BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KWAHERI DITO April, 20, 2008

Filed under: Developing News,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 5:30 PM

Pichani ni jeneza lenye mwili wa Marehemu Ditopile likiingizwa katika gari ya wagonjwa la Jeshi la Wananchi Kikosi cha Pangawe, Morogoro. Mwili wa Marehemu Ditopile tayari umesafirishwa kutoka hospitali ya mkoa wa Morogoro kwenda Dar-es-salaam kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugano.

Marehemu Ditopile anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kinyerezi (nje kidogo ya jiji la Dar) baada ya swala ya alasiri.Kabla ya hapo kutakuwa na swala na nafasi ya mwisho ya kutoa heshima kwa marehemu nyumbani kwake Upanga kuanzia saa nne asubuhi.

Picha kwa hisani ya Lukwangule blog.

Advertisements
 

9 Responses to “KWAHERI DITO”

 1. solange Says:

  hahaha kweli ghafla duuuu, mhh kazi kweli, haya poleni familia, huyo mke mdogo mbona kazi anayo.

 2. hellen Says:

  mungu akulaze mahali pema peponi upumzike kwa amani,pia napenda kutoa salamu za pole kwa familia na ndugu wa marehemu,tunajua mlipenda ila mungu kampenda zaidi,kazi ya mungu haina makosa.

 3. changalamacho Says:

  Morogoro kuna ani?

 4. michelle Says:

  Heee kwani alikuwa na wake wangapi? basi kama alikuwepo na wa pili ndo atajua mambo ya kuingilia ndoa za watu ndo hayoooo. Huko mji kasoro bahari alikuwa akifanya nini? ndo kwao? basi poleni Mungu awatie nguvu.

 5. Jackline Says:

  Mungu ailaze pema roho ya marehemu Ditopile mahali pema peponi lakini mbona ghalfa pana utata hapo mmmhh!!!!!

 6. Twaha Figo A-City Says:

  Mungu ailaze roho ya marehemu Dito mahala pema peponi ,AMIN

 7. michelle Says:

  Mi bado najiuliza imekuwaje ghafula namna hii, ua wamemnanihiiiiiiiiiii (wamemkolimba nini?) maana huko home hamchelewagi.

 8. rachel Says:

  POLENI AMILIA JAMANI tumempenda sana ila mungu kampenda zaidi, tanzania tunazidi kuondokewa na watu muhimu mungu tusaidie.

  mungu aiweke roho yake mahala pema peponi
  ameni

 9. annabell Says:

  jamamni huyu ni yule ditopile aliyempiga konda/dereva risasi au mwingine? .


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s