BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PM WA KENYA April, 22, 2008

Filed under: Siasa,Swali kwa Jamii,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 2:57 PM
Tags:

Pichani ni Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Amolo Odinga. Raila ambaye amechaguliwa hivi karibuni kuchukua madaraka hayo mapya nchini Kenya ni miongoni mwa wanasiasa wazoefu wa nchini Kenya.Watu wengi hivi sasa wanajiuliza; Kenya wamewezaje kumaliza tofauti zao(at least kwa sasa) wakati sisi mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar unaonekana kama ndio kwanza unaanza?

Advertisements
 

24 Responses to “PM WA KENYA”

 1. Said Says:

  Huyu jamaa shujaa kama baba yake Jaramogi Odinga,
  lakini kubwa hapa sio kuwa hule mgogoro ulikwisha!
  bali walilazimishwa kuumaliza watake wasitake.

  maana pale walichukuwa wanagombania ni zamu ya kabila
  gani kutawala Kikuyu au Luo? na mambo hayo ya ukabila
  kenya walikuwa nayo siku nyingi
  Tatizo Zanzibar nalo ni la siku nyingi,lakini ukweli kuwa
  hata siku moja serikali ya mseto haitakuwepo!kutona na
  katiba zina gongana kuna ya muhungano na ya Zanzibar
  Lakini acha tuwachie wenye kujua kusukutua midomo
  mimi simo

 2. Kamanzi Says:

  Odinga kwangu hajawa shujaa hata siku moja. Lakini kabla sijaendelea naomba nieleweke kuwa simpendelei mwizi wa Kura Kibaki. Tatizo la huyu jamaa ni kutaka utawala kwa gharama zote. Katu sioni akili kwa mtu kukubali chuki ya kikabila pamoja na mauaji ya watu wasiopungua 1000 eti sababu tu anataka utawala. Cha kusikitisha ni kwamba wakati Waluo na Wakikuyu wakiuana yeye aliiamishia familia yake nje ya nchi. Kajamaa ni kafisadi ka kiutawala. Leo ametulia kwasababu amepewa uPM lakini chuki baina ya wakenya haitaisha kamwe na kama umewahi ishi Rwanda au Burundi ndio utaelewa nikisemacho.

  Kama nilivyotangulia kusema, ni kweli kura ziliibwa lakini katika kutafuta haki hatuchochei ukabila. Mauaji Kenya hayakua random, yalikuwa systematic kuonyesha wazi kuwa yalikuwa mauaji ya kimbari. Mtu mmoja akasema AMANI INATANGULIA DEMOKRASIA. Nieleweke jamani kuwa sipendelei akina Kibaki waibe kura ila tunapotaka kushinikiza serikali tujiepushe na mambo mawili; Ukabila na Udini maana hayo ni moto ambao ukiwashwa hauzimiki unapozwa tu kwa muda. Mwishoni mwa mwaka jana kabla ya uchaguzi nilikuwa Nairobi, tension ilikuwapo lakini manageable. Leo hii waluo na wakikuyu wanachekeana kinafiki. Wanasiasa washakabidhiana vyeo huku wananchi wanasagiana meno.

  Watanzania hebu tuungane kuing’oa CCM madarakani mwaka 2010 ila tujiepushe na Ukabila na Udini. Dhambi hizi mbili hazisameheki jamani. Ohoo.

 3. Amina Says:

  Kamanzi nimekupata sana tu..mi huyu odinga pia kwangu hajawa shujaa,kweli kura ziliibwa na yeye alikua anapita kusema kaibiwa kura sasa iweje leo apewe upm na akubali?hata kama walilazimishwa waumalize lakini ye alitakiwa ashikilie msimamo wake wa kura zirudiwe kuhesabiwa haraka…ila kibaki mbishi jamani mh

 4. Mtukwao Says:

  mmmh, mie sikjui kama Laila ni shujaa au la ila nakubaliana naaliyo yasema Said 100%.

  kwani nakumbuka baba wataifa alisema kuwa “dhambi ya ubaguzi huwa aiishi, mkiianza haita waacha itawufuata siku zote. haita wabakisha itawatafuna mpaka mwisho”.

  kweli huu ndo ukweli

 5. mimi Says:

  binafsi simtaki kabisa Raila awe raisi. Ndo alitaka kuwa raisi huyu? mavazi tu yanaonyesha ni mtu wa namna gani??

 6. Makumbi Says:

  Kwa kweli Odinga sio shujaa bali muuaji! tena muuaji mkubwa. Wizi wa kura hata yeye akiingia madarakani hatachelea kufanya hayo! Wakati kina kibaki wanajipanga kuingia madarakani kama wapizani wa Moi, kati ya mambo waliyokuwa wanasisitiza ni uchaguzi huru ndani ya kenya na zaidi walikuwa wanamwona Moi ni mwizi wa kura, lakini baada ya kibaki kupata madaraka aliyoyafanya hadi wapinzani walioungana kumweka madarakani wakasambaratika sote tunajua.Kwa nini odinga apanie kupata madaraka kwa garama ya damu za watu? Hakuna ndugu yake wa karibu hata mmoja au wa familia yake aliyepoteza maisha katika kuhakikisha Odinga anapata madaraka. Watanzania ni ujinga wetu ndio unaotufanya hadi leo hii tunaburuzwa na mafisadi toka CCM.Tukiamua kama alivyosema ndugu yangu, ccm tunawangóa! Hatuna haja ya kuomba watu wauane au wachomeane nyumba kama njia ya kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini. Unayemwita odinga shujaa sikuelewi, fikiria wale wote waliopoteza maisha kwa kuchomwa moto ndani ya kanisa ingekuwepo familia yako na ikateketea ksijui ungemwita shujaa au vipi? Siku oding akipata madaraka naye atataka kutawala milele hata kwa kubadilisha katiba. Mungu ibariki tanzania yasitokee yale ya kenya bali akili za watanzania zifunguke na kuiondoa ccm madarakani!

 7. Mimi naamini kabisa tatizo lililotokea kenya mwaka jana si la kikabila kama wenzangu hapo juu wanavyoonyesha. tatizo kubwa lilikuwa ni wizi wa kura. Bwana odinga alishinda uchaguzi, na Rais aliyekuwa madarakani hakutaka kuachia uongozi.
  Ninaamini kabisa kama Odinga angeshindwa katika uchaguzi ule hari isingekuwa kama tulivyoshuhudia. kwake angekubali matokeo tu.
  Nawasihi watanzania wenzangu tuache tabia ya kuwalisha watu maneno, kama ukabila kila mahari upo, hata hapa tanzania kwa kiasi fulani upo. chunguza chaguzi za vyama kiwe tawala ama upinzani utagundua tu kama upo.
  Haya turudi kenya, bwana odinga alipata kura nyingi tu za kumuwezesha kuwa rais wa nchi, je? ina maana waliomchagua walikuwa ndugu zake tu? jibu ni siyo, nafikili ni makabila yote walimchagua na ndio maana watu waliingia mitaani kuandamana wakipinga matokeo.
  Nasikwamba walilazimishwa kupatana kama tunavyosadikishwa, ni utashi wao wa kisiasa uliwapelekea kuamua njia hiyo ili kuinusuru nchi yao.

  Tatizo katika nchi zetu za kiafrika vyama tawala havipo tayari kuona vinaachia madaraka hata palipo na ukweli kuwa sasa wameshindwa. tazama ZIMBABWE. bwana mugabe ameshindwa siku nyingi lakini hataki kuachia madaraka, anafikili yeye ni Zimbabwe na Zimbabwe ni yeye na bado tunampigia makofi na kumpongeza utazani wote sisi ni vipofu.

  Kwa tanzania ni ngumu sana kufikia hari ile ya muafaka kama waliofikia wenzetu wa kenya kwa kuwa sisi hatuna dhamira ya kweli ya kisiasa. daima sisi ni watu wapropaganda. viongozi awapo tayari kutatua tatizo la kweli la zanzibar. tatizo kubwa ni la kimtazamo kuhusu uhuru wa visiwa hivyo. upande mmoja unaamini kuwa uhuru ulipatikana mwaka 1963, na kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanywa kimakosa kwa kuwa ilipindua serikali harali.

  Upande mwingine unaamini kuwa mapinduzi ya mwaka 1964, ndiyo yaliyoweka serikali harali ya zanzibar na kupata uhuru kamili.
  Lakini upande mmoja sasa umejirudi na uko tayari kwa serikali ya mseto kwa kuwa ndio njia pekee ya kuleta mshikamano na udugu. lakini upande mwingine auko tayari kwa jambo hilo kwa kuwa unajiona kuwa ndio upande sahihi zaidi, hivyo narudi katika point yangu ya mwanzo niliyosema kuwa hakuna dhamira ya kweli katika kufikia muafaka katika visiwa vya zanzibar. hivyo tuwapongeze wakenya badala ya sisi kuwaingizi maneno mdomoni mwao juu ya ukabila.

  Pamoja na madhaifu yao, lakini wenzetu wanayo dhamira ya kweli ya matatuzi ya migogoro yao inayowasumbua.

 8. fukara Says:

  Nakuunga mkono bwana kamanzi na naomba ieleweke kuwa 2010, CCM itoke madarakani kwanjia ya amani.
  Naomba sana iundwe tume huru ya uchaguzi narudia tena
  tume huru ya uchaguzi bila hivyo CCm itaendelea kutunyonya sisi wa nyonge
  MUNGU IBARIKI TANZANIA watanzania tuamke jamani.
  Najua wakati wa kampeni takrima zitatawala fedha vikanga kofia na fulana, naomba huko vijijini pokeeni lakini siku ya kupiga kura chenge ,karamagi na lowassa na wengine ambao hawajakamatwa kwa ufisadi tusiwape kura.
  Namaanisha ccm isirudi tena bungeni
  Vyama m badala maana siwaiti wapinzani naomba sana mjiandae saa ya ukombozi ni sasa mmefanya kazi nzuri naomba sasa msiache mkia jipangeni vyema maana mkishindwa wakati huu watanzania wameamka ,hamtapata nafasi kama hii tena maana wengine wenu mmeshaanza kuzeeka
  Kila la kheri watanzania wote!!!!!!!!!

 9. changalamacho Says:

  Wenzetu wa Kenya wameweza kuleta shinikizo zilizofanikisha kuleta mageuzi ya kisiasa japo kwa sasa kwa sababu haikuwa jitihada ya mtu mmoja tu.Ni jitihada za kikosi kizima cha vijana wa Kenya wenye elimu na uelewa mkubwa wa siasa waliochoshwa na uozo uliokuwa ukiiteketeza jamii nzima ya wakenya.It was a Movement of young and Middle-aged Kenyan Intellectuals who were determined to see political change taking place in their country by getting rid of the corrupt and restoring funtional multiparty democracy for the benefit of all Kenyans.

  Dhamira,Umoja na Umakini ndio uliowawezesha Vijana Wasomi wa Kenya kuleta mabadiliko makubwa ya kiutawala ambayo yatabadilisha kabisa sura ya Kenya kisiasa katika siku za karibuni.Hapa kwetu ni tofauti.Bado tuna tabaka kubwa sana la vijana ambao hawakupata bahati ya kusoma zaidi ya shule za msingi na ambao ndilo kundi lililo athirika zaidi kuliko makundi mengine katika jamii kwa ukosefu wa ajira, ukosefu wa nafasi za kujiendeleza kielimu, kwa kutokuwa na stadi zozote zile za kazi au maisha(lack of vocational skills).Kisiasa hili ni kundi la ‘wayumbaji’ au ‘swinging votes’ utakapo kuja uchaguzi wowote wa kisiasa.Ni watu wepesi sana kununulika au kudanganywa na wajanja wachache ili kutimiza malengo yao ya kisiasa.Wakishafanikiwa huamua ‘kuwatosa’ vijana hao na kuwaacha wakiwa hawana msaada wowote mpaka hapo watakapo wahitaji tena uchaguzi mwingine utakapo wadia.Kwa bahati mbaya zaidi,hata hao vijana ambao tutasema walibahatika kupata elimu kidogo au sana ni baadhi yao tu ndiyo wenye moyo wa uzalendo kwa nchi yao.Baadhi yao ni wale ambao kisiasa wataitwa ‘opportunists’ au ‘wanafiki ndumilakuwili’ ambao hawana msimamo wowote wa kiitikadi au kuukataa ufisadi na usaliti kwa nchi yao.Wao watakacho jali zaidi ni fursa zitakazokuwepo katika kutwaa mali au ajira za upendeleo katika ngazi za juu hata ikiwa sifa hawanazo za kushika nafasi hizo za uongozi.Kwa hiyo mgawanyiko uliopo baina ya makundi hayo ya vijana wetu ni TATIZO NA KIKWAZO KIKUBWA KATIKA KUFANIKISHA MAGEUZI YA MAANA HAPA NCHINI tofauti na ilivyokuwa kwa vijana wenzetu wa Kenya.

  Wakati sasa umefika kwa Vijana wetu hususan wenye elimu kutambua kwamba FUTURE YA NCHI HII IKO MIKONONI MWAO.Wakikubali kununuliwa au kurubuniwa na baadhi ya wanasiasa ambao hivi sasa wamedhamiria kuiteketeza nchi yetu kiuchumi basi wajue nchi hii itazidi kudidimia zaidi katika lindi la umaskini wa kufikiri na wa kipato pia.Watanzania watajikuta wakigeuzwa MANAMBA katika nchi yao wenyewe.Watajikuta wakigeuzwa kuwa WAKIMBIZI katika ardhi yao wenyewe.Hakuna Kijana atakaye penda hilo litokee.Kwa hiyo kuweni vijana katika starehe zenu lakini wakati huohuo muwe watu wazima katika tafakuri zenu na maamuzi yenu.Suluhu ya Zanzibar ni suala la muda tu.Wapo baadhi ya viongozi waliopo Tanzania Bara ambao wamekuwa wakinufaika kwa kipindi kirefu kwa kuwepo mfumo huo wa Muungano baina ya Bara na Visiwani.Hakuna sababu yoyote ya maana ya kutokuwepo kwa Katiba Mpya itakayo imarisha zaidi Muungano wetu ndani ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa.Katiba iliyopo sasa haiwezi kukidhi mahitaji hayo yaliyotokana na mabadiliko ya kisiasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.Kuendelea kulazimisha kuwepo kwa Katiba ileile kwa matarajio kwamba italindwa kwa mabavu ya dola ni kukaribisha fujo na ghasia za kisiasa hapa nchini bila ya faida yeyote.Lakini kutokana na kumeng’enyuka kwa nguzo za uhafidhina ndani ya CCM inatarajiwa kwamba katika siku za usoni watjitokeza vijana wenye mwelekeo sahihi zaidi ndani ya CCM watakao baini ukweli na kuyakubali mageuzi kwa nia safi kabisa bila ya uzandiki na fitna ya aina yoyote.Hilo likichelewa sana kutokea basi ‘nguvu ya umma wa watanzania’ itachukua mkondo wake.Tuwe na subira lakini tuwe makini vielvile.

 10. Amina Says:

  yohana tumekuelea sana ila kwenye la na ra jaribu kutofautisha unanichanganya sana…ni hayo tu

 11. zachariah Says:

  jamani nimepitia comment zenu nyingi nimeona munamawazo ya kimapinduzi! inapendeza””” bt point yangu iko hivi kumng’oa ccm itakuwa ngumu ndugu zangu. CCM bara huwa inashinda kiuharari kabisa na cha ajabu hicho chama kingine cha CUF inaonekana hakina democracy kabisa ndani ya chama chao cuz toka niko darasa la 5-hadi leo niko mwaka wa 3 wagombea naona waleleX2 kwa nn wasipishe wengine ili watanzania wajenge amani nao!!??
  Na issue ya Mugabe cyo kwamba Mugabe anakataa kutangaza matokeoo issue ni wale wanajeshi waliopigania uhuru miaka ile nd’ wanaompa kiburi Mugabe kuwa asiachie ngazi kwa kusema nchiii hii haiwezi ongozwa na mpinzani ambaye amekuta ki2 kiko sawa katika nchii hiii!
  Na vile vile hapa bongo wanasiasa we2 ni vibaraka tuu kwani baadhi yao wanapewa post za kwenda kupiga kazi nje ya nchi na Mh! nd’ mana wapinzani wa hapa bongo wako kama Joka la Kibisaaaaa. nimawazo tuu washikaji!

 12. Gervas Says:

  Msifikiri mambo yako shwari Kenya. wale waliokuwa wanauana chuki badoo ipo tena kubwa tu, wataendelea kuuana kimya kimya. Usitegemee watu waliokuwa wamekimbia makazi yao wawe na furaha kwani si maisha tu ya wenzao yaliyopotea, bali mali yao pia. Wote Odinga na Kibaki hawakuwa na moral considertions towards Kenyans lives bali madaraka. Kuna haja ya kuwasifia?

 13. Gervas Says:

  Ni kweli Tembo wapiganapo nyasi ndo zinaumia. Wakenya wamekufa kwa kutoelewana kwa viongozi wawili tu wa siasa. Mgogoro wa Zanzibar msiuchukulie juu juu, tayari umeshawagawa wananchi wa zanzaibar. Chochote kikitokea Mtamsikia Seifu huyooo..Wingereza afu watakaotoana roho ni walala hoi. Tuyaangalie kwa umakini maneno ya wanasiasa, kwa nini wanasiasa watufanye tuchukiane sisi wananchi? ni kweli tukijitolea kuuana kwa ajili yao kutawala tunapata faida gani? tutasoma bure? Kodi hazitakuwepo? Zanzibar itabadilika kuwa Bahrain? Wazanzibari CCM na CUF saizi hawachangamani kabisa, misibani, tayari Upemba na Uunguja umeshamiri. Hata maadili ya dini zao wameshaweka kando. Jamani tuyaangalie maneno ya wanasiasa kwa makini, na tufikirie

 14. hombiz Says:

  yote mawili mafisadi tu. Hakuna kiongozi wa kweli ktk Afrika ya leo. Wote ni vibaraka wa mabeberu wa kizungu toka nchi zilizoendelea.

 15. Mtukwao Says:

  OH nilikosea mie namuunga mkono kama sio mguu bwana “Kamanzi” na sio “Said’ kama nilivyiosema hapo mwazo. lol!!!!!!!

 16. Amina Says:

  He mimi nikusahihishe,ulitaka avae suti muda wote?kwani hapo kibaya kipo wapi?hilo shati la asili ya kiafrika na hizo kofia wakenya wengi wanatumia,hata kama yupo kijijini kwao kuona wazazi ashinde na suti au?makubwa haya

 17. Chala Says:

  mimi mtazamo wangu kama angekuwa shujaa asingekubali hata huo upm,, roho za watu zaid ya 1000 sikazi ndogo angekubali kwa namna nyingine ili watu wasiendelee kuuana wakafanya kiutuuzima hayo mambo yao.

  na hayo ndio yatakuja kutokea Znz tusipoangalia,,,, tuwe makini sana… wenzetu hao viongozi kwenye vurugu mmeshawahi kusikia kaumizwa mmoja wao? ila sie tu kisha wao ndio wananeemeka….

  Mnisamehe wapendwa wa TZ wenzangu nimewachukia sana viongozi wa Africa hususan hawa wa kwetu kuanzia juu mpaka chini……

 18. mbilimbi Says:

  Maalimu Seif bado ana nguvu za kutosha za kukiongoza chama hadi hapo sisi wenyewe wanachama wa CUF tutakapo mruhusu akapumzike lakini siyo kabla ya hapo.Viongozi wenzake serikali Katiba zitawazuia wasigombee tena baada ya vipindi viwili vya utawala lakini kwa Maalimu Seif hilo halitomgusa,yeye ataendelea kudunda mpaka CCM ing’olewe madarakani visiwani Zanzibar kwa njia ya kidemokrasia kabisa katika uchaguzi ulio wazi,huru na wa haki bila ya mtu yoyote kuibiwa kura.Na kura zote zitahesabiwa nje peupe kila mtu akishuhudia kwa macho na matokeo kutangazwa palepale kituoni.Prof. Lipumba naye hali kadhalika hali ni hiyo hiyo.Sasa wanaume mkae chonjo.Ufisadi wa kuiba kura katika uchaguzi mkuu ushapatiwa dawa.Mwenye kukubalika kwa Wazanzibari basi halali yake achaguliwe alete maendeleo zaidi hapa visiwani bila ya upendeleo.Muungano udumishwe lakini katika Katiba iliyo bora zaidi ya Muungano.Labda huyo kizabi na.12 zachariah atakuwa amenielewa.Kina Seif na Lipumba wataongoza hadi pale sisi wenyewe wanachama wa CUF tutakapo waruhusu wakapumzike, lakini siyo kwa wao wajitakie wenyewe, usha nsikia!

 19. tonny Says:

  Jambo la muhimu ambalo Raila Odinga (ofcourse na wenzake) amefanikiwa kulifanya katika historia ya maisha yake ni kuacha katika kumbukumbu za mageuzi ya kisiasa katika bara la afrika ( political landmark ) ni jinsi gani nguvu ya pamoja ya vijana wasomi wenye uchungu na nchi yao au bara zima la afrika wanavyo weza kutoa shinikizo za kisiasa zitakazo weza kuleta mabadiliko ya Uongozi wa nchi pamoja na magumu yote yaliyopo ya kukabiliana na nguvu za dola ambazo zipo pale kwa maslahi ya watawala waliowaweka madarakani.Shinikizo hizo mara nyingi hujibiwa kwa vitisho vya kifo au kufukuzwa kazi au hata kuvuliwa uraia wako au kuwekwa kizuizini au jela kwa maisha yako yote.Lakini cha muhimu zaidi ambacho kitamfanya Raila Odinga aibuke shujaa katika jukwaa la siasa za bara za afrika ni kule kuwa miongoni mwa wanaharakati wa kwanza kabisa katika bara la afrika katika kupigania kuwepo kwa mfumo wa demokrasia ambao utahakikisha kwamba Kiongozi wa Juu kabisa wa nchi atakuwa Waziri Mkuu Mtendaji ( Executive Prime Minister ) ambaye atatoka katika Chama cha Siasa ambacho kimeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi ya wabunge wengi zaidi kuliko vyama vingine vya siasa vilivyo shiriki uchaguzi.Kwa maana hiyo, waziri mkuu ndiye atakaye kuwa Mkuu wa Serikali ( Head of Government ). Na waziri mkuu pamoja na serikali yake itaweza kuondolewa madarakani wakati wowote Bunge litakapo pitisha kura ya wengi ya kutokuwa na imani na serikali hiyo. Hilo likitokea uchaguzi mwingine utaitishwa na vivyo hivyo waziri mkuu mwingine atapatikana. Ili kuiweka nchi katika hali ya usalama zaidi kiutaratibu Mkuu wa Nchi ( Head of State ) ambaye katika mfumo huu wa utawala ataitwa Rais wa Nchi asiye mtendaji mkuu ( Ceremonial President ) atapatikana kwa utaratibu maalum utakao kubalika kikatiba. Mara nyingi iwapo muda wa Waziri Mkuu kuwepo madarakani ni miaka 5, basi busara zitahitaji Rais wa Nchi aweko madarakani kwa kipindi kirefu kidogo kuliko kile cha waziri mkuu, kwa mfano miaka 7, ili kusudi hata kama akija waziri mkuu mwingine mpya nchi haitatetereka kiuongozi. Na Rais wa Nchi kwa kawaida ndiye atakaye husika na Ulinzi na Usalama wa Nchi ( Commander of the Armed Forces ). Japo Waziri Mkuu pia kwa kushauriana na Rais wa Nchi bado atakuwa na sauti kubwa karika kuipeleka nchi yake vitani au la baada ya kuruhusiwa na Bunge kufanya hivyo. Waziri Mkuu ndiye atakaye teua mawaziri wote pamoja na watendaji wakuu wa serikali. Teuzi nyingine zitafanyika kwa mujibu wa katiba. Kitu muhimu hapa ni kwamba tofauti na mifumo iliyopo katika nchi nyingi za afrika na Tanzania ikiwa mojawapo katika mfumo huu ambao kina Raila na wenzake wamedhamiria kuujenga nchini Kenya , ni kwamba Madaraka yote aliyobebeshwa mtu mmoja tu aitwaye Rais mtendaji (Executive President ) yatasambazwa kwa viongozi mbalimbali wa juu pamoja na taasisi husika za dola na serikali. Kwa njia hiyo demokrasia itakuwa imeimarishwa zaidi katika nchi na tahadhari ( safeguards controls ) zitakuwepo ili kukabiliana na matumizi mabaya ya madaraka ambayo yamekithiri katika nchi nyingi za bara la afrika. Kwa maoni yangu, huu ndiyo mfumo bora zaidi wa kiutawala katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa ambao utazifaa nchi nyingi za bara la afrika katika kudhibiti mipasuko itakayo sababishwa na tofauti za kikabila, dini au rangi. Katika mwaka mmoja ujao wenzetu wa Kenya wamejiwekea malengo ya kuifanyia marekebisho makubwa Katiba ya Nchi yao ili kufanikisha azma hiyo. Sasa kama yupo ambaye hauoni ushjaa wa Raila basi huyo ni zumbukuku wa masuala ya kisiasa. Shukrani nyingi ziwaendee wenzake Raila kina Rutto, Balala, Mudavadi, na wengine wengi .

 20. Sawa dada Amina nimekuelewa, nitajitaidi kuwa mwangalifu, lakini usisahau kuwa wakati mwingine lafudhi ya makabila yetu yanatufanya kuandika herufi ndivyo sivyo.

 21. Amina Says:

  yohana umenichekesha utetezi wako una ukweli ndani yako

 22. frank kasera Says:

  NYIE WOTE AMBAO HAMMTAKI RAILA NI MAFISADI TU HAMNA LOLOTE. YAANI MTU AKISHINDA ANYANG’ANYWE TU USHINDI WAKE. RAILA SIO KAMA AL GORE AMBAYE ALISHINDA LAKINI AKAKUBALI KUSHINWA ILI KUEPUSHA SHARI.

  HAYA MPINZANI WA MUGANA MORGAN T. AMESHINDA UCHAGUZI MKUU NA MUGABE ANAKATAA KUNG’ATUKA JE HIYO NI HAKI? MORGANI NI MFISADI?

  NYIE KABLA HAMJAROPOKA LAZIMA MJUE UKWELI WA MAMBO MSIPAYUKEPAYUKE TU…
  LIKE HIS FATHER WAS,, RAILA WAS NOT GOING DOWN WITHOUT A FIGHT AND THAT IS ALL PARTY OF DEMOCRATIC PROCESS…..
  KANSAS CITY, KANSAS

 23. Bigy Says:

  Wote ni wamoja tu.Wakishapata pesa wanapeleka ktk miradi yao. hakuna aliyewahi kamatwa, kufunguliwa mashtaka na kufungwa kwa kuiba, ubadhirifu wala u-dictator.Vitoto tunavyozaa vinaona haya na vitayaendeleza zaidi na zaidi. Tujifanyie uchunguzi tuone tatizo liko wapi. I believe there must be a problem somewhere within us which , if not figured out soon, will bring (to our continent) more harm-never experienced before in our history.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s