BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MWINYI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO! May, 21, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:55 PM

RAIS mstaafu Ali Hassan Mwinyi (83) anatarajiwa kuongoza msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kupambana na Ukimwi nchini.
Msafara huo ‘Changamoto ya Kilimanjaro’ ambao unaratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) utaanza Juni 14 mwaka huu na utajumuisha wapanda mlima 53, akiwemo Mzee Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. James Msekela.

Taarifa iliyotolewa na GGM na Katibu wa Changamoto ya Kilimanjaro 2007, Sean Jefferys anasema maandalizi muhimu yamekamilika na tayari wapandaji 53 akiwamo Rais mstaafu Mwinyi tayari wanafanya mazoezi kujiandaa msafara huo.
Rais Mstaafu Mwinyi alisema amekubali kushiriki katika changamoto hiyo baada ya kuridhishwa na malengo yake, ambayo ni kukusanya fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini pamoja na kujihusisha na kuwasaidia waathirika.

 

Mstaafu Mwinyi aliwaomba watu binafsi na kampuni wamuunge mkono na kudhamini ushiriki wake kwa kuwa kwa njia hiyo tu kutaleta maana ya ushiriki wake.
“Umri wangu ni miaka 83 na mwaka jana wakati nazindua changamoto hii niliwaomba watayarishaji nami nataka kupanda mwaka huu. Wengi wao hawakuniamini na hata kwangu haukuwa uamuzi mwepesi lakini ni funzo la jamii,” alisema Mwinyi.

Kwa mujibu wa Jeffrey’s kampuni zilizojitokeza kudhamini upandaji huo mwaka huu ni pamoja na Anglo Gold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya GGM, Celtel Tanzania, Barrick Gold, Pan African, Atlas Copco, Sandvik na Afrikan Explosives. Nyingine ni Rhino Lodge, Air Tanzania, Kilimanjaro Kempinski Hotel, ATS, Sarova Hotel, Coastal Travel and Tours na Zara Tours.

Habari hii kwa hisani ya Lukwangule.

Advertisements
 

17 Responses to “MWINYI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO!”

 1. michelle Says:

  Kumbe huyu mzee ni wa longi duuu.
  Hongera mzeee.

 2. Amina Says:

  we mzee unataka kujiua?shauri yako,mi nafanya kazi kampuni ya tours umri huo hauruhisi aliekushauri nani?kipindi chote ulikua wapi au unatafta umaarufu?ngoja uji balali

 3. trii Says:

  hapo langu jicho.

 4. DUNDA GALDEN Says:

  RUKSA ALHAJ KWA HILO.NI JINS GAN BADO UNA MOYO NA WATU WAKO.MIM NAKUTAKIA KILA LA KHERI HILI FUNZO KWA JAMII

 5. binti-mzuri Says:

  mmh jamani haya si matusi,Mwinyi kupanda kilimanjaro!?!?!na mie ntaenda kupanda himalayas!

 6. binti-mzuri Says:

  hahaha amina umeuaaa

 7. Gervas Says:

  kupanda mlima sio lazima afike peak, anaweza kwenda mita kama mia tatu si tayari kapanda? au maana ya kupanda mlima ni mpaka ufike kilele? Big up, mzee ruksa.

 8. likelle Says:

  Dada usimdisresapect mweshimiwa Alahaj we nedna kapende himalaya..ila kama yeye anajua hawezi asingesema anaenda…watu bwana..don ever disrespect others…
  N alhaj…..ur the gretest…inshallah may Allah make u leave longer n healthier.

 9. Amina Says:

  binti mzuri kausha ni ushauri tu…maana ya kupanda mlima ni kufika peak ndiyo we gervas!kama wapo ambao hawafiki peak basi ujue wanajifurahisha tu

 10. buyu Says:

  Mzee Rukhasa! yakhe unataka kucheua Pilau na pocho pocho bure!Lakini Jaribu nakuamini sana Ustahadhi

 11. Chala Says:

  Mzee ruksa panda tu kama afya inaruhusu wewe mwenyewe umeamua its ok then… mi nakuombe kheri inshaallah ufanikiwe kuupanda bila matatizo.

 12. binti-mzuri Says:

  we likelle we mwenyewe umenidisrespect hapo!

 13. Msanii Says:

  KUPANDA MLIMA RUKSA!!!

 14. binti-mzui Says:

  hahah@ buyu

  eti kucheuaa … jamani mze mwinyi mi nampendaga sana,ila naona asiupande huo mlima

 15. tish Says:

  Hongera kumbe hajawaji kupanda mlima na kufika kileleli jamani bas ajitajidi kufika

 16. Mama wa Kichagga Says:

  Kupanda KLM sio kazi ili mradi uwe mtu wa mazoezi maana kuna mwendo wa TZ 11 (miguu) siku 3 kwa wastani wa masaa nane kwa siku.

  Kama wewe huna mazoea ya kutembea umbali mrefu kwa miguu usisubuti kujaribu maana hata kibanda cha mwanzo hufiki. Na kaka mtu ana ugongwa wa pumu chondechonde asitafutie kifo maana kila unaposonga mbele kutokana na urefu wa kutoka usawa wa bahari (Altitude) pressure inapungua na hata wazima inaleta tabu mara nyingine.

  Otherwise, Baba Mwinyi kama hana hayo matatizo Uhuru Peak atafika bila wasiwasi wowote maana najua anamazoezi mazuri. Hivyo umri ni ugonjwa tuu wa akili mtu kujiweka kuwa ooo siwezi hiki na kile nimezeeka! “AGE IS A DISEASE OF MIND, BUT IT DOES NOT MATTER”.

  NB: Kama hujawahi kupanda mlima KLM jitahidi uende maana kuna mambo mengi mazuri ya kufurahia na kujenga afya yako pia.

 17. wajukuu Says:

  Shikamoo Mzee Mwinyi kwa Busara zako! Wakati wa Uongozi wako Nchi ilikuwa IMETULIA. Sasa watanzania wameanza kubaini tofauti. Kwamba Debe tupu haliishi kutika. Mungu akujalie Afya Njema.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s