BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MARIA-HEMED MANETI & VIJANA JAZZ BAND April, 25, 2008

Filed under: Burudani,In Memory/Kumbukumbu,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:07 AM

Mapenzi ni dhana pana sana. Ni dhana ambayo mpaka hivi leo mwanadamu bado anahangaika kupata ufafanuzi wake. Hata hivi leo tukiuliza hapa hivi mapenzi ni nini,tunaweza kupata maoni zaidi ya hata elfu moja huku kila mmoja akiwa na maana au tafsiri yake kuhusu mapenzi. Usishangae kama tafsiri hiyo yaweza kuwa tofauti kabisa na yako au yangu!

Bahati nzuri au mbaya ni kwamba mwisho wa siku wote tutakuwa sahihi. Kila mmoja anaruhusiwa kutafsiri dhana ya mapenzi au penzi kwa kadri anavyoona yeye au kwa jinsi ambavyo “mvua inakuwa imemnyeshea”.Si unakumbuka kwamba aisifiaye mvua imemnyeshea?

Upana wa dhana ya mapenzi huenda ndio hupelekea kila kukicha wanamuziki wanazidi kutunga na kuimba nyimbo kuhusu mapenzi. Mapenzi hayajaanza jana wala leo na hayatokaa yafikie mwisho.

Pamoja na hayo, zipo nyimbo za mapenzi ambazo wenzetu wanaotumia kizungu huwa wanasema “it has stood the test of time” kumaanisha kwamba wakati sio kitu kwake kwani kitu hicho(nyimbo) bado kinapendwa na kitaendelea kupendwa kwa wakati mwingi ujao.Mfano mzuri wa nyimbo za aina hiyo ni ule uitwao Maria (Mary Maria) ulioimbwa na Vijana Jazz Band enzi hizo ikiwa chini ya uongozi wa Hayati Hemed Maneti(pichani). Katika wimbo huo utamsikia Maneti akilalama kutokana na penzi zito alilonalo kwa “mtoto” Mary. Baadhi ya maneno kwenye wimbo huo ni kama;

Kwa kweli sasa nimenaswa
Sina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh

Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeee
Na wala sitapenda mpaka nife,
Mpaka nife, mama Mary oooh

Bonyeza player hapo chini upate burudani kamili ya wimbo Maria.Kama unaye umpendaye, huku naye anakupenda kwa dhati na wala sio “for convenience” basi muite mwambie mcheze kidogo wimbo huu.Nakutakia Ijumaa Njema.

Advertisements
 

11 Responses to “MARIA-HEMED MANETI & VIJANA JAZZ BAND”

 1. sally Says:

  Wimbo umetualia sana huu maneno matamu!

 2. Edwin Ndaki Says:

  Ijumaa ipo pale pale..

  Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa juma.

  tutafika tu

 3. Mswahilina Says:

  Asante BC. kwa kutukumbusha enzi zetu.

  R.I.P. Hemed Maneti.

 4. Kwa kweli wimbo huu umenikumbusha mbali sana. na hasa nakumbuka siku Hemed maneti alipoaga dunia. siku hiyo nilikuwa nipo nyumbani, nikingojea kipindi cha michezo cha RTD ambacho kilikuwa kikirushwa hewani kuanzia saa mbili kasoro robo.
  Basi ghafla tu baada ya kipindi kuanza mtangazaji ambaye namkumbuka alikuwa Julius nyaisanga alianza kupiga wimbo huu na alipoukata akatufahamisha kuwa Maneti atunaye tena. ilikuwa ni usiku wa huzuni kubwa sana.
  Jamani tukubali ama tukatae zamani kulikuwa na muziki na ndio maana wakati fulani nilimshauri mdau mmoja kuacha kufananisha wanamuziki wa sasa na hao wa zamani.

  Mungu aiweke mahari pema peponi roho ya Hemed maneti. AMINA

 5. Dullah Says:

  Thanks BC. Mziki kipaji jamani sio juhudi, marehemu Maneti he never strugle to sing or writte a song.

 6. DUNDA GALDEN Says:

  Hatari kubwa ijumaa tena leo home is beast jag älskar mitt land music jätt bra
  usiombe uzame kwenye dimbwi hilo na ukweli utabaki pale pale pindi unapomlove some one ayay ayay shukrani ziwaendee wote wapenzi wa BLOG hii na kwenu BC
  iki kibao kizito(unaweza kupendwa au kupenda mpaka watu wakauliza kwani anampendea nini?kwanza yuko hivi na hivi wengi usahau penzi ujenga daraja usipime hapo hatari)ijumaa njema
  chafosa chai goda(Victoria Australia)

 7. Gervas Says:

  nimetoka shuleni mchana, nimetulia nasubiri lunch huku nasikiliza kipindi cha mchana mwema kwenye redio yetu ya mbao….1986!!! , ha-ha-ha, Matty, Michelle, Edwin mlikuwa wapi enzi hizo?

 8. Gado Says:

  Raha ya kuwa mwanamziki ni nini?
  Maana wanamziki wengi ukumbukwa na kumwagiwa sifa
  pale wanapokuwa hawapo tena duniani!
  ndio watu na washabiki uwakumbuka kwa umahiri wao!?
  kwanini tusiwafagile wanapokuwa hai? japokuwa na wao
  wajione kuwa mchango wao katika jamii ni muhimu?
  mimi sipo hapo! nawachia wenye kujua kusukutua
  midomo

 9. Zitto Says:

  Wimbo umenikumbusha mbali sana. Asante

 10. J.J Says:

  Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeee
  Na wala sitapenda mpaka nife,
  Mpaka nife, mama Mary oooh

 11. mtanga line Says:

  duuuuuuuu marehemu Manet manake enzi hizo nipo school babake mhhh sasahivi nina 40 somthing akili ziliniruka kama kaniimba mimi vile aaah hii inanikumbusha sipendi maisha tena mpaka nife waliobaki nitawadanganya tu bye mtanga ndani ya sauzi cape town


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s