BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

OBAMA AANDIKA HISTORIA MPYA MAREKANI! June, 3, 2008

Filed under: Breaking News,Special Interest News,Uncategorized,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 9:45 PM

Barack Hussein Obama ameandika historia mpya nchini Marekani. Anakuwa mmarekani mweusi wa kwanza kuwa mgombea rasmi wa urais kutoka katika mojawapo ya vyama vikuu vya kisiasa nchini Marekani.Bonyeza hapa kwa habari zaidi.

Advertisements
 

44 Responses to “OBAMA AANDIKA HISTORIA MPYA MAREKANI!”

 1. Majita Says:

  Siyo Barack Hussein Obama.Ni Barack Obama.Kwani ukilelewa na baba wa kambo unachukua na jina lake??mmh watu wa mama Clinton wanalia kweli sisi full shangwe.

 2. Ms Bennett Says:

  bravo obama, nimefurahi sana kusikia habari umeshinda.nakuombea ufanikiwe na utetee haki za ndugu zetu weusi huko, wamenyanyasika mno.Mungu ibariki Afrika, Marekani Amen.

 3. Ms Bennett Says:

  obama kwa tabasamu kama JK vile,mi nadhani wakiwekwa kwenye mashindano ya kutabasamu sijui nani atashinda.lol

 4. Bablii Says:

  Perfect…!

 5. changalamacho Says:

  Obama ana nafasi kubwa ya hata kumshinda Mac Cain mgombea toka chama cha Republican.Kwa kweli hii itakuwa historia kubwa kwa Wamarekani Weusi na Ushindi Mkubwa hata kwa Bara lenyewe la Afrika.Obama amedhihirisha uwezo mkubwa wa kushawishi na kuongea.Hakika ni mwenye kipaji cha kuhutubia watu wakazikubali hoja zake.Amekubalika kwa Wamarekani wote weupe na weusi bila ya kubagua.Tumwombee kwa Mola aweze kushinda.Akishinda uchaguzi na kuwa Rais wa Marekani Waafrika katika Bara la Afrika wasitegemee Mteremko kwamba sasa Afrika itapata upendeleo maalum kutoka Marekani madhali sasa Rais wa Marekani ni Mmarekani Mweusi.Kwa wenzetu kule ‘Urais wa Nchi’ ni Taasisi na siyo ‘mtu mmoja binafsi mwenye mamlaka yote,akisema kasema,akiamua kaamua’ kama ilivyo huku kwetu kwenye Katiba Mbovu isiyo kidhi demokrasia halisi.Lakini angalau ule msemo wa ‘Zimwi likujualo halikuli likakwisha’ pengine utafanya kazi iwapo Obama ataingia Ikulu ya Marekani hapo baada ya uchaguzi wa Novemba mwaka huu.Tuombe,Tusali, na Tutambike Obama ashinde ngazi zote za Uchaguzi ili amani irejee tena hapa ulimwenguni na kila mmoja wetu apate ahueni japo kidogo ya maisha bora zaidi.GOD BLESS!

 6. EdwinNdaki Says:

  nI HABARI NJEMA…hatimaye ndoto za watu maarufu waliopita imetimia.Martine luther..he had a dream..2pac aliamini kwenye changes..na aliamini angetokea siku moja mtu mweusi kutikisa anga za juu.

  Huu sio ushindi wa watu weusi tu la..bali ni ushindi wa binadamu dhidi ya wale wenye mawazo hasi kwamba mweusi hawezi.

  Kilicho baki ni duwaa kwa Obama aingie “MAGOGONI” ya Usa river.

  Bravo obama..ukipata muda njoo na wewe tutembelee huku geza ulole unawafuasi kibao

 7. Anon Says:

  Obama was born in Hawaii. His father was from Kenya, his mother was from Kansas who had moved to Honolulu with her parents. Kwahiyo Obama sio mmarekani mweusi bali ni mwafrika na kuna tofauti hapo kati ya wamarekani weusi na waafrika. Tujivunie kwamba amekuwa mwaafrika wa kwanza kuongoza dunia na sio marekani tu.

 8. matty Says:

  hongera du!Mrs Clinton now pumzika umechoka kampet mzee!vijana oyeeeeeeeee!

 9. binti-mzuri Says:

  EDO NDAKI U INSPIRE ME..i couldnt agree more.. huu ushindi sio wa Obama pekee, ni ushindi kwa mwafrika/mweusi yeyote na kwa yeyote ambae yuko kwenye position ambayo anaambiwa hawezi wakati anaweza. so for all you my fellow people out there, dont give up!

 10. MieBana Says:

  Obama akishanda amenisha kwa chama chake na watu wake wa america,hamna hatakachokufanyia mwafrika.Nchi zetu inabidi zijengwe na sisi wenyewe.tusije tegemea eti kwa kukaa tu kunasiku tutakuja kuwa sawa na ulaya au america.So ndugu yangu mwafrika hauitakia kupoteza muda kwa hilo,labda uwe tu shabiki kwasababu Msela ana kauafrika ndani yake,it`okey.But let spend our time with new Plan+strategy for new Tanzania

 11. baker Says:

  Duh ebwana weeeeeeeeeee! apo ni full yaani sasa ndio majamabo yanaiva. Big up sana mkuu BO, mWENYEZI AWE PAMOJA NA WEWE.
  CIAO

 12. Dumayai Says:

  sina hakika kama habari hii umeandika kwa kuwa unamshabikia Obama au ni kutojua ukweli, tafadhali fuatilia habari hiyo kwa umakini halafu usahihishe toleo lako. Obama hajashinda bado, ingawa ana nafasi kubwa ya kushinda. Ikiwa mama clinton atakubali kumuachia basi hapo ni habari nyingine lakini kama mama ataendelea na msimamo wake alionao hadi muda huu natuma haya maoni then Obama hajashinda. Mpaka sasa hakuna aliyefikisha idadi ya kura zinazotakiwa ili mtu awe mgombea kupitia chama cha wademokratiki.

 13. Tandamba Says:

  Dumayai,
  Mbona umeandika hiyo comment yako kwa jazba?BC wapo right kabisa.Obama keshashinda.Kama huamini basi kalagabaho.Namba za delegates alizokuwa anahitaji ni 2,118 na Obama so far keshapata 2,154 huku akiungwa mkono na the so called super delagates kibao.

  Hillary anachofanya hivi sasa ni mchezo wa kisiasa tu huku kila mtu mwenye kufuatilia haya mambo kwa makini(sio wewe Dumayai) anajua kwamba mama anataka apewe U-Vp.Kwani kama mama Clinton akisema hajitoi mbio zitaenda wapi?Wewe unafikiri Marekani ni bongo nini ambapo watu hawana heshima kwa sheria na taratibu nini?

  BC oyee ..naungana nanyi katika kumfagilia Barack Obama..go Obama wawawaaaaaaa

 14. JMbigy Says:

  Ni kweli kwamba ni faraja kwa ulimwengu wa watu weusi na wengine wote wanao’baguliwa’ duniani. Mzazi wake wa kiume alikuwa mkenya mwafrika mweusi kitu ambacho kitasaidia jitihada kudhihirisha kwamba hata weusi tunaweza.
  Hata hivyo kama alivyosema mmoja wetu hapo juu, usitegemee obama kwamba akiwa rais ndo atatufanya wengi wetu wa waafrika tuache ufisadi, ukabila, udanganyifu, kutofata sheria, udini, imani za kishirikina na kutopenda kazi….LA! Ni sisi wenyewe ndugu zanguni. Si Bush aliyetufanya tuwe tulivyo sasa! Ni sisi wenyewe nikiwemo na mimi.

 15. binti-mzuri Says:

  dumayai whats with the criticism?appreciate my friend..

 16. Amri Kamala Says:

  Naamini kwamba; pamoja na ushindi alioupata Obama, bado anamuhitaji Hillary ili Democratic waweze ku-secure kura nyingi wakati wakishindana na Mccain under Republican! I hope chama chao [ Democratic ] kitawajumuisha pamoja ili waweze kukubaliana na kutatua matatizo madogo waliyonayo kwa mda huu. Otherwise kura nyingi zinaweza kuchukuliwa na Maccain siku ya uchaguzi mkuu November, 2008. Tandamba! Nakubaliana na comments zako zote zinazohusiana na topic hii. Stay blessed!!

 17. aa mohammed Says:

  hafai huyu kidonge cha lami itakuwa jamatini kaingia golo kwa nini hatokei mzungu akampa shaba ama sivyo duniani hakutokalika

 18. Chris Says:

  BTW who cares? Huyu jamaa ametokea kuwa na kismati cha kupendwa na watu kama Kikwete! Aangalie asije boronga kama Kikwete! Weusi kokote pale wanampenda simply b’se he’s black! But what’s his foreign policy? Is the policy beneficial to you? Kukiwa na mgongano wa interest za bongo na USA, where will his interests lie? Obviously, the US interests will outweigh the other interest! That means he’s going to safeguard the interests of USA FIRST kama yoyote yule atakaechaaguliwa!

  Binafsi I dont care nani atakuwa Raisi, maana wote ni wamarekani na watasafeguard interest zao KWANZA. Meaning whoever will be the next president, we’ll keep depending on their crumbs. Kama walivyosema waarabu msitarajie jipya lolote kwa huyo jamaa maana Bush ashaandaa miongozo ya mbele yote!

  That’s my opinion and I stand to be corrected!

 19. Mzee wa Machale Says:

  Wasiwasi wangu ni kwamba wasije mtoa roho Mjaruo wa watu maana haya majamaa hayaaminiki hata kidogo lipokuja suala la mtu mweusi kuwatawala endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mkulu!.Tumuombee uzima!

 20. DUNDA GALDEN Says:

  HOME AGAIN.SAFI OBAMA LAKINI BADO KUNA KAZI NZITO KATIKA KAMBI YA G.BUSH LAKINI KWA HATUA ULIO FIKIA. ANGALAU WAAFRIKA NA BLACK AMERIKANS WATAJIVUNIA
  Chafosa wasijitele home again

 21. polisi Says:

  Nina furaha isoyo kifani kwa ajili ya ushindi wa daraja la kwanza.Isipokuwa haina maana kama ndio ameshakuwa raisi isipokuwa akikubali kumpa hillary unaibu raisi,itakuwa rahisi kwake kumshinda Mcain. kwasababu kutakuwa na uhakika wa wafuasi wa hillary kwa asilia 50 kumuunga Obama mkono na kumpa kura zao.Hapo mzee Mccain ataambukia patupu.
  Swali ni kwamba ” JE WAMAREKANI WATAKUBALI KUONGOZWA NA MTU MWEUSI” kwa ushauri wangu kwa obama,naona ni bora ajiongeze ulinzi kwani hao jamaa wenye urangi wanaweza kumpiga shaba,yani kama kuku.He should really take care.

 22. Chala Says:

  duh hapo sawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa am happy for Obama jamani na kweli mzee wa machale maana hawa watu hawatabiriki…. lakini inshaaallah kwa uwezo wa mwenyezi Mungu atafika tu.Maana M/Mungu akisema kitu kuwa basi hata binaadamu afanye nini kitakuwa tu.

 23. binti-mzuri Says:

  am in love with Obama!!

 24. Jirani Mdaku Says:

  we Miss Bannett, naona hiyo Hussein imekukera, na utakereka sana..jina lake ni Baraka Hussein Obama, utake usitake Obama ana damu ya Kiislamu kama alivyokuwa na damu ya Kiafrika, majina yake yamevunjwa vunjwa na kubasilishwa badilishwa huko Marekani lakini iwe isiwe baba yake ni Jaluo, Mkenya na muislamu….mama yake alikuwa anapenda kuolewa na Waislamu mara mkenya na mara Muindonesia…kama wewe unavyojiita miss. bennett kwani jina la kibant hilo, labda la babako alokulea, sasa na Obama hivyo hivyo.

 25. Amina Says:

  kwani obama ni nani?

 26. pyupyu Says:

  We polisi acha hizo,unataka kusema Obama alifika hapo kutokana na kura za watu weusi tu.

  McCain should be well prepared

 27. MAMII Says:

  Nadhani kitu cha kwanza obama atamleta bibi yake aliyeko kenya kijijini maana tumeona cnn kuwa anakoishi hamna hata umeme…Then wa kenya free visa to USA…Na mimi itabidi nihamie kenya,,,haahaa natania

 28. matty Says:

  Mh! LANGU JICHO!!!!!!!!Amina rafiki yangu huyu Obama ni Mr. Politician wa USA.

 29. matty Says:

  Binti Mzuri tukusaidieje???

 30. binti-mzuri Says:

  what is bloody wrong with people of this generation??WEWE JIRANI MDAKU what is the point of you bringing unrelated topics on this particular topic?unatka tu majibishano yasiyo na afya.what matters is not either obama is christian or muslim,what matters iis that he represents us black people as a whole.

  matty mme wa mtu huyoooo 😦 but i was referring to the song ‘obama girl’ sang, unaitwa am in love with obama.na ndio niliokua nimetoka kuusikiliza. its just amazing how much suport this man has in the USA. nina imani ikitendeka haki,he will get presidency

 31. JMbigy Says:

  Binti-mzuri kuna siku anaongea point nzito sana kama leo. She has really impressed me with her stand that what matters is not whether Obama is muslim or christian.
  Africa tumekuwa na udini na ukabila na makundi ya ajabuajabu ambavyo hadi leo sijaona matunda yake.
  Ila nilistuka Binti-mzuri aliposema “I am in love with Obama”. Kikawaida ilikuwa sahihi ila kama ni ile kumpenda kwa nanihii.. nilihofu kwani Obama keshaoa na ingem-Monica Lewinskyfy B-Mzuri. Ila nashkuru katatua utata wa “I am in love with Obama”.

 32. His real name is BARAKA OBAMA, but he did not know how to write it in Swahili even one day himself when he was talking about his Kenyan father he tranlated is name LUCK in English PAMOJA NA KUWA BARAKA SIDHANI NI LUCK IN ENGLISH, KWANI LUCK NI BAHATI. Jamaa ni ji mkali nimesoma kitabu chake leo ni cha moto wa kuotea mbali. Anaweza kushinda, kwa mimi kumuingiza H.CLINTON itakuwa kosa kubwa kwake kwa vile muda wote alikuwa aki-advocate CHANGE his winning buzz word, sasa itakuwa CHANGE gani hiyo akimchukuwa H.CLINTON back, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumrudisha mme wake pia Ikulu, sasa akina MacCain watamuuliza CHANGE gani hiyo ulikuwa unawadanganya watu kwa kuwarudusha wale wale wa zamani, ana kazi nzito lakini anaweza kushinda kirahisi sana kama atajipanga vizuri.

 33. matty Says:

  He!thanks Binti mzuri nimekupata tuko pamoja !!!!karibu huku!!!!!!!!!!!

 34. Matteo Says:

  Sio Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa kwanza kupata nafasi ya kugombania nafasi ya uraisi wa Marekali bali pia MJALUO wa kwanza kupata nafasi kubwa kama hiyo marekakani.

 35. Ed Says:

  Jina la baba yake ni Hussein, however Barack halitumii. There is nothing wrong to be hussein, ijapokuwa Barack hajawai kuwa exposed kwenye Islamic religion.

  Hope for America
  Obama 2008
  http://www.barackobama.com

 36. hombiz Says:

  Matteo, mwenye comment # 34 hapo juu, Barack Obama ni mmarekani mweusi wa kwanza kuwa Presidential Nominee wa Democratic Party nchini Marekani. Hakuna mmarekani mwingine mwenye asili ya Afrika aliyewahi kufikia hatua hiyo. The history has been made so far!
  Hayati Martin Luther King, Jr. aliwahi kutamka kwenye enthusiastic speach yake kwamba, nanukuu
  “I have a dream that one day this nation will rise up and live out the true meaning of its creed: “We hold these truths to be self-evident, that all men are created equal.”Mwisho wa kunukuu.
  GOD BLESS AMERICA and the WORLD at large.

 37. binti-mzuri Says:

  haha JMbigy nimecheka sana eti ‘ingem-monica lewinsky’ lol, thanx 4 making ma day man.

  mkwelele ilo nadhani linatokana na obama kuzaliwa na kukulia huko majuu.ila barack sio kiarabu hicho?japo tuna ‘baraka’ kwa kiswazi

 38. hombiz Says:

  Samahani kidogo. Mfupa hauna ulimi. Nilimaanisha kusema Barack Obama ni the First African American to be US Democratic presidential candidate, na sio nominee.

 39. hombiz Says:

  uuups! Excuse me The first Kenyan White American to be…. you know that i`m talkin` about..Ha-haaa!.

 40. binti-mzuri Says:

  hombiz: ‘GOD BLESS AMERICA’!?!?!?

  haha people dont be brain washed, just becoz Obama mweusi,haimaanishi ntashabikia marekani

  MUNGU IBARIKI TANZANIA,
  MUNGU IBARIKI AFRICA

 41. hombiz Says:

  Binti-mzuzuri acha hizo. Hapa tunaongelea USA, Tanzania inaingiaje?
  After all, hiyo Tanzania yako na Afrika vitabarikiwa vipi wakati viongozi wake wote ni mafisadi ya kutupa? You are the one who is brainwashed by being told that Tanzanians are peaceful people while the corrupt puppet leaders exploit the country’s wealth to the exorbitant level.They don`t care about you binti-mzuzuri.

 42. neema Says:

  Hongera Obama ,Haya ndugu zangu watu ulimwengu mzima umefurahi obama kufikia hapo.Msidhani ndiyo mwisho wa ubaguzi wa rangi no. hizo vitu vyote alivyohaidi vitakuwa hewa tu kama unavyoona hao politicien wanavyo ahidi kila siku ndiyo hivyo.Kila mtu anataka kula anavyoweza akipata chance anyway godbless America and Godbless Africa.
  Obama heee usitutie mchanga wa macho ?
  Only i ask you stop war Iraq and Afganstan remove your troop
  from there we tied to see blood…… We want to see money and
  gas price going down………..
  People they sufer downthere no food, no medical ?
  Forcus on that ?
  Peace

 43. maryciana Says:

  Obama! goodluck

 44. Ludana Ibrahim Says:

  Big up Wamarekani kwa kuonesha ni jinsi gani DEMOKRASIA yenu ilivyokomaa kwa kuweza kumchagua Baraka Obama kuwa RAIS WENU. BARAKA omba EKIMA kutoka kwa mwenyezi MUNGU .
  Rudisha amani mashariki yakati na wakumbuke waafrika ndio WAZAZI WAKO MUNGU AKUSAIDIE ni hayo tuuuuuuuuuuuuuuuuuu.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s