BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAJIRANI HUZIMA RADIO-SIKINDE June, 20, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:04 AM

Haya tena waungwana.Mwisho wa wiki ndio ushaingia.Fursa nyingine ya kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.Yaani kama vile ambavyo katika ule usiku wa kumaliza mwaka(New Year’s Eve) watu tunavyojiwekea malengo,basi mimi naamini hata wiki moja tu ikikatika,unaweza fanya hivyo hivyo.Sababu ni ya kawaida tu;yaliyopita yeshapita,hayarudi tena!

Leo kwa upande wa burudani tuna ombi rasmi.Wakati wa burudani ya wiki iliyopita,msomaji na mtoa maoni wetu mmoja aliomba sana kuusikia wimbo wa Majirani Huzima Radio kutoka kwao DDC Mlimani Park almaarufu kama Wana-Sikinde.

Piga picha hii,mume na mke hawapatani,kila siku ugomvi hauishi.Wanaporejea kutoka makazini ni ugomvi mtindo mmoja.Kwanini huwa inatokea hivyo?Na je majirani wanaozima radio zao ili wawasikie jinsi “pwagu na pwaguzi” wanavyogombana wanawasaidia au ndio wanajiambukiza maradhi ya kugombana kila mara?Nini ushauri wako? Usikilize wimbo huo hapo chini kisha uniambie.BC inakutakia wikiendi njema.

Advertisements
 

15 Responses to “MAJIRANI HUZIMA RADIO-SIKINDE”

 1. Mwakyusa Says:

  BC,mmenikumbusha mbali sana ndg zangu. Hongereni kwa kazi nzuri ya kutupa mambo ya kale. I wish you all the best guyz.

 2. EdwinNdaki Says:

  Ijumaa njema wadau.

  nimekumbuka kipingi cha kina pwagu na pwaguzi mida ya jioni jpili RTD.Matty upo hapo?

  pamoja watu wangu..naenda mapumziko ya juma tutaonana j3.

  wasalaaam

 3. EdwinNdaki Says:

  kumradhi..mstari wa pili kutoka juu naomba usomeke..nimekumbuka KIPINDI na si kipingi..si unajua mambo ya ijumaa wengine tayari tumeanza kuchachua…aa aaa

  gervas upo?

 4. Maabadi Says:

  Asante kaka!

 5. DUNDA GALDEN Says:

  SAFI BC MZIKI WA NGUVU UJUMBE WA KUMWAGAAA
  PIA IMENIKUMBUSHA WAHENGA.WAKIGOMBANA CHUKUA JEMBE UKALIME WAKIPATANA KAVUNE…SASA MJIN RAIA UZIMA RADIO KUSIKILIZA UGOMVI WA PWAGU NA UPWAGUZI
  LONG TIME MIZIKI YA NYUMBANI NAWATAKIA WIKI
  END NJEMA.NANYI WAOSHA VINYWA SASA
  BASI NI WAKATI WA KUSAMEHEANA NA KUGANGA YAJAO
  Chafosa

 6. Angeline Says:

  BC sijui nianzeje? Mmenikumbusha mbali saaaana enzi za redio Tanzania na kina anko J. Pia nimemkumbuka baba yangu(RIP) alikua anaupenda sana huo wimbo hasa pale kwa pwagu na pwaguzi. Nadhani ntaupiga huu wimbo leo siku nzima. Ubarikiwe.

 7. masumbuka Says:

  If I could turn the Clock back!Enzi hizo Ukimwi bado.Elfu Tano mfukoni unaweza ukatesa kwa sana tu!Na Sikinde ilikuwa imekamilika.Nashangaa Viongozi wengi waliopo katika ngazi za juu walikuwa wakijirusha sana katika magoma ya Sikinde enzi hizo!Lakini leo hii Sikinde ipo hatarini kusambaratika kwa sababu ya Uchakavu wa Vyombo vya Muziki na kutopata Support ya kutosha kutoka kwa Wapenzi wake wa Jadi,sijui inakuwaje wadau, Haipendezi hii hata kidogo. Namtupia changamoto Rais wetu Mh.Jakaya Mrisho Kikwette hebu alitupie macho suala hili nyeti na tete kwa wapenzi wa Muziki wa Kitanzania. Sikinde kwa Tanzania inaweza kufananishwa na OK Jazz kwa Congo DRC! Kwa wote wenye uwezo na mapenzi mema kwa muziki wa kitanzania fanyeni hima. Kina Bitchuka , Shabaan Dede na wenzake bado wangalipo. Jamani Wakopesheni Set nzima ya Vyombo watalipa polepole ndiyo mwendo! Tusiruhusu hazina hiyo pekee ya muziki wa kitanzania ambayo hivi sasa ni Lulu kwa Taifa ipotee bure! Hatutawatendea haki hawa mashujaa wetu! I Pray for you Sikinde, Bitchukaz and Dedez!Aza Waiz have a nice weekend!

 8. Amina Says:

  mhhhhhhh..mi navuta pumzi enzi hizo naona nilikua ng’aaaaa

 9. kahindi Says:

  kwako maabadi…hope kiu yako imekatika..BC na mimi naomba next friday uniwekee kitu SELINA…ohhhh selina piga moyo konde,oh selinaa,utafanikiwa oo selina…wadau tuonane jumatatu….take care guyz..kwa heriniiiiiiiiiiiii

 10. Matty Says:

  Nipo Edwin Ndaki, nadhani mimi na Amina tulikuwa vichanga maana nyie kakazetu mlikuwa mnabanjuka kwa kwenda mbele!

 11. binti-mzuri Says:

  kumradhi,out of topic kidogo,ila hivi wewe matty ni mwanamke au mwanamme??

 12. kahindi Says:

  mhh…bint mzuri una matatizo humu ndani ya bc.

 13. Matty Says:

  Binti mzuri kuuliza si ujinga shost! wala hujakosea maana jina langu ni tungo tata wengi wanajiuliza, hili jina linakirefu ila nimezoeleka kuitwa Matty.
  Inshort i’m a beautiful girl in& out hahahahahahahahahahahahahahahahah karibu sana!

 14. binti-mzuri Says:

  thanx matty..maana niliona unatumia ‘shost’ n.k. nikabutwaa…lol..maana nna mshkaji anaitwa matty na ni mwanaume short for mathew,so nikawa sina uhakika.thank for letting me know though.. maana swali lilikua direct kwako,nashangaa viumbe vingine vikasimama

 15. Matty Says:

  hahahahahahaha! Binti mzuri hao viumbe wengine inabidi uwazoee tupo tofauti sana…ok mimi kwa kirefu naitwa Mattylda.your welcome!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s