BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“TUME ICHUNGUZE KIFO CHA BALALI”-DR.SLAA May, 22, 2008

Filed under: Developing News,News — bongocelebrity @ 7:17 AM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amependekeza kuundwa kwa tume huru ya kimataifa itakayochunguza mazingira ya kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Advertisements
 

49 Responses to ““TUME ICHUNGUZE KIFO CHA BALALI”-DR.SLAA”

 1. binti-mzuri Says:

  umbea tuuuu! sasa mntaka mkafukue maiti?

 2. Gervas Says:

  Dr. Slaa umesema kweli, sababu, bila balaliMafisadi walioshiriki naye wamepona maana tunasikia ni vigogo. Hata nashangaa sijui kamati ya Mwanyika itatoka na nini kama sio changa la macho tu. Mwezi mmoja ulikuwa unatosha kabisa kumhoji balali, kupata ukweli na kuwashitaki wahusika. Ni wazi kwamba public opinion ya watanzania ina kiu ya kuona pesa zinarudi na haki inatendeka. Lakini ni mara ngapi Serikali inapuuzia public opinion ya Watanzania?. Bila kuondokana na huu ubabaishaji, basi tutaendelea kuwa masikini wa mwisho duniani milele maana watu tunaofikiri kuwa watatukomboa na tunawapa madaraka ya kukaa ikulu, ndo wamekuwa wanywaji wa uji wa mgonjwa…na hatimaye mgonjwa anakata roho, hao hao wanaenda kuishi ng`ambo. Edwin Ndaki, mimi nafikiri kwa hili hatutafika ng’oooooo!

 3. DUNDA GALDEN Says:

  KUKIWA NA KIFO MENGI USEMWA
  KUNA WAFURAHIA
  KUNA WANASIKITISHWA
  LAKIN WENGINE UJIULIZA JE?
  NAKUSAHAU KILA MTU LAZIMA ATAKUFA

 4. likelle Says:

  sasa bwana Slaa unataka serikali ifanyeje na wakati muhusika ameshakufa…tena unasema kwa herufi kubwa eti kama nilivyosema awali kama bwana balali akifa……du…mi pia ningetaka kuona hitma ya bwana bilali ila kama ameshakufa sa we unataka serikali iutoje huo ushadi toka kwa marehemu cha muhimu we enedelea na uchunguzi wa kesi sio marehemu….ndo maana si waTz atuendelei sa we huo uchunguzi wa kifo we utatusaidia nini sisi watz…aghhh

 5. kamanzi Says:

  Mi nnachotaka ni hela zetu zilizoibwa tu. Kama Balali kauawa au la hiyo hainihusu. Mafisadi leteni pesa yetu mkitaka kuuana iye ni shauri yenu.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Walaani Mafisadi

 6. bino Says:

  umesema ikweli slaa, tumechoka na hawa viongozi wasioheshimu hakiz abinadamu, sasa tuwashitaki kwa kuficha ukweli wa mambo kuhusu wagonjwa viongozi.

 7. Mtukwao Says:

  Ha, siamini yani humu kunawatoto! maana naona kuna watu wanaongea kama watoto wa miaka miwili vile.

  wewe binti mzuri “pls think twice before u say something”

  sio kwamba nakuingilia uhuru wako wa kuongea but pls if u really love u country then ‘try to show some sympathy ‘

  Kifo cha Bilali kina utata na lazimema kichunguzwe, anasiri nyingi za serikali anazijua na yeye anaweza akawa ndio “initiator” au “middleman” tunaweza tukajikuta inchi ilisha uzwa sikunyingi kwa waarabu!

 8. tish Says:

  jamni heee acheni hii ishu ni kubwa tu kuna wanausalama wawili tayari wamewauwa katika hii ishu na bado wanaendelea kuua tu. Kwani hamkusikia watu wawili waanguka PCB basi uchunguzi bado unaendelea na wanausalama wa taifa wameuliwa na bado mafisadi wanatesa tu lakini TUACHE MUNGU AITWE MUNGU.

 9. michelle Says:

  Ni lazima waendelee kuhujumu nchi maana ndo tabia zao, sasa wasipoiba na kuifanya nchi ionekane masikini itakuwaje?

  Maana hawa watu ni wasanii hujawahi ona wanaiibia nchi na kuwaibia wazungu wanaofikiri nchi inahitaji msaada ,wageni wakitoa msaada nao unagawanwa juu kwa juu , zile dollar alizotoa Bwana Kichaka mmeziona zikowapi? nchi ya kisanii ajabu. MKONO WA mUNGU (BWANA) UWE JUU YENU MAFISADI, NA BADO MTALIPIZWA MPAKA VIZAZI VYA NNE, MTAKUFA KILA LEO NA WATOTO WENU WATABAKI YATIMA KAMA BIBLIA INAVYO SEMA, TUBUNI NA KUZIACHA NJIA ZENU MBAYA.

 10. michelle Says:

  Jingine tutaaminije kama kweli umekufa maana hata maiti haijarudishwa nyumba, pengine ni usanii tu wa kukimbia kujibu mashitaka, lakini hata akijificha Mungu atashughulika naye tu, unaweza ukajificha kwa mwanadamu lakini si kwa Mungu.

 11. Subby Says:

  Mhu! sasa kama huyo bwana kafa kikweli kweli kwa maradhi, kafa siku yake imefika, kafa kwa kufisadiwa, ukifanyika huo uchunguzi anaoutaka Dr. Slaa na majibu yakapatikana hizo siri alizoenda nazo kaburini ndio zitatoka? Atafufuka na kusema hayo wanayotaka watu waseme? Kila siku kuunda tume, nyie hamjui uundwaji wa tume bongo ni namna tu ya kula pesa maana posho yake si ndogo. Si bora hizo pesa za kutaka kuchunguza mtu kafa na nini zingepelekwa zikanunue vifaa vya kuwasaidia kinamama wajawazito vijinini na kuwanusuru na vifo wakati wa uzazi. Ukisikia tume umekaa na bado inataka kuongezewa muda ujue watu wananufaika na ulaji. Kama mlikuwa hamjui ishu ya political economy kwenye conflict na peace making ndiyo hiyo. Watu wananufaika kiuchumi na migogoro kwa kuundwa kwa tumes, ndio maana muwafaka wa ZNZ hautakuwa ng’o mpaka waondoe posho za wajumbe wa tume. Na labda hiyo tume huru anayotaka Dr.Slaa atuambie ni nani ataifinance, kwa sababu ni tume huru, Chadema wajitolee basi kufinance kwa sababu kama itakuwa financed na serikaili we know ‘who pays the piper……….!

  Let the man rest in eternal peace kama ana makosa Mungu ndiye hakimu wa kweli na wa haki! Wengine waliiba mpaka pesa za walemavu na ndio vimbelembele kuonyeshea vidole wenzao na asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe!

 12. Chala Says:

  jamani mie nina swali, Kwani hiyo PCB huwa haitoshi kuchunguza mambo kama haya ? mpaka kuwe kunaundwa tume??? mimi hilo sijalielewa kdg waTz wenzangu….halafu katika uundaji wa tume hasa tume hasa hizo tume huru ni lazima wanaowekwa wawe katika serikali na wabunge tuu? vipi kuhusishwa kwa wananchi wa kawaida ambao wanaweza kujiamini na kujitolea wakawa pamoja na hao wabunge na serikali whatever wanavyounda lakini na wananchi wa kawaida wenye uchungu na nchi yao wakashiriki …

  Me i don trust anybody kwenye hii serikali hasa hao maPCB sijui PCCB coz walionyesha kitu cha ajabu sana dodoma wakati wa uchaguzi wa NEC ya CCM imani yangu ikaisha kabisa juu yao…

  yani hapo tutaongea weee lakini unadhani wanajali hao mafisadi ” mtu aliyezoea kula nyama ya mtu ataendelea tu hawezi kuacha inakuwa ipi kwenye damu ” alisema nyerere..

  nasikitika tu kwamba pesa yote wanayochukua wanasahau kabisa kama kule vijijini ndugu zetu bado kabisa wanaishi maisha ya tabu, huduma muhimu bado ni duni kwa maada hata zahanati ipombali na makazi ya watu, akina mama wanapata tabu sana , mmh kweli kuna binaadamu ambao hawana uchungu kabisa.

  Ila inshaallah mwenyezi mungu nasema Innallah Maaswabirina” Kila mwenyekusubiri mwenyezimungu yuko pamoja nae” ngoja tuone mwisho wake…

  Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

 13. binti-mzuri Says:

  mtukwao…i know people dizaini yako…maybe na wewe fisadi vile vile

 14. BLACKMANNEN Says:

  Kwa maoni yangu mimi “Balali” hakufa, bali soo la “EPA” ndiyo lililokufa. Balali bado hai, amebadilishwa sura nyingine katika hospitali aliyokuwapo kwa kutumia fedha za EPA, na amenunua maiti ya mtu mwingine kwenda kuzika, ili aendelee kuishi bila usumbufu na kutumbua mihela ya EPA!

  Je, kwani Dr Balali alikuwa na uraia wa Marekani pia? Tangu lini mmeona mtu raia wa nchi nyingine hata kama ana kibali cha kuishi nchi hiyo, akazikwa nchi ile anayoishi bila sababu kubwa ya kufanya hivyo? Kwanini ilichukua muda mrefu kujua kifo chake kwa viongozi wa Tanzania? Kwanini wanandugu hawataki maiti ya ndugu yao iletwe Tanzania? Hata kama ni yeye mwenyewe alitaka azikwe Marekani, alijuaje kuwa angekufa huko Marekani kama haikuwa mipango yake ya kujificha baada ya kuona hali ngumu iliyokuwa ikimwandama? Kwanini viongozi wa serikali ya Tanzania wawaamini ndugu za Balali pekee yao? Kama ni kweli Balali kafa, kwanini hawakuruhusu Watanzania walioko huko Marekani waione maiti ya Balali na kuithibitisha kuwa kweli alikuwa yeye? Kama sio mambo ya uwongo, naiomba serikali ya Tanzania ichukue vipimo vya DNA kuthibitisha kuwa aliyezikwa huko Maryland, Washington DC ni Dr. Balali kweli!

  Watanzania wote katika habari za kifo cha Balali tuliitegea familia pekee kutueleza na kutuelekeza cha kufanya, kwanini?

  Kwa kutumia akili yangu, mimi siamini kuwa Dr. Balali atakuwa kweli amekufa, bado hai, amejibadirisha sura na kutangazwa kufa ili kuua soo la EPA.

  Blackmannen

 15. JBigy Says:

  umbea wa Dr. Slaa uko wapi?Kuna tatizo gani uchunguzi kufanywa wa kifo cha Balali?Huyu ni kiongozi/mwajiriwa ‘mkubwa’ wa nchi ambaye, kwa namna moja ama nyingine, kifo chake ni vema kikachunguzwa.Ni mtu anayehusishwa na mambo kadhaa ya kiTaifa.
  Wakati mwingine kuingiza ‘uswahili’ kwenye mambo ya msingi kwa kurahisisha vitu kutaka viende ‘kienyeji’ bila utaratibu ni suala la kuangalia sana. Hivyo mimi binafsi sioni tatizo la maoni ya Dr. Slaa.
  Pia kuna watu wana-attack wachangiaji kama wachangiaji badala ya kutoa hoja zinazo-attack hoja za wachangiaji wengine. Hawa ni watu wanaochukulia vitu kijumla na huongea bila ‘framework’ yoyote.
  Anachosema ‘mtukwao’ ni sahihi. kuchunguza kifo cha Balali si umbea ila ni kwa maslahi ya Tanzania. Tusiongee tu kama hatujui tunaongea nini.Hapa si uwanja wa mipasho bali ni uwanja wa uchangiaji wa mawazo wenye manufaa kwa maendeleo ya nchi yetu.

 16. binti-mzui Says:

  Jbigy i dont care what your opinions are, ic are about mine

  usiniingilie uhuru wangu,kuna kitu kinaitwa ‘freedom of speech’ na ‘conflic of thoughts’…thats what you think,and this is what i think..kama unakubaliana na mtu kwao thats okay and fine with me,because i cant care less …

  sasa unavyoanza kusema nachangia hoja zinazo-attack thats your own opinion,even though in my opinions naona i have been attacked- by you and mtu kwao.lakini like i said, those are my opinions.

 17. binti-mzui Says:

  umbea wa Dr. Slaa uko wapi?Kuna tatizo gani uchunguzi kufanywa wa kifo cha Balali

  KUNA TATIZO GANI UCHUNGUZI USIPOFANYWA WA KIFO CHA BALALI.

 18. binti-mzui Says:

  Michelle wewe ni Tomaso kama yule wa kwenye Biblia. huamini kma hajafa,wewe kama nani. tukumbuke,kama na sisiingekua ndugu yetu watu wanataka washuhudie maiti yake,ni jambo tusingelipenda. dk balali alikua mmarekani. why he got the job and he isno longer atanzanian citizen,i do not know, hapo wakulaumiwa ni kiongozi wetu. secondly, familia yake yote inaishi marekani, wamzike huku na wanataka kwenda kupalilia majani na maua kwenye kaburi la mpendwa wao,yani kila siku wapande ndege au???TANZANIANS WHAT ARE WE TALKING ABOUT!!!!!!!!!!!!!!?????????? choice ni ya mtu wapi azikwe jamani,sawa!???!?!?!?!? amefariki na tangazo limeshatolewa marekani kwenye funeral home for further reference nendeni michuzi blogspot… NA TUACHE USHAMBENGA!

 19. Subby Says:

  Mnaposema huyu ni kiongozi/mwajiriwa mkubwa wa nchi siwaelewi, au alirudishwa tena kuwa Gavana baada ya kuvuliwa cheo chake na serikali, kwani bado anahesabika kuwa ni mwajiriwa wa BOT/serikali? Mbona naona kizungumkuti, ninavyofahamu kisheria Almarhum Balali alifukuzwa kazi, ugavana wake ulitenguliwa na Mh. Rais. Ni sawa mtu leo aseme kuwa mawaziri waliojiuzulu ni viongozi wakubwa wa nchi kwa nyazifa zao wakatisi viongozi ingawa kuna priviledge ya kujiuzulu bado unapata heshima fulani si ambayo ni tofauti na kufukuzwa kazi! Bwana JBigy hebu tufafanulie huo utata maana penye wengi hapaharibiki neno.

  Pamoja na hayo bado nashikilia msimamo wangu hakuna haja ya kuwatafutia ulaji kina Slaa na wenzake kwa kuunda Tume, tume tume my foot, niambieni ni mapesa mangapi yanatumika kuwalipa wajumbe wa tume ambayo yangenunua madawa na kujenga madarasa ya shule!

 20. trii Says:

  Gervas —nakubaliana na wewe sheria za TZ zinatumika kwa wa lala hoi tu,ila viongozi haziwahusu.lzm wazibiane kwani hizo pesa hakula mwenyewe.KASUSURA alikatamwa mara1 hata muda wa kujieleza hakupewa.Lowasa ameishia wapi?mmmmmmmmmmmmmmm

 21. Mie Bana Says:

  Wabongo amkeni Jamani,Siku huzi Kwa nchi za Dunia ya kwanza kunatekenolojia ya kubadilisha sura,jinsia man kuwa dem na dem kuwa kidume,sasa hapo kunachezo limechezwa,Jamaa kafa tar 16 May wewe taarifa unakujapata 5 Days after,”Think Before”” I LOVE MY COUNTRY TANZANIA..Wabongo tuamke,DK SLAA kila kitu unapenda tume tume tume sasa na hao makachelo wa upelelezi wa Police watafanya kazi gani? au Unajisikia furaha kumtima unapoona Pesa za walala hoi zinavyopangiwa bajeti hewa na hizo tume…………

 22. SANIA Says:

  Hivi we hapo juu unaejiita bint mzuri sikuelewi elewi unachokiongea naona ni pumba tu. wakafukue maiti iwasaidie nini? au ili iweje? kinachotakiwa hapa sio kufukuwa maiti kama unavyosema wewe mara ooh umbea sijui ndio mtoto wa huyo balali? au wewe unauchungu zaidi ya watanzania?
  waache wadau wanaochangia vitu vyamaana wachangie bana aalaah! unanitia asila kweli wewe.

 23. binti-mzuri Says:

  subby ongea usikikeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  tume tume tume – ili wapate hela ya kuongeza proteini na carbohydrates sio!?wakati sie tunaishia na maharage ya mbeya

 24. binti-mzuri Says:

  mie bana kwani kifo cha mwalimu J K Nyerere,mliambiwa siku hiyo hiyo??incase you dont know,we found out 3 days after…unless if your going to question that as well.

 25. Subby Says:

  Kufa kwa Balali kutauaje soo la EPA? Mie nashangazwa na hizi propaganda tunazolishana wenyewe maana inawezekana kabisa wengine ni wahusika wenyewe na wanakazana kuuza idea ya kufa kwa Balali ndiyo mwisho wa EPA. Kwa kuwakumbusha tu ishu ya EPA imeanza kushughulikiwa wakati Balali akiwa mgonjwa na Gavana wa BOT, ripoti imetoka yeye akiwa yuko nje kafukuzwa kazi akiwa nje. Sasa kesi ya EPA inausinaje na kufa kwa Balali? Kwa sababu ushahidi wa makabrasha nani na nani wamechukuwa pesa uko BoT kwani aliondoka na mafile yote yanayoyuhusu EPA, kwani huko kupeana pesa kulikuwa verbally au kwa maandishi, maana kama kulikuwa verbally basi ingebidi mpaka yule aliyeidhinisha kutoa pesa awepo, na kufa kwake kungewanufaisha waliochukua hizo pesa maana kungekosekana ushahidi.

  Ninachikiona hapa ni opportunist ambao hawakawii kurukia jambo kwa maslahi yao, hata mimi ningekuwa fisadi ningekazana kuandika magazetini na kila mahala kuwa midam Balali amekufa basi na kesi ya EPA imekufa. Sasa tusubiri tuone huo utabiri wa kifisadi watu wanaotaka kutuletea hapa kama hiyo kesi itakufa. Mafile yapo na watu wanajulikana msianze kutuletea longo longo hapa ili muendelee kupeta! Endeleeni kurudisha pesa mpaka zirudi zote! Balali hakuondoka na ofisi wala Benki.

 26. binti-mzuri Says:

  SANIA wewe umeongea point gani zaidi ya kuniponda mimi?au na hiyo point!? basi tuwaache na wenye pointi waongee..mie na wewe twendee

 27. any Says:

  You guys go back to work. The guy is gone, period! au mtu ukiwa fisadi Mungu anasitisha siku ya kukuita hadi uchunguzi ukubalike. Enough! ebooooooooooooo

 28. BLACKMANNEN Says:

  Mimi sitageuza nilichosema tangu mwanzo kuwa huyu Balali amejibadirisha sura kwa “Plastic Surgery” hapo hospitalini kwa kutumia mahela ya EPA, ili kuliua soo hili. Aliyekufa sio Balali, na kama viongozi wa serikali ya Tanzania wanataka kujua ukweli huu waombe kuchukua DNA kwa huyo marehemu aliyezikwa.

  Kwanini Watanzania, waendelee kuyaamini maneno ya wanafamilia ya Balali? Kwanini wanafamilia hawa hawakutaka Watanzania wengine waione maiti ya Balali?

  Kitu kingine kwa viongozi wa Tanzania, walikuwa wanajua kuwa Dr Blali nin raia pia wa nchi nyingine, kwanini walimpa nafasi kubwa ya uongozi kama huo? Je, sheria za Tanzania zinaruhusu jambo hilo? Ninaomba jibu lenu viongozi wa Tanzania akiwemo Mh. Kikwete!!!!!!!!

  Blackmannen

 29. Dullah Says:

  Binti mzuri jahazi wanaitaji mwanamipasho mwingine!

 30. binti-mzuri Says:

  blackmanen where is your proof kwamba kafanya plastic surgery!!?..tusiongee tu,tuongee kwa facts!!

 31. binti-mzuri Says:

  dullah unataka kuongea na mie tu wewe!!! haloooooooooo

  nasemajeee… no tume, no blaa blaaa …. Balali is dead,and so is your money.. nextttttttttttttttttttttt

 32. binti-mzuri Says:

  ziliwatokeeni
  zilizogawanyikaa
  kama ndimi za motooo
  zilizojawa Roho Mtakatifu

  zilitiririka,titiririka
  zilitiririka,titirika
  zzilitiririka tiririkaaaa

 33. Amina Says:

  du…hapa kazi ipo mi kimya leo

 34. Mie Bana Says:

  Weee Binti-Mzuri mzima kweli au ? au umechanganyikiwa na ufisadi,it sounds like dem-man,coz unacomment Pumba tu,Try to be in modern world with modern technology.au wewe ni ccm nini? Nyerere aliuliwa ili watu wapate chance la kufanya hivi vitu vyote vinatokea tz.Nyerere the same day amekufwa taarifa zimetoka out sasa wewe unataka nini???????

 35. L.JOSEPH.L Says:

  Ndugu yangu Slaa (padri)
  Huna hata huruma kwa fedha za umma
  maana tukianza kufukua makaburi tunamukosea Muumba. kama unazo fedha zako mwenyewe tambaa mpaka Washington hospitali alikofia kuna kumbukumbu za kiini cha kifo chake. Dr aliyedhibitisha kifo chake ameandika harafu uje uhutangazie umma na hapo utakwa Mzalendo halisi,.

 36. binti-mzuri Says:

  mie bana YOU DONT KNOW WHAT UR TALKING ABOUT,naomba uulize kwanza kabla ya kucomment. nyie mmetangaziwa nyerere kafa,kauwanja kenu ka taifa kimeshafanyiwa marekebisho na banda lishajengwa,kesho yake karudishwa mkaenda kupanga foleni kwenye jua kali kutoa heshima za mwisho,wewe NANI kakwambia u were told the same day!?habari ndio hiyo. mimi najua Balali alikuwa mwizi,fisadi,au chochote mnachomuita,u r missing the point here,what am saying ni kwamba AMEFARIKI sasa whats the point!!!??!? balali is dead,hate it or love it… get with the program mie bana,dont just start talking without facts

 37. Matty Says:

  Haya afadhali rafiki yangu Amina umesema huna la kusema mimi nimesahau nilichotaka kusema maana hapa leo naona mipasho kwa kwenda mbele.
  Afe asife Mungu ndie mtoa hukumu na pesa za EPA ndo zimeshasahaulika, sijui ni lini tutapata viongozi wakweli nchi hii wote ni wakina MR.POLITICIANS NAONA HAWANA JIPYA KABISA!

 38. hombiz Says:

  Siasa za Bongo siku zote zinaongozwa kwa nguvu za giza.
  Mimi nadhani marehemu Balali aliwekwa na mkapa pale BOT ili atumie elimu yake na ujuzi wa mambo ya uchumi na fedha ktk kuwasaidia mafisadi kulihujumu Taifa. Nakweli hilo liliwezekana. Lakini kama mnavyojua tena ndugu zangu, “unaweza kuwafanya baadhi ya watu kuwa ni wajinga kwa wakati fulani, lakini huwezi kuwafanya watu wote wajinga wakati wote”. Hicho ndicho kilichoendelea. Nahisi marehemu balali kafanywa mbuzi wa kafara baada ya siri yao nzito ya kuhujumu BOT, kugundulika na kuanikwa wazi na Dr. Slaa akisaidiana na wazalendo wengine wenye uchungu na nchi yao. Hivyo basi, baada ya kuona kuwa marehemu Balali ndiye aliyekuwa jikoni kwenye kashfa hizo, basi serikali imeona itumie wasaa huo kunyofoa uhai wake kabla mafisadi wengi serikalini hawajaumbuka ikiwa ni pamoja na Kikwete na serikali yake ambao walizitumia baadhi ya fedha za BOT ktk kampeni chafu za uchaguzi uliowaingiza madalakani.

 39. Katambuga Says:

  Hebu nikusaidie kidogo mdau wa BC kwa jina Binti-Mzuri(?) wa May 27, 2008 masaa ya 8:24 , na hapa ninukuu machache uliyo yasema,’ What am say ni kwamba ‘AMEFARIKI,SASA WHAT’S THE POINT ? BALALI IS DEAD, HATE IT OR LOVE IT…..,get with the program mie bana , DONT JUST START TALKING WITHOUT FACTS ‘, mwisho wa kunukuu. Wahenga walisha sema ‘ KUCHAMBA KWINGI MWISHO KUSHIKA MAVI ‘. Sasa wewe ndugu yangu upupu umejipaka mwenyewe. Tambua kwamba kati ya watu watako soma maoni yako hapa Wapo watu waliokuzidi sana Akili na Maarifa. Wewe mwenyewe unajiona umesha fika na una jua sana. Uwe mwangalifu katika kuandika. Siyo kazi kubwa kubaini msimamo wa mtu au anatetea maslahi gani ukipata fursa ya kusoma mawazo yake na hisia zake kama ulivyo lipuka wewe hapa bila ya kujitambua. Nadiriki kusema kwamba kwa uzoefu nilio nao wewe siyo Binti wala Mwanamke kutokana na kauli zako. Tumesha kujua wewe ni nani.Pole sana. BORA BASI uandike jina lako halisi au hata la ushabiki tu lakini usiwapakazie kina mama kwa kujiita binti-mzuri lakini maneno na matendo yako hayaendani na heshima walionayo kina mama. Be yourself. Kama umeajiriwa (kama walivyo ajiriwa mazumbukuku wengi kwa kazi hiyo na hilo tunalielewa) basi nakushauri urudi tena shuleni ukasome,vinginevyo utamwangusha ‘ BOSI WAKO’ . Pole sana mdogo wangu. Try to be a little bit more SMART in your presentations! Dont be a CopyCat. CIAEO ( chauw)!

 40. any Says:

  haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Katambuga? nimecheka hadi basi.

 41. binti-mzuri Says:

  katambuga ur good at quoting me,i think ukiscroll juu,utapata something else to quote..au nikikusaidia ni hii:

  ‘i dont care what your opinions are, ic are about mine

  usiniingilie uhuru wangu,kuna kitu kinaitwa ‘freedom of speech’ na ‘conflict of thoughts’…thats what you think,and this is what i think’

  wewe na ujuzi wako,etc etc etc wa kujua wanawake,wanaume,watoto,illiterate people and literrate people is of your own beneficial,that i dont care about KWANZA UMEKUJA KUCOMMENT HAPA,SIO KUJUA JINSIA YANGU WETHER AM A GIRL,BOY,BISEXUAL,GAY OR LESBIAN thats my business to handle!!!… dont comment on me as a person,comment on the facts that i write… tusipotee!

 42. binti-mzuri Says:

  najua watu mtakasirkia for me to say this,but i have to.. tatizo la hii board,watu wengi mnapenda kusapotiana,mtu akitoa point otherwise mnaona ‘oh no its wrong,huyu vipi huyu’ mnasahau kuna freedom of speech! mtu anaweza sema watever they want to say,as long as they felt like saying it – wewe as a person,you cant argue with them for being them,but argue with the opinions.

  ivi siku hizi kuna degree za kujua jinsia za watu au tunasafishwa vinywa???

 43. DUNDA GALDEN Says:

  KATAMBUGA BIN SAFARI NDEFU
  HABARI NDIO HIYO NAMI NILIKUWA NAWAJIBIKA (CHUNGUZA)NJE YA MKATABA HUYU BINT MZUR KWELI AU BISNESS BINT MATANGAZO LAKIN SASA NIMESHAFAHAM NA WENGINE PIA MAANA MABINT WAZURI TUWAJUAO SISI……………………………..

 44. JBigy Says:

  Nilichogundua binti-mzuri hujui maana ya freedom of speech. Freedom of speech does not mean you should say whatever that pours out of your mouth. Thinking before saying makes humans humans. Otherwise you will end up ‘criticizing’ others with uncritical assertions. It seems like una-base arguments zako juu ya kilichokwishasemwa. You seem to be happier when you counter-attack other people’s opinions regardless of whether or not these opinions are sound/true.
  Pia acha jazba na ligi. The claim that you don’t care about other people’s opinions except yours tells me what type of person you really are. If you think your opinions do not interact with others’, you better stop posting your stuff. You can keep them cause those are the only ones you care about!

 45. ndugu yenu Says:

  jamani mnapoteza mwelekeo wa forum hii,lakini binti mzuri is somehow right,lets discuss facts and not personalities;bc please bring another topic!this is saturated already: how about mkapa na ufisadi na mali na pension za ajabu na wizi na kuuza nchi kwa wa south na wadosi wanaotudharau na kutuona hovyo ..whats going to be the fate of such issues,how about uchumi wetu,umaskini,miundombinu,uhaba wa madaktari,vifo vya watoyo na wajawazito,mfumuko wa bei,petroli,nauli,njaamafuriko,nomoabomoa,machinga,muafaka wa zanzbar,how about safari za jk na viongozi wengine,matumizi ya serikali,msshangingi,posho za wabunge,wahindi na wachina na uchumi wetu,buzwagi na buhemba,tanzanite na kiwira ……..tunafanyaje???????

 46. binti-mzuri Says:

  haha jbigy am done with you!

  because umejicontradict mwenyewe hapo hapo kwenye comment yako!

  nakunukuu: ‘Nilichogundua binti-mzuri hujui maana ya freedom of speech. Freedom of speech does not mean you should say whatever that pours out of your mouth. Thinking before saying makes humans humans’ IF FREEDON MEANS UHURU SPEECH MEANS MANENO YANGU, THAT MEANS NI UHURU WA KUONGEA..SASA KAMA NINA UHURU WA KUONGEA KILE KILICHOKUA MOYONI MWANGU(AS IN DUKUDUKU LANGU) WHY SHOULDNT I????? UNASEMA I SHOULDNT SAY WHATEVER THAT POURS OUT OF MY MOUTH,MEANING I SHOULD SAY WHAT POURS OUT OF YOURS AMA I SHOULD CONSIDER YOUR FEELINGS?BUT IS THAT FREEDOM THEN!? I THINK THATS ‘CONSIDERATION OF SPEECH!’…..THAT YOU ARE TALKING ABOUT!LOL. NOT FREEDOM OF SPEECH…..NIMECHUKUA SIASA,I KNOW WHAT AM TALKING ABOUT.

 47. binti-mzuri Says:

  The only country that has freedom of speech is united states of America. Wengine wote tunajidanganya, theres no freedom whatsoever, and from the population that we have here in this blog itself,its sad for me to conclude that i’ve lost hope!.

  HakiElimu wanasema ‘tuna haki ya kuongea’ wameongea,Wizara ya Elimu ikafanya mbinu wakafungiliwa mbali.

  wanabongo fleva wakiimba nyimbo e.g. segere, mikasi zinafungwa after 2 months kwa kukiuka haki,mila na desturi WHAT DESTURI!?WHAT MILA?WHAT HAKI? if u ask me,its them wanaoingilia haki za watu. Bush katukwana in sooo many songs, but im telling you,i’ll bet you 5000 bucks kama kuna mtu yeyote bongo ambae atapata gutts for rapping about ‘ufisadi’

  JAMANI EMBU TUSIINGILIE HAKI ZA WATU. AM IN 21ST CENTURY,AL PRETTY MUCH BLARP ABOUT WHAT I FEEL LIKE, WHENEVER AND WHATEVER TIME I LIKE.. CALL ME INSENSITIVE,BUT I CANT CARE LESS,AM SURROUNDED WITH INSENSITIVE PEOPLE LIKE YOU. LOOK AT ME,AND REFLECT IT TOWARDS URSELF,UR PRETTY MUCH AS INSENSITIVE AS I AM,BECAUSE IF YOU WERE SENSITIVE,I WOULD HAVE BEEN ONE… LORD HELP THEM,NOT ELECT ME A MBUNGE,MAANA SIJUI ITAKUAJE.

 48. maryciana Says:

  binti mzuri big up kuhusu comment yako kwamba BASATA inazidi kufungia nyimbo nyingi.hiyo ni kweli kwani hata mwimbo wa seya haupigwi tena siku hizi maredioni. umefungiwa,sasa sisi tunasikiliza mwimbo siyo madhambi aliyoyafanya mwimbaji.Tanzania tulipata uhuru 1961,ila bado ni wafungwa!

 49. ITEITEI Says:

  tatizo la viongozi wetu wanadhani wananchi hawajui kujumlisha moja na moja nakupata 2 kama si 11,
  ingekua ni serikali makini kama za wenzetu huko duniani basi kifo hiki kingechunguzwa mpaka mwisho lakini serikali hii ya rais mwoga,mfyata mkia basi kitu kama hicho cha kuchunguza ni IMPOSBO coz wanajua nini kilichomuua!
  ITEITEI hapa


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s