BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BALALI AAGA DUNIA May, 21, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News — bongocelebrity @ 10:15 AM

Habari ambazo mpaka sasa bado inakuwa ngumu kidogo kuzithibitisha kutokana na usiri au ukimya kutoka pande husika,zinapasha kwamba aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania,Daudi Balali, amefariki dunia huko Boston,Massachusetts nchini Marekani na kwamba anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa huko huko Boston.

Tunaendelea kuzisaka kwa undani habari hizi ila kwa sasa unaweza kubonyeza hapa ili kuendelea kuipata habari hii.

Advertisements
 

41 Responses to “BALALI AAGA DUNIA”

 1. binti-mzuri Says:

  WANASEMAGA KWAMBA MADHAMBI HULIPIWA DUNIANIIII

  POLENI KWA WAFIWA

  BALALI I HOPE YOU CONFESSED UR SINS

 2. Kamanzi Says:

  Kwanini nasikia harufu ya mtu kukolimbwa? Balali ulikuwa unataka kulipua bomu nini? Sasa watanzania tutakosa kuujua ukweli wa mambo kuhusu wezi wetu wa EPA. Jamani anayejua haya mambo atupasie basi hizi habari.

  Kwa ndugu wa Balali poleni sana kwa msiba mzito. Tunachochukia ni ufisadi sio mtu na Balali nae alikuwa mtu kama wengine.

  Mlioko hai akina kama Chenge kazi kwenu maana ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji.

  Kama kawaida yangu namalizia kwa kusema Mungu ibariki Tanzania, Mungu Walaani Mafisadi.

 3. maryciana Says:

  acheni uroho mbaya jamani… huyu Mzee Rajabu Balali i can confem amefariki dunia siku walau mbili zilizopita: habari zimetoka kwa isiders wa BOT(BANK OF TANZANIAN), na amefariki Boston na atazikwa Boston kesho.

  inallilaaah raujun!

 4. leila shakum Says:

  jambo silielewi,ni kwanini hakuweka bayana mfumo mzima kabla ya kifo chake?wanaosema kwamba ‘i hope he confessed his sins’ wewe madhambi yako umeshayatubu?ashakum

  huyu baba hakuwa mwizi,ila bodi yake ndio iliojaa wezi nasikia ameacha list ya everyperson involved kwa ndugu yake,na itabainishwa soon.. I CANNOT WAIT to clear my uncle’s name

  R.I.P DOCTOR DAUDI BALALI MKENGA

 5. miss sinza Says:

  aise hili ndilo jiji la kandoro..mtu kafariki,watu wanasherehekea kudadadadeki!!!

 6. mkereketwa Says:

  Jamani, mlio waislamu tunaamini kila binaadamu atafikwa na mauti na mwenzetu katangulia. Kwa misingi ya imani yetu sisi waislam tuanaamini sasa hivi yuko mbele ya haki! Hivyo kilichobaki ni sisi kumwombea kwa mwenyezi mungu ampe tahfif na kumsamehe madhambi yake na kumwomba atuelekeze sisi tuliobaki kufuatat njia yake aliyotuongozea. Na si kuyasema mabaya yake an kumuhukumu hapa duniani, ndiyo maana katika uislamu hata kama jirani yako unajua anavitendo viovu basi mauti yakimshika waislam wote hukusanyika na kumwombea ikiwa yeye ni muislam despite of whatever judgement watu watakazompitishia. Family ya balali hapa washington na Tanzania nawapa pole sana, suala la msiba ni gumu na Mwenyezi mungu awape uvumilivu muweze kumsitiri ndugu yetu, mtanzania mwenzetu. I hope hii haitakuwa mwanzo wa kashfa na kupambana bali kuwafariji wafiwa, tusisahau mila na desturi zetu jambo la msiba si la furaha unless wanaofurahia hawajawahi fiwa na kama hujawahi fiwa shukuru mungu maana hujui machungu yake. Poleni sana

 7. usinijue Says:

  Changa la macho hilo wabongo kinachofanya asizikwe kwao ni nini, maiti imeharibika haiwezi kusafirishwa,ama his last wish asizikwe bongo, kama watu wengine wanasafirishwa tena kwa michango itakuwa yeye vijisent wa pili ……but if its true then inalilah waina irahirajuhun..

 8. Mama wa Kichagga Says:

  Natamani ningekuwa RAIS LEO HII KWA MIEZI 6 TUU!

  Ningewaondosha nchini mafisadi wote wakatumikie adhabu ugenini na waishie huko huko halafu nijenge taifa lisilo la ufisadi.

  Nimuinue Baba , mama na watoto mayatima wanaoangamia kila kukicha shauri ya ufisadi! Hivi roho zetu ni za mawe au chuma kiasi cha kutokuyaona matatizo ya mlala hoi?

  Eee Mungu wape viongozi wetu pamoja na hawa mafisadi moyo wa nyama ili waweze kuona na kutatua mfumo huu wa matatizo TZ kwani kwa utendaji wao na mwelekeo wao watakuja kutufikisha pabaya zaidi muda sio mwingi!

 9. Chris Says:

  I don’t wanna believe if he has really died! Sthg may be going on. Na kama amekufa kuna mkono wa mtu hapo!

  Miezi sita inaelekea ukingoni! Usicheze na fisadi! Kuna muda tulisikia ameongea na watu na kutoa dukuduku lake that if lolote likitokea (LIMETOKEA SASA) kila kitu kianikwe. Tunataka kianikwe sasa kwa mhusika alieambiwa!

  Usicheze na mafisadi aiseeeee! Hiyo chain ni ndefu sana! Sidhani kama hawa watu wana Mungu wanaemuamini!

  Tunasubiri na tamko la serikali baada ya report ya miezi sita ambayo ninaamini atakua kwenye mkumbo japo marehemu! Wasijeachia mali za wadanganyika kisa amekufa!

 10. binti-mzuri Says:

  we leila shakum nitolee shombo mie, nenda kamsalie ur ‘uncle’ sio unacontradict watu hapa..mlikua wapi akiandamwa na kashfa,mlikua wapi alivyofukuzwa kazi,leo kafariki ndio mnajifanya mnataka haki!

 11. DUNDA GALDEN Says:

  INNALILLAH WAINA RRAJUUN
  HAKIKA KIFO KINATOSHA KUWA MAWAIDHA
  MBALI NA YOTE MWENYEZI MUNGU AMSAMEHE
  MAKOSA YAKE SISI BINADAM I WAKOSAJI MBELE YA SUBHANNA

 12. Dinah Says:

  Mapesa yetu ndio hatuyapati tena? Isije akawa kabadili ID na kilichofanyika ni kuiua ile ID ya awali ya kifisadi!

 13. bonny Says:

  Jamani huyu hajafa yuko hai amejificha mahali kusudi ale pesa yake bila matatizo

 14. Gervas Says:

  Yoote kwangu ni sawa tu awe amekufa au hajafa, au wamemficha, kila kitu kina mwisho wake. Binadamu utafanya ubabe, ujuzi, utatumia mamlaka hata uchawi ulionao….lakini at the last you will be judged hapa hapa duniani. Kwa hiyo naomba watu wawe watulivu tu. Hata kama wamemficha ataishi maisha gani ya kujificha na niwapi ambapo wabongo hwafiki hapa duniani?

 15. liko Says:

  Dear my fellow Tanzanians, we have just learnt that Balali is no more. Let us treat him with honesty and respect, at this moment he doesnt have room to defend himself as God has made his decision that will come for everyone of us. I do believe whether he was involved in frauds or not, he has left clear message on this issue or not but being a believer by the name of God justice will be served. GOD BLESS THE SOUL OF DR BALALI AND GIVE HIM FORGIVENESS FOR ALL NORMAL HUMAN WRONG DOING. AMEEN

 16. MSEAMA Says:

  huyu hajafa kwa mapenzi ya MUNGU huyu ameuliwa kama walivyouliwa wakina KOLIMBA, SOKOINE NA wengineo, lkn ndio hivyo hatuna la kufanya mpini mmeshiika nyinyi serikali ila kumbukeni dunia ni njia na ipo siku tutafika huko ambao mungu ametupangia, Serikali hii ya mafisadi ikiongozwa na fisadi na msanii mkubwa J.. kundi la mawaziri mafisadi chini ya mwenyekiti wa mafisadi tanzania MKA.. wameamua wamuue baada ya kusikia BALALI anataka kuongea ukweli wa mambo ulivyo, baada ya kuvumilia kwa muda mrefu kubeba zigo la madhambi peke yake. ndio maana hawakumkamata siku zote kumbe walikuwa na mpango wa kumuua. Waziri mkuu fisadi mchanga alikiri mwenyewe kuwa mafisadi walioiba fedha za EPA wakikamatwa nchi itakuwa hatarini sasa ka sio mawaziri na wakiongozwa na vigogo wengine wa serikali yao chini ya mwenyekiti wa mafisadi MKA… NA makamu WAKE Ja.. nani mwengine anayeweza kuiyumbisha amani ya nchi?????………SIKU ZOTENCHI HUYUMBISHWA NA WAKUBWA WA NCHI NA SIO MAKAPUKU WASIOKUWA NA MADARAKA. LAKINI IPO SIKU UMMA TUTAINGILIA KATI,

 17. baker Says:

  Duh ebwana wee kazi kweli kweli! Hii ndo bongo Dari salama. Mi yangu macho.

 18. kimk Says:

  Kifo cha huyu bwana ni sawa na cha savimbi/Garang kwa sababu wote walikuwa wanatesa wananchi wao.Tofauti ni kuwa huyu aliiba na kusaidia wezi wakati wazazi wanajifungulia juu ya baiskeli.
  Kifo chake kimefanywa siri,sasa kama serikali ilikuwa haijui alipo wamepata wapi taarifa.
  Hii serikali ya JK imeshaua ushahidi wa kesi ya EPA maana shahidi mkubwa hayupo.
  Watu wanapeta na kodi za walala hoi.
  Kwahili JK historia itakuhukumu.

 19. Ragwire Says:

  Jamani,
  Balali hajafa ni mzima kabisa, hii ni njama hawa watu wametunga ili asije kulipua bomu linalowahusu wakubwa.

  Balali yupo hapa Bostoni ni Mzima. CCM mbona mnazika mtu angali hai?

 20. Amina Says:

  mhhhh haya mi sina hata la kusema..balali kafa au hajafa?ana ana ana do kachanika basto,ispilingi matido,kaja…a,us..zi unanuka tena sana,sana kabsaaaaaaaaaaaaaa

 21. madongo Says:

  mmhhh huo ni uongo mkubwa sana tena sana Balali yupo sana jana tuh nimepishana nae supermarket ananunua chakula cha mbwa wake hapa BOSTON sa hiii mnatangaza amekufa…

 22. mavoo Says:

  kama kweli kafa ni mipango ya Mungu yeye ndiye atakaye muhukumu kwa kila kosa alilotenda na kama kweli siku hiyo ya mwisho ipo kama wanavyosema kila mtu atabeba mzigo wake.

 23. SALLY Says:

  Rest In Peace Dr. Balali

 24. Pearl Says:

  binadamu anaweza kufichwa jambo lakini watu wakumbuke kuwa MUNGU hafichwi jambo lolote.
  “time will tell everything”.

 25. Ed Says:

  Can someone from BC prove this? I guess since everybody in Tanzania declared Balali death then he died.

  Kan Lay and Enron nightmare. It is not over until the fat laidy goes to sleep. I am waiting kuona picha za mazishi, unless otherwise nita declare consipiracy theories zangu ambazo zitamake sense kwenye masikio yenu.

  Nitakwenda DC this friday, am looking to see maombolezo. Other than that we’re going to start the whole nightmare.

 26. trii Says:

  nashindwa niamini nini ,upande mwingine naamini kama hajafa upande mwingine naamini kafa,kasheshe tupu.

 27. SANIA Says:

  RIP DAudi Balali

  kila mwanadumu anamapungufu yake yeye mweyewe na mola ndio anajua kilamwanadamu anamachungu yake yeye mwenyewe na mola ndio anajuaaaaaaaaaaa

  Dunia ni njia jamani.

 28. binti-mzuri Says:

  ivi nyie watu mnaongea pumba gani….. AMEFARIKI DUNIA…why on earth would people lie to the nation!!!!??!?!?!?!??!?! subirini serikali iwatangazie,ndio mmfunge vinywa hivyo…. we Rwagire upo Boston ya Kimara au?

 29. magari Says:

  Duh kwa kweli mimi naungana na mchangiaji alosema ,afichwe,asjifiche ,hukumu ya mungu still their hawezi kuukimbia uso wa mungu. Na kama amekufa basi tumwachie mungu afanye kazi yake tusihukumu ,ila tulobaki tujifunze toka kwake , mimi kwa imani yangu kila uovu wowote mwanadamu unaofanya una malipo yake ila ni siri ya mungu tu unaweza kuadhibiwa mbele ya dunia au mbele yake mwenyewe .hivyo tuombeane ktk kutenda mema kwani binadamu wote tu dhaifu tunaishi kwa msaada wa mungu tu ikiwa tunafanya yote mema bila kumkosea maanani !

 30. salma Says:

  mh!!!!!!!! kazi ipo! haya balali kajibu vizuri kwa mungu

 31. XXX Says:

  sasa wabongo hav got somthin to tok bout..

 32. Zemu Says:

  poleni ndugu wa Marehemu.Mungu alitoa na Mungu amwetaa,Jina la Mungu litukuzwe.Na kama hajafa wameficha,Mung sio wa kiivyoJicho lake lake na matendo yake yanatisha ka nini.

 33. Muga Raymond Says:

  Everybody has got weaknesses and strengh’s, do not judge a person due to the failures in particular areas, that is a sin, as it’s written that, only the creator can judge us. Though he was caught up frauding, it could’ve been the evil’s temptation, and everyone of us fail to resist temptation sometimes, I guess what am tryin to say is, we should also remember his contribution to the development of this country, and get to honour and respect him for that. MAY GOD REST HIS SOUL IN PEACE.

 34. binti-mzui Says:

  muga raymond isnt UFISADI a sin then,wewe unaeja sins!

 35. Meremeta Says:

  Muga Raymond, umechemka, hicho kizungu chako inahitaji usafishaji wa maji ya moto, ni chafu kweli.

  Meremeta

 36. binti-mzuri Says:

  hahahah meremeta nimekaa kwenye screen yangu na kucheka kwa kweli!

 37. samaki Says:

  Eti wanasema kafa kwa ngoma. Lakini ukitizama sura yake ya picha za mwishoni ..mmmm. Haya dada zetu mlo kuwa mnatesa na ma- vogue.

 38. Matty Says:

  mh!kila nafsi itaonja umauti awe amekufa au hajafa yote sawa tu naona maana hela za EPA wala hazirudi,tumwachie Mungu ndo mtoa hukumu.

 39. hombiz Says:

  Balali!? Kwa nini umeondoka na siri ya wazi?

 40. any Says:

  Mtasema sana, lakini he is gone, so is EPA! sasa? rudini maofisini mkatengeneze pay checks, Balali kashamaliza kazi yake!

 41. hombiz Says:

  wakiwepo wananchi wengi kama wewe any hapo juu, bongo haitaendelea. Hizi ni tuhuma nzito sana ambazo ni lazima zifanyiwe kazi na sheria kuchukua mkondo wake kiufasaha. Kila mtu akisema kama unavyosema wewe “any”, ufisadi hautapungua na hatimaye kufa kabisa. Watanzania lazima tushikie bango swala hili la EPA na kashfa nyingine zote hadi mwisho wake. Ikiwezekana tuandamane nchi nzima na kualika vyombo vya habari kama BBC na CNN katika maandamano hayo.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s