BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 20 May, 25, 2008

Filed under: Maisha,Photography/Picha — bongocelebrity @ 12:05 AM

Pichani ni wasanii wa Kikundi cha Splendid wakiigiza kama Mama mjamzito akiwa na watoto wake wakiwa wamekaa kwa masikitiko.Hii ilikuwa ni wakati wa shughuli za uzinduzi wa Kampeni ya Kukataa Kunyanyaswa Kwa Wanawake zilizofanyika jijini Dar-es-salaam jana.

Kama inavyoonekana pichani mama mjamzito amezungukwa na majukumu ya watoto wake bila kuwapo kwa mzazi mwenzake(mwanaume). Sasa ingawa waliopo pichani wanaigiza tu,hali halisi ndio hiyo katika jamii zetu.Single motherhood linazidi kuwa suala la kawaida katika jamii zetu.Nani wa kulaumiwa katika hili?Ni wanawake au wanaume? Jamii je?

Hii ndio picha yetu ya wiki na ni kwa hisani ya Athumani Hamisi.

Advertisements
 

3 Responses to “PICHA YA WIKI # 20”

 1. DUNDA GALDEN Says:

  Jana JK alibonyeza kingora kuashiria sasa mpambano umeanza kati ya wanaonyanyaswa na wanyanyasaji.kwei inasikitisha sana mwanamke kakatwa masikio na baba mkwe wake bila sababu yakinifu.mwengine kapigwa lungu la tumboni hali akiwa ana mjamzito kisa chapombe alivyoludi numbani kakuta ugali na mboga ya majani na hakuacha hata cent sijui alitaka kula nyama hatar sana,sasa kama umemuona ana maana hafai au changu kwanini usimuache na kumpa kipigo cha nguvu?uko bongo hswa mikoan tuachenhayo mambo jaman
  chafosa

 2. Jennas Says:

  Hawa watoto hakika ni wasanii nimebahatika kuhudhuria maonyesho yao mawili matatu wanayoalikwa wanafanya maajab kuleee
  Chakushangaza ni watoto wadogo walikuwa hawana msaada kielimu hadi kampuni fulani imejitolea kuwasomesha na kujihusisha na kila kitu.
  BC naomba ufanye mahojiano na hivyo vitoto viwili visichana please….

  Haya kwenye swala la unyanyasaji wa wamama sijalijulia adhabu yao me naona waweke kama mtu akikutwa ama kukabiliwa na shutuma yakumnyanyasa mwanamke basi achinjweeeeeeeeeeeeee
  Tumechoka kuachiwa mia mbili mezani ukikutwa ujapika unakula kichapo………

 3. Mkwaya Says:

  Nimesikitika sana kusikia hawa watoto hawakuwa na msaada kieleimu, siku zote nilizokuwa nawaona nilidhani wanasoma. kwa kweli natoa shukurani kwa hiyo kampuni iliyowasaidia hao watoto… na ninaamini hawatajuta maana hawa watoto wanakipaji cha pekee, wanahitaji kusapotiwa na serikali na makampuni wapate maonyesho zaidi ili waweze kujisupport kimaisha. Ila kwa kipaji walicho nacho wakipata na elimu Splendid litakuwa kundi la kihistoria kwa sababu naamini watoto wao wataishi maisha yao wakienzi kundi hilo ttena kiutalaamu zaidi.

  kwa watu wa blogs endeleeni kuwatangaza kote duniani wapate soko, watoto wanaburudisha sana wakubwa na wadogo. Wanapatikana kila jumapili pale kijiji cha makumbusho karibuni mfurahi pamoja nao.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s