BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NI BINAMU13.COM May, 12, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Mtandao — bongocelebrity @ 12:06 AM

Kwa wengi siku hizi anajulikana kama Binamu.Lakini alipoingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki aliitwa MwanaFalsafa.Jina lake kamili ni Hamisi Mwinjuma(pichani).Ni mshindi wa tuzo maarufu za Kili.

Tangu aingie kwenye fani ya muziki,sifa moja ambayo amekuwa nayo ni kuwa na mashairi au lyrics kali. Ilikuwa ni lazima uwe na uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili ili upate maana halisi ya nyimbo zake.Uwezo wake wa kwenda sambamba na mapigo (beats) za kimuziki huku akighani ipasavyo mashairi yake ni jambo linguine lililomfanya awe mmoja miongoni mwa wanamuziki wa B Flava wenye mashabiki lukuki..

Hivi karibuni MwanaFA amezindua tovuti yake rasmi.BC tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ujio wa tovuti hiyo,muziki wake,mipango yake ya baadaye na mengineyo mengi.Kwanini ameiita tovuti yake binamu13.com? Ana mipango gani katika miaka mitano ijayo? Anasemaje kuhusu ujio wa mwanamuziki 50 Cent nchini Tanzania hivi karibuni?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Kwanza hongera sana kwa kuzindua tovuti yako rasmi hivi karibuni. Pia pongezi nyingi kwa mafanikio ambayo umeyapata tangu uanze kazi za muziki.Mambo yanakwendaje?

MwanaFA:Thanx a lot cuz…Mungu anasaidia sana juhudi zangu zinatoa mwanga wa mafanikio!Nazingatia sana nguvu zake kwenye kila ninachofanya.Najua kila kitu kilishapangwa naye hata kabla sijazaliwa na ninachofanya ni kufumbua mafumbo aliyoniwekea kupata niliyopangiwa kuyapata humu kunako dunia yake.

Mambo kama kawa ndugu yangu…

Labda kabla hatujaenda mbele sana naomba nimpe pongezi na shukrani zangu za dhati my boy Ahmed Babajide kwa kuweza kufanikisha kuwepo kwa tovuti hii.Mungu ataifanya kazi yako yenye thamani siku za karibuni Ahmed.Thanx a lot.

BC: Jambo la kwanza ambalo tumeliona pindi tulipopata habari kuhusu ujio wa tovuti yako rasmi ni kwamba tovuti yako umeiita binamu13.com.Wengi tunafahamu kuhusu jina Binamu lakini hatujui kuhusu namba 13.Unaweza kutuambia namba 13 inamaanisha nini?

MwanaFA: 13 is my birthdate..March 13th!I am a Pieces,like Osama,MethodMan and many others…hahahaha..and I’ve been using the name binamu 13 sehemu kadhaa kwa muda sasa!sikiliza tena intro ya ‘hawajui’ utanifahamu…

BC: Mara nyingi mtu anapoamua kuanzisha tovuti yake anakuwa na malengo fulani maalumu.Kwa msanii kama wewe lengo mojawapo la wazi ni kutumia tovuti yako kujitangaza na kuwasiliana kirahisi na mashabiki wako wenye uwezo wa kutembelea mtandao.Mbali na lengo kama hilo,unategemea kupata nini zaidi kutokana na kuwa na tovuti yako mwenyewe/rasmi?

MwanaFA: Sababu za wazi kabisa baada ya hizo ulizoziorodhesha awali ni kujaribu kuitumia kutafuta njia za kufanya biashara ipanuke.Kwa ulimwengu tulionao watu wengi zaidi wanaweza kukufikia kupitia mitandao kuliko sehemu nyingi nyingine,hasa walio mbali sana na Africa nilipo.Nikijaribu kuwa realistic,hakuna namna msanii wa uzito wangu ataeleweka bila ya kuwa na tovuti.Muda wa mimi kuwa na tovuti yangu rasmi ulishafika.

BC: Kwa kiasi kikubwa tovuti yako imeandikwa katika lugha ya kiingereza kitu ambacho kwa kiasi fulani kinamnyima mshabiki wako asiyefahamu kiingereza nafasi ya kuitembelea na kuifurahia kama sio kusoma yaliyomo.Unaweza kutuambia kidogo kwanini sehemu kubwa umeiweka katika kiingereza?

MwanaFA: Aaamh…kama nilivyosema katika swali lililopita,nalazimika kuwa karibu wa wapenzi wa kazi zangu,HASA WALIO MBALI NA NILIPO.Wengi wanaofahamu Kiswahili tu na sio kiingereza kilichotumika sana kwenye tovuti yangu wapo nilipo…Africa,na hasa Tanzania ambako wana namna nyingine lukuki za kupata habari za maendeleo ya kazi yangu kirahisi.Simaanishi hawatakuwa na nafasi ya kujua kupitia tovuti,no..kadri tunavyoendelea tutakuwa tukijaribu kumfanya kila mmoja ajisikie nyumbani kuipitia…kila mmoja ni binamu yangu!

Binamu a.k.a MwanaFA akiwapa ladha murua mashabiki wake,mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hivi karibuni.

BC: Mashairi au lyrics za nyimbo zako, matumizi ya lugha ya Kiswahili ni mambo ambayo yanavutia sana wapenzi wa muziki kiasi kwamba wengine wamewahi kutania kwamba huenda kila unapokwenda huwa huiachi nyuma kamusi ya Kiswahili.Kuna ukweli wowote katika hilo? Je unadhani lugha ya Kiswahili ina nafasi gani kimataifa kupitia muziki?

MwanaFA: Hahahahahaa…sina hata kamusi yenyewe mpwa!Nalichukulia hilo kama compliment anyway!..ukijaribu kuangalia kazi zangu za karibuni nimejaribu sana kurahisisha Kiswahili ninachokitumia ili kuondoa matatizo ya watu kutafuta kamusi ili waelewe nimesema nini…muziki tunaofanya yafaa uwe wa kumpumzisha mtu na sio kumuongezea mzigo wa mawazo..najua unanielewa kama uliwahi kuwa Africa.

Nafasi ya lugha ya Kiswahili sio kubwa kwenye muziki wa kimataifa kwa kweli.Lakini muziki pia unaweza kutumika kukitangaza Kiswahili chenyewe kama utafanywa katika viwango vya kimataifa.Bado tunajaribu kuutoa huu muziki na Kiswahili kwa wakati mmoja.Hakuna namna tutashindana na kina Jay Z kufanya muziki mzuri kwa lugha yao.,so we better stick to ours!

MwanaFA(kulia) akiwa na mshirika wako wa karibu,nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya au AY.Kwa pamoja hivi karibuni walitoka na kitu,Habari Ndiyo Hiyo.

BC: Tanzania hivi karibuni imekuwa ikipata bahati ya kutembelewa na wanamuziki mashuhuri kutoka nje na hususani Marekani. Hivi karibuni mwanamuziki 50 Cent na kundi lake la G-Unit walikuwepo nchini Tanzania na wewe ulikuwa mmojawapo miongoni mwa wahudhuriaji.Unadhani ziara kama zile zinawasaidia ninyi wanamuziki wa kizazi kipya kwa namna yoyote ile?Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuna mambo yoyote ya msingi ambayo mnajifunza kutoka kwao?

MwanaFA: Yeah,kiaina..Japo kitu haswa tunachoweza faidika nacho toka kwao ni kupata exposure.Nadhani waandaaji wa hayo matamasha wangekuwa wanajaribu kufanya utaratibu wa kutuunganisha nao kufanya kazi za pamoja.Naamini tutatangazika mno kwa mtindo huo!Imagine ujio wa Akon mathalan,angeweza fanya wimbo japo mmoja na msanii wa ‘bongo’,ingekuwa ni hatua ndefu ajabu…sawa 50 is expensive and all,hatuwezi mshawishi hata atupe Lloyd Banks ama Yayo afanye a single verse kwenye wimbo mmoja wa kibongo kweli?lol!Yafaa tuwashawishi watusaidie kujaribu kuuvusha muziki wetu.

BC: Ukitizama mbele kiasi,tuseme kama miaka kumi ijayo hivi,unadhani muziki wa kizazi kipya utakuwa wapi? Na wewe mwenyewe nini malengo yako katika miaka hiyo kumi ijayo?

MwanaFA: Well,sina uwezo wa kuona sana mbali hivyo,ila kama kila kitu kitakuwa kwenye reli za juhudi zetu pengine tutakuwa kwenye nafasi ambayo raggatone ipo sasa…tuombe na kuwajibika!

Binafsi najaribu kujijenga vizuri nisishindwe japo kukumbukwa baada ya kuachana na muziki na pia nisitetereshwe na maisha pindi ujana utakapokwisha.Nafahamu sitaweza kufanya ninachokifanya milele hivyo najiandaa.I realy do,na namuomba Mungu sana anisaidie niweze fikia ama kuvuka malengo.

BC: Mwisho ungependa kuwaambia nini mashabiki wako,mashabiki wa muziki wa kizazi kipya?

MwanaFA: They should keep faith in me and I’ll never let them down.

Tembelea tovuti ya MwanaFA kwa kubonyeza hapa.

 

31 Responses to “NI BINAMU13.COM”

  1. Ed Says:

    Real hard worker young man. Kabla ya kujulikana kwenye dunia ya hip hop kijana alikuwa matata sana, lakini badaa ya kujulikana kwenye ramani ya bongo flava, things has change. MwanFa displine yako ipo juu
    Big up
    Kutoka kwa black skin fan#1

  2. binti-mzuri Says:

    NAMPENDA SANA HUYU KAKA.. AMESIMAMA KIMISTARI…KILA LA KHERI

  3. Bablii Says:

    Unapotaja wasanii bora, sio bora wasanii wa muziki wa kizazi kipya bila kuweka jina la Mwana Fa utakuwa “unakufuru”.
    Ni msanii anaejuwa muzuki unakuwaje, sio kupiga kelele tu!

    Ana vitu vyote muhimu katika muziki; Anatunga mashairi yenye maana, yenye vina, lugha fasaha ya kiswahili na vionjo vyake, anajuwa kutofautisha L na R kimatamshi, anajuwa kupangilia beti za wimbo wake, ana style mzuri ya kufikisha ujumbe wake, anasauti ya kisanii, anajuwa “kufloo” na mistari, ana “personality “mzuri.

    Zaidi ya yote anauwezo wa kutunga na kuimba nyimbo za aina zote kama vile mapenzi, maadili n.k

    La mwisho na muhimu kwa msanii, huyu jamaa ni “very
    cooperative”

    Wanamuziki wengine wachache waliopo kwenye hadhi yake ni Pof J na na FidQ ( Ila huyu hana personalty)

  4. binti-mzuri Says:

    BABLII I AGREE TOTALLY!!!..MANENO YA WAZI TENA YENYE BUSARA..MMH..WANIPA SHAUKU,NA WEWE NI MWANA-UNDERGROUND MUSICIAN NINI!?..ILA HUYO FID Q NI MTU WA BIFU SANA AISEE,JAPO NAE ANAJUA KURAP,ILA NI MTU WA KUTAKA KUCOMPARE SANA NA MTU WA COMPETITION MFANO MZURI NI NYIMBO ZAKE MWENYEWE AMBAZO ALIMSEMA SOGGY DOGGY NA MFALME SELE

  5. J Bigy Says:

    Hata mimi namfagilia sana Binamu. Na naungana na Bablii kuwa wanamuziku wengine kama mwanaFA ni Prof J n.k.Nyimbo zao hazichuji kirahisi.

  6. zaina seif Says:

    Binam kazi nzuri zaidi ya sana mchumba nakukata dau ile mbaya.

  7. TATU Says:

    NASIKIA HARUFU YA ANKALA

    HIVI NASIKIA ETI HELO NENO LA HABARI NDIO HIYO LILIKUWA LA Q CHILLAH KWA HIYO HAWA WAMEEGEZA ALILI2MIA KWENYE WIMBO WA WANAUME GANI SIJUI ALISHILIKISHWA KABLA YA WIMBO WA DAR MBAKA MORO MWISHO WA WIMBO HUO QCHILLAH ANAMALIZIA NA KUSEMA HABARI NDIO HIYO

    ILA BINAMU NA MWENZIO AY MKO JUU SANA NA WIMBO WENU HUO HABARI NDIO HIYO.

    MICHANO HIYO MWANANGU.

  8. jamilah Says:

    you rock meeeen, kweli we unaendana na jina lako mwanafalsafa kwa sababu unaitumia lugha(kiswahili)vilivyo, bi up and keep doing!!!!!!!!!

  9. Kaka Poli Says:

    “Lakini Alikufa kwa Ngoma”

    Of all the best Kiswahili hip hop songs, the above titled one will always remain #1 on my best list.

    Personally, I have known MwanaFA back in all good days when I was busy and serious with Dolph Mobb, a HipHop Crew. Cuz had alot of dreams wit muzic and he was good in putting the rhymes on top of our headz.

    To date, he still got that click and remains to be my #1 MC with lyrics, flow, personality, name it all!!

    U r the man Cuz!!

  10. binti-mzuri Says:

    kwani nani anamuandikia lyrics mwanafalsafa?ni swali..cause i have heard otherwise

  11. Mike Says:

    Binamu upo juu sana, hongera mzee! Ushauri wa bure: Tovuti yako ni nzuri lakini naomba ujitahidi kuweka “UPDATES” kila mara, kwani vi-tovuti vingi vya kibongo vinaboa, mambo ni yale yale tu kila siku yaani, “leo ni kama jana”
    MCeez wa Bongo wengi mnafanya kazi nzuri lakini bado kilio changu ni kwa Ma-prodyuza, beat hafifu sana, muziki hauchezeki!

  12. Didi Says:

    Binamu upo juu sana hongera mzeya,All the best kiswahili hip hop songs.

  13. nipala m Says:

    B upo juu ile mbaya mtu mzima thanks kwa kutupa raha mafansi wako ohooooooooo mzukaaaaaaaaaaaaaa h ndio hiyo.

  14. mankya nkya Says:

    habari ndo iyoooooooooooooooooooooooooooooooooo big up ma brozzzzzzzzzzzzzz

  15. violet Says:

    your real gud men,keep it up binam……Habari ndiyo hiyo

  16. violet Says:

    no comment

  17. Ceaser Says:

    Mwanangu B nimekusoma vizuri tangu ingekuwa vipi,aina noma mtu wangu,kaza kamba kwani wasanii wanaotaka kukushusha wapo wengi.
    Niga hiyo imetulia,hasa ktk lile la nangoja ageuke.Yaani kwa jinsi mistari ilivyo mitamu,anaweza ageuke alafu wazungu hawaaaaaaaa.
    Mzukaaaaaaa

  18. Annie Says:

    Hey MwanaFA. Congrats Cousin. You are doing a great job. I always like your tracks. I really like your style. It really shows that you think twice before realising your work. Keep it up.
    Have given a listen to bado nipo nipo kwanza. Waoh! it is really a touching number. It is really nice and I think it teaches a lot.
    Congrats once again. Keep on keeping up binamu.

  19. kagambo Says:

    ebanaee, nakupa big up sana mtu wangu,nafagilia kazi zako zote mkubwa,kuhusu kuibuka kwenye video mi nahisi bado nipo nipo,sababu sija pata mwaliko toka kwako binafsi,lakini video zingine tuambiane bana au sio

  20. Binya F Says:

    Bado niponipo mwana,
    ni balaa mzeya unatisha inajulikana kuwa we kwa mabinti (wanadafada) usahauliwe lakini sio kuoa. we ni mkali kiujumla kula zangu kwako zipo nyingi sana.

  21. zara Says:

    hongeara sana binamu,we luv yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
    aah unanitega

  22. Oyamjomba big up sana nakuku bali alafu tume fanana kama ndugu kaza buti mjobma

  23. juliuswillison Says:

    Ebwana ukoo juuile kinyama nimimi pacha wako mbona amji kulakiti moto hapa legho Ebwana kazeni Buti unakiswahili ambacho akiso meki

  24. MiMi Says:

    Mwaaaaaaaah FA

  25. Mary Mkwaya Malamo Says:

    mmh!

  26. tanysa Says:

    big up ila punguza pozzzzzzzzzz!!!!!!!!

  27. watubwana Says:

    watu bwana,katika wasanii wa bongo wanao jua umuhimu wa elimu wewe ni mmoja wapo,nashukuru sana kaka kwa kwenda shule itakusaidia sana cz muziki wa bongo unahitaji zaidi ya kipaji,unahitaji elimu na unahitaji mtu uwe unaangalia mbali na sio hapo ulipo.hongera kwa kazi zako nzuri.kua smati siku zote,usijione wewe ndo wewe,jiheshimu,kua msikilizaji kuliko muongeaji,mkumbuke MUUMBA wako siku zote na usikome kumsifu kwa anayokujaalia.thanx bro

  28. Susan Says:

    Binamu, u been the mastermind in Game since way bak. . .yo stil doin it tight man! Salute u Godfather, the Don himself!
    Kip it rockin!

  29. changa Says:

    mzee wa falsafa nimekukubali sanaaaaaaa

  30. e bwanaaee siunacheki mipasuo ndo nyimbo nilioikubali ile mbaya kaza msuli kaka achana na wazushi kaka

  31. oya mwana fa,mi nakukubali sana na nayafahamu mambo ya mziki kiasi fulani.usimjibu inspectar haroun,kwa ngoma yake bado upo upo,atajikukuta fala.anatafuta fame kwa kutumia beef.let him be creative.


Leave a reply to watubwana Cancel reply