BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KANUMBA NA TUZO YA HESHIMA June, 4, 2008

Filed under: Filamu/Movie,Sinema,Swali kwa Jamii,Television,Tuzo — bongocelebrity @ 1:54 PM

Muite Steven Kanumba.Hapa ilikuwa wiki iliyopita wakati wa utoaji wa tuzo za Vinara wa filamu Tanzania. Waandaaji wa tuzo hizo walimpa Kanumba Tuzo ya Heshima kutokana na mchango wake katika maendeleo ya filamu nchini Tanzania.Kuna watu wanakubaliana na uamuzi huo wa waandaaji wa tuzo hizo na kuna ambao hawakubaliani wakisema kwamba ni mapema mno kwa Kanumba kupewa “tuzo ya heshima”.Wewe unasemaje?

Mwingine aliyepewa tuzo ya heshima ni Ngumbagwe Misayo au maarufu kama Thea.Ukitaka kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya na Steven Kanumba siku za nyuma,bonyeza hapa.

Photo/A.Mrisho

Advertisements
 

44 Responses to “KANUMBA NA TUZO YA HESHIMA”

 1. Chris Says:

  Hivi Mzee Jangala, Mzee Small, Mama Haambiliki, Majuto, Pwagu na Pwaguzi ( Pwagu najua ashakufa) lkn hao wote wameshakufa? Inamaana mchango wao hao watoa hizo tuzo hawakuuona? Na watoaji hizo zawadi enzi za udogo wao, walikua hawabanduki redioni wakati wa kipindi cha akina Jangala na hao wengine! Na utakuta hata huyo Kanumba labda kati ya hao mmoja wao ndiyo alomvutia kuingia hiyo sanaa. Labda criteria hatuzijui walizotumia. Ila binafsi hakustahili kbs! Ufisadi kila mahala umetawala!

  Tatizo nililoliona ni kwamba mpewa tuzo ni UNPROFESSIONAL na mtoa tuzo ni hivyo hivyo! Ushabiki tu na personal interest zimetumika! Na ninafikiri wameangalia zaidi hawa akina Kanumba wameanza wika time za luninga while wale walikua time za redio! Wa luninga wanajulikana sana cuz they’re noticeable mitaani kuliko wa enzi za redio. Proffesionals ilibidi wapewe hiyo kazi.

  Binafsi wameanza vibaya hizo tuzo zao. Doa hilo ni kubwa sana! Maana hata kama hao wakongwe walishakufa, tuzo wangepewa hata wanafamilia.

 2. Pearl Says:

  Chris mi nakuunga mkono tena sana tu,hili swala la tuzo za heshima mi sijakubaliana nalo and I am very sorry to say that,m nadhani it was suppose to go beyond kwasababu kuna hao watu walioanza muda mrefu kuigiza kama aliowataja ndugu chris hapo juu,kuna kina bishaga,waridi aisha,richie hawa pia walikua watu wa mwanzomwanzo kuonekana kwenye runinga,though walikua wanaigiza tamthilia lakini wameleta hamasa na mchango mkubwa sana,JAMANI HIVI KWELI WATU KAMA HAWA HAWAJACHANGIA LOLOTE KWENYE FANI HII YA UIGIZAJI!!!!????? NANI ALIKUA HAANGALII MAMBO HAYO THOSE DAYS!!!???

  Kuna wengine mbali na kanumba ambao pia walistahili tuzo ya heshima jamani.
  Halafu mi nadhani hili zoezi wangeweza hata kuwashirikisha wananchi hata ktk kupiga kura kwa sababu wananchi ndo wanaziangalia kazi za hao watu kwahiyo we are in the good position to judge,if at all we were involved at first place.

  All in all to me the heshima awards haijani-impress naona kama kuna mtu anafanyiwa promotion wkt haja-deserve.

  Mi ni hayo tu jamani.

 3. Juma Mpongo Says:

  Kwa mujibu wa maelezo ya waandaaji mimi naona ni sawa kumpa Kanumba, wamesema kuwa kwa 2007/2008… Sasa hao akina Jangala kwa mwaka huo uliolengwa na waandaaji wamefanya kitu gani? Tuache chuki binafsi jamani, Kanumba amefanya mengi katika filamu kwa kipindi hicho kilichotajwa na waandaaji, tuache Kasumba ya kuon a wazee pekee wakipewa tuzo za heshima, yaani ni kama kusubiri mtu afe ndo umsifu alikuwa mwema! Hongera waandaaji!

 4. Amina Says:

  Chris umemaliza kila kitu nilichotaka kusema…asante sana!nawewe kanumba tuoneshe ile tuzo yako ya hollywood ipo wapi?

 5. blaggada Says:

  tatizo ufisadi umeenea kila mahali ona sasa yaani mnawaacha wakonge kina mzee small,majuto,bi chau mnawapa kinakanumba waj uzi au mmesahaun mambo yao nini ac heni izo kaeni chini mfikilie kabla ya kutoa tunzo hizo

 6. mimi Says:

  sijapenda mkao wake

  well jamaa anakipaji ktk kuigiza ila ningependa kumsahuri aachane kabisa na habari ya kuimba maana anasauti mbaya sana

 7. Jennas Says:

  Chris umenibamba mana nilivyoanza kusoma hoja yako nilivyoona kuna marehemu katika listi yako nilipania kukuambia hata wanandugu napewe tuzo wawekewe ndani ama hata kwenye kaburi lake kwa kazi aliyoifanya akiwa hai.

  Pili me cjaona kazi kubwa sana waliyoifanya hadi kupewa hizo tuzo mana hata kama ni za wachanga basi kuna wakongwe zaidi ya kanumba kama kina bishanga na kina waridi cjui ambao ndiyo walianza mwanzo mwanzo
  Ila kama nikuwapokonya basi ningekuwa wa kwanza kwenda kuwapokonya niwakabidhi watu wazima na cyo wauza sura mnawalewesha misifa mapema hawa wauza sura, hawa wasanii wanaochipukia ndiyo maana hawaachi madharau kwa wakongwe wa filamu.
  Kwanza sifatiliagi hizo filamu zao ngoja tu ninyamaze zangu…..La muja de la vida………..

  Hivi mzee pwagu amekufa ama ni mama hambiliki ndiyo alikufaga?

 8. Paka la jikonil Says:

  Kiufupi hawa watoa tunzo hawajui watendalo wamepotea katika njia ya uwokovu wa sanaa na walegee na washindwe. hivi huyu Kanumba amechangia nini katika sanaa ya filamu Tanzania ?. hawajawaona kina mzee Small , majuto ambao wapo hai wangetoa tunzo hiyo hata kwa familia ya mzee
  jongo ili kumuenzi wangeona haifai basi wangempa hata
  Bishanga ingetosha .kwa mpango huu tutafika kweli ?.
  mdau Paka la jikoni-uk

 9. Pearl Says:

  Juma Mpongo ni hivi mwaka huu ila sikumbuki ni mwezi gani ila FIFA ilikua inatoa tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora aliyechangia ktk fani ya michezo 2007/2008 unajua nani ndo alipokea!!! ilikua ni “PELE”.
  Sasa kwani PELE bado anacheza mpira!!?.Hiyo sasa ndo tuzo ya heshima,kwavile hii tuzo ya waigizaji ndo inaanza nchini kwetu it was proper to recognize hata waigizaji wa zamani kwa kuthamini mchango wao ktk fani hii.

  Mi ni hayo tu.

 10. Catherine Says:

  Namuunga mkono ndugu yangu juma,acheni chuki nyie wote ni watanzania,hao watu wa zamani walikua na filamu au tamthiliya?nafikiri hizo tuzo zilikua za filam na siyo tamthiliya,na vigezo walivyotoa inampasa kanumba kupewa tuzo kwani ameitangaza Tz kwa kiasi flani naamini ataitangaza zaidi kwani bado ana nafasi kubwa tu,kubalini mabadiliko watanzania muungeni mkono,sidhani km majumbani mwenu mnaangaliaga kazi za hao mnaowasema.

 11. matty Says:

  Hata kama ni ustar nywele nazo zinakalikiti au??samahani kama nakuingilia maungoni.
  Chris Mtani wangu unapatikana wapi maana kichwa kimetulia ile mbaya umemaliza everything kwakweli!

 12. Chris umemaliza kila kitu mtu wangu sina la kuongeza

 13. Kamanzi Says:

  Ndugu Juma Mpongo hata kama walihusisha 2007/8 pekee mi bado nadhani akina Kingwendu wapo more relevant kwa jamii ya kitanzania kuliko warembo kama Kanumba.

  Wanaudhi sana hawa watu, yaani utakuta filamu imejaa kizaramo lakini inaitwa kwa ‘kidhungu’ eti Copy, Fake Pastors, Stranger n.k. Kama iko kidhungu mwakimanya kwanini msikitumie moja kwa moja?

  Kwanza wana recycle filamu za kinigeria tu hawana lolote. Mafisani wa kisanii hawa hakuna namna nyingine ya kuwaelezea. Nalaza kesi yangu mpaka hapo.

 14. Dullah Says:

  Mi nadhani tuzo imetolewa katika tasnia ya filamu na katika mwaka 2007/08. hapo ni sawa kukataa kumpa tuzo ricardo Kaka ya 2007/08 eti kwa kuwa pele alicheza vizuri kipindi hicho.
  Mi naona tatizo ni la waandaaji kwani ilibidi kuweka kategori ya watu hao kina mjee jongo ya mfano…!
  N sidhani kuwa Kanumba aliwapangia wamuandalie kategory ili ashinde. Big up kanumba, ukipendeza muuza sura! mbona sasa unafanikiwa? Acheni mipasho nyie kama vipi mkajiunge na Jahazi, TOT au hat watoto wa kandoro wanahitaji vipaji vyenu!

 15. pyupyu Says:

  Nafikiri kigezo kikubwa walichotumia hapa ni kuona nani kawika zaidi kipindi hii cha luninga kama alivyo sema Chris!
  Pia ni mara ngapi huyo mhusika ametokea kwenye hizo filamu sabini na mbili walizo zikusanya.

  Basi kama ni hivi haitaleta maana kwa mana ni wengi watajitahidi kutokea kwenye filamu ama kujitanga zaidi hata kwa njia zisizo sahihi ilimradi waonekane,mwisho wa siku waonekane wana mchango mkubwa sana kwenye hii sanaa.

  Labda hatuelewi walikuwa wanamaanisha nini haswa walipokuwa wanasema tuzo ya heshima.

  Watufafanulie ni vigezo gani wanavyotumia kumpatia mtu tuzo ya heshima.

  Waliofariki ni mzee Jongo,Bi Hambiliki,mzee Pwaguzi na Mzee Keto kama sikosei.

 16. JBigy Says:

  kama walivyosema chris,paka la jikoni, n.k., Bongo usanii, uongo, unprofessionalism na ubabaishaji havitaisha. Pia filamu nyingi nilizoziona wana’desa’ toka Nigeria na west na hivyo hata ham ya kuziangalia haipo kabisa. Bora waigizaji wa zamani na wachekeshaji ambao wanaonesha mambo ya jamii ya TZ. Watu kama jongo(marehemu), waigizaji wa mambo hayo, na vikundi vingine haijawahi kutokea kupewa tuzo kwa mchango wao. Leo hii hizi ‘movie’ za kukopy toka Nigeria na kwingineko zinaonekana bab kubwa. Mimi ntaendelea kucheki za Original(toka Nigeria na west) hadi hapo watakapotoa vitu vinavyoakisi mazingira ya nchi ya Tanzania.
  UFISADI ni Donda ndugu.

 17. cecy Says:

  duh i respect mtoaji maoni wa kwanza
  big up!!!!cant say much bali kukuunga na maoni yako
  its true ukizungumzia sanaa za maigizo lazima
  uzungumzie hao watu

 18. Cris, I respect you comments. Thank you!

 19. Amina Says:

  duh..chris kawa supastaa humu leo!hatari..matty upo wapi?

 20. annie Says:

  Jamani nadhani hajaelewa hiyo tuzo ya heshima kapewa vp
  ila kifupi alistahili kupata hiyo tuzo,
  maana wamesema hiyo tuzo wanatoa kwa mwaka 2007/2008 waliofanya vizuri
  sasa wangempa jangala mwaka 2007/2008 kafanya lipi jamani???
  lkn ingekuwa miaka ileeeeeeeee labda…

 21. Chris Says:

  Amina LMAO! Lakini wanaosema tuzo ni za 2007/2008 nawashangaa! Ndo maana Kanumba na Thea hawakuwemo in either of the lists! Na wamepewa tuzo ya heshima kwa mchango wao wa fani husika, na si kwa mwaka 2007/08! Swali la kujiuliza inamaana mchango wao unazidi hao wakongwe?

 22. mtukwao Says:

  jamani tusiige kila kitu bila kujua maana or what is the history/story behind it!!

  Watanzania tupendane na tuelezane ukweli si tu ktk siasa bali hata katika mwonekano wetu sisi wenyewe ktk macho ya watu.
  mie nikitaka kumjaji kwa kutumia hiyo picha na ukilinganisha na tunzo aliyopata haviendani kabisa!!!

  hilo pozi haonyeshi kama ni mwingizaji bali anaonekana kama ni model wa mavazi!nakama ni muigiaji then he looks unproffessional actor!!

  pili mapozi la simu mh!! labda kama ulikuwa unapromote tigo!! which I doubt!! anaonekana mwoga wa camera with low self-esteem.
  Then wabongo tujitahidi kuvaa simple but smart/ sexy!!!!!!!!! mavazi mengine ni vurungu machoni pa watu hata kama ni mazuri!!!!!!!!!!!!hayo ni yangu kwa leo.

 23. JMbigy Says:

  mtu kwao umeongea nlotaka kuongea.nashkuru.
  Pia tulishaamini kwamba ili kitu kiwe right basi tufate wanachofanya mataifa ya magharibi. Mi nahisi ndo chanzo cha mavazi ya Kanumba. Otherwise basi anatangaza mavazi. Tatizo letu hatujui kuwa ‘simple’ but clean and ‘sexy’ kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu.
  Hata hivyo nampa hongera Kanumba kwa kuigiza.

 24. matty Says:

  Amina nipo mtu wangu, nashukuru umelitambua hilo sasa itabidi tufanye kafunction kafupi kakumpongeza Chris humu ndani kwa point zake nzuri, jamani hata shule mtu akiwa wa kwanza kwenye mtihani si kuna kautaratibu kakumpongeza???au makofi kidogo nk.
  Amina hii parrrrrtyyyy itafanyikia kwa Dan pale Darajan na mweka hazina ni wewe, Edwin Ndaki atakuwa mlangoni maana ni mtu wa miraba 4, mimi na Kekuu tutakuwa wasambaza mitungi (ulanzi), binti mzuri atakuwa anakaribisha wageni tetetetetetet!
  Chris unasemaje mtani wangu juu ya hili wazo??????
  Gervas uko wapi???

 25. Chris Says:

  Infwakti Matty Kokubanza hilo litakua wazo zuri sana! Kuna vituko sana humu BC! Aiseeee sema itakua lini! Unajua Matty kuna akina Amina, sasa yule Amina mpya ndo awe mgeni rasmi! Hahahahaaaaa!

 26. rose Says:

  tuache utani jamani kanumba ni handsome bwana,kama ningepata bahati ya kuwa karibu nae.sijui?ila kinachonishangaza ni kwanini ni mpole sana?mara kibao anaandikwa ktk vyombo vya habari lakini hasemi chochote ina maana hasikii au?hongera kwa tuzo ya heshima hakika wewe ni nembo ya film tanzania, i love u….rose..mikocheni.

 27. poty Says:

  Yuko busy kaka wa watu hana mda huo nimewai kupishana nae street za posta akiwa ktk gari lake yaaani full tinted na yeye aliposhuka kavaa miwani watu kibao wakimshangilia akiwapungia mkono huku akiingia ktk duka la nguo ila nimegundua kitu rose kwa kanumba ana aibu sana ndio maana huwa ni mtu wa kujificha ficha nampa big up kwa ma movie yake ni noma hasa hili la point of no return alilopiga na wema sepetu hakika anastahili tuzo ya heshima.

 28. LOMY Says:

  HONGERA STEVEN KANUMBA NO MATTER WHAT U RE A WINNER.

 29. cute Says:

  i love uuuuuuuuuuuu kanumba………congrats

 30. Amina Says:

  hata mi nilitaka kusema hilo suti..na micheni famba ya nini..mwe

 31. matty Says:

  Mh!Chris umesema hapa kuna kina Amina wangapi?maana mimi sikuwepo kipindi fulani kileeeeeeeeeeee mimi niliyemzoea ni AMINA ORIGINAL wa tokea kile kipindi kileeeeeeeeee
  haya hii party itakuwa mwisho wa mwaka tukijaaliwa inshaalah!

 32. binti-mzuri Says:

  haha mtu kwao nimecheka.. umeongea pointi

  matty – wageni hawatapungua kama ndo ivo!

 33. neema Says:

  You look good hommi ? Next time dont sit like that ? And i dont want to hear you somebody………………
  Its me hommie………
  Peace

 34. Amina Says:

  Matty mi ndo Amina original humu,kwani huyo mwingine katokea wapi?hebu ajisalimishe haraka

 35. kekue Says:

  Matty umejichagulia kwenye usambazaji mitungi??? ninajua sababu, tehe tehe!!!!!!

 36. matty Says:

  hahahahahahaha Amina Chris huyo anasema kuna kina Amina mimi nikajua may be wapo wengi lakini all in all mimi nakujua wewe original…tuko pamoja mtu wangu!
  Kekuu we haya unajua nini sasa???kwani sector ya mitungi sio nzuri???

 37. Catherine Says:

  Jamani warembo taratibu na Kanumba wa watu huyo mtachapwa,shauri zenu,comment zisivuke mipaka tafadhali.Haya gold zenu ziko wapi nyie mnaosema anavaa mafamba?punguzeni majungu midomo mirefu km nywele za kibrasil,nyie hayo mabati yenu hamuyaoni?na mtapata tetenas soon nawaambieni.

 38. maryciana Says:

  amina wewe si ndio amina yusuf aka gal power auu??? hahahahahaahhaha

 39. masumbuka Says:

  Kwasababu suala la utoaji TUZO ZA FILAMU hapa nchini linaonekana kuwa suala geni ni vyema na busara kwa Waandaaji wa Tamasha hilo kubuni utaratibu utakao wawezesha waigizaji wote wa zamani waliojitokeza kuwa mashuhuri na kupata sifa kubwa katika kuiendeleza fani hiyo hapa nchini watambulike rasmi kwa mchango wao kitaifa kwa kupewa Tuzo Maalum kila mmoja kwa mchango wake ili hata utoaji huo wa Tuzo hizo katika miaka ya mbele utakapo fanyika ‘ kile kiporo cha kuwa na kundi la waanzilishi wa fani hiyo hapa nchini kutotambulika kitaifa na kupewa heshima yao kwa kupewa Tuzo za Kitaifa kitafutika na dosari hiyo haitakuwepo tena’. Nawatakia mafanikio mema. Kanumba ni Muigizaji mzuri na amejitahidi vya kutosha katika kuwajibika katika fani yake. Kumpa Tuzo ni kumtia hamasa zaidi ili afanye bora zaidi na kwa wenzake nao pia wawajibike zaidi.

 40. Matty Says:

  Kwako Catherine,
  Usizuie watu kutoa mitazamo yao humu sawa?kila mmoja anaomtazamo wake katika picha inayowekwa hapa kumbuka picha moja maana elfu sasa sioni sababu ya wewe kutuambia tunamidomo mirefu how??wewe wakwako mfupi?si unyamaze?hakuna anayebabaika na huyo muigizaji hapo juu watu wanasema kile wanachokiona!

 41. XXX Says:

  tuzo ya heshima wanapewa wazee walioanza hizi ishu sio mtoto wa juzi kanumba na thea walibidi wapewe wa zamani na hao waliotangulia mbele za haki wangepokelewa hata na ndugu zao..namuunga mkona cris kwa asilimia 100% pia mdau aliehoji mbona pele anaendeleaga kupewa tuzo mpaka leo?

  Kanumba muongo na hiyo tuzo ya holiwood yake kama ingekuwa kweli wabongo na misifa yao angeishai advertise magazeti yote tungeiona…

 42. Amina Says:

  we bc bana tu

 43. binti-mzuri Says:

  catherine u came out a bit harsh!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s