BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ONYO KUTOKA BASATA June, 2, 2008

Filed under: Tangazo/Matangazo,Tanzania/Zanzibar,Uncategorized — bongocelebrity @ 10:39 AM

ONYO KUHUSU BAADHI YA BENDI KUWAONYESHA WANENGUAJI NUSU UCHI KATIKA MAJUKWAA YA MUZIKI.

Hivi karibuni Baraza la sanaa la Taifa(BASATA) limeshtushwa na kasi ya mmomonyoko wa maadili ya watanzania kwa baadhi ya bendi za muziki wa dansi nchini kutumia majukwaa ya dansi kwa makusudi kudhalilisha wanenguaji wa kike,kudhalilisha watazamaji na kuwaharibu watoto wadogo kwa baadhi ya wanenguaji wakiwa na vichupi na wanengfuaji kuonekana kuwa nusu utupu.

Baadhi ya wamiliki wa bendi wameiga tabia ya baadhi ya wanamuziki wa nchi jirani kwa kuonyesha wanenguaji nusu utupu.Tabia hiyo imechukuliwa kama biashara katika kumbi za maonyesho ya muziki na mbaya zaidi ni kwamba biashara hiyo haiishii hapo bali imewafikia watoto wadogo kwa kuona dhambi hiyo kupitia vyombo vya habar.Hayo tumethibitisha katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na watendaji wa Baraza kati ya tarehe 24/5/2008 hadi tarehe 1/6/2008.

BASATA linachukua fursa hii kuwaaasa wamiliki wa bendi zenye tabia hiyo kuacha mara moja na ikithibitika kuendelea kuvunja agizo hili,bendi hizo zitachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia kufanya maonyesho au kuzifutia usajili.

Aidha tunawaomba wamiliki wa vyombo vya habari kuacha kuwaunga mkono wadhalilishaji hawa kwa kutoonyesha au kuchapisha picha za wanenguaji waliovaa vichupi ili kulinda maadili yetu ya kutoharibu kizazi chetu ambacho hivi sasa kinaharibiwa kwa kuonyesha watoto mambo ambayo hawastahili kuyaona katika umri walio nao.

Ni nafasi hii pia tunawaomba wanenguaji wakike kuacha kutumika kama chombo katika biashara za watu kwa kudhalilishwa utu wa mwanamke.Aidha BASATA linawaomba wanaharakati wa haki za binadamu,wanaharakati wa masuala ya wanawakae kutokaa kimya katika suala hili,kwani maadili ya watanzania yanapobomolewa umma wa watanzania ndio unaoteketea.

Pia wadau wa muziki tunawaomba zikatae bendi zinazoonyesha vichupi na wasiositiri mwili wa mwanamke hadi watakapobadili tabia hizo,tukiweka tafakari kuwa,watazamaji wangejisikiaje kama binti zao na dada zao wangecheza na vichupi mbele yao.

Tunaamini kuwa biashara ya muziki itafana kwa kuwa ubora wa muziki wenyewe unaoambatana na uzingatiaji wa maadili (mila desturi)na kamwe vichupi havitaupamba muziki mbovu kuwa muziki bora.


D.Lauwo
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BASATA

2 JUNI,2008

Advertisements
 

14 Responses to “ONYO KUTOKA BASATA”

 1. kanjanja Says:

  Anza kwanza na TOT RESPECT bendi ya CCM! Akili zenu ziko kwenye NGONO tu basi mkiona mapaja ya mwanamke.

 2. BATTY JULIUS Says:

  BASATA,FUNGENI PIA MTV ISI ONEKANE TZ,SABABU AFRIKA YA LEO IMEVUTIWA NA WASANII KUTOKA MAREKANI,MITINDO YOTE UIGWA FROM MTV,AHSANTE BC

 3. trii Says:

  mi wananichanaganya tuu,sasa mkiwakataza wa hapo bongo na kwenye tv full vichupi tatizo litakuwa bado pale pale,maadili siku nyingi yalisha potea na tusiwasingizie wana muziki.usiku kwenye kumbi za starahe mtoto atafata nini?na watoto wa siku hz ndo wana jua mamno kuliko tunavyofikiri.

 4. binti-mzuri Says:

  haha ndo yale yale!

 5. Chris Says:

  Ukisikia unafiki ndo huo! Hapo mzizi wa tatizo haujatatuliwa. Kila sehemu imejaa wakware! Hata humo BASATA wakware wamo! Hivyo badala ya kuanza kutoa onyo kama hilo nafikiri kwanza ni muhimu kwa jamii nzima kubadili attitudes.

  Atitudes zikibadilika ni rahisi ku-cope na challenges kama za vichupi hivyo. Hainingilii kichwani kupiga marufuku wakati TVs bado zinaonyesha zaidi ya hivyo vichupi thru TV programs mbalimbali na maadili ya uvaaji mitaani inazidi “kupinda”.

  Binafsi naona its sthg that needs a holistic approach kati ya actors wote. Maana hilo onyo ni ka-part kadogo sana! Lakini inaonyesha ni jinsi gani tusivyo kuwa na sectoral coordination.

 6. Amina Says:

  waacheni watuoneshe mambo bwana nyie vipi

 7. maryciana Says:

  batty julius umeongea point saaaaanaaaa big up!

 8. michelle Says:

  Acheni kwanza ufisadi wa mali za nchi na vijisenti, bila hivyo vichupi havitakoma CCM oyeeeeeeeeeeeeee

 9. Jbigy Says:

  Kama wote mlivyosema hapo juu ni kweli kwamba tunajikanganya.Tutazuia ya kwenye maluninga na internet?
  Pia imefika wakati miwazo yetu tuiondoe kwenye ngono all the time. Mtu akivaa nguo fupi hata wakati wa joto tunamtolea mimacho as if hatujawahi kuona utupu!
  Tubadili mi-attitude yetu ili tusiishie ‘kutamani’ watu ovyo wakiwa na nguo ‘fupi’. nguo si tatizo, tatizo ni miwazo tuliyonayo kuhusu ngono.Mbona watu kibao wanavaa nguo ndefu lakini ukiwakuta angle huwezi amini? Mbona mimi niko huku nanihii naona kawaida watu wakivaa vichupi wakati wa summer na hamna anayetoa mimacho?kama ni maadili yashaporomoka kitaaambo tusisingizie wanenguaji wanapovaa nguo fupi.
  DU!

 10. matty Says:

  mh!sina la kusema leo yote yameshasemwa.

 11. Mama wa Kichagga Says:

  This man seems to lack technology and change awareness!

  Shame on him!

  Jamaa anaonekana butu sana labda akisafiri atapata awareness na atabadili mtizamo wake juu ya mavazi! Tena yaelekea hajawahi ona wanawake wakiwa mazoezini na vibukta maana nazani atapata kupooza mwili (stroke) kisa kaona mapaja.

  Hivi, mbona babu zetu na hata mabush men hawakuwa na mavazi? Kwa kuwa walikuwa na attitude njema wala katika jamii zao hapakuwa na matatizo ya ubakaji kama uliopo hivi sasa.

  “JAMANI TUBADILI FIKRA ZETU NA NAMNA YA KUFIKIRI. TUWE WABUNIFU WA MAENDELEO ZAIDI YA KUKALIA KUTOA MAONYO YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU”

  Lauwo umechemsha sana kaka yangu, I am sorry for that & I can’t back u up for this kind of stupid thinking!

 12. Chikala Says:

  HIVI HAO BASATA WANAOGA NA NGUO? KILA KITU KINA MAHALI PAKE.HIZO BENDI HAZIPIGI MAKANISANI WALA MISIKITINI.MWISHO WATAKAZA cONDOM ZISIUZWE MADUKANI.ACHENI USHAMBA.

 13. JMbigy Says:

  BASATA wamekosa la kufanya na wamechemsha kwa hili. Wahubiri change of attitude na sio kupangia watu kuvaa nguo.Mbona sisi wakurya wanawake walikuwa wanatembea matiti nje(mabinti) na bado walikuwa wakiolewa bikra!Tubadili mitazamo tuache miwazo ya ngono tuuuu na kutowezajizuia.

 14. hombiz Says:

  BASATA linatakiwa kushughulikia maswala muhimu kama HAKI MILIKI ambayo ndio muhimu zaidi kwa sasa ktk kuinyanyua sanaa ya BONGO.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s