BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DUNIANI KUNA MAMBO-SIKINDE May, 9, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:12 AM

Mambo vipi?Ni ijumaa tena.Mwaka 2008 unazidi kuyoyoma.Sijui ni mimi tu ambaye naona mwaka unaenda kasi kuliko kawaida au na wewe pia unaona hivyo hivyo.Kuna wakati huwa natamani siku ingekuwa na masaa 38 labda ningeweza kutimiza baadhi ya malengo ambayo hivi sasa yanakuwa magumu kuyatimiza kutokana na ufinyu wa muda. Lakini kama anavyopenda kusema msomaji wetu Edwin Ndaki,tutafika tu!

Kama kawaida yetu,Ijumaa ni siku ya kuvuta pumzi kidogo kwa kupata burudani kutoka enzi zile ambazo wengine wanasema;when music was music.Sijui wanamaanisha nini.Leo tunarudi kwa wakongwe Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde) na wimbo wao Duniani Kuna Mambo. Hivi ni kwanini ulimwenguni kuna binadamu ambao kamwe hawataki kumuona binadamu mwenzao akifanikiwa? Sikiliza ujumbe huu makini.

Wimbo huu ni utunzi wake Suleimani Mwanyiro huku waimbaji wakiwa Bichuka, Muhidini Gurumo,Cosmas Chidumule. Solo gitaa la kwanza chini ya Joseph Mulenga na la pili chini ya udhibiti wa Abel Baltazar. Rhythm guitar lilipigwa na Mwanyiro huku bass guitar likidhibitiwa na Abdallah Gama.

Halafu hilo basi kwenye picha ni Leyland au?BC inakutakia Ijumaa Njema.Kumbuka Ukimwi Bado Hauna Tiba.

Advertisements
 

17 Responses to “DUNIANI KUNA MAMBO-SIKINDE”

 1. trii Says:

  nyimbo zote za zamani hadi sasa bado ukizisikia hazichoshi,sio siku hz wimbo unavuma mwezi 1 tu basi+na mpenzi mapenzi kila mstari.hata video zoa vile vile na kujishika shika sehem ya zipu hapo mbele ya suruali,na kurusha rusha mikono bila mpangilio.

 2. Kwa kweli leo mzee umekuja na kitu cha uhakika. sikinde wakati huo ilikuwa imetimia na ilikuwa atumwi mtoto dukani bwana.
  Sauti ya bichuka na maalim gurumo, thobias chidumule na Hamisi Juma ilikuwa inaweza kumtoa nyoka pangoni. bass gitaa la bwana gama, na masolo list, mulenga, baltazar ilikuwa kama wamezaliwa na magitaa. hongera sana kwa kutukumbusha muziki harisi wa tanzania.
  Mudhui yenyewe ya wimbo yako wazi, fanani anawakilisha kwa hadhira ujumbe uliowazi kabisa, kuwa duniani kuna mambo unapokuwa umkimya wanakufatafata kwa maneno ili wao wakupe sifa mbaya hata ukifanya jambo zuri wao watakukashifu kwa vile wamezoea kusema ee waseme mwisho watachoka. yaani ujumbe ambao daima autachuja na utakuwa na maana siku zote katika maisha yetu.
  Ninaomba vijana wa sasa, wasitoke bure katika nyimbo hizi wajalibu walau kuiga na wajifunze jinsi muziki unavyotakiwa kuwa na mwisho wawe watunzi bora na sio bora kutunga tu.

 3. Edwin Ndaki Says:

  BC nashukuru sana kwa kutambua kuwa ipo siku tutafika tu.

  Leo ni ijumaa hakika hazigandi siku kama alivyochagiza Judith Wambura”JD”.

  Watu kusema,kuchonga,roho za korosho kutopenda kuona wengine nyota zinang’aa ni jambo la kawaida.

  Kikubwa ni kumtanguliza mungu katika mipango yako na kuchukulia kama changamoto chuki zao.

  Hakika kama ulivyosema BC..when music was music..kazi nzuri sana..hao ndio wazee wa NGINDE…ukipenda waite sikinde.

  Ijumaa njema.

  tutafika tu.

 4. Chris Says:

  Nimelikubali hili songi aiseeeee! Mnaosema nasemeni sasa! Mara ze comedy hawako njiani, mara Kinje kasukuma sana watu kutokea kwenye picha na senti hamsini, mara Mnyika alisisitiza kwenye NUKTA tisa… Mwisho wa siku utalala na kila mtu ataendelea kivyake…. Tushirikiane………

 5. Maasai Says:

  Duh sio mchezo manake hilo basi ni Leyland CD wakati huo mambo yalikuwa sio mchezo….. BC, keep up the good work mnatisha manake!!!

 6. Bongo lala Says:

  BC tunashukuru kwa jitihada zenu. Ila nina ombi moja kwenu, tafadhalini jitahidini mtupatie zile nyimbo za zamani ‘original’ na sio zilizokarabatiwa aidha na wale wale walio wahi kuzipiga mwamzoni ama na ‘wajasiamali’ wapya, kwani huwa zinakosa ile radha yake halisi. But, keep it up.

 7. DUNDA GALDEN Says:

  Home sick make my filling happy.kweli nyumban mbali sana na uku ughaibun lakin angalau BC inatupa fikra za kuto sahau nyumbani.baadh ya watu wenye wivu majungu na fitna haweshi kusema nani hata yule pia baada ya kuwa na wivu wa maendeleo wao wanachonga sana nilikuwa nyumbani likizo kwa kuwa nililudi kimya kimya na mambo yangu yalikuwa kimy kimya wengi wakaanza kusema jamaa kachoka sasa tapeli hata nikifanya jambo zuri wao maneno hayaishi
  TUWACHE WASEME MWISHO WATACHOKA SAFI BC KEEP IT UP
  chafosa chai goda ,Darwin Australia

 8. DUNDA GALDEN Says:

  KWELI WHEN MUSIC WAS MUSIC.NOT BAD SOUND MAKE MUSIC BAD HIZI ZA KALE HAZICHOSHI KUSIKILIZA KATU ABADAN
  HUU USIA KWA WALIMWENGU,LAKIN UKIWA FISADI MWIMBI HUU HAUKUTETEI TUTAKWAMBIA MPAKA DAKIKA YA MWISHO IKIBID UTAZOMEWA PIA
  CHAFOSA CHAI GODA

 9. Ramadhani Says:

  Hiiiii!!!!!! Hapa wazee wa BC! nawapigieni saluti!!???
  ukisikia mziki wa dansi wa Tanzania ndio huu,yaani
  miziki wa kiutu uzima! sijui vijana wa kizazi kipya
  watajifunza nini?kutoka kwa wakongwe hawa

 10. Gervas Says:

  Sijui kama hili basi bado lina break, au linatumia break ya kigingi.

 11. Edwin Ndaki Says:

  Gervas mambo vip?

  usiwe na wasi wasi kuhusu “break” za basi ilo cha msingi litafika tu.

  Umesahau lile la kwetu la ukwayani ..isuzu….break ilikuwa mkononi hasa tukienda kupiga “game” New Guinnea” na ile milima au tukienda “Co..war..Key..”..aaaaa

  poa kaka mi nawai mwarufote….

  pamoJAH

 12. […] smooth like honey. If nothing else, pay him a visit so that you can listen to DDC Milimani Park in the title track from the release Sikinde as well as read the great write up that he has on Mbaraka […]

 13. mdau morogoro Says:

  umejichanganya kidoogo rhythm guitar alikuwa abdalla gama , bass guitar suleiman mwanyiro ila picha inakumbusha mengi unaweza kulia kwa furaha

 14. binti-mzuri Says:

  hahah chris pale juu umenichekesha! 😀

 15. Gervas Says:

  Edwin..mambo poa mshikaji. duh umenichekesha saana, afu umenikumbusha mbali. Nilikuwa sikuoni room, au ndo ulikuwa umekula arua? Darasa lako linaendeleaje? uje uwalete bongo hao wanafunzi wako wafanye field study, au vipi?

 16. J Bigy Says:

  Kinachosababisha nyimbo za zamani hazichuji ni kwa sababu kwanza wanamuziki wa kipindi hicho walifanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuimba. Pili waliokuwa wanaimba walikuwa wengi wao ni wale wenye vipaji. Siku hizi yeyote asiye na ajira anaimba. Pia kuna wengine wanatunga wimbo siku moja na kurekodi. Hakuna editing ya maudhui wala ya fani.
  Pia zamani wanamuziki walikuwa hawalewi na sifa-umaarufu wa kibongo-kirahisi.siku hizi akitoa kasingo kaka=hit tu ‘analewa’ sifa na kutukana watu ovyo akiwauliza “hivi unanjua mimi?”.Pia BAADHI yao wanaimba ili wajulikane wapate vibinti na vibwana. Wakishatimiza hilo hawana haja ya kuwa na “adabu” katika fani zao.
  Hata hivyo kutokana na ushindani uliopo kwa sasa naamini wanamuziki wengi watakuwa wakifanya maandalizi ya kutosha.
  POOOOOOOOOOOOA.

 17. kahindi Says:

  trii nakuunga mkono….ni kweli kabisa nyimbo za zamani hazichuji na pia hazichoshi kusikiliza,ddc na mlimani park wana hazina kubwa sana ya nyimbo tamu,zinazofundisha,kukosoa na hata kuburudisha…alafu kinachoniudhi ni interviews wanazofanyiwa hawa wanamuziki wa zamani..kama juzi nilikuwa nawatch tbc 1 ati mzee gurumo anahojiwa na wale watoto wawili lisa na mussa…ckupenda kabisa kkwani yule mzee gurumo wale si size yake kabisa..kwanza muziki wenyewe hawaujui wanamuuliza maswali ya juu juu tu,kifupi ni kwamba yule angestahili kuhojiwa na mtangazaji kama Julius Nyaisanga na au hata chacha madinga..bc nifikishie maoni yangu tafadhali….ni hayo tu kwa leo…


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s