENO YA HEKMA SANA NAUNGANA NA WEWE WANASEMA HIVI UKIMNYOOSHEA KIDOLE MWENZIO ANGALIA VIDOLE VINGINE VINAMUELEKEA NANI? JIBU KAMA SIO WEWE JAMANA WADAU TUWE WEPESI WA KUSAMEHE NI HAYO TU.LEO HII UNAWEZA UKAWAKUTA HAO HAO FAMILIA YA MAREHEMU HASSAIN MBONDE WAKISHIRIKIANA VIZURI TU MSIBANI MKABAKI VINYWA WAZI.

  INALILAH WAINALILAH RAJIUN

  NAWATAKIA FAMILIA YAKE WAWE NA MOYO WA SUBRA

  WADAU PUMZI ZISITUDANGANYE

 26. ummy Says:

  Hivi we subby unaongeaga nini?kila mtu anawazo lake la kuandika humu isipokua matusi tu ndo hayaruhusiwi…..usifundishe watu cha kuandika hapa, ndiyo kafa lakini na ubaya wake lazima uzungumzwe,umekaza joho la mwenyezi mungu unaleta tarabu hapa

 27. Matty Says:

  Mungu awalaze roho za marehemu mahali pema peponi Amina….yeye pamoja na yule dereva wa daladala aliyeuawa.

 28. Mtukwao Says:

  Jamani embu tusijaribu kuwanyamazisha watu wasiseme yaliyopo moyoni, nawao ndio njia yao ambayo wanweza kumsamehe Dito.

  Everybody praying dini’s card!!

  Kama Dito aliomaba msamaha kwa Mungu hilo sisi hatulijui, lakini nawezakuhakukuakishia kuwa Dito hakufanya “Toba ya kweli”. Kwasababu kama alitubu, basi angekubali kosa alilo tenda au angekanusha ila lazima angeomba msamaha wale ndugu wa devere wa daladala, especialy wazazi wa marehemu then aombe msama kwa Mungu wake. Huwezi kuomba upatanishi kwaMungu wakati yule huyekosana naye hampatani. “huwo ni uwendawazimu kama si ucrazy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!”‘

  Lakini baadhi yetu sisi tuliobaki unapotutajia jina la Dito kumbukumbu ambazo zinatujia ndizo hizo baadhi yetu wamezitaja hapo juu. na hamuwezi kuziondoa akilini mwetu au kutulazimisha kuzisahau kwa kutumia vigezo vya dini!!!!

  Aliyoyatenda yote yameingizwa ktk history ya Dito hapa duniani na zimeandikwa/ zitaandikwa ktk vitabu vya historia ya Tz. Ktk historia ya mbinguni hiyo tumwachie Mungu, sisi tutaongelea ya hapa duniani.

  Mbona Sauli aliuwa watumishi wa Munguna alifanya toba, lakini mpaka leo bado tunahubiriwa juu mauwaji aliyoyafanya?? Mbona Yuda alimkana Yesu nahatujui kama alitubu au la, lakini bado wanahubri kuhusu kumkanakwake Yesu.

  Acheni watu waseme ukweli. Hatufurahii kufa kwake but kufakwake hakutuzuii kumzungumzia matendo aliyoyafanya!!! Sikwasababu tunamchukia au hatujamsamehe la hasha, ivyo ndivyo tulivyo mjua!!!!!!!!!!!!!!

 29. Dinah Says:

  He looks/looked good at 60,
  Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yote uliyotenda hapa Duniani, uende salama.

 30. Kekue Says:

  Mtu kwao u mk ma dy!!!!!! R.I.P Ukiwaona.

 31. `Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana liimidiwe. Binadamu tujifunze kuwa maisha yetu hapa duniani nimafupi sana na kwamba atujui tutakufa lini. kwa hiyo hatuna budi kuishi maisha mema na ya kumpendeza mungu.

  Roho mbaya na visasi vitatuangamiza na kututenga mbali na mungu. usimfanyie mabaya mwenzio kwa kuwa ujui cha mbele ni kipi na kuwa utakufa lini.

 32. Saidi Situ Says:

  Amina nimeshindwa kuliona nisaidie liko kwenye post gani hilo dongo? Kama ni humu basi huyo mtu hakutaja jina langu.

 33. Saidi Situ Says:

  Ok nimeliona Amina. Thanks ila sina majibu.

 34. Gebo Arajiga Says:

  Napenda kutoa pole kwwa wot wanaaohusikaa naa msiba hu mzito nadhaani mungu amtoa na mungu ametwaa

 35. mkereketwa Says:

  Jamani, hebu Watanzania someni vitabu vya mwenyezi mungu, mbona mnaandika kama wote ni mapagani? MMesikia umekutwa mswala chumbani alikofia. Mwenzenu pepo ameishaiona, Mwenyezi mungu ni mkubwa wa kusamehe, piga goti mlilie atakupa na kukusamehe kosa LOLOTE LILE. Nyie mnapiga domo mwenzenu amepumzika peponi! Kwani najua ni mwanazuoni mzuri. Kaisoma Quran yake alfajiri na kujihukumisha kwa mwenyezi mungu, nyie mnaopiga domo mmejiombea madudu yenu mnayoyafanya? Jiulizeni kwa nini mwenyezi mungu kamchukua labda kulikuwa na fedheha inakuja! Kaamua ampumzishe kiumbe wake aliyemtii. DO YOUR OWN DEED LIVE HIM ALONE. Pole Auntie Aswila na Watoto jamani kwa msiba huu mkubwa. Inshallah MWENYEZI MUNGU ataleta rehma zake.

 36. Subby Says:

  Neno Kibri ni joho au nguo ya Maulana au ni Joho la Mungu ni mojawapo ya mafundisho ya kiislam, kama wameimba kwenye taarabu hayo ni ya kwao kwani ni mengi wanayoimba.

  Hayo niliyoyasema ni kutaka kuwaausia waislam wenzangu wasikengeuka na haya mambo ya duniani, kwani sie waislamu ni jukumu letu kuamrishana mema na kukatazana mabaya. Na hata hilo la kusema mwenzio akifikwa na msiba usifurahie ni mafunzo ya dini pia. Wenyewe wanafahamu na hapa nimewalenga waislam kwani wajibu wao wanajua wanapaswa kutamka nini panapotokea msiba, na wala si amri yangu wala sina uwezo wa kumkataza mtu au kumzuia mtu asifanye atakalo ni katika kukumbushana maamrisho ya Mungu yanasemaje. Ndio maana nilivyoanza kusema nilitanguliza neno waislam, kwa sababu hayo ndiyo mafundisho niyajuayo. Na wanaojua mafundisho ya dini nyingine pia kama mama wa Kichaga na yeye ametoa mchango wake kulingana na mafundisho ya dini yake.

  Iwapo kama kuna mtu nimekwaza anisamehe lakini nitasimama pale pale kwenye mafundishoi kuwa kazi ya kuhukumu ni ya Muumba, kwa sababu tungepewa sie hiyo kazi hakuna ambaye angebaki hapa duniani!

 37. hombiz Says:

  Marehemu Ditopile alifanya nini Novemba 4, majira ya saa 1:00 usiku katika eneo la njia panda ya Bagamoyo na Kawe wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam?. Jibu ni kwamba alimuua Hassan Mbonde ambaye alikuwa ni deleva wa daladala.
  Halafu alfajili ya April 20, 2008 ktk hoteli ya Hilux iliyoko mkoani Morogoro, Ditopile akiwa na mkewe mdogo aliamka mwenye afya njema na kusali sala ya alfajiri na kisha wakaanza kuangalia vipindi vya runinga halafu mauti yakamkuta, mkewe akiwa amepitiwa na usingizi. Kafa ghafla bin vuuu!.

  Swala moja kubwa linalonifurahisha juu ya kifo hiki ni kwamba marehemu Ditopile alimkumbuka Mola wake kwa sala kabla hajafariki. Natumaini alitumia wasaa huo kutubu zambi zake zote na kuwa msafi wa roho kabla hajafariki. Kama hivyo ndivyo, basi bila shaka MOLA atamlaza pema peponi. Natumaini pia kuwa alimuombea na Hassan Mbonde ktk sala zake ili naye apumzike kwa amani, pema peponi.
  MOLA aliwatoa, MOLA amewatwaa.
  AWAPUMZISHE KWA AMANI.
  AMINA
  NB: Ndugu zanguni. Inafaa tujifunze kuishi na kumtumikia MWENYEZI MUNGU saa zote kwani hatujui siku wala saa. Ulevi wa madaraka, ufisadi, jeuri hasira na maovu mengine mengi hayatatusaidia lolote siku ya mwisho. Afadhali hata marehemu Ditopile alipata japo nafasi ya kusali muda mchache kabla ya kufariki. Sisi tuliobaki duniani hivi sasa tukeshe tukiomba kwani hatujui siku wala saa ya muda wetu wa kuondoka hapa duniani. Pia haijulikani kama tutapata japo wakati wa kuungama dhambi zetu mbele ya MUUMBA.
  Narudia tena, ni vema tukikumbuka kusali na kuishi maisha ya kiadilifu siku zote za maisha yatu ili tuwe na nafasi nzuri zaidi ya maisha baada ya kifo huko tuendako.

 38. michelle Says:

  Mhhh Mtukwao nakuunga mkono sana kwa poit zako, Kwanza kabisa pole kwa familia ya marehemu.

  Ukweli ni kwamba tunakuwa wanafiki sana, huyu ndugu aliua, hawa madereva na makinda wanudhi sana lakini huwezi kujichukua hatua ya kua mtu, as if wewe ni Mungu.

  Pia tusijaribu kujidanganya kwa kumuombea huyu mtu msamaha kwa Mungu kama yeye mwenyewe hakuomba msamaha basi sisi twafanya kazi bure tu, huyo Mr Ditto hakuwahi kuwaomba msamaha familia ya huyu konda na hakuwahi kukiri mbele ya mahakama kuwa alifanya kosa, tazama Mungu hadanganyiki wala huwezi kumsahaulisha kwa kujifanya kufanya sala za mapema usubuhi, apandacho mtu ndicho avunacho.

  Ni huzuni sana mtu anapofia dhambini hata malaika mbinguni na vyote huwa kimya. sijue niseme nini kama hakurekebisha mambo yake itakuwa ngumu sana hata tukiombva vipi, basi Mungu na atusaidie.

 39. mimmy Says:

  Huyu marehemu Ditopile ameshakufa, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa hatua yake na kumwombea kila la kheri kwa safari yake hii ya mwisho. lakini vilevile HISTORIA NI HISTORIA, itakumbukwa tuuu, iwe ni mbaya au nzuri itakumbukwa.

  Ditopile aliua mbele ya watu wasiopungua 35, hata kama iliingizwa siasa hapo katikati kwa kutokana na madaraka aliyokuwa nayo enzi za uhai wake hapa duniani. hiyo watu hawataacha kukumbuka na kuizungumzia, LEO hii yuko mbele ya mola wake, huko hakuna ujanjaujanja ila ni AMAL yako tuu.

  Mungu mpunguzie adhabu za kabri inshaalah!

 40. ummy Says:

  ok basi subby pole basi kwa msiba uliokukuta

 41. sally Says:

  Mungu akulaze mahali pema pepon

 42. fatma Says:

  ina lillahi wa ina illahi rajiun…
  hakika mwenyezi Mungu yupo nasi sote
  ila sio vizuri kumzungumzia vibaya maiti..
  hata kama mtu alitenda maovu mangapi nafsi yake
  anaijua yeye na Mungu tuu.
  Unaweza mlani au muhukumu marehemu hapa duniani
  ila hujui ahera kapata nini…
  wote tunaenda kwa Mola tumuuombeeni mwenzetu apte
  kuiona pepo kwani hatuwezi jua kati ya yeye mnayemuita muuaji na sisi nani atahukumiwa na Mola…

  inshallah Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi
  amin

 43. fatma Says:

  mkereketwa
  nakuunga mkono sana na Mwenyei Mungu
  akuzidishe hekima na imani
  Inshallah…

 44. obare merc Says:

  Jamani labda tuache kuongea saaaaana, maana wengine waona si vyema kumzungumza maiti wa wenyewe, mi naona tu pia kuwa tusimseme huyu mutu kwa kuwa Waislam wenyewe wanaruhusiwaga tu kuua, labda ndo sababu hata huvaa mabomu tena hupata dhawabu kwa Mola wao, sasa inabidi tu tusiseme ilimradi Dini yao yawaruhusu basi.

 45. Mtukwao Says:

  Kunatitofauti kati ya “KUMUHUKUMU MTU” na “KUZUNGUMZIA MATENDO YA MTU”.

  Hakuna hata mmoja anaye muhukumu DITO. ila tunasema yake aliyo yatenda yawe mabaya au mazuri tutayaongelea.

  WaTz tuache unafiki wa kupamba maiti/ marehemu.

  Mtu akitenda kosa mnamlaani vikali but hilo kosa hugeuka na kuwa jema mara tu mtu huyo anapokufa. ….oh marehemu alikuwa mtu…..

  “mwema sana, alipigania haki za wananchi sikuzote”,…… wakati huku alikuwa FISADI na HASIYE NA HURUMA kama Mh. Chenge yani hata spire yake haijapatika duniani.

  “mpole sana”… wakati ni JEURI kama alivyo MKAPA.

  “alipenda watu wote”….. wakati alikuwa mtu ASIYE NA UTU hata akadiriki kuuwa mtu hadharani eti kwasababu tu kagonga “SUV” yake kama alivyofanya DITO.

  “wenye heshima kwa kila mtu bila kujali maskini au tajiri” ….DHARAU zimewajaa mpaka kwenye kope za macho mpka kuwaambia watu “hii inchi inawenyewe” kama walivyo sema nduguze DITO bila kujua kuwa hii dunia ina ONLY ONE OWNER ambaye ni GOD”.

  “Mchapa kazi”….KILAZA, mkuu wa MAFISADI na hasiye jali wanainchi wake kama alivyo KIKWETE.

  “Mkimya, Asiye penda kunungunika” ….while ni mlalamishi asiye kubali makosa yake hata kama kosa linaonekana waziwazi kama alivyo LOWASA.

  “mpenda Amani”….. while kila siku ni kuandama na mikutano ya uchochezi kama alivyo maalimu Seif na Lipumba.

  “Hakuwahi kugusa mali ya mtu”….wakati ni WEZI wakubwa kama walivyo Mramba, Yohan, Msabaha, Sumaye, Karamanyi na Bilali pamoja na mtandao wote wa mafisadi.

  anyway ngoja niishiye hapo maana sitawamaliza, but nawaomba msome vizuri Comment za watu. Kuhukumu mtu ni dhambi hatamimi nakubali but up to this point hakuna anaye muhukumu Dito. Watu wanaongelea tu mambo aliyo yafanya and how do they know and will remember him!!!!!

  Wewe unayesema kuongelea maiti ni dhambi…mhh sijui unatumia kigezo gani….maana “mituwe wote ni marhemu ” nabado tunawaongelea.

  Watu tukumbuke kuna kitu kinaitwa “freedom of speech” as long as hamtumtukani mtu wala kumdhihaki busi let us talk.

 46. ummy Says:

  we obare unaleta mengine hapa na udini ehh?kwani wakristo hawauwi?wachaga wangapi majambazi arusha huko wanauwa?umeanza ehh

 47. annabell Says:

  pole kwa familia
  nimeshangazwa sana
  ila ndio hivyo,
  what comes around goes around

 48. obare merc Says:

  Ummy usinielewe vibaya, hili ni kweli si swala la dini,
  ni kweli wachaga na makabikabila mengi wapo majambazi wanaoua,kwa wale ambao ni wakristo wanaua tu lakini wanajua hawaruhusiwi kabisa.

  Ila kwa dini ya waislam nasikia wanaruhusiwa na hupata dhawabu kubwa, hivyo sikwamba namlaumu ila nilichosema ni kwamba kama dini yake inamruhusu msimsakame sana pengine yeye alikuwa na amani moyoni mwake, na ndugu zake walimtetea pale mahakani wakisema kuwa nchi ina wenyewe sasa sisi tunalaumu kitu gani?

  pengine wao huku peponi sa hii wanakimbizana tu na pisto zao na mwingine kwanye kibasi chake wanamfurahia Mungu wao kama ni kweli wanaruhusiwa kuuana, halafu wote siwalikuwa dini moja basi msiwazogoe sana jamani.

 49. michelle Says:

  mmmmmmmmmm nanihiiiiiiiiiiiiiii

 50. Ummy Says:

  Mi mwislamu lakini ninavyojua uislamu unaruhu kumuua kafiri ambae ni adui yako lakini siyo kivyovyote vile kama alivyofanya dito siyo maelekezo ya dini,kwahiyo we usiingize dini hapa na usiongee vitu kwa kuhisi tu kua na uhakuka navyo

 51. obare merc Says:

  Sasa wewe Ummy kafiri ni mtu wa namna gani, au kafiri yupi,maana hata mtu mwenye makosa hutakiwi kujichukulia haki mkononi na kuua maana wewe ni nani hata kutoa roho ya mtu, kama hujawahi umba taha sisimizi unawezaje kutoa uhai wa mwengine? ina maana huyo dreva alikuwa kafiri?

 52. michelle Says:

  Ummy na obare poleni kwa msiba wa huyu ndugu, maana naona mmeumia sana, msijilipue kwenye site hii amani tu.

 53. obare merc Says:

  Jamaniiiiiiiiiii BC mbona mnabinya comments zangu au ni ubaguzi tujue?

 54. michelle Says:

  Mwacheni mwenzenu apumzike vizuri, hakuua ni uongo tu!!!!!!!!!!!!!!

 55. Ummy Says:

  we obare soma comment yangu na uelewe vivuri,mi sijasema dereva alikua kafiri,ila uislamu unafundisha kuua adui yako,na simtetei dito kua dereva alikua adui yake…..we unakurupa na kuongea vingine

 56. Swordfish Says:

  You can say INALILAH WAINALILAH RAJIUN thousand times, but the buttom line is Dito is a COLD BLOOD KILLER. He took innocent life and his family danced in court making fun of Mr Mbonde’s family. Nobody is interested if he prayed before his death ’cause that is between him and his god. Nobody has right to take anybody’s life. You live by the gun YOU DIE BY THE GUN. One thing to learn here “YOU CAN’T CHEAT DEATH” He could’nt answer in this world because he was somebody and he killed mlala hoi. BUT GUESS WHAT, GOD WILL ASK HIM THE SAME QUESTION, WHY DID YOU TAKE INNOCENT LIFE?

 57. binti-mzuri Says:

  seemaa swordfish,we sema sie wengine tusikilizeeee!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s