BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HAPPY MOTHER’S DAY TO OUR SWEET MOTHERS. May, 11, 2008

Filed under: African Pride,Familia,Sikukuu,Uncategorized,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 12:03 AM

Katika nchi nyingi za magharibi,leo ni Mother’s Day au kwa maneno mengine Siku ya Mama.Leo ni siku maalumu ya kumkumbuka,kuutambua na kuuthamini rasmi mchango wa mama yako katika maisha yako.Huu ni utamaduni wa kimagharibi ambao unazidi kuenea kwa kasi ulimwenguni kote zikiwemo pia nchi zetu za kiafrika.Sasa hii sio kumaanisha kwamba katika siku zingine usimkumbuke,usiutambue wala usiuheshimu rasmi mchango wa mama yako.La Hasha!Kila siku,kwa walio wengi, ni siku ya mama. Kwetu sisi waafrika ndio kabisaa.Ndio maana kuna ule usemi kwetu wa Nani Kama Mama?

Itumie siku ya leo kumkumbuka mama yako.Kama kwa bahati mbaya alishaiaga dunia,basi chukua muda maalumu kumkumbuka,kumuombea na muhimu zaidi kumuenzi.Kama upo karibu na mama yako,basi mkumbatie na umkumbushe kwamba unampenda na unamtakia kila la kheri katika maisha.

Ni muhimu pia kukumbuka kwamba, kama binadamu,huwa inatokea wakati mwingine tukakosa kuelewana.Ndio.Huwa inaweza kutokea tukakosa kuelewana hata na mama zetu! Kama hali ipo namna hiyo katika maisha yako,itumie siku hii kusameheana na kuweka mambo sawa na mzazi wako.Jinsi moja nzuri ya kuweza kusamehe ni kujiuliza swali;Je kuna ulazima au manufaa yoyote ninayoyapata kutokana na kutokuelewana huku? Usiwe mgumu wa kusamehe ili nawe upate kusamehewa.Sote tunakosea katika maisha.Kama leo basi ni kesho.Usisite kutenda lililo jema leo.

Katika kuisindikiza siku hii,tumekuchagulia wimbo maalumu kutoka kwa mwanamuziki mkongwe wa nchini Nigeria, Prince Nicco Mbagga.Wimbo unaitwa Sweet Mother. Huu ni wimbo maalumu kwa kina mama wote.Kinamama,tunawapenda na tunawathamini.Bila ninyi dunia si dunia.Bonyeza player hapo chini upate burudani,sikiliza ujumbe uliomo ndani ya wimbo.Happy Mother’s Day!

Advertisements
 

25 Responses to “HAPPY MOTHER’S DAY TO OUR SWEET MOTHERS.”

 1. Mswahilina Says:

  Mama mama mama, Mama yangu mzazi;
  Mama nilikaa tumboni kwako miezi tisa;
  Mama ulininyonyesha kwa muda wa miaka miwili;
  Mama ulinilea vyema;
  Mama wewe ndiye chimbuko la elimu yangu;
  Mama Mwenyezi Mungu akulinde na akupe maisha marefu. Amen.

  Mwenyezi Mungu mbariki kila Mama duniani. Amen.

 2. Angeline Says:

  Happy mothers day to my mummy Merina and my elder sisters Esther and Rosie . And happy mothers’day to all mothers out there…… Nani kama mama?

 3. Ladslaus Modestus Says:

  Happy Mothers Day
  To my beloved Mummy Felistas.
  To my sisters: – Theodosia, Secilia, and Beatrice.
  To my beloved wife Agnes.
  Happy mothers’day to all mothers all over the World.

  MUNGU AWABARIKI WA-MAMA WOTE.
  NANI KAMA MAMA ?

 4. tish Says:

  Nakupenda sana mama daima upendo wako hauwezi isha, pumzika kwa amani na upendo siwezi kusahau mema yote ulionifanyia na HAKUNA KAMA WEWE MAMA ohhhhhhhh,,,,, God rest her ina peace

 5. DUNDA GALDEN Says:

  Nakutakia maisha marefu na yenye furaha mama yangu
  niko mbali kimwili mama yangu lakin nafsi niko nawe hakuna atakae weza tena kuniweka miezi tisa tumboni isipokuwa wewe ndie uliweza hilo nitapenda wote lakini wewe kila siku utakuwa namba moja kumbuka katu siwezi kukulipa mangapi ulio weza kwangu bali hili kubwa dua na upendo ni kwako na mzazi mwenzio yaaani father
  allah barik kipenzi cha roho yangu mama
  Chafosa chai goda

 6. Vanessa Says:

  Kaka yangu kama machozi yangeweza kuingia humu, blog yako ningeilowesha.
  ASANTE, ASANTE SAAAANA!!!!!
  Hakuna kama MAMA!!!
  SI WALO HII DUNIA AMA YA MWENYEZI MUNGU!!!
  GOD BLESS THEM!!!

 7. Mama wa Kichagga Says:

  Namshukuru sana MUNGU kwa ajili ya MAMA yangu na kwa ajili ya wamama wote duniani (nikiwemo mimi).

  “NANI KAMA MAMA? HAKUNA KAMA MAMA”

  http://en.wikipedia.org/wiki/Mother

 8. Chala Says:

  Hakuna kama mama “”” Nampenda sana mama yangu ni mtu wa muhimu sana katika maisha yangu””” nawapenda pia akina mama wote wa Afrika na duniani kote mungu awepe baraka zaidi na kuwasamehe dhambi zao kwa kuwa kazi waliyonayo duniani ni kubwa.

 9. sally Says:

  Happy mothers day

  Nakupenda na nakutakia maisha marefu na yenye baraka Mama yangu Agness Coin Hinjo! Japo najua umemmisi mzazi mwenzio ambaye katutangualia lakini jipe moyo mama sote njia yetu ni moja.

  Nawatakia wamama wote duniani kheri na baraka na maisha marefu yenye amani

 10. binti-mzuri Says:

  HAKUNA KAMA MAMA!!!!!!!!

 11. Gervas Says:

  Mmmmmm!!!! Hivi hao wakina mama hizi salaam wanazipata? je ni kweli wengi wa mama zetu wanaielewa hii mazas dei? ni kautamaduni ka wazungu ila ni kazuri kukaiga ila sijui km walengwa wana habari km kuna siku km hii.

 12. Gervas Says:

  Naona kama tunampigia mbuzi gitaa vile!!

 13. J Bigy Says:

  Hivi sisi sikuku zote tunadesa toka magharibi?Mara Valentine, mara mother’s day?Mara…..kiiiiilakitu tunacopy tu!Hivi hatuna zetu?
  DU!

 14. iai Says:

  Kama ni kitu kibaya na unaiga utaonekana we chizi lakini kama ni kitu cha upendo is notbad kumwambia mama yako unampenda. Ni kweli wamama wengine hawajui lakini wengine wanalijua hilo ndugu yangu. Na kwawale wasio jua si mbaya ukamwambia mama yako leo ni siku ya mama duniani na ukampa zawadi yako au maneno yako yoyote mazuri na yenye upendo. Kama alivyo andika BC kwa wale wenye ugonvi na wazazi wao ni vizuri siku kama hiyo kumaliza kila kitu.
  okay nawatakia kila la kheli wamama wote duniani

 15. sweetoh Says:

  MAMA NI MAMA JAPO RIKWAMA,
  MAMA NI MAMA MPAKA KIAMA.

 16. binti-mzuri Says:

  nyie huko juu vipi,embu shukuruni mama zenu…kama tamaduni za kizungu ndio ishu,mbona mnavaa nguo,si kaleta mkoloni..enzi zenu nyie mikeka tu…kama ni hivyo,basi na turudi enzi zile

 17. Gervas Says:

  Binti-Mzuri, wazungu ni utamaduni wao na wala sisi hatusemi kumshukuru mama ni vibaya, swali je ataipokeaje hiyo ukiishia kumwambia Happy mothers day maza wa kiswazi atakuona mzushi tu. Kwa mila zetu unapotoa hiyo shukurani lazima iendane na kitu flani..namaanisha zawadi, Mkwanja, kipande cha Kitenge n.k, wanaouelewa huu uzungu wa mazas dei ni wachache. Nani kakudanganya kuvaa kumeletwa na mkoloni? Kwanza hii ni gender issue, lazima kuwe na Fathers day. sitaki kuanzisha mjadala.

 18. binti-mzuri Says:

  we ishu za gender,kapeleke united nations,mwanaume kabeba mimba for 9 months??DO YOU KNOW WHAT ITS LIKE,TO HAVE AN EMBRYO IN YOUR STOMACH FOR 9 MONTHS..ofcourse hujui,kwasababu hujawahi ku-experience.. a mother is linked to a baby,na they are only separated akimzaa,na kitovu kikikatwa,but apart from that,they were one.. a father has a position katika maisha ya mtoto,but am sorry to say this,u cannot compare,i repeat you cannot compare to amothers connection na mtoto..ujumbe wako huu GERVAS…na kuvaa kumeletwa na mkoloni,cotton shirt ulilovaa saivi,lililetwa na mkoloni,japo saivi sie nd tunafuma..enzi zetu ni migomba tu ilikua inatusitiri..kataa

 19. Gervas Says:

  Haya bwana Binti umeshinda, maana tukianza kujibizana hapa tutakesha ila msg yangu delivered

 20. J Bigy Says:

  Hatuwezi ku-predict tungekuwa tunavaa nini kwa sasa kama mkoloni asingekuja. Nani ajuaye labda tungekuwa na nguo zetu pia.Ni suala la muda(kama hakuna rushwa).Hata wazungu enzi za zamani walisafiri kupita kwenye masnow kwa mbwa waliofungwa kamba pamoja wakivuta vitu na watu. Kwa sasa wana tekinolojia ya ajabu na ya juu.
  Lugha, tofauti na mavazi, ina nguvu sana. Unapopanua mdomo kumwambia mamaako happy mother’s day sidhani kama mama wa kawaida anaelewa labda wale wamama waliowaambia mama zao ‘happy mothe’s day’ pia.sisi pia tuna njia zetu kuonesha tunawapenda mama zetu si lazima hii ya kuletewa.
  Tutizo letu hatuigi vya msingi tunaiga ‘elementary’.Mbona hatuigi kutokula rushwa, kufanya kazi kwa bidii, kutokuwa wasanii(waongo), kutokutetemekewa na wananchi tukiwa viongozi ama tukisoma kidogo n.k?Tuige na hivyo basi sio kuvaa,happy mother’s day, n.k.

 21. binti-mzuri Says:

  SASA KWANINI MNASHEREHEKEA BIRTHDAY,KAMA HAMTAKI KUIGA!!!?!!?!?..anyway kama walivyosema watu wengine, tukianza mabishano hayaishi leo..my message has been delivered!

 22. J Bigy Says:

  Birthday unasherehekea wewe, sio mimi.Point sio tuorodheshe sherehe zote kama birthday n.k, suala ni kutokimbilia vitu ambavyo hata mtoto anaweza kuiga na havina msingi. Iga issue complex za kuokoa taifa kama nilizoainisha hapo. Uongozi bora, teknolojia, kupunguza usanii, majungu, kupunguza imani za kishirikina n.k.Mimi pia natakiwa nijifunze toka kwao hivi vitu vya msingi.Ila hizo birthday na valentine fanyeni kwani ni so ‘elementary’.Ndo ule ule msemo wa “mimi maskini yaani hata kuvaa nishindwe?” hope mine has been clearly derived too.

 23. joan.t Says:

  mama ni nguzo katika maisha nampenda mama kuliko kitu chochote duniani,sitamani hata kuolewa ili nisimwache mama,
  wewe ndio kimbilio langu hapa duniani.nakupenda sana mama.
  ubarikiwe na bwana

 24. binti-mzuri Says:

  j bigy,it hasnt been delivered!! umesema : ‘suala ni kutokimbilia vitu ambavyo hata mtoto anaweza kuiga na havina msingi’ … wewe unaona mtoto kuiga kumshukuru mama yake katika siku maalumu,japo tunamshukuru Mungu kila siku kwa ajili ya mama, na maybe kumnunulia kadi au hata maua,ni kitu sio cha msingi!?…. this is ufisadi!!!!!!!!!

 25. Mdau Muungwana Says:

  Vizuri na safi sana. Hata hivyo nafikiri mwanamuziki huyu hatoki Nigeria kama inavyosomeka katika utambulisho. Kumbukumbu zinaonyesha anatoka Sierra Leone. Na hata lugha iliyotawala wimbo ni Kreole kutoka Freetown. Hebu jaribuni kuangalia vizuri.
  Big up kwa kazi zenu.
  Mdau Muungwana.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s