BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 16 April, 20, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,Photography/Picha,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM
Tags:

Pichani ni mtoto mdogo akihangaika kutafuta maji huko mitaa ya Tandika jijini Dar-es-salaam kama alivyonaswa na mpiga picha wa Global Publishers.Kama ilivyo kwa picha zingine za jinsi hii, insha yenye maneno yasiyopungua elfu moja inaweza kuandikwa kwa kuitizama tu picha hii.

Kwa upande mwingine, hii ni kukumbusha kwamba “Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania” bado ni safari ndefu sana.Ni safari ambayo inahitaji mchango wa kila mmoja wetu na wala sio viongozi peke yao ingawa kimsingi uongozi mzuri ndio “injini” ya maendeleo na maisha bora kwa kila mtanzania.Hii ndio picha yetu ya wiki hii ambayo imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Global Publishers.

Advertisements
 

17 Responses to “PICHA YA WIKI # 16”

 1. Gervas Says:

  Kwa viongozi hawa tulio nao, Maisha bora kwa kila mTZ ni ndoto. sio kwamba pesa hatunazo Tanzania, Zipo na zinatosha kabisa kuondoa matatizo ya Maji, barabara na Mipango miji ila tu ubinafisi umetawala ubongo wa watawala. Nimeshangaa sana kusikia kuwa hata mpango mzuri wa nyumba uliopo sinza saizi ni juhudi za mzungu aliyekuwepo enzi hizo kinondoni ambapo pia alipigania kutandazwa mabomba ya maji. Yaani hata kujipangia miji yetu napo tunasubiri mzungu? Viongozi wetu wanashindana tu kuvaa suti za ulaya, kununua magari ya gharama na kuwekeza kivyao huku wakipigia kelele wananchi wachangie maendeleo. Hivi usingekuwa huu ufisadi uliogunduliwa au hata wizi ambao inawezekana kabisa ulishafanyika lakini wananchi hatuujui Tanzania tusingekuwa tunalalamikia maji, elimu, Afya na mabarabara na njaa inayotukabili mpaka tunaletewa misaada ya chakula na nchi zenye majangwa kama misri.

 2. Papin Says:

  Duh!!!! Mtoto atakuwa analia kalamimishwa kwenda kuchota maji kwa kuchapwa bakora. Noma kishenzi mzazi wake!!

 3. maria Says:

  kweli hii picha inasikitisha kweli, huu ni unyanyasaji wa watoto, mtoto mdogo hivo amebebeshwa ndoo nne, hivi huyu mtoto hana dada hana kaka, hana mama wala baba???its soo sad.haki ya mtoto ipo wapi hapo???

 4. sweetoh Says:

  Halafu watu wanasema “vijisenti”, na wazirudishe tuwatengenezee wananchi mabomba ya maji, madawati na vifaa vya shuleni na uniform kwa watoto kama hawa.
  Kazi kuvaa suti tu kumbe wezi tuuu!

 5. Bob Sankofa Says:

  “Mama wa mtoto huyu yu wapi, mbona nyumba yao hapo kulia “haina” madirisha? maana wameyaziba kwa mabati. Kwa nini yule baba kule nyuma hatoi msaada wowote kwa mtoto huyu na ndoo zake? Je huu si utumikishaji wa watoto? Kwani sheria za kazi zinasemaje kuhusu swala hili?”

  Haya ni baadhi ya maswali amabyo mtu unayapat kutokana na picha hii. Kuyajibu maswali haya unaweza kujikuta umepitiliza yale maneno elfu moja ya insha anayotuambia bwana BC.

  Picha za namna hii huwa hazijirudii, bahati ya kupata picha hii huja mara moja na ni juu ya mpiga picha kuamua kuichukua au kuisusia bahati hiyo.

  Picha safi sana, inaamsha fikra zilizolala.

 6. Malenga Says:

  Kweli maisha bado ni kitendawili ambacho kimekosa mfumbuzi,washirika naweza kuwahakikishia kwamba kwa kasi hii tutafika, lakini tutachelewa sana.

 7. DUNDA GALDEN Says:

  Ni kwelI MH Ramadhani Ukiwaona Ditopile Mzuzuri hatunae tena duniani.mbele yake nyuma yetu.mungu amsamehe makosa yake Inshallah,
  Picha ya wiki inasikitisha mtoto mdogo na madumu ya maji hatujui hatayapa umbali gani.masomo yanamsubili.hajui nini kitachotoke kesho ikiwa ahadi alizo haidiwa ni nyingi sana na utata unaongezeka pale watu wana mabilioni na wengine husema vijisent.itakuwaje pale nafsi yake itakapochoka na kauli za ahadi na kebehi eti vijesent ikiwa hana uwakika wa maji?
  chafosa chai goda(DARWIN)

 8. Subby Says:

  Picha inasema mengi na huwezi kutoa judgement kwa kuangalia picha tu ukajua ni nini hasa kimetokea. Wazungu wanatumia sana picha kwa ajili ya propaganda na kuchezea akili za watu. Hapo ingekuwa huyo mtoto kabeba ndoo yenye maji kichwani hapo ningeweza kukubaliana na maelezo yaliyotolewa kufuatana na hiyo picha. Nina maswali yafutayo kabla sijasema lolote kuhusu hiyo picha ningependa kujua yafuatayo

  1. Ni umbali gani anaoishi huyo mtoto na anakoenda kuchota maji?
  2. Ni maji ya bombani au kisimani? Maana nimekulia Tandika napafahamu vizuri sana, kuna visima na mabomba ya Dawasco yaliyo majumbani mwa watu.
  3. Hizo ndoo zina uzito wa kilo ngapi?
  4. Je huyu mtoto hajatumwa kweli na mama yake kupeleka maji kisimani au bombani ili mama yake aje azifuate baadae?
  5. Je ni kweli analia kwa sababu hataki kupeleka ndoo alikotumwa au anaogopa kupigwa picha?
  6. Mtoto huyu anaishi na mzazi au mlezi au ni mtumishi wa mtu (wako wanaowachukua watoto wadogo kama hao na kuwafanya watumishi wa ndani)
  7. Na kama ni mtoto wa aliyemtuma kupeleka ndoo kisimani au bombani kuna ubaya wa mzazi kumtuma mtoto wake au ndio yale ya kuiga wazungu watoto ni kula na kulala?
  8. Suala la umri wa huyu mtoto, picha peke yake haiwezi kutupa umri wake maana kwa uswahilini umbile na umri ni vitu tofauti, ana miaka mingapi?

  Hapo ndipo ninaweza kusema lolote kuhusu picha ya huyo mtoto na matatizo ya maji Tandika. Mie nilipokuwa mdogo tulikuwa tuntumwa kupeleka vikapu au vitu dukani kupanga foleni ya chakula kusubiri gari la ugawaji lilete chakula dukani na kwenda kuweka foleni ya maji pia.

 9. baker Says:

  Duh kweli apo ni balaa alafu hilo ndo jiji kubwa la Tanzania yetu!!! jamani wabongo kazi tunayo ni ngumu kufikia maisha bora kwa staili hii na uongozi huu wa sasa wenye bahadhi ya viongozi wanaojali maisha yao na si ya Watanzania wote. Kwa kweli inasikitisha sijui kama ni wote wanaotambua kuna watu wanaokabiliwa na matatizo kama hayo. Mungu Ibariki nchi yetu Tanzania

 10. Amina Says:

  huyu dogo atakuwa katumwa na mama yake atangulize ndoo,ye atakuja nyuma nionavyo mimi

 11. Mtukwao Says:

  Mmh!!! Im Speachless, too sad!!!

 12. Mtukwao Says:

  Mmh, 4real inasikitisha na inaogopesha!! but hiyo ndio Tanzania yetu tunayo ipenda na hao ndio viongozi wetu tunaowapenda.

 13. hatbah Says:

  hii ndio temeke ilivyo maisha haya mfano huyu mtoto ndio tunayo temeke.mbunge hana analolifanya tumbo linazidi kua kubwa kwa mapochopocho.

  wakati kina,chenge,lowasa,karamagi,msabaha,zakia mejhi,sumaye na mkapa wanakula kuku kwa mrija huku kina yahe tunakufa huku tunajiona kifa cha mateso.

  sasa ukisema ufuatilie huyu mtoto anakoishi ni balaa.hapo katumwa maji akirudi nyumbani akauze miguu ya kuku,utumbo,karanga,au vitumbua mpaka saa nne usiku ndipo arudi home ale alale.

  akiumwa aende temeke hospitali kama mamake hana pesa basi ndio atakufa hivi hivi.bado shule.

  hivi mbona watu wanamuogopa mkapa?hiyo hoteli aliyojenga afrika kusini na ile ya lushoto mbona wabunge hawajadili?au ndio mpaka maaskari wa interpole waje kama ilivyokua kwa chenge?kwa hiyo kesho nanihii nae atajiuzulu huku anaingia mjengoni bungeni kama raia mwema.lowasa kachaguliwa na wananchi na zakia aliyechaguliwa viti maalum anafanya nini bungeni?

  hivi ni waziri gani aliyefuzu anapoulizwa swali kuhusiana na mapungufu fulani anasema”mimi sikujua kama wananidanganya”kweli shule ipo hapo?halafu mpaka leo anaendelea kula posho kwa uzuri gani hasa?vyeo kibao kesho kaenda huku kesho kula tena kiserikali inakuaje?kwa nini hawa watu wasiondolewe kabisa wanachangia nini bungeni zaidi ya kueneza semina na elimu ya ufisadi?

  jk,pinda,sheni,sitta ,hamuyaoni haya?tizama maisha ya wanyonge!!!mtizame huyu mtoto halafu nenda katizame mitoto ya chenge na lowasa hausigeli mpaka wa kumnawisha chooni,wakati huyu midoo kikiri mpaka amekomaa wakati bado mdogo.

  si cuf,chadema,wala chukua chako mapema wote hawafai kwa kweli ila malipo duniani!!!

  kila mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake ila mwenzangu kamba ya chenge inamashetani.bilioni moja ingeweza kufanya mangapi katika kuokoa maisha ya watanzania mahospitalini na kielimu?tumeumbwa na usahaulifu ila huu sasa umekua ugongwa.

  leo muhindi ndio amekamta reli sasa.huyu muhindi mwenyewe kwao kama tandika au tandale kwa tumbo sasa unategemea nini?wahindi wanasifa ipi ya kuendeleza reli?ona wanavyotuibia kariakoo na posta kila mahali.kwa nini tunapenda kuamini sana ngozi nyeupe?

  tunawafanya biashara wangapi wakitanzania ambao wangekalishwa chini na serikali basi wangeweza kuingia pale.lakini leo tunamsapoti muhindi tunamuacha mtanzania si bora basi mgetafuta wachina kama mlishindwa wazungu maana mmeona waafika hawafai.mtampaje mtu shirika ambaye haja fikia requirements?mtu hana vigezo inafikia hatua akope kwanza ndio aanze kazi kwa nini hakukopa kabla.

  ninawasiwasi kwani kapuya anamiliki bendi ya acudo impact wana wa kupekecha pekecha sasa inakuaje?kapewa nini na hao wahindi wasiojiweza?bado mpaka sasa hawawezi kuvunja mkataba!!!!

 14. Gebo Arajiga Says:

  Jamani kiukweli picha hii mimi mwenyewe sijaona umaana wake mpaka kupewa hadhi ya kuwa picha ya wiki bora angebeba hata ndoo moja tu lakini ikiwa na maji iwwe kichwani au waapi lakini hapo inaawezekana kao laabda kweli ni hatuaa mbili toka hapo alipopigwa pichwa naa labda ametumwa kwenda kupeleka ndoo ili mama yake aje kubeba

 15. sally Says:

  Inasikitisha sana kwakweli maisha yetu ya Tanzania, tunaishi tofauti sana maisha yetu. Huwezi kumkuta mtoto wa kibosile kabeba mindoo kama vile alafu maeneo yenyewe sasa ndo hivyo Bongo Tambalale.

 16. Twaha Figo A-City Says:

  Ebwana sasa hali hii tunayoiona ni hapohapo Dar ambapo ndipo ilipo ikulu ua JK,yaani mambo haya yapo poa na mdomo na ikulu ya JK,sasa je huko vijijini mambo yatakuaje?Changamsha bongo mwenyewe.

 17. chuma Says:

  Halafu ninyi mnaoishi maisha ya aina hii mnasema mnaishi jijini au kijijini ndani ya jiji?
  Mimi nilifikiri huyu mtoto yuko katika kijiji cha dutumi, kule morogoro, kumbe ni dar! Nani kapima jiji hili?
  Yote ni pambavu na mafisadi


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s