BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ASANTENI/SAMBULUMAA BAND May, 23, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM

Mwisho mwingine wa wiki ndio umeshawadia.Mwaka unazidi kuyoyoma.Kwa upande mwingine,hii ni wiki nyingine ngumu kwa watanzania.Kuna msiba ambao kila mtu anasema lake.Hujui hata umuamini nani kwani yule ambaye ungetegemea akuambie ukweli,yeye pia anakupa sound!Anadai na yeye hajui, na yeye sio msemaji.Sasa msemaji ni nani?

Pamoja na yote,maisha lazima yaendelee,au sio? Kwetu sisi hapa BC,imekuwa ni wiki ya furaha.Mwaka mmoja tumetimiza.Shukrani nyingi sana kwa salamu na pongezi kutoka kwenu.

Kama kawaida Ijumaa ni siku ya kupumzisha akili kidogo.Wimbo wa leo ni Kadiri Kansimba kutoka kwao wana Sambulumaa Band ambao hivi majuzi Michuzi alibandika picha zao na habari nzuri kuhusu maendeleo ya Lister Elia ambaye alikuwa mmojawapo miongoni mwa wanamuziki waliokuwa wakiunda Sambulumaa Band.Huu ulikuwa utunzi wa Kasoloo Kyanga.Miziki hii ya zamani kwa kweli inatakiwa iwe dira kwa wanamuziki wa leo kwani miaka nenda miaka rudi bado ukiisikiliza utaburudika.Tunakutakia Ijumaa Njema.

NB:Usisahau kulog in katika bongoradio.com kesho(Jumamosi) mchana saa saba(1:00pm) za Chicago(Central Times) kusikiliza mahojiano ya BC na radio hiyo.Ukitaka kujua itakuwa saa ngapi hapo ulipo bonyeza hapa.

Advertisements
 

21 Responses to “ASANTENI/SAMBULUMAA BAND”

 1. Mswahilina Says:

  Big up BC,

 2. DUNDA GALDEN Says:

  home sick.hiyo music Bc wakat huo wana music walikuwa si mchezo si kukulupuka tuu mashairi siku hiyo hiyo redion no,
  pia kulikuwa na matukio ya kweli yaliotokea yaliogusa jamii
  sio sasa wakati ushakuwa ukuta.Balal kafa wengine wanasema Boston wengine Washington amefariki toka ijumaa wenye habari wameuchuna sijui sijui kila kona si utata huo.Mf.akitokea mwana mziki kuimba swala hili music wake utapendwa miezi kazaa alafu raia hawana habari tena yote kutokana na nyakati
  Ahsanten Bc music unamafundisho uwaminifu wa mapendo naokekana mjinga .hakuna ukweli mara mjomba hahaha hatari sana.kila lakheri wachangiaji wiki end njema
  chafosa chai goda

 3. Kamanzi Says:

  Kinachonisikitisha ni kwamba wanamuziki mahiri kama hawa wote wameishia kwenye maskini ilhali miziki mizito kama hii ilitakiwa iwaingizie mamilioni ama kweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu. Big up wanamuziki wote wa zamani. Wanaojiita wanamuziki siku hizi ni vifisadi tu vya muziki maana hawana ujumbe, hawajui kutumia ala za muziki wakati mapato yao ni makubwa kuliko ya wanamuziki asilia kama hawa.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Walaani Mafisadi.

 4. galasa Says:

  Namuomba Rais Kikwete amuachie huru Viking Nguza pamoja na wanawe kwa kutengua adhabu ya kifungo cha maisha kwa kosa walilotuhumiwa kulitenda.Nguza kama mwanamuziki mkongwe aliyekuwa akipendwa na wafuasi wengi wa jinsia zote ni mmoja wa wasanii wale waliokuwa wakizongwa sana na wapenzi wa kike waliomtaka urafiki wa mapenzi na alidiriki kuwakimbia kama ilivyo kwa wanamuziki wengi wa rika na daraja lake.Nguza siyo serial rapist,siyo reial killer,siyo jambazi sugu mtumia silaha,hana rekodi ya ujambazi wala ya kuua watu.Ni mtu alikuwa na kazi yake yenye mafanikio makubwa na alibeba heshima kubwa katika jamii.Alichangia sana katika uhamasishaji wa jamii katika siasa na maendeleo ya jamii.Alisaidia sana kuinua vipaji vya wanamuziki waliochipukia hapa nchini.Kupitia sanaa yake ya muziki alisaidia sana kupunguza ujambazi na uhalifu nchini kwa mafunzo na kutoa burudani iliyowafanya wale waliofikiria kujikita katika uhalifu waende kwenye kumbi alizostarehesha ili kupata burudani.Kumfunga yeye binafsi na watoto wake wote kifungo cha maisha hakika ni uhalifu mbele ya mwenyezi Mungu.Ikiwa Mungu yupo tayari kutusamehe kwa makosa yote tuliyotenda iweje sisi binadamu tuwe na roho ngumu kiasi hicho cha kukataa kufuata mafundisho na mfano wa mwenyezi Mungu mwenyewe.Nawaomba wanablogu wenzangu tusimtupe Nguza na wanawe kama vile ni watoto yatima waliokosa marafiki,wapenzi,wafuasi,ndugu na jamaa hapa Tanzania katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini tokea enzi za Bendi ya Maquis hadi balaa lilipomkuta.Nguza alizaa watoto katibu wote wa kiume na mwanamke mtanzania.Ni mtu aliyeipenda Tanzania kwa moyo wake wote.Kosa lake halikustahili kifungo cha maisha.Ni kosa linalorekebishika.Nguza akiachiwa na wanawe anaweza kurejea maisha yake ya kawaida na kumcha Mungu.Tusimchukize Mungu kwa Kuwatendea maovu wale wasio na mtetezi.Rais Kikwete sikiliza kilio chetu!

 5. usinijue Says:

  I wish ningeupata huu wimbo daaaah,bc nyie mnazidisha homesickness…big up wazee

 6. binti-mzuri Says:

  naikia huyo lister elia,hilo jina la elia kajibandika,eti sio surname yakee!

 7. JBigy Says:

  Wimbo mzuri na umetulia.Pia una ujumbe.Nyimbo nyingi za zamani zinachuja taratibu mno kwani zilikuwa na maandalizi ya kutosha na wengi wa waimbaji walikuwa na vipaji.

 8. kimk Says:

  BC,mnatutesa jamani,bonge la homesick. BC tunawaomba msamaha maana wiki tatu mfululizo mnazisulubu nafsi zetu kwa mavitu ya hisia.
  Hebu sikiliza ala zinavyorindima,muziki wa zamani kiboko.
  Sasa hivi kelele tupu na akina twanga,plus n.k

  Thanks BC.

 9. Muddy Omar Says:

  TUNAOMBA RAIS JAKAYA KIKWETE AMFUNGUE NGUZA VIKING!! NGUZA KACHANGIA MAENDELEO YA MZIKI WA TANZANIA KIASI KIKUBWA,MBONA” MAUMBA” KAFUNGWA MIAKA MICHACHE NA ALIKUA ANATEMBEA NA WATOTO WA SHULE?AKINA KISODA MA TERRORISTS BANDIA WALITEKA NYARA AIR TANZANIA WALIFUNGWA MIAKA 15,MHESHIMIWA JK EBU ANGALIA HATA KESI YA R.KELLY MAREKANI HAWEZI FUNGWA MAISHA!!!WE WANT NGUZA TOBE FREE NA FAMILIA YAKE, AHSANTE BC.

 10. shuhuda Says:

  Mkuu wa Upelelezi katika Kituo ambacho upelelezi wa Tuhuma zilizomkabili Nguza Viking pamoja na wanae yeye mwenyewe baadaye alikuja kabiliwa na tuhuma nzito za kuhusika katika mauaji ya wachimba madini wa Mahenge na kujikuta katika mkono wa sheria na kulazimika kuwekwa Rumande.Sijui kesi yake imeishia wapi.Lakini alikuja wekwa Jela baada ya kilio kikubwa sana cha wanahabari na wanajamii kuhusu tukio lile baya la mauaji.Na uchafu mwingine mwingi.Katika mazingira kama hayo nani ambaye hawezi kuingiwa na chembe ya wasiwasi kwamba pengine hata Nguza Viking na Wanae nao pia walibambikiziwa zile tuhuma ili kutimiza malengo ya wabaya wake?Hata kama kweli kosa lile alilitenda Nguza,hivi kweli katika Mila zetu za Kiafrika Baba Mtu unaweza kushiriki na Wanao uliyewazaa wewe mwenyewe katika vitendo vya kufanya zinaa katika nyumba moja mnayo ishi pamoja tena kwa kupokezana zamu au hata kwa kupishana zinaa hiyo mkiifanya kwa watoto wadogo wa shule za msingi?Kwa shida gani ya kukosa wanawake?Hulka ya wanamuziki wote ni kupendwa na kupapatikiwa sana na wanawake wa rika mbalimbali kiasi cha hata kuwakimbia baadhi yao.Huo muda na vishawishi vya kumfanya Nguza atende uhalifu huo pamoja na wanae wote bila ya yeye binafsi kutotambua kwamba jambo lile ni la hatari na lazima litakuja vuja na kutambulika hadharani vilitoka wapi?Hebu tumwogope Mungu jamani.Haki ni kwa kila mtu.Kosa la zinaa ni la kimaumbile,linaweza kabisa kurekebishika.Iweje mtu aliyeishi miaka yote kwa uadilifu mkubwa leo hii yeye na familia yake yote wafungwe kifungo cha maisha kwa kosa kama hilo?Watu wanaua kwa makusudi na wanapewa mdhamana na kuachiwa huru.Mafisadi wakubwa ambao kwa vitendo vyao wataweza kusababisha vifo vya maelfu ya watu kwa kukosa Tiba kwa ukosefu wa Madawa mahospitalini wanaachiwa huru wakipeta.Iweje mtu mnyonge kama Nguza na Familia yake yote isulubiwe kiasi hicho bila ya huruma na ustaarabu wowote?Adhabu aliyo itumikia Nguza Viking na Wanae hadi sasa imetosha.Nawaomba wanablogu wenzangu tumwombe Rais Kikwete amwachie Huru Nguza Viking na Wanae wawe Huru ili wamtumikie Mungu katika nafasi nyingine!’Ombeni Mtapewa’.Salini mkimtukuza Mungu,hakuna lisilo wezekana.

 11. binti-mzuri Says:

  we muddy omar umetumwaaaaaa

  umetumwaaaaa

  toka hapa … abake watoto wadogo halafu eti aachiweeee!! mtajijuu ngusa aozee jela tu,toeni pumba in this forum jamani!!… sasa aachiwe ili iweje.wewe leo ukibakwa au mwanako au ndugu yako akibakwa,je ungependa mbakaji aachiwe huru??? LET NGUSA VIKING PERISH IN THE SUN! malipo hapahapa dunianii.. babu seya ni mbakaji,and am not happy with that.

 12. binti-mzuri Says:

  nyie vipi wewe?shuhuda toa pumba,fasta fasta

  nguza abaki jelaa..atolewe ili iweje na kwasababu zipi hasa?mnafanya mchezo with the law eeh?

 13. Muddy Omar Says:

  Binti Mzuri Tanzania ni nchi ya demokrasia huwezi kukataza mtu kutoa maoni yake,ao nenda kuishi katika Idd Amin Dada Land,kifungo cha maisha Tanzania ni kesi ya Uhaini,Ujambazi sugu n.k…kesi ya Nguza angefungwa kama Maumba…

 14. binti-mzuri Says:

  nasemaje..UMETUMWAAAAA .. hapa umegonga mwamba,nguza akiachiwa mie naenda kuandamana!

 15. DUNDA GALDEN Says:

  SOMA SHERIA KWANZA ALAFU UTOE MAONI SIO KUKULUPUKA TUUU,NA KILA MTU ANA HAKI YA KUTOA MAONI.BINT MZURI SIJU KAMA MZURI KWELI AU LAH LAKIN SAFI KWA KUJISIFU MWENYEWE ILA USISAHAU KILA MTU ANA UHURU WA AINA YOYOTE BILA KUVUNJA SHERIA AU UKIWA UNA UBIA NA BC BRITHERS HAPO SAWA ANDIKA UNACHOTAKA KWAO SAWA TUU
  NEVER CHANGER MY IDENTIT CHAFOSA

 16. Kisanola Says:

  Huyo anaye jipachika kivuli cha Binti Mzuri wala si binti wala mwanamke..Kina mama ni watu wenye huruma na busara sana.Nguza akifungwa maisha haitokusaidia chochote wewe punguani.Au wewe ndiye mmoja wa wahalifu na watoa rushwa wakubwa waliosababisha Nguza na wanae wafungwe maisha na sasa unaogopa akitoka CHA MOTO UTAKIONA?Sisi hapa tunajaribu kulinda heshima ya Taaluma ya Sheria.Kwamba it will go on record kwamba katika kesi kama ya Nguza mambo mengi ya kimsingi na ya ‘common sense’ tu hayakuzingatiwa.Kulikuwepo na msukumo wa nguvu za giza.Mimi ni mpenzi tu wa Muziki wa Nguza na mwanae Papi Kocha na ninashinikiza Nguza na wanae waachiwe siyo kwa sababu zozote zile bali ni kutokana na kuheshimu UTU NA UBINADAMU kwa kumwogopa Mungu.Matumizi mabaya ya madaraka katika Mahakama katika kutoa hukumu kwa watuhumiwa au waliothibitika kutenda makosa(hakuna kosa duniani lisilo sameheka) bila kuzingatia utu na haki (kwa kutambua udhaifu wa kibinadamu) ni DOSARI KUBWA inayo idhalilisha Taaluma Y Sheria kama Mhimili wa kutoa,kutenda na kulinda HAKI kwa wote bila ya kubagua. Kwa Mwenyezi Mungu hakuna Tajiri wala Masikini, hakuna Msomi au Mbumbumbu, hakuna Mweupe na Mweusi, hakuna Waziri au Rais, sisi sote tutakabiliwa na hukumu iliyo sawa bila ya upendeleo wala fitna! Kwa nini tutoe mfano mbaya kiasi hicho kwa wale watako kuja baada yetu.Wewe unaye jiita Binti Mzuri nimekufuatilia na sasa nimeshakujua wewe ni nani, maana kila mara nilipo andika kumtetea Nguza na Wanae wewe mwenyewe umejitokeza tena na tena kudhihaki jitihada hizo bila ya kuficha CHUKI ZAKO BINAFSI dhidi ya Mnyonge Nguza. Nakushauri fuatilia kesi ya Zombe na wenzake jinsi itakavyo kwenda mahakamani. Arobaini za Mwizi zipo ukingoni.Huwezi kushindana na Mungu wewe! Nakuhakikishia Nguza atatoka Jela muda si mrefu halafu nitakutafuta nikupe salamu zangu!

 17. binti-mzuri Says:

  kisanola WHAT ARE YOU TALKING ABOUT,nifatilie kesi ya zombe ili iweje?zombe ataozea jela and so will ngusa viking. wewe unajiona mtetea haki sio?nakuuliza swali moja tu: je mwanako wa kiume angekua amebabu seya na huyo ngusa viking,ana umri wa miaka 9 na amefanyiwa zaidi ya mara moja,isitoshe alikua anatoroshwa shule pale mapambano hahudhurii madarasa,anaenda kubabu seyiwa,ungejisikiaje kusikia huyo mtu ametoka?

  JAMANI.. tusisahau kwamba,hii ni historia kwenye jina la ngusa viking,ambayo labda hataipenda na ataijutia kwasababu limemchafulia jina lake,LAKINI kwa wale watoto na familia zao, HIKI NI KIDONDA WATAKACHOKAA NACHO MIAKA YOTE.kovu halitapona na wengine wanaweza athirika kisaikolojia..wasiweze kupata hata wapenzi au kuzaa. vitoto vilikua bikra vile,bikra yao imevunjwa na mbakaji. jamani jamani jamani. eti wanawake wana huruma,kwahiyo nimuhurmie hata mbakaji,jambazi au fisadi kisa mie mwanamke? atolewe,haki isitendeke eti kisa mie mwanamke? HUU NDIO UGANDAMIZAJI WA WANAWAKE kwanza nani kasema wanaume hawana huruma?kama wewe huna,its you as a person,usiongelee watu!- mie sisubirii salamu,nakupa zangu sasaivi NGUZA VIKING SHALL PERISH IN THE SUN- kampelekeeni machungwa na mananasi

  chafosa chai goda – binti mzuri inaweza kuwa mzuri wa tabia,mzuri wa maumbile au mzuri wa kuongea kwahiyo ‘MZURI’ doesnt specify where exactly am mzuri at.. so dont make conclusions please! na kwanza huna self-esteem wewe, sasa unataka nijiseme mbaya, i believe mimi mzuri,hata kama watu wataniona mbaya,because i got self-esteem

 18. Muddy Omar Says:

  Nampongeza sana Lister Elia kwa mafanikio yake makubwa.Bila shaka na wengine wote waliokuwemo katika Bendi ya Sambulumaa.Leo kupitia Blogu hii ningependa kuwachokoza wanablogu wenzangu kwamba ifike mahali Binadamu tumrejee Mwenyezi Mungu.Nawaomba nyote kuanzia leo hii tarehe 19/05/2008 tushikamane pamoja katika kumwomba Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete aingiwe na Moyo wa Huruma na hakika Malaika wa Mungu amshukie ili akisikie kilio chetu sisi Watanzania ambao tulithamini sana mchango wa Nwanamuziki NGUZA VIKING toka maika yote alipokuwa na Bendi ya Maquis hadi Balaa lilipomkuta yeye pamoja na Wanawe wote wakajikuta wakihukumiwa Kifungo cha Maisha kwa makosa ya kijinsia.Wanablogu wote tushikamane kumwomba Rais Kikwete amsamehe Nguza pamoja na Wanae wote ili wawe huru na warejee maisha yao ya awali na kumtumikia Mungu.Siyo tu kwamba adhabu ile ilikuwa KALI KUPITA KIASI lakini lazima niseme hapa kwamba Adhabu ya Kifungo cha Maisha ni adhabu inayostahili kwa makosa ambayo Mtuhumiwa hawezi kabisa kurekebishika na hivyo kuwa hatarishi kwa maisha ya binadamu wengine.Kosa la kijinsia ni kosa la kimaumbile ambalo mtu anaweza kabisa akabadilika na kurejea katika maisha ya kumcha Mungu.Akawa mtu tofauti kabisa na vile wengine watakavyofikiria .Makosa ya Uuaji(Murder cases/Serial Killers),Majambazi Sugu wanaotumia silaha,Mbakaji Sugu na Muuaji(Serial Rapist/Serial Killer),nk,haya ni baadhi ya makosa ambayo hata mfungwa akiachiwa huna uhakika naye kwamba hawezi kuyarudia tena.Lakini kwa makosa yaliyomkabili Viking Nguza na Wanae kwa hakika ni makosa ambayo mtu anaweza kurekebishika na kuyaacha kabisa na akarejea maisha yake ya kawaida na kuwa raia mwema kama wengine.Nalisema hili kwa uchungu nikielewa kwamba Nguza na Wanawe walihukumiwa na kufungwa maisha kama vile ni watoto yatima waliokosa mtetezi kabisa wa kuwasaidia.Nguza ana asili ya Congo DRC lakini ameishi kipindi kirefu sana hapa nchini na karibu watoto wake wote aliwazalia hapa hapa nchini kwa mwanamke wa kitanzania.Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa nathubutu kumhesabu Nguza na Wanae kama Watanzania kabisa wenye uchungu na nchi hii kama wewe na mimi na watanzania wote.Katika kazi yake ya muziki Nguza alitoa mchango mkubwa sana katika Uhamasishaji wa Jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Tanzania kuanzia mambo ya siasa na CCM hadi masuala ya kitamaduni.Amesaidia sana kuwainua vijana wengi wa kitanzania katika fani ya muziki.Katika kazi yake ya muziki Nguza alikuwa akipendwa na kila mtu.Wanawake wengi hupenda wanamuziki wenye majina makubwa.Vivyi hivyo Nguza nina hakika alikabiliwa na kipindi kigumu cha kuweza kuwakimbia wanawake wengi waliomzonga wakimtaka urafiki wa mapenzi.Hilo limewakabili wanamuziki wengi waliopata mafanikio makubwa katika fani ya muziki.Kiasi kwamba hata Nguza alipokuja kabiliwa na mashitaka yale yaliyomkuta hata akafungwa maisha kwa kweli sisi wapenzi wake wa muziki tuliekuwa naye karibu sana katika maisha yake yote jijini Dar es salaam tulishikwa na bumbuwazi tukishindwa kuamini yaliyo mtokea Nguza na Wanae.Lakini yaliyo tokea yalisha tokea hatuwezi kurudisha mkono wa saa nyuma.Kilicho baki ni kwa rehema zake Mwenyezi Mungu mimi binafsi namuomba Rais Kikwete atumie uwezo alionao na kutoa Msamaha kwa Nguza Viking pamoja na Wanawe warejee maisha yao ya uraiani.Ikiwa Mwenyezi Mungu anasamehe kila kosa binadamu alitendalo,basi na sisi hapa duniani tuchukue mfano huo wa Muumba wetu.Kile kitendo tu cha kumfunga mtu maisha ‘mbele ya Mwenyezi Mungu siyo haki,ni dhambi nyingine’.Mtu atafungwa maisha tu iwapo kosa lake HALIREKEBISHIKI au kuwepo kwa mtu huyo katika Jamii ni HATARI KWA WANAJAMII WENGINE KATIKA MAISHA YAO.Nguza hakuwa na historia ya ushenzi kiasi hicho.Hakuna Binadamu asiyetenda kosa.Adhabu ya Kifungo cha Maisha siyo kwa Nguza tu bali pamoja na Familia yake yote kwa kweli MBELE YA MACHO YA MWENYEZI MUNGU HAKIMPENDEZI HATA KIDOGO.Kupitia Blogu hii nawa asa wanablogu wenzangu tumtupie Rais Kikwete kilio hiki chetu sote,hatuwezi kumwacha Nguza yatima kama vile hakuwa na wapenzi na marafiki hapa Tanzania.Rais Kikwete atoe msamaha kwa Viking Nguza na wanae watoke nje na wawe watu huru,wao siyo tishio la amani hata kidogo.Ewe Mwenyezi Mungu pokea kilio chetu!Tutaendelea kuhesabu masaa,siku na miezi macho yetu yakielekezwa kwa Rais Kikwete kuhusu Msamaha huu!Sote katika nyakati tofauti tumemtendea Mungu Makosa lakini alitusamehe.Nasi tutende vivyo hivyo,kwa utukufu wake Mungu,Amina.

  Tarehe May 19, 2008 5:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Wanablogu

 19. binti-mzuri Says:

  halafu unaongea nini,eti hakimpendezi Mungu hata kidogo sasa ubakaji ndio unampendezesha? rejea KATEKISIMO,BIBLIA NA QURAN BEFORE WRITTING ‘NONSENSE’ REGARDING MAANDIKO YA MUNGU,KWANI HIYO NI MOJAWAPO YA DHAMBI PIA

 20. maryciana Says:

  mi siwezi mhukumu mtu duniani,ila huu mwimbo wa seya mbona haupigwi siku hizi BASATA vipi jamani?

 21. hombiz Says:

  mimi nimesikia kuwa Nguza Viking alikuwa anatembea na mke wa kigogo mmoja serikalini ambaye alikuwa anawania madaraka kabla ya kipindi kile cha uchaguzi. Sasa inasadikiwa kuwa Babu Seya alionywa kuwa aachane na huyo mke wa kigogo, lakini hakutaka kusikia. Habari za udaku zinazidi kupasha kuwa uhusiano wa Nguza na mke wa kigogo ulisababisha mtafaruku hata ktk familia na kupelekea ndoa kukaribia kuvunjia. Hapo udaku unapasha kigogo akaona anapelekea kupoteza mke na mali zake through taraka. Hapa ndipo kigogo akaamua kuchukua hatua za kumkomoa babu seya. Hivyo dodoso hizo zinadai kigogo akampikia babu seya bonge la kesi ambayo imemfanya aishie gerezani kwani system nzima ya polisi, mahakama na magereza inaendeshwa na hao vigogo ambao wote wanajuana and they work as a team!.
  Kama kweli babu Seya alitenda kosa alilokabiliwa nalo akiwa na wanawe, basi hukumu hiyo kwake mimi sioni kama ni mbaya na nitaungana na Binti-Mzuri. Ila kama kesho hiyo ni ya kubumba a.k.a Kubambikizia, basi hilo siwezi kukubaliana nalo kabisa. Kama alitembea na mke wa kigogo, hilo sio swala la kumkomoa na kumfunga maisha. Sababu huyo mwanamke inawezekana ni malaya na haiheshimu ndoa yake. Hivyo basi, kigogo angetakiwa ku-deal na mke wake na sio babu seya!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s