BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HAPPY FATHER’S DAY June, 15, 2008

Filed under: Burudani,Maisha,Sikukuu,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:52 AM

Leo ni siku ya kina baba.Kwa kutumia ile lugha ya malikia,tunaweza kusema Today is Father’s Day! Ni siku maalumu ya kumkumbuka baba yako,awe hai au awe alishaaga dunia. Ni siku ya kukumbushana upendo,amani na kutakiana mafanikio mema baina yako na mzazi wako.Kama kumetokea kutokuelewana kati yenu,basi siku hii inaweza tumika kama fursa nzuri ya kurekebisha mambo.

Bila shaka tunakubaliana kwamba kama ilivyo kwa mama,bila baba hakuna mtoto.Kwa maana hiyo mchango wa baba na mama katika malezi ni jambo muhimu.Kinachohitajika ni kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Kuisindikiza siku hii,sikiliza kwa makini Wosia huu mzito kutoka kwa Baba kwa kubonyeza player hapo chini.Kisha zingatia yasemwayo katika wimbo huo.Happy Father’s Day.

Advertisements
 

14 Responses to “HAPPY FATHER’S DAY”

 1. Chris Says:

  I like the song! But honestly sikujua kama na sisi ma-faza tunasiku yetu!

 2. Ladslaus Modestus Says:

  Mwanangu, yasikie mafundisho ya Baba yako, wala usiiache sheria ya Mama yako, Maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, na mikufu shingoni mwako (Mithali 1:8,9).

  Baba yangu Mpendwa Modest Msanya, ilimpendeza Mungu kukutanguliza mbele ya haki hapo siku ya Alhamisi tarehe 4 Agosti 2005.
  Mama yetu mpendwa Felista (mke wako), Sisi wanao pamoja na Wajukuu tulikupenda sana lakini aliyekuumba alikupenda zaidi.
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe Amen (Ayubu 1:21).

  Baba wewe ukishirikiana na Mama ndio Chimbuko la Elimu yetu.
  Baba wewe ukishirikiana na Mama ndio Chimbuko la Utajiri wetu.
  Baba wewe ukishirikiana na Mama ndio Chimbuko la Maendeleo yetu.
  Baba wewe ukishirikiana na Mama ndio Chimbuko la Jinsi tulivyo siku ya leo.

  RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE, ASTAREHE KWA AMANI. AMINA.

 3. DUNDA GALDEN Says:

  SONGI BABU KUBWA USIA WA NGUVU HAKIKA BABA TUTAFUATA USIA WAKO KWELI UZEE UMEKUFIKA BILA KWENDA KWA MJUMBE WALA MAHAKAMANI

 4. hombiz Says:

  najisikia furaha sana kumtunza baba yangu kwa kadri ya uwezo wangu. Ni nani kama baba!?
  Ladslaus Modestus, pole sana kwa kuondokewa na wazazi. Natumaini huko waliko wanayasimamia maisha yako. Cha muhimu kufanya ni kuwakumbuka kwa sala na kuweka kumbukumbu zao hai.

 5. binti-mzuri Says:

  chris ujumbe wako huo!BECAUSE ULINICONTRADICT ONCE ABOUT THIS!

 6. Chris Says:

  What contradiction Binti-mzuri?

 7. Ladslaus Modestus Says:

  Hombiz asante sana kwa kunipa pole;
  Isipokuwa kama nilivyoandika, Mama yangu Feslista bado yu hai (anadunda), isipokuwa Baba yangu Modest Msanya ndie alishatutangulia mbele ya haki. (Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe, Amen).

 8. Matty Says:

  Nothing than Dad!

 9. Matty Says:

  RIP my lovely dad! & all dad who passed away!may almight God rest their soul in eternal place AMEN.

 10. any Says:

  happy fathers day japo nimechelewa kuiona hii.
  Ila kwa wale wanaume waliobaka ndo watoto wakazaliwa, wanaotelekeza watoto, abusers like wanaowataka binti zao kimapenzi, wanaowaingilia watoto wao kiume kinyume nyume, hao wasipongezwe wao wapelekwe jela na au wanyongwe hadi wafe.
  THE REST HAPPY FATHERS DAY YOU DESERVE THIS.

 11. hombiz Says:

  Asante kwa kunikosoa Ladslaus Modestus. Namtakia maisha marefu yenye fanaka mama Feslista .
  peace

 12. binti-mzuri Says:

  chris naongelea ile post ya mothers day. there was some negativity there,lakini naamini yameisha now that you have fathers day too 🙂 .

  r.i.p to my dad… he was the coolest dad alive.

 13. kahindi Says:

  R.I.P.my lovely dad…u left us many years ago..we miss u sanaa baba.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s