BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

AFRIKALI May, 31, 2008

Filed under: Burudani,Sanaa/Maonyesho,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:37 PM

Kundi la muziki asilia la AFRIKALI (pichani) lenye makao yake makuu jijini Dar-es-salaam. Umeshawahi kuwashuhudia AFRIKALI jukwaani? Siku za nyuma tuliwahi kuandika kidogo kuhusu kundi hili.Bonyeza hapa usome tulichokiandika na mjadala uliozuka.

NB: Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu,wiki hii hatukuweza kuwa na burudani ya kawaida ya ijumaa.Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.Ijumaa ijayo mambo kama kawaida.

Advertisements
 

ZAIDI KUTOKA MISS UNIVERSE 2008 May, 30, 2008

Filed under: Fashion,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:46 PM

Kulia ni Miss Universe Tanzania,Flaviana Matata, akifuatilia shindano la kumtafuta mrithi wake jana.Unaweza kuwatambua hao warembo wengine alioketi nao?

 

MISS UNIVERSE TZ 2008 NI AMANDA

Filed under: Fashion,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 10:10 AM

Mrembo Amanda Sululu(pichani) jana aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2008. Shindano hilo lilifanyikia jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jijini Dar-es-salaam.Kwa maana hiyo Amanda ndiye anarithi taji kutoka kwa Flaviana Matata mrembo ambaye mwaka jana alifanikiwa kuiletea sifa Tanzania baada ya kufanikiwa kuwemo katika tano bora ya mashindano hayo katika ngazi ya dunia yaliyofanyikia nchini Mexico.

Tatu bora-Katikati ni Amanda Sululu,kushoto ni Jamila Nyanga(mshindi wa pili) na kulia ni Eva Babuely(mshindi wa tatu)

Mashindano ya Miss Universe mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai katika ukumbi uitwao Crown Convention Center(Diamond Bay Resort) mjini Nha Trang nchini Vietnam.Zaidi ya washiriki 80 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki.

BC inampa hongera Amanda na kumtakia kila la kheri mbele ya safari.

 

REHMTULLAH DURING TEMPTATIONS SHOW May, 29, 2008

Filed under: Fashion Designer,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:58 PM

Mbunifu wa mitindo ya nguo anayekuja juu kwa kasi nchini Tanzania,Ally Rehmtullah,akipita jukwaani kuwasalimia na kuwashukuru watu mbalimbali waliohudhuria show yake iliyofanyikia katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jijini Dar-es-salaam wiki iliyopita.Rehmtullah aliita show yake Temptations.Kwa habari zake zaidi unaweza kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa.

 

KUTOKA “MAMBO HAYO” MPAKA… May, 28, 2008

Filed under: Burudani,Filamu/Movie,Sanaa/Maonyesho,Television — bongocelebrity @ 8:35 PM

Sanaa ya maigizo na filamu nchini Tanzania ina historia ndefu.Katika historia hiyo yapo majina au sura za wasanii ambao, upende usipende, huna budi kuthamini mchango wao katika sanaa hiyo kwa njia moja au nyingine.

Hapa naongelea wasanii kama Kemi(pichani) ambaye ni miongoni mwa waigizaji wazuri nchini Tanzania.Wengi bado wanamkumbuka toka enzi zile alipotoka na MAMBO HAYO.Kemi ni jina lake la kisanii.Unalijua jina lake kamili?

 

WANAWANIA TAJI LA MISS UNIVERSE TANZANIA ’08 May, 27, 2008

Filed under: Fashion,Sanaa/Maonyesho,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 7:11 PM

Pichani ni washiriki wa shindano la urembo la Miss Universe Tanzania 2008, wakiwa katika picha wakati wa uzinduzi wa kambi kwenye Hoteli ya Belinda, Kunduchi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hapo jana Mei 26,2008. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika keshokutwa kwenye Hoteli ya Movenpick Royal Palm jijini Dar-es-salaam.

Photo/Msimbe Lukwangule

 

MISS UNIVERSE 2007 NA DR.MIGIRO May, 26, 2008

Filed under: Fashion,Uncategorized,Urembo — bongocelebrity @ 4:37 PM

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr.Rose Asha Migiro(katikati) alipokutana na Miss Universe 2007, Riyo Mori(kushoto) jijini New York mwezi uliopita.Mwingine katika picha(kulia) ni Mwakilishi Maalumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP),Tokiko Kato.

 

Nchini Tanzania,maandalizi ya shindano la kumtafuta mrithi wa Flaviana Matata(Miss Universe Tanzania 2007) yanaendelea vizuri kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni ya Compass Communications ambao ndio waandaji wa shindano hilo kwa upande wa Tanzania.Nani atamrithi Flaviana?Ni suala la kusubiri na kuona.

UN Photo/Paulo Filgueiras