BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

Queen Kase/Msondo Ngoma June, 5, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Swali kwa Jamii,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:46 PM

Haya tena.Wikiendi nyingine imewadia. Kwa wengine ni wakati wa kujongea kiti kirefu na kupata moja moto, moja baridi. Kwa wengine ni wakati wa mapumziko.Kwa wengine ni wakati wa ibada,wakati wa toba.Kwa wengine ni kazi kama kawaida.Kumbuka kwamba kutafuta kazi pia ni kazi!Dunia ndivyo ilivyo.

Piga picha hii.Kaka yako ameaga dunia.Kutokana na mila au taratibu za kifamilia, unatakiwa kurithi mke wa kaka yako.Zaidi ya yote wazazi wako ndio wanakuomba ufanye hivyo. Wanakupa sababu kibao zikiwemo kwamba familia “isiende mbali” nk.Watoto wa kaka yako wanahitaji “father figure”.Ili mradi tu, sababu chungu mbovu.

Unasita,unatoa sababu zako kibao.Kwanza unaanza na ile inayotegemewa na wengi.Unawaambia wazazi mambo ya kurithishana wake yamepitwa na wakati.Siku hizi kwanza kuna maradhi na isitoshe unathamini kwenye ndoa itokanayo na penzi na si vinginevyo.Lakini kumbe sababu hasa ni kwamba unaye mpenzi wako umpendaye.Unaye malikia au barafu wa moyo wako.Mwenyewe unamuita Queen Kase.Kichwa kinakuuma, ufanyeje? Hebu toa msaada kidogo ndugu msomaji.Ungelikuwa wewe ungefanyaje?

Ujumbe huo umo katika burudani yetu ya leo.Wimbo unaitwa Queen Kase kutoka kwa Msondo Ngoma. Bonyeza player hapo chini uusikilize. Tunakutakia wikiendi njema.

Advertisements
 

11 Responses to “Queen Kase/Msondo Ngoma”

 1. EdwinNdaki Says:

  swadaktaaa..ni ijumaa nyingine tena.

  Hakina Sauti ya TX MOSHI bado tutaikumbuka.

  Msondo kweli baba ya muziki.

  RIP… Moshi TX william

  wadau nawatakia ijumaa njema wakati tukiserebuka kuhusu Obama..nyota njema..Huonekana asubuhi..

  pokeeni salamu kibao kutoka huku Geza ulole

 2. DUNDA GALDEN Says:

  WAZAZI WAKITAKA LAO.NA MILA ZETU ZA KIBANTU UNA SABABU WATAKAOKUSIKILIZA.SASA IKIWA BROTHER KAFA NA NGOMA ITAKUWAJE.AFADHALI WAZAZI WA SASA BAADH YAO
  WANAKWENDA NA NYAKATI
  BC SAFI KWA KUPUNGUZA MAKALI YA SAKNA MITT LAND
  Chaii goda

 3. Kisu kikali Says:

  Hiii!!!wazee wa BC ! big up!
  hapa lazima tukubali kuwa MSONDO NI BABA LAO!
  na ni baba ya mziki afrika mashariki,lazima tujivunie
  baba la mziki

 4. Zemu Says:

  BC :Msondo ni bomba.
  Kuhusu kurithi kwa hilo kwa kweli nawapa laivu wazee kwamba haiwezekani na lolote na liwe.Issue hapo ni kuwapa shule ya nguvu bila kufichaficha kuhusu athari za kurithi.Najua watakomaa lakn nami nitakomaa kwa kudadavua mambo kwa makini.

 5. Malenga Says:

  Asante BC. Mambo ya ndoa mazito sana hayawezi kuelezeka kifupi.Pia ndoa zina mengi..Sasa ukirithi ndoa ya kaka yako(Sijui km mila hizo zipo bado)Lakini ujue utarithi na yaliyokuwamo ktk ndoa hiyo…Kwa wengine ni furaha kwasababu hutatoa mahali tena ukizingatia sasa hivi unatozwa mpaka mpaka mkaja wa Shoga!!!!(Utani)..Lakini kubwa nile shemeji(zamani)sasahivi mkea apokuchojolea nguo na kukufanya uwe huru na vile vilivyokufanya umuite Shemeji? Naona hapo kamtihani kidogo…Sijui kimaongezi akikuambia kaka yako alikuwa hamfikishi…utajisikiaje?Kwamba kakukumbusha msiba au utaona ni heri ungeanza kuiba toka kaka yupo hai?? Haa haa kweli maisha kitendawili kila mtu anamajibu tofauti…Huko ndiko kulala handigwa handigwa!!

 6. EZEKIEL N M Says:

  ALOO! HIZO MILA ZA KIZAMZNI ZISHINDWE KABISA NA ZIREGEE. KWELI MSONDO NI BABA LAO

 7. Msondo hawachuji,hawaboi,hawachoshi kusikiliza.Msondo baba lao.
  Edo kibindi vipi?

 8. usinijue Says:

  Unajua kitu kimoja nyimbo za zamani hachuji kutokana na ujumbe wasanii walikua wanazichungulia jamii zinamatatizogani then wanaelimisha,unapata burudani na ujumbe juu…………sio watu kujiita wazee wapamba,sijui mzee wafarasi ujumbe kwenye muziki wanaotupa ni majisifu kwenda mbele so kile unachojisifu leo kesho hakina mpango na wimbo unachuja,lakini cheki nyimbo za marijani mzee darasa tosha,mfano wosia wa baba,masudi na nyingine nyingi mwaka wowote ukizisikiliza ujumbe wake unakwenda na wakati…………..big up bc tupeni burdani

 9. EdwinNdaki Says:

  Ndabagoye..tupo kaka tunajicelebrisha hapa kwenye uwanja wetu.

  nitakuja kukutembelea home kwako maana nina siku kibao sijafika mitaa hiyo.

  Mimi mwenyewe kwangu nimeama nimeamia mtaa wa 7 kama alivyosema Mwishehe Mbaraka.

 10. kapisi Says:

  hapa lilipo hili basi ni mitaa ya ilala kama sikosei.

 11. Wakuu heshima mbele sana, Msondo Ngoma kweli ni afya yaaani wakulu muziki wa kiutu uzima huu, heshima wka kina Zahoro Bangwe, Mabere, Masharubu, Kamanda Gurumo, na George Bush Mnyali.

  Na heshima zangu za dhati na moyoni kwa Mkulu wangu Marehemu TX Moshi, toka Polisi Jazz hadi Msondo Kita Kita, salaam kwa wakulu wote wa Msondo Ngoma.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s