BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WAMAREKANI NI WAJINGA? June, 17, 2008

Filed under: Comedy/Vichekesho — bongocelebrity @ 10:30 AM

Ushawahi kusikia mtu akikuambia kwamba Wamarekani huenda ndio wanaongoza kwa “ujinga/umbumbumbu” duniani kote? Inasemekana wamarekani wengi hawajui hata kwamba duniani kuna nchi zingine,mila zingine nk.Pia inasemekana kwamba baadhi yao mahali wanapopajua ni hapo hapo walipozaliwa na kukulia.Kuna wengine wanaamini kwamba ili aweze kusafiri kutoka New York kwenda Illinois basi ni lazima awe na passport.Je unaamini kwamba wamarekani ni wajinga? TV moja ya kutoka Australia iliamua kuwahoji baadhi ya wamarekani kuhusu mambo mbalimbali.Tizama video hiyo hapo chini.

Advertisements
 

25 Responses to “WAMAREKANI NI WAJINGA?”

 1. Tanzanian Female Says:

  Funny funny shi*! Hahahahaha

 2. binti-mzuri Says:

  ahhaha eti unaitaji visa from new york to illinois nimecheka wallahi! ngoja mi nibaki na umbumbumbu wangu!

 3. hombiz Says:

  Duuh! Hiyo kali. Ushauri wangu ni kama ifuatavyo
  Kwanza kabisa, nadhani itabidi wabadili mitaala ya masomo ya jiografia na historia. Badala ya kujifunza historia na jiografia vya marekani pekee, itabidi wabadili na kufanya masomo hayo yawe ya kimataifa. Nnaposema ya kimataifa, namaanisha wajifunze ni jiografia na historia za nchi nyingine duniani. Kwa mfano huko Bongo hata mtoto aliyemaliza shule ya msingi anajua kuwa kondoo wa sufi huzalishwa kwa wingi huko Australia na mlima mrefu kupita yote barani afrika ni kilimanjaro ambao uko Tanzania na si Kenya kama baadhi ya wageni wanavyofikiria. Na ukiwauliza Iddi Amini ni nani wanakueleza George Bush ni nani watakueleza kuwa ni raisi wa Marekani, tena bila hata kusoma huko shuleni. Lakini cha ajabu marekani ambayo ina maendeleo ya kila namna, watu wake bado wako nyuma sana katika ujuzi wa jiografia na historia ya nchi mbali mbali duniani.
  Pili, nadhani vyombo vya habari vya marekani vinapaswa kunyumbuika na kujaribu kuonyesha vipindi vyenye mafunzo mazuri kwa raia wake juu ya marekani yenyewe na dunia nzima kwa ujumla. Ni jambo la kushangaza kuona kuwa vyombo vya habari vya Marekani hupoteza muda mwingi kuzungumzia watu maarufu wa nchi yake kuliko hata mambo muhimu yanayoendelea duniani kote kama vile mgogoro wa Durfar, Chad, Zimbabwe, Naijeria na Somalia. Wao wanachoongolea muda mwingi kuhusu Afrika ni mbuga za wanyama, watu wa vichakani-bush man. Nakadhalika. Ndio maana sishangai kuona wananchi wake wanakuwa na uelewa mdogo kuhusu jiografia na historia ya nchi mbali mbali duniani. Ndio maana sishangai kuona wamarekani wanadhani waafrika tunaishi pamoja na wanyama pori huko porini. Mbaya zaidi, unaweza kukuta msomi wa chuo kikuu huko Marekani ambaye mpaka leo hii hajui kama Afrika kuna nchi zaidi ya 50 na pia kuna majengo mazuri, bababara nzuri na kadhalika.
  Narudia tena,mitaala ya masomo(jiografia na historia) na vyombo vya habari vya marekani, vinapaswa kubadirika kulingana na mapendekezo niliyotoa hapo juu.
  Hayo ni mawazo yangu!

 4. JMBigy Says:

  Ni kweli Hombiz. Vyombo vya habari vya marekani ni moja ya visababishi ya ujinga wa atu hawa. Kubweteka kwamba wao ndo wao na kila kitu kiko kwao na kwamba watafia hapa kwao ni sababu nyingine inayowafanya wajinga inapokuja kujua mambo ya dunia kwa ujumla na hata baadhi nchini mwao. Siko wakijua umuhimu wa kutokuwa ‘wajinga’ watauondoa.Tuombe wasijejua umuhimu huo too late.

 5. mtz Says:

  Moja ya vitu kinachowaua Wamarekani ni kwamba hawapendi soka. Soka ingewafunza ku-appreciate nchi nyingine. Wamarekani wanadhani kila kitu chao ni best. Mmenikuna sana, Americans are sooooo dumb.

 6. trii Says:

  mmmmm makubwa,ndo maaaaana.

 7. Ms Bennett Says:

  BC sio ujinga bali kutokana na proganda ambazo nchi za magharibi zimekuwa zikichangia sana. kuna rafiki yangu mmoja yeye ni mmarejani mweusi ambae amewahi kutembea sana afrika,alikuwa akiniambia west countries zimekuwa zikipiga propaganda haswa kuhusu afrika, kwamba afrika ni backwards,60% ya waafrika wana ukimwi wengi wanahofu ya kuambukizwa kama wataconnect na wenzao wa afrika.
  wamekuwa wakifundishwa hivyo kwenye social life.pia kuwa kila mtu afrika has bones in their noses and swing from trees.
  ndo maana utakuta wamarekani weusi wengi hawapendi kujichanganya na wenzao watokao afrika kutokana na propaganda, kama alivyosema mdau mmoja hapo juu marekani wanatakiwa wabadilishe system yao ya historia na jiografia ndo watu wao watafumbuka macho.

 8. DUNDA GALDEN Says:

  kweli kazi bado kubwa watu hawamji hata Koffi Annan?du
  ukiona kwako kunawaka kwa mwenzio kunateketea
  sijui kama inamaana sawa na hii GOD BLESS AMERIKA
  sasa ni wakati wa TZA wote kusema japo mara mojakwa siku
  GOD BLESS TANZANIA..
  chafosa

 9. Mtukwao Says:

  yasemwayo ni kweli kabisa na hiyo kideo inaonyesha sura halisi ya hawa watu. yani nivilaza kupita kiasi ni yiyo lugha tu ya english ndo inawasaidia. tena ni hiyo english ya kuombea maji mtaani, lakini ukiwapeleka darasani kwenye english 101 yani hawaoni ndani. hawajui proper english wanaongea slang, na slang haikubaliki darasana.

  iimijitu ni mijinga sana, yani weacha tu!

 10. maryciana Says:

  mh watu wengine kwa kujifanya wanajua humu!… wajinga wamevundua mobile phones, wajinga wamevumbua mcdonalds(kutwa hamkosekani),wajinga wamevumbua tv,mtv,hollywood.. wajinga hao hao na nyie si ndio wafuasi wao?basi na nyie wajinga vile vile

  makao makuu ya UN yako wapi vile?new york siyo..je ipo msumbiji?

 11. Dave Says:

  Please go to youtube and find Mis teen USA alipoulizwa swali na kujibu utumbo mtupu.Ni kweli,the problem yao Ni hiyo shule zao za awali hazitilli mkazo Geographia ya Dunia.

  Baada ya kusema hivyo,Tanzania ni watoto wangapi wanaelimu ya awali?Je wanajua geographia ya dunia?Mimi nafikiri hata kwetu tunatizo kubwa kuliko la America,kuna watoto wengi wanumri wa kwenda shule na hawapo shule.

  Kumalizia tu ni kuwa America they have good proportional ya wajinga na very very intelligent people.While Tanzania we have wajinga kweli kweli na just smart people.

  Maoni yangu
  Dave

 12. well Says:

  kama watanzania walifundishwa kutoka utotoni kwamba amna nchi nyingine nzuri duniani kama yao wangekuwa na majibu kama hayo.kujua iran iko wapi hakukupi ugali …

 13. sinyorita Says:

  Tatizo hawataki kujua dunia na nchi zingine zinavyoendelea, wao wapo busy na maisha yao hata watu wote wakifa duniani hawatajali. Wanafundishwa shuleni but wakishaondoka wanayaacha kwa sababu wananona hayawahusu, inasikitisha. Thats just pure ignorance and one day it will get back to them.
  Ndio maana wanpigwa na mabomu.

 14. Swordfish Says:

  Before you comment kwamba wamarekani wajinga, you need to know definetion of “mjinga” Is mmarekani kutojua Iran or Comoro ilipo inamfanya awe mjinga? au mmarekani kutojua mwenyekiti wa AU ni rais Kikwete wa Tanzania makes him mjinga? Ni watanzania wangani wanajua kijiji cha ipogoro kilipo, au wangapi believe Nyerere is still the president? or C.C.M is the only party in TZ?. Are they wajinga? I can guarantee that most commentator here don’t even know much about other part of TZ besides Dar, Mwanza……Moro. Is this makes you mjinga? I DON’T THINK SO. Right now I don’t even know tuna mikoa mingapi……Why should I care? [back the day – 20]. I’m I mjinga? Watanzania wajinga because tourist has been in Zanzibar na mlima kilimanjaro and we have not? Wanakijiji wa ushirombo don’t even know if there is an elevator…ni wajinga?. One thing you don’t know is, there re 50 states in US and average of three BIG CITIES in each of these states. Why should america care about TOKYO and not NYC? Why should they care about Paris instead of Las Vegas? You can live in NYC and never been in Albany or live in Los Angeles and never been in Sacramento or San Diego…are you mjinga? Most american can’t afford to take day off to travel to NYC or DC. Why should they, tha’s their question? If your hobby is travel the world, then fine you should know about Iran or Zimbabwe. If you care about environment, then you should know about KYOTO. Here in Dar, every body know Kobe BUT somebody in LA might not know who this guy is because he/she is not a BASKET BALL FAN. I used lived in New Jersey couple of years ago and NEVER knew who my governor or mayor was, BUT I knew mayor Guliani of NYC and Governor of California. Was I mjinga? When I tell my Tanzania hommies about never been in HOLLYWOOD for all those years that I have been in US…….I know for sure wananiona mjinga………BUT am I mjinga? I can go over and over………but I’ll make it short by telling you this….YOU WILL NEVER KNOW ABOUT AMERICANS AND AMERICA UNLESS YOU LIVED IN AMERICA. THIS IS A CONTINENT….

 15. binti-mzuri Says:

  duh swordfish umeongea pointi…kula 5 babake!

 16. peter ndio mimi Says:

  yaani swodfish what icn say to u is u need aproper serious diognosis..unapoint in some parts lakini ukiangalia vitu vingi ulivoandika hasa mwisho wa comment yako ni kama kuonyesha tht u kno americans better than anyonea else aliotoa koment kwa hii blog..na akili yako ilivokua mbovu unasema kabisa eti hujui tanzania inamikoa mingapi ila unajua marekani inastates ngapi…yaani we ni one of them kabisa(ignorant)..imagine eti mtu hujui kwenu kuna vyumba vingapi ila unajua jirani yako ambaye hajui hata kama we upo duniani au bado unarevolve kutoka nyani kwenda binaadamu,anavyumba vingapi,sebule,makochi hadi vyoo vingapi we ni mtumwa kama wajinga wenzio wote wasiopenda maendeleoa ya nchi yetu..kazi kusema nchi yetu haiendelei itaendelea vpi na nyinyi mnaotakiwa kuiendeleza mmeshupalia ya nchi nyingine ambazo haziwahusu..

 17. maryciana Says:

  HAHA posti ya 16 inafurahisha

 18. Leila Shakum Says:

  there is a girl called ‘maryciana’ who posted in June, 18, 2008 at 11:05 am post number 10. WOW! you clearly dont know what you are talking about.i have been here in the usa in maryland for 10 years. but what are you saying that usa invented tv and phones. phones were invented by alexander bell who was scottish. tv was invented by a belgian. you probably got mcdonalds correct but the rest is..am sorry to say..rubbish!

 19. Swordfish Says:

  Peter tha’s my point! So, let me ask you this…….kwa sababu sijui Tanzania ina mikoa mingapi naqualify kuwa mjinga? Nikikuuliza Wha’t our national GDP? What % of our budget are contributed by donors? Inflation? To me these are basic things that any citizen should know and care about BUT I can guarantee you, nenda posta mpya na camcorder and start asking these questions [you can figure out starting with you] Huu ndio ulimbukeni…….kufikiria kwamba somebody should know what you know. Open your mind bro….pamoja na kujua tanzania ina mikoa mingapi you might be one of them out there. The point I was trying to make was, NOBODY HAS RIGHT TO CALL SOMEBODY NAMES kisa umemuuliza question that he/she might never know. I remember when I was a kid, my dad or his friends used to ask me these pop questions like majina ya baraza la mawaziri, or reli ya kati inapita mikoa ipi? or hotuba ya kilimo cha kufa na kupona Nyerere aliitoa wapi? or big three region ni zipi? and kids smartness used to be judged based on these damn questions. GUESS WHAT……My daughter know nothing about these questions and she is still smart. Kama unaamini wamarekani wajinga…kisa hawajui some of these questions [which they have no business to deal with ni the first place] then tha’s you.

 20. missy Says:

  i completely agree with “peter ndio mimi” yani huyo mtu alikuwa anataka kutuambia tu kuwa amekaa marekani na anaijua marekani as if we care…kusema ukweli mimarekani ni MIPUMBAVU BWANA…he actualy seem like one of them ignorant americans who doesnt know nothing…i even doubt ka ni mbongo..

 21. kaduna Says:

  Hivi ukienda kariakoo ukawahoji wale wapita njia kuhusu international affairs picha itakuwaje? hakuna nchi isiyo na wajinga ila inategemea umeilenga hadhira gani!

 22. PdoneIT Says:

  Based na hiyo interview ni kweli hao WOTE waliohojiwa ni wajinga with a capital W. Mtu gani anashindwa kutaja nchi inayoanziwa na herufi ambayo nchi yake mwenyewe ni jibu la kwanza?
  Swordfish u tried to bail ’em out brotha but u know what? these dudes cant get bail, they are pretty much DUMB.

 23. kimpo Says:

  Hapo kuna vitu viwili, hiyo video it might be true au ni conspiracy
  Ila naweza agree kitu kimoja most of developed countries wananchi wanakuwa hawana habari na nchi nyingine, hata nchini yao especialy kama imegawanyika katika states, maana kila state inajitgemea kama nchi, sio USA tu hata South Africa wananchi wengi hawana habari na kinacho endelea dunian, unaweza amini kuna baadhi ya wa southAfrica wanajua Tanzania ni moja ya sehem ya nchi yao…………

 24. Hayo ni mambo ya kawaida, kwani hata watanzania pia wako hivyo hivyo, usiniambia mtu ambaye yuko kijijini huko Rukwa anajuwa lolote juu ya passport na matumizi yake, au anaweza kujibu kwa ufasaha hayo mswali waliokuwa wanaulizwa hapo na huyo bwana, hata hapo Dar ukimsimamisha mtu umuulizia mtaa fulani uko wako atakuambia sijuwi, hayo ni mambo ya kawaida na yapo kila mahali, kukifanyika utafiti wa kina pengine sisi wa tunaweza kuwa wajinga zaidi ya wa-USA.

 25. none Says:

  Hii ni kwasababu wamarekani wanaamini nchi yao inatawala dunia kwahivyo hawahitaji kujua mambo mengine ya nje.. hawajui geography wala history ya nchi yao wenyewe..


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s