BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NINI NA KWANINI? April, 28, 2008

Filed under: Mawazo/Tafakuri,Swali kwa Jamii,Uncategorized,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:55 PM

Yapo mambo ambayo pindi yakitokea kila binadamu hushikwa na butwaa na kutokutambua mara moja kwamba nini kimetokea,kinatokea au kinaelekea kutokea. Mojawapo ya mambo kama hayo ni kama kitendo kilichotokea hivi majuzi pale katika hospitali ya Muhimbili ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 12 ajulikanaye kama Ramadhani Mussa(pichani) alikamatwa akiwa na kichwa cha mtoto mdogo, Salome Yohana (miaka 3) alichokuwa amekibeba kwenye mfuko wa Rambo!

Tukio hilo la aina yake,la kusikitisha na hata kuchosha akili limeandikwa na blogs mbalimbali na pia vyombo karibuni vyote vya habari nchini Tanzania.Kwa sababu habari yenyewe bado inazua mijadala mbalimbali, tumeona sio vyema kukunyima wewe msomaji na mtembeleaji wetu, fursa ya kutoa maoni yako kuhusiana na tukio hili.Nini maoni yako kuhusiana na tukio hili? Ni uchawi, imani za kishirikina, matatizo ya akili au ni nini hasa? Kwanini watoto?

Isitoshe,mtoto Ramadhani Mussa, ambaye hivi sasa anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar-es-salaam akiendelea kuisaidia polisi na uchunguzi, yawezekana ndio jina au tukio lililotawala vinywa vya watu wengi hivi sasa.

Kama hujapata fursa ya kusoma habari mbalimbali kuhusu tukio hili,unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa na hapa na hapa.

Wakati huo huo,gazeti la Uwazi(mojawapo ya magazeti ya Global Publishers), hivi leo wametoa habari ya kina ya tukio hili kama ambavyo unaweza kuiona katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo hapo chini.Unaweza kuisoma habari hiyo kamili kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

29 Responses to “NINI NA KWANINI?”

 1. J.J Says:

  wasiachiwe na serekali,si wauliwe tu,na wauliwe kwa kinyama, kama alivyomfanya yule mtoto wa miaka 3

 2. mtukwao Says:

  “mtoto wa nyoka ni nyoka” hatasikumoja mtoto wanyoka hawezi kuwa “paka”.

  hivyo huyo mtoto ni mwanga/mchawi, napia wazazi wake ni wanga tu!!

  wachai wapo hapa duniani hata Bible inatuambia. pia imewaonya inamesema ” olewao wachawi na waabudu sanamu”

  hivyo simshangai sana, ina inasikitisha tu kumuuwa kikatili mtoto wa miaka “3” tu. she had alote to live for!!

  pole kwa familia ya mtoto aliye chinjwa kikatili.

 3. Kamanzi Says:

  Huyu mtoto anatumiwa na mafisadi ili kuwalinda kishirikina. Mafisadi wameanza sasa kula nyama za watu na kunywa damu lakini vyovyote vile mwaka 2010 mafisadi wote nje hakuna cha uchawi wala baba yake nani. Tanzania oyeeeeee!

 4. Amina Says:

  we bc uchawi na imani za kishirikina ni kitu kimoja…ila mi naamini hivi vitu vipo ila watu wanajidaigi wazungu hawaamini ila yakishakukuta siku ndo unafunguka akili ala kumbe!

 5. Kwa maoni yangu tukio ili ni kubwa sana na ndani ya tukio ili kuna jambo lililofichika. mimi nafikili tukio ili alipo kiuchawi sana wala kishilikina, nina wasiwasi kuna jambo tu lipo katikati ya huyo mtoto na watu wengine.

  Nafikili mtoto huyo anatakiwa kuhojiwa na wapelelezi waliobobea, lazima ufanyike upelelezi wa kina ili kutambua jambo hili.
  Siku chache zilizopita tuliambiwa mtoto huyo na mwenzake walipatikana katika paa la kanisa mojamara baada ya kudondoka na ungo. lakini baada ya uchunguzi pale hospitali ya taifa muhimbili ikagundulika kuwa awakuwa wachawi na pia wana akili timamu. jambo hili liliwasononesha watu wengi waliotaka jibu tofauti na hilo.

  Sasa mtoto huyohuyo siku chache baada ya kuachiwa anapatikana na tukio lingine na sasa linafanyika mahali pale palipotoa jibu kuwa mtoto huyo alikuwa na akili timamu na si mchawi, hapo kwa maoni yangu kuna walakini na ndio maana nikatoa hoja yangu ya kufanyika uchunguzi makini. pia asikari aliyekuwepo getini pamoja na huyo mfyeka majani, lazima wahojiwe kwa kina na kuthibitisha kama kweli walimuona akinywa damu na kula hicho kichwa alichokibeba.
  Hapa hoja yangu ninaijenga kuwa uenda ni tukio lililotengenezwa ili kutimiza malengo fulani.

  Lakini kutengenezwa uko hakumuhusu baba na mama wa mtoto kwani wao ni wahanga kamili wa tukio hili na kwa kweli nawapa pole sana kwa msiba huu mkubwa. mungu awape nguvu na heri nyingi katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.

  Mwisho baada ya upelelezi kukamilika mtoto huyo pamoja na wote waliohusika kwa mauaji hayo wapelekwe mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji ya mtoto asiye na hatia.

 6. Liz Says:

  Nahisi kuna mambo ya ushirikina hapo, mtoto wa miaka 12 kufanya mauaji peke yake? utata! Serikali yetu haiamini imani za uchawi lakini kwa kweli hayo mambo yapo. Jeshi letu la Polisi lisiyachukulie haya mambo juu juu, huyo mtoto ni tishio maana mwenyewe kakiri kumchinja mtoto Salome. Maisha ya kijana huyo pia yako mashakani maana watu wakiona anazunguka mitaani watachukua hatua zile zinazochukuliwa Shinyanga, kwa kuhofia watoto wao kuchinjwa na kutafunwa.

 7. binti-mzuri Says:

  aisee ni suhirikina tu huo,si ajabu huyo mtoto ramadhani alikua anatumiwa…yasikitisha

 8. sally Says:

  Jamani Tumuombe mungu mbona inatisha!! Nafikiri wazazi wanatakiwa wahojiwe may be wanajua au la! Pia wana sema huyo mtoto alisha pimwa kucheki kama yupo ok au anamatatizo ya akili wakasema yuko sawa. Sasa katoto wamekauwa bila kosa masikini inasikitisha sana kwakweli. me i have nothing to say wadau bali imeniuma kukatisha maisha ya mtoto wetu.

 9. Ms Bennett Says:

  ni uchawi/ushirikina na sio matatizo ya akili.

 10. Chris Says:

  He’s so young and look so decent, huwezi amini kama yeye ndo aliefanya huo ukatili. I saw the pictures, its really gruesome. But nafikiri ni nguvu za giza zilizomtawala ndo zilizofanya afanye huo unyama.

  Hilo tukio limetokea hapo Dar ambapo “pamechangamka”. Sijui huku vijijini.

  Nafikiri ni swala la kuchukuliwa kwa uzito wa kipekee. Tusijadili kwanza jinsi ya kutoa hukumu mapema kabla ya kujua kiini au kuondoa mzizi kwanza. Tatizo litatuliwe kwa kuanzia kwenye kiini kwanza, ndo kama kuna hukumu ifanyike, but kama ni nguvu za giza ndo zinazomuongoza, he is so young, zikiondolewa hizo nguvu and be given another chance, he can be a good kid and like other citizens fulfil his positive dreams.

 11. baker Says:

  Duh bongo sasa inatisha atujakaa sawa mafisadi mara watu wanakula watu jamani mbona nchi yetu inakuwa na story za jabu namna hii??? duh kweli bongo kazi ipo. Mungu saidia Mungu saidia uku tunapokwenda panatisha.

 12. binti-mzuri Says:

  wewe J.J wa hapo juu uliekuwa wa kwanza kucomment,kumradhi ila wewe na hao wachawi sioni tofauti zao..unataka wauliwe kinyama,kama yule mtoto alieuliwa kinyama WEWE NI NANI HASA KUTOA HUKUMA KAMA HIYO??HATA IMAMU AU PAPA MWENYEWE HAWEZI KUNYOOSHA KIDOLE NA KUSEMA WEWE CHINJWA..walichofanya nikibaya hilo nalijua,ila MWENYEZI MUNGU atatoa hukumu.mimi naona wafungwe jela maisha tena wasiachiwe!

 13. Celine Says:

  Ni jambo la kusikitisha na kukera pia. Mtoto wa miaka 12 ni mchawi! tena muuaji! Mpaka kafikia stage hiyo ina maana ana uzoefu na hizo shughuli. Kwa maelezo niliyoyasoma haina haja ya ushahidi zaidi. Kila kitu kiko wazi. Wasimcheleweshe asije akatoweka kiaina na kuzua mabalaa mengine makubwa zaidi.

 14. Gervas Says:

  Amina nakubaliana na wewe kabisa. Tatizo Serikali eti Haitambui Uchawi/Ushirikina sababu tu ya kufuata mambo ya Uzungu/Ukoloni. Wakumbuke kuwa hii ni Afrika na uchawi upo na unaharibu na kuuwa watu vijijini na mijini, ni part ya utamaduni potofu wa Kiafrika. Nyerere na Sokoine walianzisha “Sungusungu” ambapo wachawi/washirikina walikuwa wanacharazwa bakora na mambo kwa kweli yalipungua. Nakumbuka miaka ya 80 Mkuu wa wilaya ya Magu enzi hizo (Jina Kapuni Maana siku hizi huyo mama ni waziri) alianzisha msako wa kukamata wapika gongo, ilitokea siku moja aliamka asubuhi akajikuta yupo uchi katikati ya uwanja wa Mpira wa hapo wilayani, akiwa kanyolewa nywele zake. Nasikia mpaka leo hajatia maguu tena wilayani hapo. Bibi nyau pale Magomeni mapipa alikuwa na paka kama 200 hivi sijui wa nini wale. Mwanza, Bugando kuna Bibi fisi ambapo Greda lilishindwa kuibomoa nyumba yake ya matope ili wajenge barabara ya lami, mpaka leo barabara ikifika hapo imepinda na kibanda hicho bado kipo japo huyo bibi alishafariki. Uchawi huu ungekuwa unatumika kwa maendeleo ingekuwa nafuu, sio kuua au kuharibu watu.

 15. Gervas Says:

  Pili Kuhusu tukio hili, mimi nailaumu Serikali pamoja na Polisi. Mtoto huyu na mwenzake walishakmatwa sehemu mbali mbali Dar awali kwa shutuma za kishirikina, lakini eti wakawaachia tu, sababu ni ajabu kukuta watoto km hao ktk issue za uchawi. Walipaswa kuwachunguza, kuwahoji na kufuatilia yale waliyokuwa wanayasema na wangebaki chini ya ulinzi au uangalizi. serikali ilipaswa kuwa na kikosi maalumu kikiwahusisha wazee wa makabila kadhaa, maana wakuali wasikubali wachawi wapo na watu wanawajua na wanajuana wao kwa wao. Maana mwizi anawajua sana wezi wenzake. Kesi z kupotea watoto kwenye miji kama ya Dar zimekuwa kawaida siku hizi, na erikali wanasubiri tu matukio km haya ndo waanze kuhangaika.

 16. michelle Says:

  Mambo haya serikali inayajua sana, maana wao wenye kila siku wanakolimbana huko Dod, simnajua yale mambo na nanihii!!!!!!!!

  Hili swala si lakupeleka au kuchukuliwa kichwa kichwa maana hapo mnacheza na shetani mwenyewe, huweza kushindana na shetani kwa nguvu za kibinadamu haiwezekani maana mtamfunga atawatoka tu bila ninyi kujua.

  Sasa waiteni Wapendwa wamhoji kwa maombi na kwa karibu zaidi ndipo mambo yote yatakuwa wazi, bila hivyo mtamjua shetani ni nani na anafanya kazi gani hapa duniani, atawavuruga mpaka, maana ameshawajua kuwa mnamchukulia kimwili.

  Hata huku Wadhungu wanakutana na mambo kama haya haya, wakifikiri kuwa wao ni wajanja, wanatumia Camera na vifaa mbalimbali kufuatilia nyayo za wachawi na mapepo, waulizeni huwa wanapatwa na nini, cheza na shetani kichwa kichwa utakoma mtafuteni Mungu anayeishi.

 17. puza tata Says:

  Samahani najua wengi mtashangaa nikiwaambia kwamba huyu mtoto si mchawi. Sijui kumuita kwa kiswahili ila kingereze ni excessive compulsive behaviour. Watu wengi wanaofanya vituko huanza na dalili za kawaida na watu hawashituki (kama kujificha kanisani). Moja huyu mtoto anapenda atention na anatamani asifiwe mtaani ndo maana kafanya vituko vingi. LKosa ubwa jamii haikutilia maanani nd maana kapaaribu na kila mtu anadhani mchawi.
  moja ya swali la kujiuliza anadai yeye na mama yake wachawi alafu yeye ni kiongozi. mnajua mila za kiafrika thats impossible. Technicaly he is a serial kiler on the making and should neverbe late loose. Killing someone make him feel in control he will do it again whenever he has a chance..

 18. J Bigy Says:

  Kama baadhi yao’ wanaenda’ pia Bagamoyo, Unategemea nini?Anayeamini uchawi anauogopa kama ukoma bwana Gervas.Ukiwa ndani ya Uchawi huna sehemu mbadala ya kukimbilia.Utafia humohumo kwani umeshajisajili.
  Vita vya majimaji tulisema risasi zingekuwa maji!Kwenye mpira tunachekelea tukisikia ‘kamati ya ufundi’,hadithi za mtu kusafiri kwa ungo na wengine kupigwa na radi kukiwa hamna dalili ya radi, kulimishwa GAMBOSHI n.k vimezoeleka masikioni mwetu na hivyo kuonekana sehemu ya maisha.
  Huyo mtoto hatafatiliwa wala walomtuma kwani baadhi ya wafatiliaji pia inasemekana ‘huenda’ Bagamoyo.
  Kwa ujumla ni MZIKI MNENE unaohitaji mchakato wenye upembuzi yakinifu.

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Inauma Sana! Tuwe waangalifu sana na tumtegemee Mungu zaidi. Nakumbuka 2000 nilitumaga kupatiwa msichana wa kazi. Jioni kama kawaida yetu tukaangusha libeneke la nguvu la sala.

  Usiku kumbe yule mtoto ni mchawi akataka kupaa ndege yake ikakataa kuruka! Tumelala ndani tukasikia mtu analilia nje maana hata kurudi hakuweza tena.

  Alipohojia alikiri udhaifu na kudai kuwa huwa wanasafiri usiku kwa ajili ya shughuli zao (cha kusikitisha zaidi alidai huwa wanawatumia watoto wadogo waliowaua)-. Fikiria nini kingeikuta familia maana alikuwa alee watoto watatu, wawili wanafunzi na mmoja miaka miwili!

  Hii habari imenikumbusha mbali na imeniongezea simanzi!

  NB: Kesheni mkiomba maana majaribu ni mengi na pia usimchukue mfanyakazi wa ndani usiyemfahamu!

 20. Mama wa Kichagga Says:

  NB:

  Huyo mtoto afanyiwe uchunguzi wa kina ili kuweza kuutambua mtandao wao na serikali iingilie kati ili tabia hii kuweza kukomeshwa!

  R.I.P Mtoto Salome

 21. ma'reen Says:

  Wewe puza tata ngoja kajamaa kakutokee usiku ndo utajua kama ni compulsive sijui nini!Unashangaa kako pembeni mwa bed milango imafungwa hakajavunja tuone kama utaanza kutafuta kwenye kamusi yako hiyo excessive…!Haka ni kagagula tu, kachawi asilia, ni DAMU YA YESU TU inaweza ku-deal na haya mauzauza otherwise mtakesha bure.

 22. trii Says:

  jamani heee yote yameshatokea,sasa tufanyeje ili yasiendelee,mi naamini huyo kijana anatumwa na wakubwa zake,je tufanyeje ili tuwapate hao ,kwa sababu hata wakimuua huyo mtoto tatizo bado halitaisha,wale wanao mtumia bado watakuwa na uwezo wa kumtumia mtu mwingine.kama hawa wachawi wanauwezo kubwa hivi kwa nn serikali isiwatumie kufichuwa mafisadi,walarushw na vimeo vingine huko serikalini????

 23. mazagazaga Says:

  Just a TIP to the Police:Huyo kijana aliyekutwa na kichwa asiachiliwe kabisa.Mtoto huyo anatumiwa na watu wazima kabisa wenye akili zao timamu lakini wenye imani za kishetani na malengo maovu kabisa ya kutaka kushindana na Mungu.Siku ile alipokamatwa pale Langoni katika Hospitali ya Muhimbili akiwa amebeba kichwa cha mtoto katika fuko la plastiki(kama sijakosea), Muuaji mhusika mkuu hakuwa mbali sana na huyo mtoto.Alikuwa maeneo ya jirani akiongozana na ye kwa nyuma ili aweze kuhakikisha huyo kijana ataufikisha mzigo huo wa kichwa kule kulikokusudiwa.Huyo mtoto hakuwa anatenda mambo yale kwa ‘Remote Control’ kama wengine watakavyo amini kishirikina.Iwapo wale walinzi wa Muhimbili Langoni waliomkamata yule kijana watabanwa zaidi ili wakumbuke sura walizo ziona pale karibu ya tukio lile,hususan mtu aliyejaribu kuonyesha huruma ya hali ya juu akiomba yule kijana asamehewe kwa sababu ni mtoto mdogo na anatumiwa kishirikina au watu wengine kadhaa,basi msako ufanyike kuwatafuta watu hao hata ikichukua miaka 20.Huyo mtoto Ramadhani kwa kumwangalia tu uso wake akiwekwa chini ya ulinzi akatulizwa akili yake kabisa na asiteswe,asipewe vitisho na apewe kila atakacho kipenda basi kuna uwezekano mkubwa siku moja ataropoka tu kitu(povide key lead or clue) kitakacho wawezesha Polisi wa Upelelezi(Police Detective) wafuatilie ule mtandao na hatimaye kuutokomeza kabisa.Na pale palipokutwa kile kiwiliwili cha yule mtoto Salome,lazima uchunguzi wa kina ufanyike haraka sana kwa kubainisha ni wakazi wepi wa eneo hilo waliotoweka ghafla kuhamia maeneo mengine, au watu wenye sura ngeni walio onekana katika maeneo hayo kwa majirani au kuzifahamu kwa undani taabia za kila mkazi wa eneo hilo lilipo tokea hio tukio. Inaelekea mtoto huyo alichinjwa usiku uleule wa kutoweka kwake na tukio hilo lilifanyika katika maeneo hayo hayo ya jirani. Lazima damu zilimwagika sana baada ya uchinjaji huo na siyo rahisi hata kidogo damu hiyo ikafutwa na kufutika kabisa bila ya kuacha madoadoa. Kwa hiyo kila nyumba katika eneo hilo ipekuliwe na kila kichaka kitakacho tia wasiwasi katika eneo hilo kipekuliwe.Lazima ushahidi utapatikana wa wapi hasa uchinjaji ule ulifanyika kama ni katika nyumba ya mtu au eneo la kichakani.Na tendo hilo lilifanywa na Mtu Mzima kabisa na siyo huyo mtoto Ramadhani.Lakini hiyo haina maana huyo mtoto Ramadhani aachiwe.Huyo mtoto ni hatari sana ambaye hakika hukumu yake ni kifo kwa vyovyote vile alivyo husika.Kama nilivyosema hapo awali,kwamba ili kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Ramadhani asipelekwe mahakamani kwa hivi sasa, atunzwe vizuri mpaka akili yake itulie awe katika hali ya kawaida, chochote atakacho taka apewe, lakini wakati huo huo wale wataalamu wa kudodosa mambo wakiendelea na kazi yao ya kumhoji polepole bila ya papara.Ipo siku ataropoka kitu muhimu kitakacho fichua mtandao mzima wa hao wahalifu. Mauaji ya mtoto Salome bila shaka yalipangwa siku nyingi. Wazazi wa Salome wajaribu kukumbuka ni kina nani waliojaribu kuwazoea kwa haraka katika siku za karibuni pengine itasaidia. Katika matukio kama haya tuzingatie busara za wazee wetu. Mara nyingi ‘Kikulacho ki Nguoni mwako’. Na kwamba ‘Fimbo ya Mbali Haiui Nyoka’. Mara nyingi mtu wa mbali asiyekujua undani wako ni vugumu sana yeye kukudhuru.Atakaye kudhuru ni yule jirani yako au mtu aliyekuzoea na kukufahamu undani wako. Tahadhari, siyo wote majirani zako au watu waliokufahamu undani wako wakawa maadui zako. Lakini pa kuanzia kupapasa nani atakayeweza kufanya unyama kama huo lazima pawe hapo katika eneo la tukio na mazingira yake.Katika tukio hilo tuamini kwanza kwamba halikufanyika kwa imani za kishirikina. Bali waliolifanya ni watu wenye Imani za Kishetani ambao wanataka kushindana na Mungu katika mambo mengi.Kwa mfano,wawe na uwezo wa kufufua wafu, au uwezo wa kulazimisha matukio ya nchi kulingana na matakwa yao.Inawezekana vilevile kwamba lipo kundi la watu lenye mawazo ya kishetani waliodhamiria kujenga hofu miongoni mwa wanajamii ili kutimiza malengo yao.Au ni mbinu inayo tumiwa na wachawi au waganga wano piga Lamli ili wakuze biashara yao kwa kujenga hofu zaidi katika jamii.Haya mambo lazima yashughulikiwe katika mapana yake bila ya kuoneana haya hata kama mjomba wako au shangazi kahusika.

 24. aNASTAZIA Says:

  Jamani hivi Watanzania tunaelekea wapi , yani kila kukicha mambo mengi na ya ajabu yanaibuka watu wameloga mpaka sasa wanaanza kukatisha uhai wa wengine kwa faida na manufaa yao. Ikiwa ugumu wa maisha unatumaliza,UKIMWI unatumaliza,Mafisadi halkazarika je tutafika jamani? Msongo wa mawazo na fikra nyingi za mambo ya kutisha tunayosikia kila siku unatupunguzia uhai. Nawapa pole wafiwa mama na baba Salome Yohana Mungu ndio anajua adhabu ya kumpa Ramadhani kama alishawahi kuumba ni haki yake uuwa pia.
  Nashauri uchunguzi ufanyike wa kina na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kwani serikali haiamini ushirikila lakini upo na sheria ichukue mkondo wake laa sivyo tutamalizana kwa hizi imani. IMENISIKITISHA SANA NASHINDWA HATA KUELEZEA.

 25. jamy Says:

  Mswiba!!! yaani inasikitisha sana, cha muhimu ni kufuatilia alifanya haya mambo na nani ili nawenyewe wachukuliwe hatua, mtoto asiachiwe afungwe maisha.

 26. mdunger Says:

  Wa TZ lazima tujiulize,kwanza wachunaji ngozi,pili mauaji ya albino na sasa mauaji ya vichanga.Hapa tunahitaji kuwa waangalifu,Tufanye uchunguzi wa kina kwa kutumia njia za kisayansi na kuangalia imani zetu za kiafrika.Kwani tunaweza kufikiri ni ushirikina kumbe sio au ni kinyume chake.Kwa hiyo,Naamini uchunguzi wa police utatupa majibu sahihi.Lakini inatia uchungu sana mauaji ya mtoto Salome.

 27. Edwin Ndaki Says:

  Kabla ya yote.

  Mwenyezi Mungu ipumzishe roho ya mtoto salome mahala pema peponi.Amina

  Watie nguvu,ujasiri wazazi wake na wapendwa wake wote walio katika kipindi kigumu.

  TATU:
  Ukweli sifahamu nini maana ya uchawi,hivyo sijui hata mchawi na uchawi.(Mtazamo wangu)

  MWISHO:
  Hilo tukio ni vema vyombo vya usalama vichukue hatua za kisheria.Ikiwemo kuwashirikisha wadau kwa pembeni kuhusu nini kifanyike kusaidia hilo lisije tokeo.

  Hapo nime maanisha watu waliobobea katika masuala ya “saikolojia” na wazee wetu wa dini na wazee wa “BUSARA”.Jibu lipo.

  Tutafika tu.
  Nalaani kwa nguvu zote kitendo hiki.

 28. Hurry Vincent Says:

  Jambo zima ni la kusikitisha. lakini kitendo cha magazeti kutoa picha ya mtoto aliyechinjwa pamoja na TV kuonyesha ni jambo la kukemewa. watoto wetu mameasilika kwa kuona picha hizo. waziri anayehusika kama hakukemea wala kuona hilo hafai kushika wizara hiyo. alipaswa kukemea na kuviondolea vibali vyombo vyote vilivyo husika kuonyesha picha ya mtoto aliye fanyiwa unyama huo, ili liwe fundisho kwa wote.

 29. leila shakum Says:

  inalilah wa barakhut alhamdulillaaaah na walaanikeee


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s