BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UNAMKUMBUKA FELA ANIKULAPO KUTI? June, 19, 2008

Filed under: Burudani,In Memory/Kumbukumbu,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 3:46 PM

Fela Anikulapo Kuti.Pengine hili ndilo jina kubwa kupita yote miongoni mwa wanamuziki kutoka barani Afrika waliovuma ulimwenguni kote.Pia ni mwanamuziki ambaye alikuwa na marafiki wengi kama ilivyo kwa maadui.Kwa wengi ni shujaa.Kwa wengi ni adui namba moja.Aliwazibia riziki zao kwa kutumia muziki wake.Lakini Fela ni nani basi?Mpaka hii leo anahesabika kuwa mwanamuziki wa kiafrika aliyekuwa na vituko kupita mwingine yeyote.Je alichokizungumzia enzi za uhai wake kinaweza kuhusishwa vipi na hali halisi ya hivi leo barani Afrika na hata kwetu Tanzania? Naomba umsikilize mwenyewe,kwa maneno yake,katika mfululizo huu wa documentary kuhusu maisha yake.Fela alizaliwa October 15,1938 na alifariki August 2,1997.

PART 2 / PART 3 / PART 4 / PART 5 / PART 6

Advertisements
 

20 Responses to “UNAMKUMBUKA FELA ANIKULAPO KUTI?”

 1. Mswahilina Says:

  BC, asanteni kwa kazi nzuri, asanteni kwa kutukumbushia huyu gwiji wa Muziki Afrika.

 2. DUNDA GALDEN Says:

  Namkumbuka pale alipojitangaza kuwa yeye ndio Rais wa Nigeria moto ulimuwakia.pia alikuwa na wake wengi kama kawa..na ule mwimbo wake Nigeria jagajaga yaani Nigeria hamna kitu ovyo ovyo na Rais wa kipindi kile akasika kwenye radio yeye Fela Kut ndio jagajaga jamaa anavituko kwisha kazi
  mungu amlaze pema Ramadhan Fela Kuti

 3. hombiz Says:

  Alikuwa msanii mwenye mafanikio makubwa ktk medani ya muziki. Kwa bahati mbaya ukimwi ulimchukua. MOLA amrehemu, apumzike kwa amani, AMINA.

 4. zyb Says:

  Nakumbuka wakati niko Secondary (boarding) walikuwa wanaleta picha zake mashuleni kuhimiza mapambano dhidi ya ukimwi maana YEYE ALIJITANGAZA WAZI KUWA AMEATHIRIKA. Kuna wimbo flani aliimba kiswahili “LEO NI WEWE …. KESHO MWINGINE …. LAZIMA TUWEKE MSIMAMO ….. WA KUUKWEPA UKIMWI …. n.k.” Tangu hapo hilo jina liko tu akilini.

 5. trii Says:

  duu kuna wimbo mmoja niliona kwenye tv yani anacheza na chupi tuu hana wasiwasi.nikawaza ingekuwa tz sijui serikali ingesemaje.

 6. mimmy Says:

  kila kizuri hakikosi kasoro, hamna shala kama Fela kuti alikuwa mwanamuziki mahiri ILA TUU alikuwa ana udhaifu wa kupenda ngono kila wakati.

  atakumbukwa kwa vituko vyake kwenye mazoezi ya nyimbo zake na umahiri wake katika kutunga na kuimba.

  Mungu amsamehe kwa yote aliyomkosea InshAllah!

 7. Amina Says:

  mi pioa nakumbuka niliona documentary yake anaimba na kichupi tu..na madem waimbaji wake wamemzunguka…..hatari

 8. Nyundo Says:

  SI JINA KUBWA KULIKO WANAMZIKI WOTE AFRIKA,
  JINA KUBWA NI LUAMBO MAKIADI LOKANZA MPENE (FRANKO)
  Ambaye amevunja rekodi ya kutunga album nyingi nakujulikana kuliko FELA

 9. john Says:

  unbeliavable character !
  Would pay to watch his move . Would wear his clothes

 10. Amina Says:

  hapa anaongelewa fela haongelewi franko…sawa

 11. Kisu Says:

  Amina!
  usijisahau kuwa mwanamziki anayeongelewa kuwa amehandikwa ndiye mwenye jina kubwa kuliko wote,
  sasa hoja ni kuwa si Fela aleyekuwa na jina kubwa,bali mtoa maoni Nyundo kamtaja Franko,sasa lipi kosa hapo????

  Franko ametunga nyimbo zaidi ya 3000 akiwa na umri wa miaka 16 tayari alikwisha saini Deal na lebo kubwa yakutawanya mziki ulaya,wakati alipokuwa na Orch.Uluningaisa.
  Kilichokuwa kinaongelewa katika maoni ni JINA KUBWA sio kuwa mtoa maoni Nyundo anachanganya habari za Franko na Ankulapo Ramson Fela Kuti

 12. binti-mzuri Says:

  kuna ule wimbo wa ‘bang bang bang’ mzuri kweli. im not very familiar with his music kwa kweli,ila nimesikia baadhi,mingine inachezeka!..r.i.p to him.nadhani he has a son who is in the business now,nimesahau jina

 13. Chris Says:

  Jamaa tulizaliwa tarehe moja!

 14. Amina Says:

  we kisu nini weweeeeeeeee…….muongeleeni tu fela na ni kweli anajina kubwa kwani uongo haijalishi kutunga nyimbo nyingi,mnaelewa maana ya jina kubwa?mfano mzuri q chief kaanza mziki cku nyingi na katunga nyibo nyingi ila ali kiba kaja juzi na hana nyimbo nyingi lakini ana jina kubwa kafunika..sijui mnaelewa maaana ya jina kubwa na kutunga nyibo nyingi?hahahaha matty upo?mi leo nimejaa tele nasubiri bc anibanie!jina kubwa na nyimbo nyingi ni kitu tofauti

 15. Matty Says:

  Kumbe Chris umezaliwa tarehe hiyo, na mwaka je???????????

 16. arosto Says:

  Mtoto wake anaitwa femi kuti, zyb sio unamuongelea file lutaaya wa uganda ambae ndie wa kwanza kujitangaza ana ukimwi kama sikosei, hata hivyo sijawahi ona hii ya fella kuti kujitangaza japo niliona documentary zake alikua mtu wa mikasi na blunt kwa sana yaani na wakati alikua msomi na baba yake alikua mtu tajiri sana. Femi, mtoto wake pia kwenye cora awards alitahadharisha watu kuhusu ukimwi na kusema hadharani kwamba ndio uliomuua baba yake. RIP

 17. Matty Says:

  ahahahahahahahaha humu ndani raha sana Amina naona BC hajakubania maoni yako! hongera!

 18. Chris Says:

  Aminaaaaaaaaaaaaaaaa! Mwaka mmoja pia Matty! Ok, Matty ni ule wa kwako halafu toa mbili!

 19. Amina Says:

  chris umeshangaa nini?

 20. Matty Says:

  Haya Chris mdogo wangu niamkie sasa nimekuzidi 2yrs!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s