BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UNAWAKUMBUKA KWANZA UNIT? April, 24, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:06 AM

Enzi zile wakati aina ya muziki ambao leo hii tunauita “wa kizazi kipya” unaanza anza, miongoni mwa vikundi vya mwanzo kabisa ni kile ambacho kiliitwa Kwanza Unit. Yawezekana kwamba kutokana na “uasisi” wao ndio maana waliamua kujiita Kwanza Unit.

Vikundi kama Kwanza Unit ndivyo vilivyokuwa vikikumbana na upinzani kamili wa kijamii kutokana na aina ya muziki ambao walikuwa wanaanza kuutambulisha nchini Tanzania kuchukuliwa na wanajamii wengi, hususani wazazi, kuwa ni uhuni tu usio na maana. Leo hii ni wazi kwamba jamii imeukubali “muziki wa kizazi kipya” kwa namna moja au nyingine. Wakubwa kwa wadogo leo hii wanausikiliza na kuucheza.

Pichani ni baadhi ya wasanii waanzilishi wa Kikundi cha Kwanza Unit. Kutoka kushoto ni KBC,Babyii, Saigoni na Chief Ramson ambaye siku hizi anajulikana kama Zavara Mponjika.

Photo Credit: MichuziJR

Advertisements
 

13 Responses to “UNAWAKUMBUKA KWANZA UNIT?”

 1. bootman Says:

  hao ndo vidume wa enzi hizo kwenye game la hiphop bongo,jamani msaada kwenye tuta,huyu saigon si alikuwa na kundi la diplomats au nalo lilikuwa part of kwanza unit?

 2. Edwin Ndaki Says:

  One watu wa2 wangu.

  siku zinavyokwenda wengine wanakaza uzi wengine ndio hatuwaelewi.

  Mara wanaanzisha taarabu(malumbano)..wengine U-marekani unazidi..vya kwetu ndio tunazidi kuvipiga chini.

  Ila bado wapo ambao tunaamini wameapa kutetea game hadi kieleweke.Achilia mbali wadosi ndio hivyo wanazidi kuwapiga sindano.

  Kila la kheri wanaharakati wa kweli kwenye game..One love

 3. mandingo Says:

  kuna jamaa mmoja alikua anaitwa bugzymalone yuko wapi siku hizi? maana jamaa alikua mkali sana kwa rap za kiinglish

 4. baker Says:

  Ebwana nawakubali sana wana ebwana nyie ndo waanzilishi ati! ni vema mrudi kwenye game kama vipi maana mziki wetu unapotezwa na wachache! kama bro apo juu anavyosema Umarekani mwingi jamani wakati mziki wetu wenyewe wakiswahili! tutajivunia nini waswahili wakati majirani zetu South na bahadhi yao wengine wanaperfom miziki yao ya asili hadi mabara ya Ulaya na Amerca na watu wanawakubali vile vile! msani wa bongo ka single kamoja ata ajauza uza asha geuka P Didy, hereni, macheni hakumbuki alikotoka maisha ni ya kunga unga, jamani kweli bongo kazi ipo

 5. Huyu nani Says:

  Nafurahi kusoma maoni ya Edwin na Baker, ila nadhani kama mtakuwa mnaijua misingi ya hiphop hapo ndio mtajua nini maana ya mabadiriko ya HIPHOP bongo. Kama mjuavyo Bongo flava ni aina ya mziki wa kibongo wenye radha mbalimbali (R&B, Hiphop, Zouk n.k). Naweza sema hivi Bongo flava imegawanyika kulingana na aina ya mziki wasanii wanafanya. Ndani ya Bongo flava tunapata vionjo mbalimbali. Labda tuangalie Mziki wa kizazi kipya Bongo ulianzishwa katika misingi gani au nguzo zipi. Mwanzo kabisa Mziki wa kizazi kipya ulikuwa umesimama katika misingi ya HIPHOP, tena hiphop ya kimarekani. Kama utakumbuka kipindi kile mziki huu unaanza watu walikuwa wakigani kwa kutumia beats za ku-copy za kimarekani ingawa baadaye tulianza pata ma-prodyuza wetu nao wakaanza kutengeneza beats kiaina ambazo zilisaidia kwa kiaisi fulani kuanza kuuweka mziki wa kizazi kipya uwe na ladha tofauti na ya Kimarekani. Mziki huu ulianza kuwa na radha tofauti hadi ikafika kipindi wengine wakaanza bishana oh nani anafanya hiphop na nani anafanya bongo flava. Kiuhalisia ni kwamba wote wasanii wa bongo wanafanya mziki ambao ninaweza nikaendelea uita Mziki wa Kizazi kipya (Bongo flava), ila humo ndani ya bongo flava tunakuja pata genres tofauti tokana na mapigo na midundo ya beats pamoja na uimbaji wa msanii. Sasa sababu madadiriko ya mziki wa kizazi kipya ni bado sana yanategemea na mabadiriko ya mziki wa Kimarekani maana misingi yake ya awali ilisimama pale, tunajikuta hata mziki wetu pia unabadirika kulingana na genres mbalimbali ambazo wamarekani wanazo, walikuwa nazo au watakuwa nazo. Kuna genres nyingine kama gangsta rap, horrorcrore, crunk n.k ni miziki aina ya hiphop ambayo ipo/ilikuwepo na bado kama bongo flava bado tunapitia katika mabadiriko yale yale. Offcourse sidhani kama tunaweza fanya kama Artists wa Marekani wanavyofanya sababu wao sheria zao haziwabani sana, Ndio maana miziki yao utakuta bado iko more gangsta, au hata ukikuta wimbo uko sweet ila bado umesimama ki-gangsta. Bongo ni ngumu kufanya muziki kama wa Kimarekani hasa upande wa kima-shairi maana mashairi ya wa-marekani yako wazi bila hata wakati mwingine kutotumia tasfida. So bado bongo hatuigi ila mziki wenyewe ndio unapitia mabadiriko unayotakiwa kupitia sababu nguzo zake za awali za Music wa kizai kipya ulianzishwa kwa kutumia nguzo zile zile za Hiphop ya zamani. Sasa ukiangalia misingi ya hiphop na hiphop revolution yake mpaka sasa hivi utagundua kwamba sasa hiphop imekuja katika hali ya kibiashara na kiushindani kukiwa na genres kibao za hihop. Ushindani si wa mashairi tu, bali ushindani hata wa kutangaza bidhaa zako au vyovyote. Pia ushindani wa nani anafanya zaidi ya mwenzie au nani ana-bling zaidi ya mwenzie. Haya ni mabadiriko ambayo watu inabidi tuyakubari. Sasa hizi mziki unauzwa sana kutokana na mauzo ya video. Technologia mpya za video zinaingia, sasa hakuna mtu anataka aone video ipo ipo tu. So siku hizi video zinawekwa katika hali ya kustarehesha. SIo tu ile wamwimbia mwanamke huku kajivalia tu miguo guo ya ajabu. Lazima mwanamke awe-blings. Zipo nguo kibao za kuwapendezesha kina dada zetu. Najua watu watasema kwani nguo za kia-Africa hakuna? Lakini lazima watu waelewe kwamba haya ndio mabadiriko ya kidunia na hatuwezi pingana nayo. Mziki haufanywi locally tu. Mziki unafanyika kimataifa so lazima tutofautishe hiphop iliyoanza jengwa kwa misingi ile ya awali ambayo hadi sasa hata wao wanakili Real Hiphop imekufa, sasa sisi tutegemee nini? Ndio tutaweza ijenga imara kuliko wao walioianzisha? Bongo flava iatendela kubadirika kadri siku zinavyozidi kwenda kulingana na muziki wa kiduni unabadirika kivipi. Watu wataimba crunks kwa Kiswahili. Watu watafanya lots of blings katika video zao. Magari yataongezeka katika video. Warembo wazuri wataongezeka katika video. Stahili za uchezaji zitabadirika. Uandikaji wa mashairi utabadirika. Kila kitu kitabadirika kulingana na wakati. Kwa atakayeweza imba mziki wa kuelimisha jamii ataendelea kuimba, kwa yule atayeamua kuimba kufurahisha tu watu(iwe watu wa aina fulani atafanya).

  Labda kitu kimoja ambacho nimekuwa sikielewi. Watu wamekuwa wakinganganiza msanii aaimbe kitu cha kufundisha jamii. Mimi sidhani ni lazima kila msanii aimbe kitu kwa ajili ya kufundisha jamii. Ni kweli wapo wenye matatizo kibao, ila sio kila msanii anayaona hayo matatizo. Siku hizi watoto wengine wanafanya mziki wametoka familia safi. Tangu mdogo anaendesha magari ya kifahari, sasa huyu unategemea aimbe nini? Au mnataka asieembe kipaji chake kipotee? Yeye ataimba labda dream yake ya kuendesha gari jingine kali, au jinsi alivyofanya makamuzi na masela wake somwhere au vyovyote vile. Kuna mambo mengine ataimba ingawa hata ujumbe anaweza imba. Itategemea anataka toa ujumbe gani. Pia mtu alikuwa maskini labda ndio kazipata unategemea aimbe nini? Asiiimbe? Au naye anyamaze kuimba sababu sasa anazo na hawezi imba nyimbo za shida shida sababu watu watamuona mzushi-shida gani wakati anazo. Anaweza imba na akaimba chochote. Vipi yule kabisa asiye nacho naye akawa masanii? Je asiimbe sababu hawezi jisifia au hawezi imba kitu kinachompa starehe? Lazima aimbe nyimbo za shida tu? Kwahiyo mimi nadhani msanii yeye ndio anayechangua ni nini akiimbe na atajua mwenyewe kama atakuwa kweli na washabiki wa kupenda nyinbo zake au lah. Kitu cha muhimu ambacho wasanii wa bongo inatakiwa wawe nacho ni Managers wazuri basi. Hii ndio itasaidia wasanii wajue nini wanakifanya.

  Kulinga na maelezo yangu nitawapa mfano Marekani kuna Hiphop ya aina mbali mbali mfano ya South ambapo utawakuta wasanii kama kina birdman, lil wayne. three 6 mafia, n.k ya East Coast na East Coast. Pia ndani ya hii hiphop kuna genre mbalimbali mfano, dirth south, miami bass, southern hardcore, crunks n.k. Hii yote ni hiphop ingawa uimbaji uko tofauti ingawa ujumbe unaweza kuwa wa aina moja katika genre zote hizi. Anaweza msanii akaimba kigumu kama walivyo kina Rick Ross, Fat Joe n.k pia mtu anaweza akaimba soft. Kwahiyo hata bongo naona ndio ilivyo. Vijana wa Arusha nadhani wana ladha yao ni Hiphop ya kibongo yenye ladha ya ki-Arusha Arusha. Wanaweza imba katika mdundo wowote. Inaweza kuwa hardcore, horrorcore au crunk au vyovyote. East Zuu nao wama aina mbali mbali, East Cost, Tanga na kina Mr Ebbo. Cha muhimu bongo tuombe namba ya produzaz iongezeke, kuwe na ushindani wa ma-produzaz kila sehemu wawe wanatoa ubunifu mpya na changamoto mpya, pia wasanii watengeneze lyf style yao kama ni gangsta ni gangsta kama ni vyovyote ni vyovyote mtaona jinsi gani mziki utakavyoheshimika. Hata wale wanaosema kuna uigwaji wataamini ukweli uko wapi.

  Mwenye maoni tuawasiliane zaidi muzikiwakizazikipya.bongoflava@gmail.com

 6. Amina Says:

  Saigon umejipachika hapo au?siulikua diplomatz?mzee wa ebwana daaaa….unanikosha na babyii pia kaka yako angekuepo ungewa mbali

 7. kaled Says:

  picha ni mpya…saigon alikuwa dpt…ebwana yu wp fresh G? rip drob n niga one….zavara, kbc na manguli wengine wa hiphop mnatkiwa mfanye tamasha moja la waanzilishi wa hiphop bongo itakuwa imetulia sana. Tutapa vionjo vya kina oj, sos b, 2proud,nigaz 2 public, gwn,nwp,hbc…willy upo wp mwana???…zara mkubwa na project yako ya wp unatakiwa uendeleze vipaji wkt unawakumbusha nyie wa2 wazima wazima mlikuwa mnafanya nini……BC weka kile kibao cha mimi msafiri KU Crew 4 life

 8. First Lady of K.U Says:

  Kaka zangu wa K.U hakuna mtu anaweza kuchukua nafasi yenu Tanzania. Watu wengi wa K.U wamepoteza maisha yao kwenye kujaribu kuikuza HIPHOP ya Tanzania na kuelimisha watu wengi kwa kutumia mziki huu. Mliwasha mwenge wa Hiphop na wote kwenye “kizazi kipya” wanatakiwa ku bow down mkitembea(kama kila nchi duniani inavyofanya kwa anzilishi wao),kwa sababu bila nyinyi wengi wasingejulikana wala kupata heshima ambayo wanapewa kwa kutumia HIPHOP leo hii nchini Tanzania.
  Hiphop imewanya muweze kuleta watoto na watu wazima kila kona Tanzania nzima…Coco Beach na sehemu zote mlizofanya kazi ya kuryhme watu walikuwa wanafurahi mkimaliza,hata kama walikuja na nyuso na roho zao zimenong’oneka.
  Hip hop is a way of living,you have to eat,breath,talk,sleep and wake up Hip hop to be Hip hop,Kwanza Unit is indeed the First Unity of Hip Hop in Tanzania…Respect it…Revolutionary Movement.Pamoja

 9. kidada Says:

  MANDINGO– Bugzymalone si yule aliyekuwa kwenye lile kundi walikuwa wanajiita NO NAME,pamoja na kina diznigga , niliwai kumuona kwenye interview moja ktkt channel ya mnet nadhani yupo south-africa, cause yule mtangazaji wakati ana fanya naye interview alimuuliza kama yeye ni mtu wa USA kwa jinsi anayoongea english
  anyway KU – CREW for life yoooh…

 10. mzalendo Says:

  muasisi ni Saleh Jabir wa nyimbo hizi si Kwanza wala mister two anadanganya watu kuwa yeye ni muasisi.
  Saleh jabir alikuwa na kina diga diga.

 11. mtaalamu Says:

  hii ilikuwa group moja ya kwanza enzi hizo wakati vijana tunaenjoy mziki siyo ubitozi uliokwepo. enzi hizo pale morogoro stores na baadaye kwa mzee kimario kiga basket . Magfu upo hapo

 12. yuthman Says:

  yap! man i gotta resp 2dem oll hawa ndo sojaz of back n’ days n2 jah will olwayz guide fi dem ,yaani ni makings ,machifu wa hip hop ya tha real roots of this knowledge ya mtu mweusi ,yap! man u kan even see kila kitu as wengine wanarepeat bt wengi wnaharibu ,hawana misingi,ya hawa ma kingi,wanajali shilingi,hawafuati hip hop lingi,hawafly high wako blank, ndo maana hawadanki,wapo wengi sana kila kona ,ishara yao sauti kubana, kaenda bilcana kesho tachonga sana,kaitwa na amina basi kasha jiona,hawakamilishi namba hip hop itazidi kutamba,watakwisha kama uturi.viburi wataishia sifuri, hip hop itawachimbia kaburi na midomo juu watakosa kauli, ebwanaeeee naenda skuliiii 2mit kwa dadiiiiiiii

 13. Abby Hass Says:

  hey every one know dat Kwanza Unit is Mzuuuka!!!,nawakubali pia endelezeni harakati kama zamani kwani nyinyi ndio waasisi,kama mzuka hata mimi ninaflow kiasi chake nipenishavu au niaje Saigon??????????????Ooooooooh Mzukaaaaaaaaaaaaa.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s