BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MNYONGE ANA HAKI? May, 2, 2008

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:06 AM

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Bila shaka umeshawahi kuusikia msemo huo.Hivi majuzi tu mheshimiwa kiongozi mmoja alitukumbusha msemo huo! Lakini ni mara ngapi hutokea mnyonge akapewa haki yake? Je msemo wa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni una maana tena siku hizi katika mazingira na dunia tunayoishi?

Dunia ya leo ukiitazama haiendani kabisa na dhana nzima ya msemo huo. Leo hii mnyonge hana haki.Mtizame yule anavyomnyang’anya “machinga” bidhaa zake bila aibu wala woga kwa kisingizio cha “sheria” wakati bidhaa zile zinaishia mifukoni mwake. Tizama jinsi kibaka anayekwapua mkate kwa sababu ya kuzidiwa na njaa anavyochomwa moto kikatili wakati aliyethibitishwa kuwa fisadi anavyotetemekewa huku akiundiwa tume ambayo nayo itatumia mabilioni ya shilingi ili kupata jibu ambalo linafahamika. Mtizame binti au mama yule anavyosumbuliwa akitakiwa kutoa rushwa ya ngono ili apatiwe ajira.Angalia haki inavyopotea mahakamani kwa sababu tu fulani kashindwa kutoa “chai” kwa mheshimiwa aliyevalia joho.Orodha inaweza kuendelea mpaka keshokutwa kama ambavyo utaweza kusikia katika burudani inayofuatia hapo chini. Ni mengi.Sitaki kukuchosha na maneno mengi.

Sasa zipo nyimbo au wanamuziki ambao wameshawahi kuzungumzia masuala haya ya haki vs mnyonge. Miongoni mwao ni Dr.Remmy Ongala alipokuwa na bendi yake ya Matimila Band.Bonyeza player hapo chini uusikilize wimbo Sauti ya Mnyonge ambao leo umeletwa kwako kwa udhamini wa EastAfrican Tube. Ukitaka kusoma historia ya Dr.Remmy Ongala kama tulivyoiandika siku za nyuma,bonyeza hapa. BC inakutakia Ijumaa Njema.Enjoy.


Advertisements
 

7 Responses to “MNYONGE ANA HAKI?”

 1. Kamanzi Says:

  Nyimbo kama hizi ndio zinanifanya niseme hatuna wanamuziki siku hizi. Wimbo unaujumbe, unaliza na wafaa kusikilizwa na jamii ya rika zote maana hauko X rated. DR. Remmy respect kwako na wanamuziki wote waliokuwepo enzi zenu maana walikuwa wanaheshimu studio na wasikilizaji ndio maana hawakurekodi isipokuwa wimbo una ujumbe.

  Sauti ya mnyonge inaanza kusikika Tanzania. Mafisadi kaeni chonjo. Ipo siku wao ndio watawaza kesho watakula nini maana kiama yao imekaribia. HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA ATI!!!

  Weekend njema kwa wadau wote wa BC hasa wale wenye uchungu na nchi yetu.

 2. Gervas Says:

  Haki ya mnyonge ipo mikononi mwa wenye Pesa na Madaraka. Hebu tembelea magereza, mahabusu hapo ndo utalielewa hilo. Siku zote mnyonge ndiye mtenda makosa, wala huwezi kutana na Fisadi gerezani. Hata tukirudi kwenye dini zetu za sku hizi muumini tajiri anayetoa michango makanisani/misikitini/kwenye ma-temple ndo wanatizamwa kwa jicho la first priority. Hivo haki ya mnyonge iko mikononi mwa wenyenazo.

 3. Chris Says:

  Huu wimbo ni full maujumbe! Esp kwetu sisi wabongo, maskini who depend on the crumbs from our corrupt leaders! Those bros n’ sis’ who live on chances….

 4. hombiz Says:

  Dr.Remmy Ongala ni msanii ambaye mimi ninamkubali toka awali kutokana na nyimbo zake zenye ujumbe wenye maudhui chanya kwa jamii. Kinachosikitisha Mafisadi wa Tanzania swala la ujumbe wa nyimbo kama hii hawauzingatii kabisa. Wanachojali ni kuihujumu nchi kwa nguvu zao zote. Bwana Gervas uliyoyasema hapo juu ni sawa kabisa. Magereza ya Tanzania ni ya wanyonge tu. Mafisadi hayawahusu kabisa. Hii yoye inatokana na kutokuwepo na demokrasia ya kweli Tanzania.
  Wale wanaodai kuwa Marehemu mwalimu Nyerere angefufuka angesikitika kwa kuona jinsi nchi ilivyo na ufisadi wa kupindukia mimi nakubaliana nao kabisa. Ila pia ni lazima pia tukumbuke kuwa pengine mwalimu angesutwa na dhamira yake pia. Nasema hivi kwakuwa yeye ndiye aliyemchagua mkapa kuwa raisi wa Tanzania na kumfanyia kampeni nchi nzima akidai kuwa ni mtu safi (Mr Clean). Kumbe huyo ndio fisadi lililobobea ktk historia ya maraisi wa bongo. Harafu muda wake ulipokwisha akawapigia sana kipenga kina Kikwete na Lowassa akidai ni askari wake wa miamvuli. Huyo Lowassa nae akaja kuumbuka na kashfa ya Richmond. Kikwete nae naweza kusema yuko mtegoni. Nahisi anaficha kikohozi tu hivi sasa. Bila shaka muda utazungumza tu.

 5. DUNDA GALDEN Says:

  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ,
  kama hasipota hatawatafuneni,
  huu ujumbe uliwafikia ndugu zetu wa Burundi.Rwanda,Kenya na kwengineko kwani binadam haki choka kwa kusubili haki yake mda mrefu utata utokea ni wazaifu sana sisi binadam pindi unapokuwa mvumilivu kwa muda mrefu.Ahasante BC kwa huuu mwimbo umenikumbusha mbali enzi zile na wakati huu
  CHAFOSA CHAI GODA(AUSTRALIA)

 6. kino Says:

  na kweli watanzania tumezidi kuoneana wivu, kusemana ovyo bila hata kupenda maendeleo ya wenzetu ndio maana hatufiki mbali.

 7. Niliwai kusema na sitaacha kusema kuwa wakati ule ndio kulikuwa na wanamuziki na muziki tanzania. mwanamuziki alifikili sana kabla ya kutunga nyimbo. na nyimbo zilizotungwa zilikuwa na maudhui, na hisia ya kweli, na kila mtualiweza kusikiliza, bila kujali kwamba ni mtoto kijana au ni mtu mzima.
  sasa tunashuhudia muziki wa kizazi kipya, ambao kwa bahati mbaya kuna ile ambayo uwezi kabisa kuisikiliza na kama ukiweza kuisikiliza basi sio mbele ya watoto wako, au watoto awawezi kuisikiliza mbele ya wazazi wao.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s