BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KUTOKA ZE COMEDY May, 7, 2008

Filed under: Burudani,Comedy/Vichekesho,Uncategorized — bongocelebrity @ 10:01 PM

Kwa wengi anajulikana kama Mpoki ingawa hilo sio jina lake halisi.Jina halisi anaitwa Mjuni Silvery.Ni kutoka kundi maarufu la kuvunja mbavu huku likielimisha jamii la Ze Comedy.Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusu Ze Comedy.Wengine wanasema bado linaendelea kama lilivyoanza huku wengine wakisema kwa namna fulani limeanza kuiacha barabara.Wewe unasemaje?

Advertisements
 

43 Responses to “KUTOKA ZE COMEDY”

 1. noah gondwe Says:

  mi naona jamaa wamepunguza kasi. unajua walipoaanza yaani m2 kumiss kipindi ulikuwa unaona kama haupo sawa. lakini cku hizi uangalie usianagalie hali ni sawa tu. Cha muhimu naomba jamaa wakumbuke kujiendeleza kimaisha isije ikawa kama hawa jamaa wa bongo flava e.g MR. N**E

 2. Duracell Says:

  Mi nadhani wameanza kuacha njia.
  Siku hizi wanachukua muda mrefu sana kuongea kuliko vitendo, tena kuongea kwenyewe hakuchekeshi. si kama zamani. alafu ubunifu umepungua. aliebaki kasimama imara ni joti tu, ye hata akionekana tu sura yake basi ni kichekesho. jamaa bonge la actor!!

  nadhani si lazima waonyeshe matukio yanayotokea sasa hivi tu, bali hata na mengine yalokwisha pita ya miaka ya tisini, kama wameishiwa kwa sasa

  kusema ukweli, kipindi cha miezi 3-4 nyuma ikifika alhamisi saa moja hata niwe na appointment ya kumuona malkia, nitaahirisha ili niangalie ze comedy kwanza. lakini sasa, hata mcheche sina tena. haisisimui kama zamani

 3. Edwin Ndaki Says:

  Binafsi naona kazi zao nzuri.Kikubwa wajitahidi hususani kwenye lugha ambazo zinaweza kuwana itilafu sana.

  Mfano siku moja joti alikuwa anahoji naomba kumnukuu..”yaani kweli mtu wakali kigogo kwa nyuma na wengine wakalia upanga”…MPAKA HAPO HAKUNA TATIZO..sasa alianza kutoa ufafanuzi zaidi..astaghafilai….ilikuwa balaaa..ukichukulia wengine wanatazama hicho kipindi wakiwa na familia nzima.

  Kubwa ya yote nawakubali,naona wanazidi kwenda mbele.Sema imefika wakati watengeze CD,DVD zenye mkusanyiko wa vipindi vyao natumaini kibiashara watapata sana chapaa nzuri.

  tutafika tu.

 4. jonathan Says:

  ni ukweli usiofichka kwamba wamechuja na kimsingi si kazi lahisi kuweza kuwachekesha watu kila wiki inahitaji ubunifu wa hali ya juu lakini jambo la kuzingatia hapa ni kuwa waangalifu wasiendelee kushuka chini nadhani wanahitaji kukaa chini na kutenngeneza mkakati utakaowawezesha kurudi katika chati yao na kuendelea kuvunja watu mbavu kila alhamisi la sivyo watazidi kuporomoka na watasahaulika kabisa yaani itabaki historia

 5. Lady S Says:

  Kwa kweli kundi kwa kiasi flani bado linavunja mbavu za watu kimtindo.

  Ila sikunyingine linakuwa halina habari za kuvujna mbavu,na habari zimekuwa c nyingi kama ilivyokuwa zamani,mie ningependa kuwaambia wazidi kukaz buti tusije wa kinai bure!!!

  nampa sana big up Masanja na Joti wanajitahidi haswa.wasipokuwepo ndio inakuwa ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kabisa!!

 6. trii Says:

  mi naona bado wapo tight ila mara chache chache wana kuwa wamepooza,lkn big up.

 7. mimi nasema bado wakofiti ıle mbaya.

 8. mohamediselemani Says:

  mimi.naona bado wako fitıııııııııııııııııııııııııııııı

 9. mimi naona bado wako fiti llekichiziiiiiiiiiiiiiiiiii na kasi yao nıilele.

 10. DUNDA GALDEN Says:

  Kweli ili kundi zuri sana labda kwangu nilipokuwa uko nyumbani Dec 2007 pale nyumbani watu wote walikuwa kwenye TV nami na kila akionga kuh huyo Joti nilicheka sana pale alipokuwa anamfahamisha kitu Masanja hakuwa elewa haraka na alipoelewa akawa anasema ahhaaaaa au mhhhhhh nanukuu Joti wewe ukiona muafrika analia kama ng:ombe ujue hapo kweli ndio ameelewa,ukweli wengi wetu tukielewa jambo lazima tutasema ahaaaahhhh au mmhhhhhhlakini yeye alikuwa na maaana mmmhhhh
  ni kweli Duracell kwa sasa kila nikiangalia ingawa nina mda mfupi sana na hilo kundi namuona Joti na Masanja ndio pekee cha msingi waziangalie kazi zao za zmani nini walekebishe wapi pa kuludisha mashabiki wao kama ilivyo hapo kama watu walivyo kuwa wanakusanyika kwenye TV zao

 11. Kekue Says:

  Wanajitahidi kwa kweli ni mambo madogo tu yakurekebisha hususan lugha anayotumia joti sometime inakuwa na utata!!!!

 12. rita malewo Says:

  Ni kweli ze comedy mpo juu ingawa kwa sasa mnashuka kwani mnatumia muda mwingi kuongea.plz take all comments as the way to improve your performance.

 13. jamy Says:

  Mi nawapa big up wote, mko juu mazeeeee ila ongezeni kasi mambo cku hizi sio mazuri sana.

 14. binti-mzuri Says:

  hahaha ze comedy nakimaindi sanaa..wafungue website,basi wengine tuwe tunawafatilia straight toka mitandaoni (kwa ambao wako busy na ambao wako nje kinchi)…manake hizi youtube sijui eastafricantube sometimes ku-load dakika 40!

 15. Bablii Says:

  Wahenga walisema (sio wahenga wa joti)

  “Kipya kinyemi, hata kama ni donda utalitia vidole ulinuse..”

  Halafu wakasema tena “Papo kwa papo, kamba hukata jiwe”

  au “Pema pasijapo pema, paki pema si pema tena..”

  Hivyo basi kimantiki jamaa bado wako juu, na hakuna tofauti mwanzo na hivi sasa, lakini kwa sababu pale mwanzo ilikuwa kipya kinyemi… Basi kila mtu alikuwa anaona hawa jamaa wako juu sana na wanachekesha sana.
  Lakini sasa ndo hivyo Papo kwa papo… watu washachoka, hawaonI tena vichekesho vyao. Hii ni tabia ya mwanaadamu, kuchoshwa na kitu.

  Nini Zecomedy?! Mtu mkewe au mumewe, waliioana kwa raha na furaha, na kwa hamu kubwa hufika wakati wakachokana, kila mtu akaona hakuna jipya kwa mwenziwe.
  Lakini mmoja wao akisafiri waka “miss” yana kwa muda, basi wakionana tena, huba huanza upya na kila mtu humuhamu mwenziwe! Hiyo ni hulka ya mwanaadamu hupenda apate likizo au aonje ladha nyengine kila siku.

  Hivyo basi cha muhimu ze comedy wajipe “break” kama miezi 6 au mwaka, then warudi kwa speed ya “light” uone wabongo watakavyo jazana tena kwenye luninga zao…!

 16. ISMA KABENGO Says:

  VIJANA ENDELEENI HIVYO HIVYO MSIONGEZE IDADI YA WAIGIZAJI HIVYO HIVYO MNATOSHA MNACHOTAKIWA NI KUBADILIKA NA WAKATI NA SOKO,NAWATAKIA KILA LA KHERI WA TZ UGANDA WANAWAPENDA SANA

 17. brotherhugo Says:

  mwanzo hawa jamaa walikuwa wakali sana, ilikuwa watu wanajazana kutizama kipindi…never miss hata kama mtu akiwa hajafika home, akikuta sehemu inaonyesha hiki kipindi anatia break na kufuatilia…
  Kipindi hicho manyumbani kwetu palikuwa hapakaliki, atakaye wahi remote ujue hatoachia hadi kipindi kiishe….
  sasa hivi vijana wamepunguza ubunifu, sijui kama wanaweza kutikisa kama walivyo tikisa enzi za mwanoni…
  Wamezidi kuongea sana na kutumia taarifa zilizo tokea katiaka jamii… Sioni kama hii ni comedy yenyewe…. mi ningewashauri hawa mabwana wabadilike kiubunifu.
  Waachane na taarifa zilizokwisha sikiki kwenye tv na radio, badala yake waje kivyao…

 18. Chala Says:

  Mi Naona wameanza kujisahau kidogo, ila wanatakiwa wakaze buti. Wanakuwa wanaongea sana ukizingitakia kipindi chao kutokana na kupendwa na watu wengi kimekuwa pia na matangazo mengi, hivyo kufanya vichekesho viwepo kidogo sasa sijui ni uvivu umewaingia , ama pia nawasiwasi wanalipwa pesa ndogo hawa jamaa wanaingiza pesa nyingi sanaa!! ila nasikia wanalipwa pesa kidogo labda wakikodishwa ndio inakuwa ahueni kidogo sasa pia kutokana na hilo wanaweza wakakosa nguvu ya kufanya kazi nzuri kwenye luninga .. ila bado wapo juu wajitahidi

  Na ushauri wangu wangekuwa ni wasanii wa kujitegemea kwasababu kipaji chao kinawatajirisha wengine kwa kazi nzuri wanayoifanya walitakiwa wawe mbali sana hasa kimaisha na ingesaidia pia kutokushuka kwao kama ilivyo sasa..
  Kwasasa hawa jamaa wapo under EATV lakini nadhani kama wangekuwa peke y ao wakawa wanaomba muda ule wa kurusha kipindi chao kwa makubaliano maalum na wanakuwa na meneja wao maana pesa watakayoipata inakuwa chini yao nakwambia kila mmoja wao angejenga na kuwa na maisha bora. ila ni ushauri wangu tu… naona kipaji chao kinawanufaisha wengine.

 19. Faizer Says:

  Nakubaliana na Babii,jamaa bado wako juu ila sisi watazamaji ndio tumeshawazoea. Ila hilo la kujipa break ya miezi 6 hapana,ni mda mrefu sana. Ukiangalia vipindi vingine vya vichekesho nchini hawachekeshi kama hawa jamaa.
  Ze Comedy juuu juuu zaidiiii.

 20. trii Says:

  kama jana wamerudia vya nyuma,wanao nifurahisha Wakuvywanga,Joti+Masanja,hawa wana fit kila sehemu.

 21. TATU Says:

  zile speed 120 kwenye kona shaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa zinapungua kwa kweli si utani ila mko juu kama kidole cha tatu zamani 2likuwa twacheka hadi basi sasa hivi kucheka mara moja moja si sana ila joti na masanja si mchezooooooooo hongereni sana.

 22. Mkwaya Says:

  Mi naona hawa vijana wanaanza kupoteza ujasiri waliokuwa nao mwanzo, inawezekana wanatishwa au wamekosa ushauri. Comedy kiliibuka na kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe mzuri na mbaya katika jamii, ila sasa naona wanapotea njia na hivi karibuni wamekuwa wakifanya vitu na kutamka maneno ambayo yanaondoa amani hasa pale mnapoangalia watu wa rika na jinsia tofauti.

  Me naona vijana bado wanaweza wanahitaji ushauri na maoni tu. Nafikiri tukitumia vizuri ile email address yao( Comedy @eatv.tv) kuwapa maoni na ushauri wataendelea vizuri sana tuuuu. Mambo ni mengi sana katika jamii yetu yanayohitaji kufikishwa katika jamii kwa malengo ya kujulisha, onya au kuburudisha.

 23. linda Says:

  kusema la ukweli kabisa vijana wameshuka halafu siku hizi wanaigiza vi2 vya kitotoooo,miezi ya nyuma,kitu kikitokea hata kama hujakiona/hujakielewa unasubiri ze comedy utakiona na kuona watu wanasemaje,kama alivyofanya mpoki kwenye issue ya visenti.kwa hiyo tunawaomba warudie hali yao ya zamani.mambo ya ufisadi hatuoni kabisaa.

 24. Mimi kwangu kushuka au kupanda sio ishu sana, mimi nipo katika namna wanavyoigiza. kwa kweli ningeomba watanzania wenzangu munielewe iki nitakachosema. hawa vijana kwa namna wanavyoigiza tutegemee matukio ya kishoga mengi siku zijazo.

  Unajua watoto daima wanaiga kile wanachokiona kwa wakubwa zao sasa hawa vijana kila mara wanaigiza kama wasichana wakijipodoa vya kutosha kupita hata wasichana tena wakitakana na kukumbatiana kama mume na mke. jambo hili ni hatari sana kwa kuwa vijana wetu na hasa wa kiume wanaweza kuzani ni utaratbu wa kawaida tu kwa wanaume kuvaa na kufanya vitendo kama vya wasichana. hii ikatupelekea kuwa na vijana dhaifu na wanaojiusisha na ushoga.

  Sisemi kama maigizo hayo yanafundisha ushoga la. lakini kulingana na makuzi ya watoto na hapa wataalam watanisaidia , upenda kuiga mambo wanayofanya wakubwa kwa kuamini ndio yapo sahihi, kwa hiyo kama tunajaa katika luniga tukiangalia vituko hivyo , basi na watoto uchukulia kuwa ni matendo halali, hivyo watakaposhawishika au kushawishiwa kujiingiza katika matendo hayo huwa wepesi kukubali kwa kigezo kuwa hata wakubwa zao wanafanya hivyo, pasipokujua kuwa yale ya wakati ule yalikuwa ni maigizo tu.

 25. Jennas Says:

  Babii nimekupata.
  Kweli kabisa wajipe break kabla watu hawajawachukia kikweli kweli
  Me nakumbuka kile cha ITV cha kina bi kiroboto enzi za marehemu max kilikuwa juu ila nasikitika kwa sasa hakuna anaekiangalia kumi kwa mmoja.

  Nakumbuka ze comedy ulikuwa ukienda dukani kununua kitu kama kuna tv basi upati mwanya wakupita upate uduma hata ukienda baa wahudumu wako radhi wajifiche chini ya meza wakodolee majicho luningani hadi iishe ila kwa sasa mtaani kimyaaaaaa hata watoto siwaoni wakitembea kama joti.

  Naona wameishiwa kidogo mana hata jana wamefanya marudio ya nyuma
  matangazo nayo kibao
  mazungumzo nayo kibao
  Kuna cku unaweza kuangalia kwanzia mwanzo usicheke kabisa.

 26. Kichwabuta Says:

  Jamaa Wamechoka kinoma,wapunguze mambo yao ya wahenga na misemo fulani inayoelekea kwenda kinyume cha maadili ya mtanzania,itafikia muda haitawezekana kuangalia ze comedy na familia,wanahitaji kushauriwa kwa hili.

 27. zachariah Says:

  unajuwa sisi binadamu huwa tuna asili ya kuchoka na kitu fulani ambacho kila siku huwa unakiona, iwe kwa mume na mke, hata marafiki tu wakaribu… Binadamu sisi tunatabia ya kukinaii ki2, mfano ni pale mwalimu anapokuwa amekufundisha mwka wa kwanza wote na bahati mbaya mwaka wa pili tena huyo huyoo, inafika mahali watu wanamkinaiii yule mwalimu ikiwa ni pamoja na kutungiwa majina ya ajabu ajabu…
  point yangu ni hiii:
  jamaaa wawe wabunifu zaidi ili kuiteka hadhira zaidi, kama ikiwezekana wawe wanabuni mtoko mpya kila siku watokapo!!

 28. Bablii Says:

  Ze Comedy wajitoa EATV

  Catherine Kassally na Mariam Mndeme.
  Kundi la Ze Comedy Alex Chalamila ‘Macklegan’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’, Emmanuel Mgaya ‘Masanja mkandamizaji’ na Sekioni David ‘Seki’ wakisali kabla ya kuanza kuongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.

  Kundi la Vichekesho la Ze Comedy la jijini Dar es Salaam, leo wameeleza azma yao ya kujitenga na Kituo cha EATV walichokuwa wakirushia michezo yao.
  Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari (MAELEZO) Kiongozi wa Kundi hilo Sekion David alithibitisha kujitoa kwa kundi hilo EATV.

  “Baada ya kuufahamisha uongozi nia yetu, nilipatwa na mtihani mgumu sana, maana niliambiwa nichague kuendelea kutangaza au kupumzika na Ze Comedy. Nimechagua kupumzika na kundi hili na sitajutia uamuzi huu hakika, mimi ni msanii msanii wa siku nyingi na nina uzoefu wa muda mrefu. Kama nilivyoweza mwazo kuiinua Ze Comedy, ndivyo nitakavyoweza kuiendeleza zaidi,’’ alisema Seki.

  Naye Kiongozi msaidizi wa kundi hilo la ZeComedy Wakuvwanga aliongeza kuwa kwa binadamu wa kawaida unapofanya kazi kwa muda mrefu inabidi apumzike hiyo ipo hata katika vitabu vya dini.

  “Unajua mtu yoyote akifanya kazi lazima apate muda wa kupumzika hata Mungu alipokuwa akiumba vitu vya dunia hii siku ya saba alipumzika itakuwa sisi watu wa sanaa hii ya vichekesho? Ni maamuzi tu na si vinginevyo,’’ alisema Wakuvwanga’

  (source global puplishers)

  Thanx God, wakuvwanga kanielewa, ndio inabidi wapumzike, kama nilivyotoa ushauri hapo juu!

 29. Bablii Says:

  ni “global publishers” sio “puplisher” kunrazi!!!!!!

 30. Dinah Says:

  Mimi nafikiri wako bomba ila wanapata taabu kwa vile kazi zao kwa wiki zinategemea zaidi matukio ya wiki iliyopita ktk siasa na jamii. Sasa ikitokea kuwa ktk wiki husika hakukuwa na matukio ya kusisimua inamaa na wao hawatokuwa na kitu cha kufanyia kazi.

  Kama walivyogusia wachangiaji wengine wanahitaji kuwa wabunifu zaidi kuliko kutegemea matukio zaidi na hakika kufanya chekesha watu kila wiki ni kazi kubwa sana haijalishi unakipaji kiasi gani lazima uongeze bidii, ubunifu na uchunguzi ambao unaweza ukafanyika hata vijijini au hata nje ya Jiji.

  All the best!

 31. ShaQq Says:

  as the days goes on lazima mzoee na kuona hawana jipya.Hata tom & Jerry ukiangalia za miaka ya kuanzia 1980 zinaboa huwezi kulinganisha na zile za 1940s wakati bado fredy zuimby yuko juu.La kufanya tuwashauri nini cha kufanya badala ya kuwalaumu kuwa wanaongea sana.Wana email address yao ya comedy@eatv.tv nadhani tuitumie hiyo kutoa maoni.

 32. binti-mzuri Says:

  sasa EATV ndio nini kumpa ultimatum seki after all the time they have been together?..mimi nasema goodluck to them!

 33. Dinah Says:

  Uongozi wa EATV wabinafsi kama sio wana wivu, kwani kuna tatizo gani Seki akipumzika na ze Comedy (kufanya nao kazi huo waendako kama Dir/Prod) na wakati huohuo kuendelea kuwa presenter wa kituo alichokuwa nacho tangu kimeanzishwa?

  Kibiashara wamepoteza mtangazaji mzuri, asie na mapozi, mwenye kipaji cha hali ya juu, mbunifu na mtundu ktk kazi zake na mwenye wapenzi/washabiki wengi ambao hakika atahama nao 🙂

  Kila la kheri ktk shughuli zenu Zecomedy.

 34. binti-mzuri Says:

  i second that DInah, roho mbaya tu!..maana sijaona ubaya wowote wa seki kufanya shuguli zote mbili at the same time,tena najua angeweza,kwani ni mchapakazi…basi tu ni mtimanyongo,wa wao kuona ze comedy wamejiengua,basi waka take it out on seki… very very wrong move!

 35. nacky Says:

  mimi naona wanajitahidi ila muda saa moja
  kurusha kipindi ni mrefu Kwao badoooo!!!!!!,wanahitaji
  shule zaidi ya sanaa.

 36. cleopa Says:

  Jamaa wako juu ila waongeze ubunifu ili kumaintain ladha ya kipindi. Kuchekesha watu na matatizo yao lukuki kuanzia kisogoni hadi kwenye unyayo ni shughuli asikwambie mtu.

  Wawe waangalifu pia wasiingie mikataba ka ya buzwagi waka buzwagika wakawaacha na mashimo ya ufukara wakati kipaji chao nguvu na muda vyote mimeshasombwa kwenye makontena ya wajanja,wakaishia kuuza sura.

  Siku zinasonga mbele hazirudi nyuma!

 37. Andrew Says:

  Typical African Comedy.It makes me sick.

 38. martin Says:

  washikaji wanafanya vitu vizuri ila waongeze ubunifu zaidi kwani wanakubarika sana Vilevile matangazo yamezidi mno kiasi kwamba ile ladha inapotea kabisa. muda mwingi wanarusha matangazo kuliko habari na vituko tunavyovitaka watazamaji.

 39. martin Says:

  big up sana kwenu

 40. binti-mzuri Says:

  we andrew kwani mzungu?

 41. joan.t Says:

  kwa kweli nashindwa nisemeje maana ninafurahishwa sana na kipindi hiki, kwanza kabisa wanatoa ukweli wa mambo bila kuogopa mtu.me nawapa big up ya nguvu mazee pull up you socks bado mpo makini msikate tamaa, jaribuni kudadisi na mengine ambayo hamjatoa yako mengi.

 42. robyone Says:

  jamaa nadhani wameishiwa ubunifu,kazi ya kuelimisha jamii kupitia maigizo ni ngumu sana na inahitaji ubunifu wa hali ya juu.wanachotakiwa kufanya ni kwamba wajitahidi kuwa wabunifu zaidi ili wabaki kuwa gumzo la sivyo wataangukia pua na kubaki kama kina ubongo wa flavar.

 43. polisi Says:

  Mi nakizimia sana kikundi cha ze comedy,ila sishangai kwamba watu wameaanza kusema kwamba spidi imepungua.kinachitokea ni kwamba ubunifu ni kawaida yake kupungua baada ya mda mrefu wa kazi nzito.ila kama inawezekana ningewashauri wafungue web site yao rasmi na waweze kusaidiwa kimawazo na kibunifu,kwa kitu ambacho wangeweza kukifanya ama tukio ambalo kwa namna moja ama nyingine halijawafikia wao.Sababu nasema hivyo ni kwamba kuna watu mitaani wenye uwezo wa kubuni kitu na ukacheka hadi mbavu kuuma.so its high time they contribute to the comedy and make it a public laughter.considering audiance age and groups.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s